*NA MWL CHRISTOPHER E.A.  MWAKASEGE*
*TAREHE 5 SEPT 2016*.
*SIKU YA 2*

*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA*
Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu aliyehai,  jana tulianza na tumesoma Mstari wa _Waefeso 5:15-17 ‘’ Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; *MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU*. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana’’._
Katika mstari wa wa 16 ndio tunapata msisitizo wa somo hili, na mstari huu una maanisha kuwa kuna muda tunaotakiwa kuukomboa ili tuweze kuutumia kwa hekima katika kutembea katika mapenzi ya Mungu. Hivyo suala la ukombozi wa muda uliopita ili ukusaidie kutembea kwenye  *zamani hizi ni muhimu sana*_

*Tuendelee na Point ya Saba*
*7  *Ikiwa aina ya maisha uliyonayo si mazuri na  yanasababishwa na aina ya wakati unaaoishi, fanya maombi ya kuingilia kati muda huo ili kubadili aina ya maisha*
*Mathayo 24:21-22* ‘’ Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo’’.
Kwa hiyo katika mstari huu tunaona ya kuwa Mungu anaingilia kati muda uliobeba hizo dhiki. Yaani hakushughulika na dhiki bali alishughulika na muda ulioleta hiyo dhiki.  Maana angeshughulika na dhiki ina maana ingeondoka kwa kitambo na baadae ingerudi tena. Mungu aligeuza lango la Muda kwa ajili ya kuwasaidia wanadamu (Mwanzo 1:1) lakini kumbuka hili Mungu yupo kwenye hali ya umilele.
Ukisoma matendo ya mitume 17;26 utaona ya kuwa Mungu aliumba  kwanza muda ndipo akaumba akamumba mbingu na nchi na mwanadamu. Katika neno la Mathayo 24 biblia inatuambia kuwa Mungu anafupisha muda wa dhiki na ina maana muda wa dhiki ukifupishwa na dhiki itaondoka maana inakuwa haina uhalali wa kutumia muda kwa sababu muda wake haupo.
Ufunuo wa Yahana 1:8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.. Yesu ni alfa na Omega yaani ndiye anayecontrol muda  japo yeye yupo kwenye hali ya umilele na sababu ni ili atawale dunia maana dunia inakwenda na muda yaani imefungwa na muda ila mbinguni kuna umilele na ndiyo maana mstari huu unasema *aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi*
*Marko 13:33* ‘’ Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui *wakati ule utakapokuwapo* Kwa hiyo kuna aina ya maombi ambayo yanashughulika na wakati utakaokuwapo na ndio maana biblia inasema ombeni na inatoa angalizo mapema, ili utakapofika wakati huo uweze kutembea kwenye zamani hizo. Na kwa kuwa hajui namna ya kufanya utajikuta umeingia kwenye siku hizo.
 *MBINU ZA KUKOMBOA KILICHOTEKWA*
Huwezi kukomboa kitu ambacho hakina thamani kwako na ili uweze kukomboa inatakiwa uwe na nguvu Zaidi ya mwenye nguvu aliyeiteka nyumba yako yaani mtekaji na uweze kumfunga na ndipo ukomboe kile kilichotekwa.
Katika maisha haya tuko tofauti tofauti na kila mtu inatakiwa atembee kwenye hatua zake yaani muda wake na usitembee kwenye muda wa mwingine.
*ILI KUPATA MBINU HIZI NI LAZIMA UJIULIZE MASWALI HAYA YAFUATAYO*
*Swali la Kwanza* _Kilichotekwa ni kitu gani, hapa tunapata *jibu lake* kuwa kilichotekwa ni muda._
*Swali la pili*  _Aliyeuteka huo wakati anatafuta nini kwenye huo wakati aliouteka_
        Jibu lake ni *1* Kuzuia aina ya maisha yaliyobebwa na wakat uliotekwa
     
*Swali la tatu* _Aliyeuteka wakati ametumia nini ili kuuteka huo wakati. 
Yaani anatumia kile kilichoumbwa ili kuubeba wakati kama lango, katika maisha ya mwandamu.
*Swali la nne* Ukikomboa wakati unapata kitu gani. Kwa hiyo ili uweze kuwa na mission nzuri ya ukuombozi yaani unakomboa kitu ambacho kinabeba vyote yaani wakati.  Kwa hiyo ukikomboa kilichobeba 
>Utapata kibebeo cha wakati 
>Wakati
>Maisha yaliyomo ndani ya wakati.
Kosa la watu wengi ni kutumia muda ambao hawana au wanatumia muda usiokuwa wakwao. Yaani hata ukijitahidi unaweza fanikiwa kwa jinsi ya mwilini lakini rohoni ukafeli. Biblia inatumbia kuwa kufanikiwa kuaanza rohoni ndio maana katika ule *Waraka wa 3 Yohana 1: 2* unasema ufanikiwe kwa kadri roho yako ifanikiwavyo. Pia katika mithali ni Biblia inatumabia kuwa kufanikiwa kwa mpumbavu kutamuangamiza.  
Ili kuweza kufanya ukombozi wa wana wa Israel Mungu anataka kukomboa *miguu na kipande cha sikio* angalia Amosi 3:11-12,Mungu hakukomboa kila kitu bali alishughulika na kilichobeba maana ukombozi wa miguu na kipande cha sikio unaokoa na vitu vingine.  Na akiwakomba miguu na masikio atakuwa kakomboa pamoja na majumba yaliyotekwa. 

*Kumbukumbu la Torati 9:26* ‘’ Nikamwomba Bwana, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, *ULIOWAKOMBOA KWA UKUU WAKO*, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.
Kitabu cha Kumbu kumbu la Torati ni Kitabu cha makabidhiano kati ya Musa na Joshua yaani ni report ya Musa kwa Joshua. Kwa hiyo kuna baadhi ya mambo huwezi pata katika kitabu cha Kutoka , na Hapa Musa anaonesha maombi aliyoyaomba baada ya wana wa Israel kuabudu ndama. 
Na alipoamua kuwakomboa wana wa Israel alitumia *lango la mzaliwa wa Kwanza*. Maana Mungu hakuvamia nchi yote na jeshi bali alitumia lango la mzaliwa wa Kwanza. Hata Farao hakujua mbinu hii ambayo Mungu aliitumia. *Kuna kuwa na kitu kinachobeba wakati na ndicho shetani anakiwanda kifuatilie na kikomboe na utakuwa umepona sana*
Habakuki alipokuwa anaomba Mungu amsidie kutokana na ile hali iliyokuwepo , *Mungu alimwambia andika Njozi*. Ina maana kilichokuwa kimetekwa ni njozi na ndio maana Mungu alisema andika Njozi. Kuna mifano mingi kwenye biblia fuatalia na utaona.
 *SHETANI ILI KUKAMATA MUDA WA MTU ANATUMIA FIKRA*
2Wakorintho 11:3 ‘’ Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije *akawaharibu fikira zenu*, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
Mithali 23:7 ‘’ Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe’’
Biblia isema tuwe makini ili yule mwovu asipate tena nafasi ya kuweza kuteka Fikra zako. *FIKRA* ni mtiriko wa wa mawazo unaotengeneza aina ya msimamo ndani ya mtu. Na hapa nataka uwe makini maana kuwa watu wanachanganya kuwa kila wazo ni fira sio kweli kwa sababu si kila wazo linalokuletea msimamo. Kwa hiyo aina ya picha iliyo ndani yako ndiyo inayofanya picha inayotoka ndani yako kuja nje yako. 
Nyumba unayoiona leo hapa nje ilikuwa ndani ya mtu kwanza. Na ndipo ikatoka nje na pia magari unayoyaona leo yalikuwa ndani ya watu mbali mbali waliyoyabuni. Yaani yalikuwa ndani ya mtu.
Na somo hili limenipa shida kidogo maana nilikuwa namuuliza Mungu kuwa kwanini unataka nifundishe watoto wako wawe kama mafundi na sio madereva. Maana kujifunza kwa dereva kuhusu gari ni tofauti sana na fundi. Kwa sababu fundi anafundishwa kujua kila kitu kwenye gari kwa mfano kama ni engine basi atafundishwa namna inavyofanya kazi na kila kipengele na ikitokea shida yoyote ajue cha kufanya. 
*Mhubiri 3:11* ‘’ Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho’’
Kwa hiyo tunaona hali ya umilele ikiwa ndani ya Roho na Mwili, ila nafsi imwekewa muda yaani ina limit. Baada ya dhambi kuingia iliharibu mfumo mzima wa maisha na kuondoa umilele kwenye mwili na kuleta mauti. Lakini japo hili jambo hili lilitokea lakini Mungu bado kuweka mwili mwingine ambao una umilele amboa kila mtu atapewa. 
Suala la muda lipo ndani ya nafsi maana nafsi ndiyo inadictate muda wa maisha. Ukitaka kujua namna nafsi inavyofanyakazi na muda ni kwa mfano safari kwenda marekani yaani unakuta unatoka huku usiku muda wa kulala afu unafika tena kule usiku muda wa kulala. Na hapo ndipo shida inatokea kwa sababu mwili na Roho yako viko marekani ila nafsi yako iko Tanzania na kama hujui cha kufaya itakuchukua mud a kidogo kuweza kwenda mabadiliko hayo. 
Hivyo ndani ya nafsi inabebwa fikra, kwa sababu kama umeokoka inatakiwa kuanzia sasa mwili, roho yako na nafsi yako vibadilike, usikoke mwili na roho tu bali hata nafsi pia ili fikra zako ziendane na wakati uliopo. Huwezi kuwa kanini na uendelee na fikra za misri.  Na ndio maana shetani anawinda sana fikra za mtu  ili aweze uzifunga.
Ukisoma *2 Nyakati 2:32* utakutana na habari za wana wa isakari  na walivyojua namna ya kufaya mambo kwa majira na Nyakati. *Waefeso 2:10* biblia inatumbia kuna matendo ambayo tunatakiwa akuenenda kwayo ili tufanikiwe.
Ukiangalia *1Wakorintho 13;11* Paulo anasema kayabatilisha mawazo ya kitoto na ukisoma *Wagalatia 4:1* Biblia inasema mtoto ni sawa na mtumwa. Kwa hiyo akili yako kama haikui na hubatilishi mawazo ya kitoto utakuwa kama mtumwa. Umri wa aina Fulani unandana na fikra au mawazo ya aina Fulani maana ukiwa mkubwa huwezi endelea kufikiri kama mtoto au kucheza kama mtoto. 
Badilisha Fikra zako pamoja na muda wako ili uweze kuenda hatua nyingine. Na ni lazima mawazo yabatilishwe. Shetani anapokujia katika fikra zako anakuja kwa roho ya uongo na kukuleta uzito wa kutafsiri agano la kale kwa jicho la agano jipya.  Maana ufalme wa Mungu ulishuka mara mbili yaani kwenye agano la Sinai (lilileta sheria) na la Daudi (kiti cha enzi)  na ndipo ufalme wa Mungu ukaja.
Urithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu pamoja na wazao wake(Upo kwenye agano la kale hauupati kwenye agano jipya)  na ili uweze kufaidi Baraka hizi ni lazima umkiri Yesu awe Bwana na mwakozi wa maisha yako yaani agano jipya maana agano la Ibrahimu liliwafikia mataifa kwa njia ya Yesu Kristo.  Na ndio maana masuala ya kidini ni masuala ya kifikra ukiona mtu kafungwa na dini shughulika na Fikra. Na Fikra ni uwanja wa mapambano wa miungu. Shetani anakuwinda ili akuteke na akufanye uishi nje ya Muda. Na ukiingia ndani ya Yesu utaanza kuwa ndani ya muda na utafanikiwa. 
Mungu anataka tuwe *wealth* yaani wealth inapimwa na muda na sio *rich* maana rich inapimwa na supply, yaani uwezo wa kupata unachokihitaji.

Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours