Njaa kali inakuja !
Unajua ni ya nini ?
Ya kukosa kulisikia Neno la Mungu.Watu watatangatanga huku na kule wakilitafuta Neno la Mungu lakini hawatalipata. (Amo 8:12)
Si kana kwamba Neno la Mungu halitakuwepo. Hapana. Litakuwepo lakini litakosa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Wahubiri wengi watakuwa wakilihubiri neno kulingana na kutaka kwao na kwa tafsiri za kuhalalisha mawazo yao. Neno la Mungu kwao litakuwa lile lisilopingana na matakwa na tamaa zao. Baadaye ukavu utatawala mafundisho yao na Roho Mtakatifu hataendelea kuwavumilia.
Na hapo ndipo watu watakapoanza kutangatanga huku na kule wakitafuta ni nani anayelisema Neno la Mungu lenye uvuvio watakosa na kuangukia kwenye nyavu zilizotegwa kwa maarifa ya kidunia na kupakwa rangi ya Neno la Mungu ili waangamie.
1. Nini kilichonifanya nikaja hapa kusali.? Kama ulikuja ukiwa mhitaji wa kuponywa ugonjwa, ulifurahishwa na miujiza,unabii, ulimfurahia mtumishi, ulipendezwa na kanisa lao au kwaya au uliletwa na wazazi wako, au kwa sababu na baba na mama wanasali hapo au chochote kile nje ya mvuto wa Neno la Mungu bado hujakutana na Mungu lazima utatangatanga tu.
2.Uwepo wangu hapa bila kuwepo mwingine yoyote ninamwona Mungu? Kama ukijiona Mungu hayupo kama Askofu, Mch, Nabii, Mtume, Mwinjilisti au watu wengine n.k hawapo bado hujakutana na Mungu. Wewe ni wa kutangatanga tu.
3. Una mguso wa Roho Mtakatifu kwa wenzako wanaompenda Yesu na una uhuru wa kweli moyoni.? Kama unakwazika moyoni unapokosolewa kwa kile unachokiamini kiasi cha kukasirika na kususa hata kuendelea na wenzako. Bado hujakutana na Mungu na wewe ni wa kutangatanga tu. (Zab119:165).
Bwana Yesu alimwambia Petro. Lisha wanakondoo wangu
Chunga wana kondoo wangu
Lisha wana kondoo wangu. Watumishi wa Mungu tulishe wanakondoo, tuchunge wana kondoo. Msisitizo lisha wana kondoo wangu ili wakati wa njaa wawe wameshiba na kujiwekea akiba. (Yn 21:15-17)
Kondoo hawatashibishwa kwamatisho na maonyo makali ya kutokwenda hukona huko. Kondoo hushibishwa na majani mazuri meroro, mabichi, Wakiyakosa watatangatanga.
Nbarikiwa sana na haya mafundisho Mungu awatie nguvu muendelee kutuelimish
JibuFuta