MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
MITHALI 17:28 Hata mpumbavu
akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba
tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila
tunachokiona tunataka kukisemea kitu.
Kuna wakati tunasikia na kukutana na
mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu,
unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa
lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa.
Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea
kitu. Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu.
Si kila ufanyiwacho ni lazima
umwambie kila mtu.
MUHUBIRI 3:1 Kwa kila jambo kuna
majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa
kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
*Ipo nguvu katika kunyamaza*
Yapo mambo ambayo tunapaswa kuongea,
kusema, lakini yapo mambo ambayo tunapaswa kunyamaza kwa ajili ya usalama wa
Roho zetu.
Ni kweli kuna wakati unasemwa sana
vibaya, unasingiziwa, unatukanwa nk nk, lakini ni lazima ukumbuke kwamba kuna
mazingira ambayo hupaswi kujibizana hata kama umeumia kiasi gani.
*Unajua ni kwanini?*
Ukisemwa vibaya, ukitukanwa,
ukidharauliwa lazima moyo utaghafilika, moyo ukighafilika lazima utakuwa na
hasira na ghadhabu.
*Ukiwa na hasira katu usitegemee kuwa
utajadiliana na mtu kwa hekima.*
Ukiongea utaongea katika uwepo wa
hasira, ukijibu utajibu kulingana na kiwango cha hasira ulichonacho.
*Sasa jiulize majibu yanayotoka
kutokana na msukumo wa hasira huwa yanakuwaje?*
Mazuri? Ya upole? Ya hekima? Ya
unyenyekevu? I am sure jibu ni hapana.
Kama jibu ni hapana that means
utaongea vitu vibaya ambavyo ni chukizo kwa MUNGU kwa sababu amesema maneno
yetu na yakolee munyu (chumvi).
Sasa badala ya kuongea upumbavu na
ukamkosea MUNGU kwanini usichague kunyamaza?
AMOSI 5:3 Kwa ajili ya hayo mwenye busara
atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.
Nimekuwa inspired sana na mwanamke
Abigaili, ni kweli mumewe alikuwa na makosa, ni kweli alikuwa mlevi, lakini
mwanamke huyu alijua ni wakati gani, na mazingira gani alipaswa kuongea na mumewe
na alijua aongee nini. Alipomkuta mumewe yupo katika hali ya ulevi, ALINYAMAZA,
alijua kuwa huu sio wakati wa kusema jambo lolote.
1 SAMWELI 25:1
Ni vyema sisi pia tukajifunza kusoma
mazingira na nyakati na hali za watu zilivyo ili tujue ni wakati gani tujibu,
tuongee nini na ni wakati gani tunyamaze
Kilinde kinywa, hakikisha haukiachi
kinene mabaya – ZABURI 50:19.
Usipoteze marafiki na kuharibu
mahusiano kwa ajili ya kinywa kibovu – MITHALI 11:9.
Ni vyema tukajifunza kujua ni neno
gani tukitamka kwa wakati/hali/mazingira gani litakubaliwa –MITHALI 10:32.
ZABURI 19:14 – Bwana na akafanye
maneno yetu yakapate kibali mbele zake MUNGU na mbele za wanadamu pia.
1SAMWELI 25:36
Umeumizwa, umekwazwa, umetukanwa,
umedharauliwa, KATIKA MAZINGIRA YA HASIRA NA GHADHABU JITAHIDI KUNYAMAZA.
Ni kweli moyo na akili na hisia
vinakusukuma kujibu, kubisha nk nk, lakini elewa impact za kujibizana ukiwa na
hasira na hizo ni bora ukae kimya.
*"AKUSHINDAE KUONGEA, MSHINDE
KUNYAMAZA
"Muwe na siku njema!
Post A Comment:
0 comments so far,add yours