Articles by "SLIDER"
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SLIDER. Onyesha machapisho yote

Je unaona kama mke wako hakuheshimu? Anahitaji upendo toka kwako. Je mume wako haonyeshi  upendo? Anahitaji heshima toka kwako.
Jinsi wewe na mwenzi wako mnavyotendeana kulingana na kila mmoja anavyohitaji, ndivyo jitihada zenu zitakapoleta matunda na kila mmoja atazidi kutiwa moyo kuendelea kutenda  mazuri kwa mwenzake na kupeelekea kuboresha ndoa yenu. Sasa ili kufanikisha hili kila mmoja wenu lazima ajue kuozungumza lugha ya upendo na heshima kwa mwenzake.
Zitazame tofauti zenu kama mtaji na sio tatizo
Tofauti kati yako na mwenzi wako haimaanishi kuwa mmoja wenu hayuko sahihi. Muombe Mungu aweze kukusaidia kuzikubali tofauti kati yenu na kukuwezesha kuzitumia kusaidiana na kufaidiana. Kumbuka mbele za Mungu wote ni sawa na mna thamani sana.
Muone mwenzi wako kuwa ni mtu mwenye nia njema
Kama mwanadamu mwingine mwenzi wako pia anaweza akafanya mambo yanayoonekana kama ubinafsi. Ni muhimu kuwa na imani kuwa mwenzi wako ana nia njema juu yako hata katika nyakati anaposhindwa kuonyesha upendo na heshima juu yako. Kumbuka kuwa ndani ya moyo wake mwenzi wako anakupenda na hapendi kukuudhi. Muombe Mungu akuwezeshe kumuona mwenzi wako kama yeye anavyomuona.
Chunga maneno yako
Maneno unayoongea yanaonyesha yaliyomo ndani ya moyo wako. Hivyo muombe Mungu aujaze moyo wako upendo na heshima kila siku, na muombe Roho mtakatifu kuifanya upya akili yako ili mawazo yako yawe mema yatakayokupelekea kuongea maneno mema yenye upendo. Kuwa mwangalifu nay ale unayoyasema kwa mwenzi wako na jinsi unavyoyachukulia yale mwenzi wako anayoyasema. Epuka kutumia maneno ambayo yatamuudhi mwenzi wako. Sikiliza kabla ya kujibu na fikiri kwanza kabya ya kuongea. Hakikisha unaongea kwa sauti nzuri ya upole na upendo na pia lugha ya mwili iwe ya upendo na upole pia. Nia kuongea maneno yanayojenga, ya kweli, yenye msamaha, ya kushukuru, ya kiMungu na yenye kutia moyo.
Tambua lugha ya mawasiliano ya mwenzi wako
Wanawake na wanaume wanatofauti kubwa sana ya lugha ya mawasiliano kati yao. Itambue lugha ya mawasiliano ya mwenzi wako, usiwe na hisia tu bali hakikisha unaielewa vyema ili kuepuka migogoro inayotokana na kutokuelewana au tafsiri isiyo sahihi. Sikiliza kwa makini, uliza pale unapokuwa na wasiwasi na azimia kujifunza na kuifahamu lugha ya mawasiliano ya mwrnzi wako. Kumbuka kutokuelewana kwa lugha ya mawasiliano na jinsi ya kuwasiliana hakumaanishi ndoa yenu ni mbaya, bali kunaonyesha tofauti ya matarajio na namna ya kuwasiliana. Jaribuni kwa pamoja kwa msaada wa Mungu kukabiliana na hali hii kwa upendo na maelewano.
Samehe
Tegemea msaada wa Mungu katika kukuwezesha kumsamehe mwenzi wako pale anapokukosea, mara zote. Kumbuka kuwa Mungu amekusamehe makosa yako na hivyo onyesha msamaha kwa mwenzi wako. Pale unapopata msamaha kwa mwenzi wako baada ya kumkosea tambua kuwa kuna uwezekano wa kuhitaji muda wa kuponya jeraha la moyo wake, kuwa muelewa na onyesha kuwa kweli umekubali kosa lako na upo tayari kurekebisha.
Timiza mahitaji ya muhimu ya mwenzi wako
Hakikisha unatumia uwezo wako kuhakikisha unatimiza mahitaji muhimu ya mke wako ya kuwa karibu naye, kuwa muwazi, kumuelewa, kumthamini, kumtunza na kumjali. Anahitaji uwe karibu naye katika hali zote, kuwa muwazi kwake na kushirikiana naye katika mawazo na mipango yako, kumsikiliza bila kujaribu kumbadilisha, kusuluhisha matatizo kwa pamoja, kumheshimu na kila wakati kumhakikishia upendo wako kwake.
Hakikisha unatumia uwezo wako kuhakikisha unatimiza mahitaji muhimu ya mume wako ya uongozi, mahusiano na kimwili. Tambua hitaji lake la kuongoza na usijaribu kuudharau uongozi wake, sikiliza kwa makini mawazo yake na ushauri, thamini hitaji lake la kuwa karibu na wewe na kuwa rafiki yake katika hali zote, na uwe tayari kwa hitaji la kimwili bila vipingamizi.
Tambua kuwa Mungu pekee ndiye anayeweza kutimiza kila hitaji la mwanadamu. Hivyo mwenzi wako anaposhindwa kutimiza baadhi ya mahitaji yako usikasirike wala  kuumia sana. Badala yake mwendee Mungu.
Angalia nia yako
Usitumie vitendo au lugha ya upendo na heshima kama njia ya kumfanya mwenzi wako kufanya kile unaachokitaka. Muombe Mungu akuwezeshe kuwa na nia safi kila wakati ili uweze kufanya jambo jema kwa nia njema na kwa wakati unaofaa, kumfurahisha Mungu na pia mwenzi wako. Onyesha upendo ha heshima kwa mwenzi wako bila kutarajia chochote kama malipo.
Chagua lililo jema bila kuangalia mwenzi wako anasema nini
Hata kama mwenzi wako haonyeshi ushirikiano kwa jitihada zako za kuonyesha upendo na heshima wewe endelea kufanya hivyo kwa moyo wa kupenda. Mungu atazilipa jitihada zako kwa kukubariki. Tamabua kuwa kwa kumwonyesha mwenzi wako upendo na heshima unakuwa unamtumikia Mungu na kumheshimu, hivyo endelea kufanya yaliyo mema bila kujali mwenzi wako anafanya nini. Mungu anaona na atabariki juhudi na jitihada zako.


Swali: "Je! Maombi ya pamoja ni Muhimu? Maombi ya pamoja ni yana nguvu kuliko ya mtu mmoja?"

Jibu: Maombi ya pamoja ni sehemu muhimu katika maisha ya kanisa, pamoja na ibada, na kanuni nzuri, kuumega mkate, na ushirika. Kanisa la kwanza lilikutana kila wakati ili wajifunze kanuni ya mitume, kuumega mkate na kuomba pamoja (Matendo Ya Mitume 2:42). Wakati tunaomba pamoja na Wakristo wengine madhara yatakua ya muimu. Maombi ya pamoja hujenga na kuleta umoja tunaposhiriki imani moja. Roho huyo huyo Mtakatifu ambaye anakaa pamoja na kila Mkristo anazifanya nyoyo zetu kuwa na furaha tunaposikia sifa kwa Bwana wetu mwokozi, zikitushikanisha pamoja kwa ushirika ambao haupatikani mahali popote katika maisha.

Kwa wale wanaweza kuwa peke yao na kungángána na taabu za maisha, wakisikia wengine wanawainua mbele ya kiti cha neema itakuwa jambo kubwa la kutia moyo. Pia inajenga ndani yetu upendo wa kuwajali wengine wakati tunawaombea. Kwa wakati huo huo, maombi ya pamoja yatukua dhihirisho la moyo wa mtu binafsi anayeshiriki. Tunastahili kuja kwa Mungu kwa unyenyekevu (Yakobo 4:10), ukweli (Zaburi 145:18), kutii (1 Yohana 3: 21-22), na shukrani (Wafilipi 4:6), na ujaziri (Waebrania 4:6). Cha kushangaza ni kuwa, maombi ya pamoja yanaweza kuwa jukwaa kwa wale maneno yao yanaelekea kwa wasikilizaji, lakini si kwa Mungu. Yesu alionya kuhusu tabia kama hizo katika Mathayo 6:5-8 mahali ambapo anatufunza tusiwe wa kuchukuliwa na upepo kama huo au unafiki katika maombi yetu, bali tuombe kisiri katika nyumba zetu ili tuepuke majaribu ya kutumia maombi kiunafiki.

Hakuna kitu katika maandiko cha kupendekeza kuwa maombi ya pamoja “yako na nguvu” kuliko ya mtu mmoja katika hali kuwa yanautembesha mkono wa Mungu. Kwa umbali sana, Wakristo wanazawazisha maombi na “kupata vitu kutoka kwa Mungu” na maombi yanakuwa mahali pa kukalili idadi ya haja zetu. Maombi ya kibibilia, huwa na sura tofauti, yakijumlisha haja zote na kuingia katika ufahamu na uhusiano wa ndani na Mtakatifu wetu, mkamilifu na Mungu mwenye haki. Kwamba Mungu kama huyo atakunja sikio lake kwa viumbe wake ambao wanaweka sifa na ibada kwa wingi (Zaburi 27:4; 63:1-8), na kuzaa moyo wa toba na kukiri (Zaburi 51; Luka 18:9-14), waanzisha moyo wenye nia na shukrani (Wafilipi 4:6; Wakolosai 1:12), na kuunda hali ya kuwamboe wengine kwa niapa yao (2 Wathesalonike 1:11; 2:16).

Maombi kwa hivyo kushirikiana na Mungu ili alete mpango wake, sio kujaribu kumkunja aingie kwa mapenzi yetu. Tunapoacha haja zetu kwa kujitoa kwa Yeye ajuaye hali zetu sana kutuliko na Yeye “chenye unahitaji kabla uulize” (Mathayo 6:8), maombi yetu yanafikia upeo wake. Maombi yametolewa kwa unyenyekevu kwa mapenzi yake, kwa hivyo kila wakati yanajibiwa , hata kama yametolewa na mtu mmoja au watu elfu.

Dhana kuwa maomba ya pamoja yanaweza mzawishi Mungu yatokana na kufasiri vipaya Mathayo 18:19-20, “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo kakati yao.” Aya hizi zinatoka katika ufahamu mkubwa ambao wazungumzia mpangilio utakaofuatwa katika kesi ya kumwadhibu mshirika wa kanisa. Kuzifasiri kama kuahidi Wakristo cheki tupu kwa kitu chochote watakacho kubaliana kumwomba Mungu, haijalishi kama ni cha dhambi au upumbavu, sio eti hakiingiliani na masingara ya adhabu ya kanisa, bali yakataa maandiko mengine yote hasa ukuu wa Mungu.

Kwa kuongezea, kuamini kuwa wakati “wawili watatu wamekusanyika” kuomba, nguvu zingine za kiuchawi zinatumika papo hapo katika maombi yetu sio uungaji wa kibibiilia, hata kama huyo mtu ametenganishwa na wengine kwa umbali wa maili elfu moja. Maombi ya pamoja ni muimu kwa sababu yajenga umoja (Yohana 17:22-23), na ni sehemu kuu kwa Wakristo kutiana moyo wao kwa wao (1 Wathesalonike 5:11) na kuwaelekeza kwa upendo na matendo mema (Waebrania 10:24).


BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze.
Neno '' KUPENDA''limekuwa msamiati mgumu sana kwa vijana wa leo, shetani amefanikiwa kwa asilimia 90 kuwanasa vijana wengi na kuwaangusha katika dhambi, akitumia msamiati huu NAKUPENDA.
2 Timotheo 2:22 '' Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi. ''
-Kwa Wasichana Kusumbuliwa Na Vijana Wasio Na Hofu Ya MUNGU Limekuwa Ni Jambo La Kawaida. Kwao Ni Kama Vile Usivyoweza Kuwazuia Ndege Wasiruke Juu Ya Kichwa Chako. Lakini Licha Ya Hayo Mimi Naamini Kila Msichana Anaweza Kuwazuia Ndege Hao Wasijenge Viota Kwenye Nywele Zake. Dada Najua Umeshindwa Kuwazuia Ndege Kuruka Juu Ya Kichwa Chako Lakini Naamini Unaweza Kuwazuia Ndege Hao Kujenga Kiota Kwenye Kichwa Chako, Shika Utakatifu Na Utunze Wokovu Wa BWANA YESU Kama Pesa.
-Mabinti jizuieni na uasherati, jizuieni maana nyie ndio mara nyingi mnafuatwa. upendo hauko katika ngono.
1 Kor 5:10 Biblia inasema ''Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.''
-Wazinzi na wenye kutamani tunao katika mazingira yetu iwe ni nyumbani au ni kazini lakini ni jukumu lako binti kukataa kutumiwa kama chombo cha kujifurahishia wadhalimu. Kataa dhambi ya uzinzi, ogopa dhambi ya uzinzi, ikimbie dhambi ya uzinzi na usifanye dhambi ya uzinzi.
BWANA YESU Anakupenda Sana Na Hataki Ukose Uzima Wa Milele Kwa Sababu Ya Hao Ndege Wanaoruka Juu Ya Kichwa.
Ufunuo 21:8 '' Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.''
-Kumbe katika watakaopelekwa jehanamu na wazinzi wamo.
-shetani analeta kila mitindo ya mavazi na mapambo ili tu kuwanasa vijana katika dhambi ya uasherati.
-Uzinzi ni moja ya dhambi zinazowakosesha wengi.
-Nduguyangu, uzinzi wa muda mfupi unaweza kukupeleka kabisa jehanamu kama hukupata nafasi ya kutubu, na sio wote wanaopata nafasi ya kutubu na kugeuka.
-Uzinzi na uasherati ni dhambi ving'ang'anizi na ndio maana shetani huitumia sana ili kuwaangamiza maelfu ya vijana, uzinzi unamfanya shetani anapata nafasi ya kukutawala.
ndugu kupitia ujumbe huu nakuomba badilika. Na kama umeona imekuwa ngumu mweleze mchungaji wako akusaidie na kukuombea maana wengi hadi wana majini mahaba.
Mithali 6:32-33 '' Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. ''
-Mvulana Leo Akimwambia Msichana "NAKUPENDA" Maana Yake Hasa Ni " NATAMANI KITU, SIO WEWE MWENYEWE BALI KITU KUTOKA KWAKO, SIWEZI KUNGOJA, NATAKA KUWA NACHO SASA HIVI, BILA KUCHELEWA. SI KITU NINI ITAKAYOTUKIA BAADAE. NINAANGALIA WAKATI HUU, NINAYO HAJA KWAKO ILI KUZITULIZA TAMAA ZANGU, WEWE NI CHOMBO TU CHA KUNIFIKISHA KWENYE SHABAHA YANGU, NATAKA KUWA NA WEWE MUDA HUU"
Hiyo Ndio Maana Ya Neno "Nakupenda" Kwa Maisha Ya Leo Kwa Vijana Wengi. Maana Halisi Ya Kijana Kama Huyo Ni Hii "NINAJIPENDA MIMI MWENYEWE PEKE YANGU TU, KWA SHABAHA HIYO NAMTUMIA MSICHANA KUKAMILISHA KUJIPENDA KWANGU".
Wasichana Wengi Nao Hujikuta Wakiingia Kwenye Upendo Huu Feki Na Kuingia Dhambini.
Ndugu Zangu Tambueni Neno Hili Kwamba MUNGU Atawahukumu Adhabu Ya Jehanamu Wazinzi Na Waasherati, Waebrania 13:4 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu. '',
BWANA MUNGU Anawaonya Wanadamu Kila Leo Ili Waache Uovu Huu. Dhambi Hii Ndio Ilisababisha Sodoma Na Gomora Kugeuka Matanuru Ya Moto Na Kuwateketeza Wanadamu Wote Isipokuwa Lutu Na Familia Yake
1 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. ''
Upendo Wa Kweli Haukamiliki Isipokuwa Katika Ndoa Takatifu Mlioingia Bila Dhambi. Kwa Hiyo Mvulana Asitaje Lile Neno Kubwa La Kusema "NAKUPENDA" Kwa Msichana Asipokuwa Na Nia Ya Kufunga Nae Ndoa Tena Asiseme Neno Hilo Huku Akiwa Na Mpango Wa Kufunga Ndoa Miaka 10 Ijayo Bali Miezi Kadhaa Ijayo.
Yakobo 4:4 ''Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU.''Wazinzi ni adui wa MUNGU, Ukianguka kwenye dhambi ya uasherati au uzinzi kwa sababu tu ulidanganyika na neno ''nakupenda'' basi wewe unakuwa adui wa MUNGU hadi utakapotubu.
Kijana na kiume au wa kike tambua kwamba wewe ni wa thamani sana mbele za MUNGU, Tunza uthamani wako na mwili wako bila kufanya uasherati.
Maombi yangu MUNGU akupe kinga kwa kila hatari iliyo mbele yako, akupe baraka kwa kila jambo jema unaloliwaza na kulipanga kwa ajili ya maisha yako ya baadae yakiwemo maisha ya ndoa, BWANA akupe jibu katika ombi lako la kumpata mwenzi wa maisha mwenye hofu ya MUNGU, BWANA YESU akupe tabasamu kwa kila chozi unalolia ukimuomba akupe mme/mke mwema, akujalie afya njema, furaha,amani na upendo. Nguvu ya MUNGU likasimame na wewe katika magumu unayopitia hadi ushindi wako na maadui zako kuanzia walio ndani hadi walio nje kwa jina la YESU KRISTO washindwe.
BWANA YESU akuondoe kwenye maagano ya ukoo na mizimu yanayokuzuia kuoa au kuolewa. MUNGU akawafunge waliokufunga,wawe mateka waliokufanya mateka,wateseke wao waliokutesa,waliokufungia uchumi wafungwe wao.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com

MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.



Hakikisha kila siku unapata muda wa kuzungumza na Mungu.

Je! Utawezaje kuzungumza na Mungu? Fuata haya maelekezo yafuatayo;

- Tenga muda maalumu wa kusoma neno la Mungu pamoja na maombi. Hapa unatakiwa utafute sehemu ambayo ni kimya na isiyo na watu. Pia unapaswa uwe wewe pekeyako kwa maana huu ni wakati wako binafsi wa kuongea na Mungu.

- Andaa vifafa utakavyo vitumia katika kuongea kwako na Mungu. Chukua note book (daftari), kalamu, Biblia yako, na ikibidi radio ndogo au muziki kwa ajili ya kusikiliza nyimbo za taratibu za kuabudu.

Muda huu ni wako wewe na Mungu; sahau yote uliyoyaacha huko nyumbani, kazini, n.k. Tumia fursa hii kusoma neno la Mungu, kumwabudu Mungu, pamoja na kuomba.

Najua kila kitu chaweza kuwa kigumu mwanzoni, lakini unaweza ukaanza kwa kutumia dakika kumi kila siku ukiwa PEKE YAKO alafu utaona jinsi Mungu anavyozidi kukuwezesha siku baada ya siku.
Hakikisha unaheshimu ratiba yako siku zote. Endapo ukiona muda wa mchana unakubana; basi tafuta nafasi usiku ambayo itakupa faragha na Mungu. Jambo hili unaweza ukalifanya nyumbani, kazini, hata mahali po pote pale unapoona unapata nafasi ya kuwa peke yako na Mungu katika sehemu yenye utulivu.

Siku zote neno la Mungu linaweza kukupa jambo jipya usilolifahamu. Je! Wapenda kuyafurahia matunda ya kuongea binafsi na Mungu? Jibu lake ni hili:

TENDEA KAZI KILA KITU AMBACHO MUNGU AMESEMA NAWE. Katika hatua hii hapa panahitajika kitu kinachoitwa UTII. Maana ya UTII ni kutekeleza kila kitu hata kama wewe binafsi unaona nafsi yako haitaki. Kutii maana yake ni kutekeleza. Basi endapo neno la Mungu likikutaka kutubu au kubadili mwenendo wako; wewe tii kila kitu ambacho Mungu amesema nawe. Ukizingatia hayo utaona kila siku imani yako na ufahamu wako juu ya neno la Mungu unaongezeka.

ZINGATIA KWAMBA: Ukristo pasipo maombi ni BURE. Biblia Takatifu inatuambia kwamba:

"Lakini Yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba." (Luka 5:16)

Yesu alikuwa na desturi ya kujitenga na watu ili apate faragha ya kuomba. Tukisoma Biblia ya Kiingereza inasema: "So He Himself often withdrew into the wilderness and prayed." (Luke 5:16) Neno "...OFTEN..." linamaanisha kuwa tendo hilo Yesu alikuwa analifanya kila mara (yaani ilikuwa kawaida yake kufanya hiyo - kujitenga na watu kwa ajili ya kupata ufaragha wa maombi). Je! Wewe wadhani Ukristo wako pasipo maombi utaweza kumshinda Shetani?

Badilika sasa; jitahidi kila siku upate muda wako binafsi ukiwa pekeyako faragha kwa kuongea na Mungu. Japokuwa unaweza ukawa na desturi ya kulijadili neno la Mungu ukiwa na watu mbali mbali; lakini fahamu kuwa unapaswa pia kuwa na muda wako binafsi wa kuongea na Mungu kila siku ukiwa wewe peke yako na Mungu tu. Ukizingatia hayo utaona mabadiliko makubwa sana katika imani yako. Fanya sasa nawe utabarikiwa.


SEMINA YA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE(MANA MINISTRY)-IRINGA:

LENGO: Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.
HATUA  ZA KUFANYA ILI UONDOKE HAPAO ULIPO AU UMWOMBEE MTU ALIYEKUJA KUOMBA MSAADA UMSAIDIE KUTOKA HAPO.

1.PELEKA OMBI HILO KWA MUNGU.Usijaribu kumsaidia huyo mtu au kujisaidia bila kumuuliza Mungu kwasababu wewe huna jibu la matatizo  yake bali kwasababu una mahusiano mazuri na Mungu na pale anapotaka maombi yake. ZABURI 107:19-20.Wana wa Israeli walipoenda kinyume na Mungu walimlilia Musa na yeye pia akamlilia 
Mungu.

2.POKEA NENO LA MUNGU UNALOPEWA NA MUNGU KWA AJILI YA HUYO ALIYEKUOMBA UMWOMBEE AU UJIOMBEE.ZABURI 107:17-20.

Unajiuliza unafanyaje? Mungu anakuletea NENO ISAYA 55:11.Ukitaka kufanikiwa kwa mpango wa Mungu lazima upokee NENO. YEREMIA anasema Neno la Bwana likanijia likasema. Kwa hiyo ni lazima usikie Neno la Bwana sio lako.

3.OMBA MUNGU AKUPE KUSIKIA MUONGOZO WAKE KWAKO KUTOKA KWENYE NENO ULILOPEWA. RUMI 10:17.

Imani huja kwa kusikia.Lazima ujue utaratibu Mungu alionao katika kukufanikisha.Imani chanzo chake ni kusikia kwa NENO LA KRISTO.
Mungu anaweza sema na wewe kupitia mistari iliyopo kichwani mwako,kusoma Biblia,CD,kipindi cha redio au Runinga ambako huwa kuna Neno ameliweka huko ili upate sikia ujumbe wake.
Ni lazima uchimbe historia ya huyo mtu au ikiwa ni wewe ili kufuatilia hiyo hali anayolalamikia kutokufanikiwa kwake au hali inayofanya kutokufanikiwa kwako.2FALME 24:1,8-10 23:36-37.Mungu atakupa maarifa jinsi ya kujihudumia wewe au mwingine.Umejua ni adhabu ya ukoo wapi ni lango ya dhambi hiyo.Wakiendelea kukalia KITI cha DAUDI adhabu itaendelea kukufuata inabidi usikae ili utoke.Kama kuna Kiti cha ukoo,familia,taifa umekalia usipotoka hapo atakuja mwingine mwisho utarudi pale pale au utatenda yale yale.
Yehoyakimu alikaa miezi 3 akaondolewa na baada ya miaka 3 akaasi akawa chini Nebukadreza(Shetani).

4.OMBA TOBA KWA AJILI YA DHAMBI  ZA MAOMBI ALIYOLETA YULE MTU AU YAKO KWASABABU YA UOVU WA WAZAZI AU WATANGULIZI ULIVYOSABABISHA WASIFUATE MAAGIZO YA MUNGU.YEREMIA 22:21.

Sio kutubu tu bali kujua mahali dhambi ilipoingia(ujana wa wazazi wao au wako),mlango wa kutokumsikia Mungu DANIELI 6:19.KUTOKA 20:5.
Mungu hapatilizi dhambi bali uovu.Kuna tofauti kati ya DHAMBI na UOVU.DHAMBI ni uasi-kwenda kinyume na maagizo ya Mungu(unatumia vitu kinyume na alivyokuagiza).UOVU ni udhaifu.
Tunatubu kwa ajili ya dhambi zetu na uovu wa babu zetu.Unaweza kwenda jela kwasababu hakukuwapo mtu wa kutetea kisheria katika lile kosa na si kwasabau umetenda dhambi.Dhambi maana yake unatumia vitu ulivyopewa kinyume na utaratibu.Mungu hapatilizi dhambi bali udhaifu,ule udhaifu unaacha kukusaidia.Wote tumetenda dhambi na kukosa utukufu wa Mungu.Udhaifu ni hali inayokaa kwenye mwili,nafsi,roho na kujenga mazingira uzao wako uliotoka kwa babu au baba.Huzaliwi na dhambi ya kunywa pombe bali udhaifu, huwezi stahimili hali hiyo,ukisikia harufu ya pombe huwezi stahimili.Kwanini utubu dhambi? ili Mungu aingilie kati ili uasi usiendelee.Mungu aingilie kati uovu, ili udhaifu huo usiendelee kwa watoto wako.Ni lazima ufute kisheria ili utoke hapo.

5.          FUTA AU ONDOA LAANA KATIKA ARDHI KWA KUTUMIA DAMU YA YESU.
YREMIA 22:29-30.

Ardhi imeandika na kutunza kumbukumbu. WAEBRANIA 9:19-24.
Damu ya YESU inaondoa na kufuta dhambi.Damu ya Yesu inaonekana kwa ajili ya mtu unayemuombea au wewe na kutaka kumsaidia.Mbinguni kuna nakala mbili.!.Nakala za makosa yako mbinguni 2.Nakala za mashtaka ya shetani kwa Mungu.
Damu ya Yesu inakuja kufuta mashtaka yote lakini kwenye ardhi yapo.Unasema nafuta maneno yote ktk ardhi yanayofanya nisifanikiwe.Ardhi imetumika kama polisi na magereza maana kesi haiwezi kwenda mahakamani kama nakala ya kesi haipo.Ardhi imeiumbiwa ikuzie kama hati,ardhi itakapoona Damu imekuja na Jina la Yesu itafuta mashitaka yote.Nebukadreza alipata nguvu toka ardhi kuwatesa wana-Israeli.

6.LAZIMA UKEMEE ROHO AMBAYO INAYOZUIA MAFANIKIO.
Kemea mzaingira ya uasi,kemea roho ya UKIWA kwasababu unaishi kama umenyang’anywa kitu(Mume,kazi,mke,uchumi,gari,biashara n.k)Kazi ya roho ya ukiwa ni kukunyang’anya uwe mikiwa,uwe na hali ya upweke.KOLOSAI 1:13-14.
Yesu anaachilia Damu na kukumboa na anaachilia hati ya kukumboa kutoka hali hiyo.

7.MWOMBEE HUYO MTU AU JIOMBEE WOKOVU NA UTII KWA MAAGIZO KWA MUNGU ATAKAYOKUWA ANAMPA/ANAKUPA NA AGANO LAKE. YEREMIA 22:29.
Maombi hayakufanikishi bali NENO toka kwa Mungu(sio kuendeda kila mkutano ukaombewe tu bali uwe unaomba Mungu akupe Neno toka kwake la kukukusaidia).
Ukitaka mafanikio Mungu anakupa Neno ili uwe msikivu kwa kukupa mawazo ili usikwame.

8.OMBA MUNGU AKUONDOLEE HALI YA UKIWA KATIKA NYUMBA YAO AU YAKO ARUDISHE KITU KITAKACHOKUONDOLEA UKIWA.

Dunia ilipokuwa ukiwa kuna kitu Mungu alikirudisha.Akikuondoa kwenye NAFASI huacha hali ya ukiwa.Habili alipouwawa hali ya ukiwa iliingia kwenye familia ya Adamu,vizazi saba mpaka Seth alipozaliwa alirejesha hali ya faraja kwasabu kuna kitu Adamu alikuwa amekosa Seth alikirejesha(Kumcha Bwana)
Mfao kwenye familia atakapopatikana mtu mmoja awe mtoto,mjukuu au kilembwe ambaye amebeba kitu flani cha wazazi ambacho wanakipenda iwe biashara,uchaji wa Mungu,uongozi n.k faraja hurejea katika familia Yeremeia 22:5

9.ISEMESHE ARDHI NA MBINGU KWA UPYA VISIKWAMISHE MAFANIKIO YAKO AU YAKE.KUMB LA TORATI 31:28-30, 30:19-20 32:1.
Unafanya hivyo ili ardhi na mbingu zitunze kumbukumbu na maneno utakayosema ili baadaye pasiwepo na cha kukukwamisha/kumkwamisha mafanikio yako/yake.



SEHEMU YA TATU (3)

LENGO:Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.
Ikiwa mtu amekuja kwako kuomba msaada wa maombi kwasababu hafanikiwi au wewe mwenyewe hufanikiwi ktk ujenzi unaotaka kujenga au aliokwisha anza kujenga au umekwama mahali unataka kumalizia fedha zinapotea.Unamuombaje au unamuombeaje?.
HATUA ZA KUFANYA ILI UTOKE AU ATATOKE HAPO.

1.PELEKA OMBI HILO KWA MUNGU.
Kwasababu jibu huna bali kwasababu ya mahusiano uliyonayo na Mungu unaye mwamini wahitaji mpeleka kwa Mungu.

2.POKEA NENO LA MUNGU KWA AJILI YA HUYO ALIYEOMBA UMUOMBEE AU KWA AJILI YAKO.

ZABURI 107:19-20,ISAYA 55:11.
Neno la Mungu lina wazo na mikakati ndani yake inayotoa mvua mvua na kunyesha ili kumea NENO la kukusadia ktk kukufanikisha.
Nchi inaweza kuwa na WAOMBAJI wazuri ila kama hawana NENO ni ngumu sana kufanikiwa.Unaomba mvua inanyesha lakini hujaandaa MBEGU ni vigumu kustawi.Ni lazima na ni sheria ya KI-MUNGU kupokea Neno ili ustawi.

3.OMBA MUNGU AKUPE KUSIKIA MWONGOZO WAKE KWAKO KUTOKA KWENYE NENO ULILOPEWA NA MUNGU ULIPOMWOMBEA HUYO MTU AU WEWE.RUMI 10:17.

Ni lazima usikie Sauti ya NENO ambayo hutengeneza uhakika(IMANI) ili kufungua macho ya imani kuona kila linalotarajiwa.Ebr 11:3.
Imani huja kwa kusikia.UTasikiaje? Kwa jinsi linavyokuja.KUMB LA TORATI 8;7,11-12.Kuna suala la umiliki wa ardhi kiroho na kimwili,kabla ya umiliki wa kimwili lile eneo lilikuwa halali kiroho kwa wao.Si unajenga tu bali kiwango cha kujenga ambacho Mungu anataka.Unajenga kwa ubora upi?.unajenga na kukaa nadani yake ni lazima ujenge na kutumia 

4.OMBA MUNGU AKUPE KUTAMBUA MASHARTI YA KIROHO YALIYOP KWENYE ARDHI INAYOJENGWA JUU YAKE AU UNAYOKUSUDIA KUJENGA.kumb 8:7,11-12.

Katika sheria za umiliki kuna umiliki wa kiroho kwanza kabla ya umiliki wa kimwili.Sheria za umilikiwa kiroho zina nguvu kuliko za kimwili
Endelea kutufuatilia Jifunze na Uelimike kwa Muendelezo wa Mafundisho.


                     
MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
MITHALI 17:28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila tunachokiona tunataka kukisemea kitu.
Kuna wakati tunasikia na kukutana na mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu, unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa.
Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea kitu. Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu.
Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu.
MUHUBIRI 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

*Ipo nguvu katika kunyamaza*
Yapo mambo ambayo tunapaswa kuongea, kusema, lakini yapo mambo ambayo tunapaswa kunyamaza kwa ajili ya usalama wa Roho zetu.
Ni kweli kuna wakati unasemwa sana vibaya, unasingiziwa, unatukanwa nk nk, lakini ni lazima ukumbuke kwamba kuna mazingira ambayo hupaswi kujibizana hata kama umeumia kiasi gani.

*Unajua ni kwanini?*
Ukisemwa vibaya, ukitukanwa, ukidharauliwa lazima moyo utaghafilika, moyo ukighafilika lazima utakuwa na hasira na ghadhabu.
*Ukiwa na hasira katu usitegemee kuwa utajadiliana na mtu kwa hekima.*
Ukiongea utaongea katika uwepo wa hasira, ukijibu utajibu kulingana na kiwango cha hasira ulichonacho.

*Sasa jiulize majibu yanayotoka kutokana na msukumo wa hasira huwa yanakuwaje?*
Mazuri? Ya upole? Ya hekima? Ya unyenyekevu? I am sure jibu ni hapana.
Kama jibu ni hapana that means utaongea vitu vibaya ambavyo ni chukizo kwa MUNGU kwa sababu amesema maneno yetu na yakolee munyu (chumvi).

Sasa badala ya kuongea upumbavu na ukamkosea MUNGU kwanini usichague kunyamaza?
AMOSI 5:3 Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.
Nimekuwa inspired sana na mwanamke Abigaili, ni kweli mumewe alikuwa na makosa, ni kweli alikuwa mlevi, lakini mwanamke huyu alijua ni wakati gani, na mazingira gani alipaswa kuongea na mumewe na alijua aongee nini. Alipomkuta mumewe yupo katika hali ya ulevi, ALINYAMAZA, alijua kuwa huu sio wakati wa kusema jambo lolote.

1 SAMWELI 25:1
Ni vyema sisi pia tukajifunza kusoma mazingira na nyakati na hali za watu zilivyo ili tujue ni wakati gani tujibu, tuongee nini na ni wakati gani tunyamaze
Kilinde kinywa, hakikisha haukiachi kinene mabaya – ZABURI 50:19.
Usipoteze marafiki na kuharibu mahusiano kwa ajili ya kinywa kibovu – MITHALI 11:9.
Ni vyema tukajifunza kujua ni neno gani tukitamka kwa wakati/hali/mazingira gani litakubaliwa –MITHALI 10:32.

ZABURI 19:14 – Bwana na akafanye maneno yetu yakapate kibali mbele zake MUNGU na mbele za wanadamu pia.
1SAMWELI 25:36
Umeumizwa, umekwazwa, umetukanwa, umedharauliwa, KATIKA MAZINGIRA YA HASIRA NA GHADHABU JITAHIDI KUNYAMAZA.
Ni kweli moyo na akili na hisia vinakusukuma kujibu, kubisha nk nk, lakini elewa impact za kujibizana ukiwa na hasira na hizo ni bora ukae kimya.
*"AKUSHINDAE KUONGEA, MSHINDE KUNYAMAZA
"Muwe na siku njema!




Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu wote.


Karibuni tujifunze Neno la MUNGU la uzima wetu sasa na uzima wa milele.
Kuokoka ni kuhakikisha Bwana YESU KRISTO yuko ndani yako na unamtii yeye na Neno lake.
''.... Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia(Mitume), Mwamini Bwana YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.-Matendo 16:30-31''

Kuokoka ni jambo la lazima sana kwa kila anayehitaji uzima wa milele.
Kuokoka kuanza na kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi kisha unaishi ukilitii Neno la MUNGU.
Kwanini ni muhimu sana kuokoka?
Biblia inasema baada ya kifo hukumu.
Waebrania 9:27 ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;''
Anayetenda dhambi akifa na dhambi zake anaenda kuzimu.
Mteule wa KRISTO mtakatifu akifa anaenda mbinguni.

Wanadamu wengi wakionywa kwamba waache dhambi husema wanahukumiwa na hutoa sababu kwamba anayeweza kuwahukumu ni MUNGU tu.
Hukumu ni Siku ya mwisho tu ila sasa ni maonyo tu na maonyo hayo yanaletwa na Neno la MUNGU kupitia watumishi, hivyo watumishi wakati mwingine huonekana kama wanahukumu kumbe wanawasaidia watu. Hakuna mwanadamu anayetakiwa kumhukumu mwanadamu mwenzeke.
Nikisema acha uzinzi na usaliti wa ndoa maana ni dhambi sio nakuhukumu Bali nakuambia kweli ya MUNGU.
Nikisema acha dhambi na okoka sasa ni kwa lengo la kukusaidia wewe.

Ni mhimu sana kumpokea YESU na kuanza kuishi katika kusudi la MUNGU la wokovu.
Baada ya kuokoka naomba utambue kwamba wewe umekuwa mtumishi wa MUNGU wa kuwasaidia na wengine ili waje kwenye wokovu.
Biblia inasema kuhusu aliyeokoka kwamba;
''Kwa maana MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU;-Waefeso 2:8''
Biblia inasema tuliompokea YESU kama Mwokozi tumeokolewa.
Kuna watu hudai hakuna kuokoka duniani lakini Neno la MUNGU ndio kweli na kweli hiyo inasema kawmba tuliompokea YESU tumeokolewa na sio tutaokolewa bali tumeokolewa tayari.
Kama hujaokolewa basi nakusihi okolewa leo kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na kuanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana.
Baada ya kuokolewa naomba ujue mambo 7 muhimu haya yafuatayo.
Hiki ndicho kiini cha somo langu la Leo kwamba ''Tumeokoka ili?''

TUMEOKOKA ILI:


1. Tumeokoka ili tuurithi uzima wa milele.

Yohana 3:16-18 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''
Tumeokoka ili tuupate uzima wa milele, hiyo ndio ahadi kuu ya MUNGU kwetu.
Kazi yetu baada ya kuokoka ni kuishi kwa kulifuata Neno la MUNGU na Kulitii.
Uzima wa milele ni kitu muhimu cha kwanza ambacho kila mwanadamu anahitaji, lakini Uzima huo uko katika YESU KRISTO pekee, hivyo anayeuhitaji uzima wa milele atubu dhambi na kuokoka kisha aendelee kuukulia wokovu kwa mafundisho na utakatifu.


2. Tumeokoka ili tumtumikie YESU KRISTO.

Yohana 12:26 '' Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, BABA atamheshimu.''
Kazi ya waliookolewa na Bwana YESU ni kumtumikia yeye.
Kumtumikia YESU ni kumfuata yeye kwa kujitenga na dhambi zote na mambo yote mabaya ya dunia.
Ukimtumikia YESU hakika MUNGU atakuheshimu.
Na wewe ukiheshimiwa na MUNGU Muumbaji wako hakika una heri kuu.
Kama umeokoka na humtumikii KRISTO nakuomba anza leo kumtumikia; kwa kuishi maisha matakatifu, kushuhudia wengine injili, mtumikie kupitia uimbaji au kufundisha, Mtumikie kwa mali yako na mtumikie kwa kujitoa kabisa ili umpende yeye tu.


3. Tumeokoka ili tuishi maisha matakatifu.

1 Petro 1:15-16 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.''
Kazi nyingine ya wateule wa MUNGU ni kuishi maisha matakatifu.
Ni muhimu sana kujua kwamba umeokolewa na BWANA YESU ili uanze kuishi maisha matakatifu.
Ni jukumu la kila mkristo aliyeokolewa na KRISTO kuishi maisha matakatifu.
Utakatifu hautakiwi kuwa wa msimu tu bali wa kudumu.
Aliyetuokoa ni mtakatifu hivyo na sisi ili tumpendeze yeye inatupasa sana kuishi maisha matakatifu.


4. Tumeokoka ili tuwe kielelezo cha matendo mema kwa watu wote.

1 Tiomotheo 1:16 ''Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.''
Mtu aliye kielelezo cha mema ni mtu wa mfano wa kujifunzia watu walio nje.
Ni muhimu sana wateule wa MUNGU wakawa kielelezo cha mema ili dunia ijifunze kwao jinsi ya kuishi maisha matakatifu.
Kama dhambi itatawala kanisani hakika itakuwa ngumu watu wa nje kuja kanisani maana hawaioni tofauti kati yao na kanisa. Kama kanisani kuna wazinzi, wachawi, watoa rushwa , wezi na Nk. Ni ngumu kuwapata watendao dhambi hizo ili waje kanisani.
Mfano ndugu wa kanisani amezini na mtu wa nje, je itawezekana vipi huyo wa nje kuja kanisani? maana anajua kabisa huwa anatembea na mtu wa kanisani.
Ni muhimu sana kanisa zima likawa kielelezo cha matendo mema ili watu wote wajifunze.
Sio Mchungaji tu ndio awe kielelezo lakini mama mchungaji na wazee wa kanisa ni wadhambi, haifai kuwa hivyo.
Sio wazee tu ndio kielelezo lakini vijana ni wadhambi, haifai kuwa hivyo.
Kanisa lote linatakiwa liwe kielelezo cha matendo mema.
Tumeokolewa ili tuwe kielelezo cha mema kwa watu wote.

5. Tumeokoka ili tuwalete wengine kwa YESU.

Mathayo 10:7-8 ''Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. ''
Tumeokoka ili tuwalete wengine kwa YESU.
Ndugu naomba ujue kwamba umeokolewa na Bwana YESU ili uwalete familia yako yote kwa YESU.
Umeokolewa na YESU ili uwalete wafanyakazi wenzako wote kwa YESU.
Umeokolewa ili uwasaidie wanafunzi wenzako kiroho.
Umeokolewa ili uwasaidie wafanyabiashara wenzako kiroho.
Mama umeokolewa ili uwasaidie wamama wenzako jinsi ya kumcha MUNGU aliye hai.
Baba umeokolewa ili uwafundishe wababa wenzako jinsi ya kumcha MUNGU wa mbinguni.
Tumeokolewa ili tuwalete watu wote kwa YESU.
MUNGU ametupa pia mamlaka katika kuhubiri kwetu ili yeye MUNGU aponye na kuwafungua watu kupitia sisi.
Ni muhimu sana kujua wajibu wako ndugu uliyeokolewa na BWANA YESU.


6. Tumeokoka ili tuwe na ushirika na ROHO MTAKATIFU.

2 Kor 13:14 '' Neema ya Bwana YESU KRISTO, na pendo la MUNGU, na ushirika wa ROHO MTAKATIFU ukae nanyi nyote.''
Tumeokolewa ili tuwe na ushirika na ROHO wa MUNGU.
Kuwa na ROHO wa MUNGU ndani yako na kumtii itakusaidia kutimiza kusudi la MUNGU kwako na itakusaidia kudumu katika Mwokozi wako YESU KRISTO.
ROHO MTAKATIFU ndiye msimamizi wa kanisa la KRISTO duniani hivyo ili tumpendeze MUNGU tunatakiwa sana tuwe na ROHO MTAKATIFU.
ROHO MTAKATIFU ndio mwalimu wa kweli ambaye tukilihudhuria darasa lake hakika hakuna cha kidunia au cha kipepo kitakachoturudisha nyuma.
Ili tushinde dhambi na mambo yote ya dunia inatupasa sana tuwe na ROHO MTAKATIFU.
Ni heri sana kuwa na ushirika wa ROHO wa MUNGU.


7. Tumeokoka ili tuufundishe ulimwengu jinsi ya kumwabudu MUNGU aliye hai.

Zaburi 29:2 ''Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.''
MUNGU wa kweli ni mmoja tu na huyo amejifunua pekee katika Neno lake Biblia.
MUNGU aliye hai huabudiwa katika kanisa la KRISTO YESU duniani.
Wateule wa MUNGU humwabudu MUNGU aliye hai na inawapasa sana kumwabudu katika Roho na kweli.
Kama dunia inamtaka MUNGU Muumbaji basi inawapasa sana kwenda kumwabudu katika kanisa la KRISTO duniani.
Waliookoka ni kanisa hai la KRISTO Duniani.
Tumeokolewa na BWANA YESU ili tuwafundishe wanadamu wote jinsi ya kumwabudu YAHWEH MUNGU wetu aliyetuumba.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.



Mwandishi wa Somo Hili.

Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili