Swali: "Je! Maombi ya pamoja ni Muhimu? Maombi ya pamoja
ni yana nguvu kuliko ya mtu mmoja?"
Jibu: Maombi ya pamoja ni sehemu muhimu katika maisha ya
kanisa, pamoja na ibada, na kanuni nzuri, kuumega mkate, na ushirika. Kanisa
la kwanza lilikutana kila wakati ili wajifunze kanuni ya mitume, kuumega mkate
na kuomba pamoja (Matendo Ya Mitume 2:42). Wakati tunaomba pamoja na Wakristo
wengine madhara yatakua ya muimu. Maombi ya pamoja hujenga na kuleta umoja
tunaposhiriki imani moja. Roho huyo huyo Mtakatifu ambaye anakaa pamoja na kila
Mkristo anazifanya nyoyo zetu kuwa na furaha tunaposikia sifa kwa Bwana wetu
mwokozi, zikitushikanisha pamoja kwa ushirika ambao haupatikani mahali popote
katika maisha.
Kwa wale wanaweza kuwa peke yao na kungángána na taabu za
maisha, wakisikia wengine wanawainua mbele ya kiti cha neema itakuwa jambo
kubwa la kutia moyo. Pia inajenga ndani yetu upendo wa kuwajali wengine wakati
tunawaombea. Kwa wakati huo huo, maombi ya pamoja yatukua dhihirisho la moyo wa
mtu binafsi anayeshiriki. Tunastahili kuja kwa Mungu kwa unyenyekevu (Yakobo
4:10), ukweli (Zaburi 145:18), kutii (1 Yohana 3: 21-22), na shukrani (Wafilipi
4:6), na ujaziri (Waebrania 4:6). Cha kushangaza ni kuwa, maombi ya pamoja
yanaweza kuwa jukwaa kwa wale maneno yao yanaelekea kwa wasikilizaji, lakini si
kwa Mungu. Yesu alionya kuhusu tabia kama hizo katika Mathayo 6:5-8 mahali
ambapo anatufunza tusiwe wa kuchukuliwa na upepo kama huo au unafiki katika
maombi yetu, bali tuombe kisiri katika nyumba zetu ili tuepuke majaribu ya
kutumia maombi kiunafiki.
Hakuna kitu katika maandiko cha kupendekeza kuwa maombi ya
pamoja “yako na nguvu” kuliko ya mtu mmoja katika hali kuwa yanautembesha mkono
wa Mungu. Kwa umbali sana, Wakristo wanazawazisha maombi na “kupata vitu kutoka
kwa Mungu” na maombi yanakuwa mahali pa kukalili idadi ya haja zetu. Maombi ya
kibibilia, huwa na sura tofauti, yakijumlisha haja zote na kuingia katika
ufahamu na uhusiano wa ndani na Mtakatifu wetu, mkamilifu na Mungu mwenye haki.
Kwamba Mungu kama huyo atakunja sikio lake kwa viumbe wake ambao wanaweka sifa
na ibada kwa wingi (Zaburi 27:4; 63:1-8), na kuzaa moyo wa toba na kukiri
(Zaburi 51; Luka 18:9-14), waanzisha moyo wenye nia na shukrani (Wafilipi 4:6;
Wakolosai 1:12), na kuunda hali ya kuwamboe wengine kwa niapa yao (2 Wathesalonike
1:11; 2:16).
Maombi kwa hivyo kushirikiana na Mungu ili alete mpango wake,
sio kujaribu kumkunja aingie kwa mapenzi yetu. Tunapoacha haja zetu kwa kujitoa
kwa Yeye ajuaye hali zetu sana kutuliko na Yeye “chenye unahitaji kabla uulize”
(Mathayo 6:8), maombi yetu yanafikia upeo wake. Maombi yametolewa kwa
unyenyekevu kwa mapenzi yake, kwa hivyo kila wakati yanajibiwa , hata kama
yametolewa na mtu mmoja au watu elfu.
Dhana kuwa maomba ya pamoja yanaweza mzawishi Mungu yatokana
na kufasiri vipaya Mathayo 18:19-20, “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu
watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba
yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina
langu, nami nipo papo hapo kakati yao.” Aya hizi zinatoka katika ufahamu mkubwa
ambao wazungumzia mpangilio utakaofuatwa katika kesi ya kumwadhibu mshirika wa
kanisa. Kuzifasiri kama kuahidi Wakristo cheki tupu kwa kitu chochote watakacho
kubaliana kumwomba Mungu, haijalishi kama ni cha dhambi au upumbavu, sio eti
hakiingiliani na masingara ya adhabu ya kanisa, bali yakataa maandiko mengine
yote hasa ukuu wa Mungu.
Kwa kuongezea, kuamini kuwa wakati “wawili watatu
wamekusanyika” kuomba, nguvu zingine za kiuchawi zinatumika papo hapo katika
maombi yetu sio uungaji wa kibibiilia, hata kama huyo mtu ametenganishwa na
wengine kwa umbali wa maili elfu moja. Maombi ya pamoja ni muimu kwa sababu
yajenga umoja (Yohana 17:22-23), na ni sehemu kuu kwa Wakristo kutiana moyo wao
kwa wao (1 Wathesalonike 5:11) na kuwaelekeza kwa upendo na matendo mema
(Waebrania 10:24).
Post A Comment:
0 comments so far,add yours