Articles by "QUESTION AND ANSWERS"
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo QUESTION AND ANSWERS. Onyesha machapisho yote
Swali: "Je! Maombi ya pamoja ni Muhimu? Maombi ya pamoja ni yana nguvu kuliko ya mtu mmoja?"

Jibu: Maombi ya pamoja ni sehemu muhimu katika maisha ya kanisa, pamoja na ibada, na kanuni nzuri, kuumega mkate, na ushirika. Kanisa la kwanza lilikutana kila wakati ili wajifunze kanuni ya mitume, kuumega mkate na kuomba pamoja (Matendo Ya Mitume 2:42). Wakati tunaomba pamoja na Wakristo wengine madhara yatakua ya muimu. Maombi ya pamoja hujenga na kuleta umoja tunaposhiriki imani moja. Roho huyo huyo Mtakatifu ambaye anakaa pamoja na kila Mkristo anazifanya nyoyo zetu kuwa na furaha tunaposikia sifa kwa Bwana wetu mwokozi, zikitushikanisha pamoja kwa ushirika ambao haupatikani mahali popote katika maisha.

Kwa wale wanaweza kuwa peke yao na kungángána na taabu za maisha, wakisikia wengine wanawainua mbele ya kiti cha neema itakuwa jambo kubwa la kutia moyo. Pia inajenga ndani yetu upendo wa kuwajali wengine wakati tunawaombea. Kwa wakati huo huo, maombi ya pamoja yatukua dhihirisho la moyo wa mtu binafsi anayeshiriki. Tunastahili kuja kwa Mungu kwa unyenyekevu (Yakobo 4:10), ukweli (Zaburi 145:18), kutii (1 Yohana 3: 21-22), na shukrani (Wafilipi 4:6), na ujaziri (Waebrania 4:6). Cha kushangaza ni kuwa, maombi ya pamoja yanaweza kuwa jukwaa kwa wale maneno yao yanaelekea kwa wasikilizaji, lakini si kwa Mungu. Yesu alionya kuhusu tabia kama hizo katika Mathayo 6:5-8 mahali ambapo anatufunza tusiwe wa kuchukuliwa na upepo kama huo au unafiki katika maombi yetu, bali tuombe kisiri katika nyumba zetu ili tuepuke majaribu ya kutumia maombi kiunafiki.

Hakuna kitu katika maandiko cha kupendekeza kuwa maombi ya pamoja “yako na nguvu” kuliko ya mtu mmoja katika hali kuwa yanautembesha mkono wa Mungu. Kwa umbali sana, Wakristo wanazawazisha maombi na “kupata vitu kutoka kwa Mungu” na maombi yanakuwa mahali pa kukalili idadi ya haja zetu. Maombi ya kibibilia, huwa na sura tofauti, yakijumlisha haja zote na kuingia katika ufahamu na uhusiano wa ndani na Mtakatifu wetu, mkamilifu na Mungu mwenye haki. Kwamba Mungu kama huyo atakunja sikio lake kwa viumbe wake ambao wanaweka sifa na ibada kwa wingi (Zaburi 27:4; 63:1-8), na kuzaa moyo wa toba na kukiri (Zaburi 51; Luka 18:9-14), waanzisha moyo wenye nia na shukrani (Wafilipi 4:6; Wakolosai 1:12), na kuunda hali ya kuwamboe wengine kwa niapa yao (2 Wathesalonike 1:11; 2:16).

Maombi kwa hivyo kushirikiana na Mungu ili alete mpango wake, sio kujaribu kumkunja aingie kwa mapenzi yetu. Tunapoacha haja zetu kwa kujitoa kwa Yeye ajuaye hali zetu sana kutuliko na Yeye “chenye unahitaji kabla uulize” (Mathayo 6:8), maombi yetu yanafikia upeo wake. Maombi yametolewa kwa unyenyekevu kwa mapenzi yake, kwa hivyo kila wakati yanajibiwa , hata kama yametolewa na mtu mmoja au watu elfu.

Dhana kuwa maomba ya pamoja yanaweza mzawishi Mungu yatokana na kufasiri vipaya Mathayo 18:19-20, “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo kakati yao.” Aya hizi zinatoka katika ufahamu mkubwa ambao wazungumzia mpangilio utakaofuatwa katika kesi ya kumwadhibu mshirika wa kanisa. Kuzifasiri kama kuahidi Wakristo cheki tupu kwa kitu chochote watakacho kubaliana kumwomba Mungu, haijalishi kama ni cha dhambi au upumbavu, sio eti hakiingiliani na masingara ya adhabu ya kanisa, bali yakataa maandiko mengine yote hasa ukuu wa Mungu.

Kwa kuongezea, kuamini kuwa wakati “wawili watatu wamekusanyika” kuomba, nguvu zingine za kiuchawi zinatumika papo hapo katika maombi yetu sio uungaji wa kibibiilia, hata kama huyo mtu ametenganishwa na wengine kwa umbali wa maili elfu moja. Maombi ya pamoja ni muimu kwa sababu yajenga umoja (Yohana 17:22-23), na ni sehemu kuu kwa Wakristo kutiana moyo wao kwa wao (1 Wathesalonike 5:11) na kuwaelekeza kwa upendo na matendo mema (Waebrania 10:24).


Swali: "Ina maana gani Yesu kuwa Mwana wa Mungu?"

Jibu: Yesu si Mwana wa Mungu kulingana na ubaba wa kawaida wa binadamu. Mungu hakuoa na kupata mwana wa kiume. Mungu hakufanya tendo la ndoa na Mariamu, na pamoja naye kuzaa mtoto wa kiume. Yesu ni Mungu katika hali kwamba ni Mungu anajithirihisha kama mwili. (Yohana 1:1, 14) Yesu ni mwana wa Mungu kwa dhana kwamba Mariamu alipata mimba kupitia Roho Mtakatifu. Luka 1:35 yasema, “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.”

Wakati wa kujaribiwa kwake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kuhani mkuu alimtaka Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu” (Mathayo 26:63). “Yesu akamwambia wewe umesema,’ Yesu akamwambia, wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Mathayo 26:64) viongozi wa Kiyahudi walimdhania kwa kukufuru (Mathayo 26:65-66). Baadaye mbele ya Pilato, “Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu” Yohana 19:7) ni kwa nini makisio yake kuwa Mwana wa Mungu yachukuliwe kuwa kufuru na astahili hukumu ya kifo? Wayahudi wilielewa vizuri sana chenye Yesu alimaanisha kwa maneno haya “Mwana wa Mungu” kuwa Mwana wa Mungu ni kuwa hali moja na Mungu. Mwana wa Mungu “wa Mungu” kusema uko katika hali sawa na Mungu-hakika kuwa Mungu- kulikuwa sawa na kukufuru kwa viongozi wa Kiyahudi; kwa hivyo walimtaka Yesu auwawe, kulingana na Mambo ya Nyakati 24:15. Waebrania 1:3 inadhihirisha haya wazi, “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”

Mfano mwingine unaweza patikana katika Yohana 17:12 mahali Yuda anaelezwa kama mwana wa “upotevu”? jina upotevu lamaanisha “uharibivu” Yuda hakuwa mwana wa uharibivu, lakini mambo hayo ndio ya kutambulisha maisha ya Yuda. Yuda anadhihirisha upotevu. Vile vile Yesu mwana wa Mungu. Ni Mungu anajidhihirisha (Yohana 1:1,14).



Swali: "Je, Yesu ni Mungu? Je, Yesu alitoa madai ya kuwa yeye ni Mungu?"

Jibu: Yesu hakunakiliwa mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe YESU kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?

Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!

Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”

Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.






jibu: Bibilia inaonyesha njia ya wazi ya uzimani.Mwanzo ni sharti tutambue yakwamba tumetenda dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu,ambayo yanafanya tustahili adhabu.Kwa kuwa dhambi zetu ziko kinyume kabisa na Mungu aliye uzima wa milele,basi ni adhabu ya milele pekee itoshayo. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).

Hata hivyo Yesu Kristo asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:23), mwana wa Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8). Yesu Kristo alikufa msalabani (Yohana 19:31-42), kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili (2Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1Wakorintho 15:1-4), kudhihirisha ushindi juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu” (1Petro 1:3).

Kwa imani ni sharti tuungame dhambi zetu na tumrejee Kristo kwa ajili ya wokovu (Matendo 3:19). Tukiweka imani yetu kwake, kwa kuamini kifo chake msalabani kama malipo ya dhambi zetu,tutasamehewa na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa sababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Imani pekee katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli ya pekee ya uzimani! “Kwa maana nimeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).

Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako,tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumuelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu,najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Nina ziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu /ya ajabu na kwa msamaha - karama ya uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa?


Swali: "Je, kuna Mungu? Je, kuna ushahidi wa kuthibitisha kuweko kwa Mungu?"


Jibu: Je, kuna Mungu? Ninaona ni jambo la kusisimua ya kwamba umakini mwingi umepawa mjadala huu. Katika takwimu zetu hivi sasa zasema ya kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watu duniani wanaamimi kuweko kwa Mungu au Mamlaka ya kiwango cha juu. Jukumu linabaki kwa wenye kuamini kuthibitisha ukweli wa kuweko kwake. Mimi nafikiri ingewapasa wale hawaamini watuthibitishie.


Kuweko kwa Mungu hakuwezi kutothibitishwa wala kuthibitishwa. Bibilia inasema inatupasa kukubali kwa imani kuwa Mungu yuko, “Na pasipo imani haiwezekani mtu kumpendeza Mungu, kwa kuwa kila ajaye kwake sharti aamini kuwa yuko na ya kuwa huwapa vitu wale wamtafutao kwa bidii” (Waebrania 11:6). Kama Mungu alingetaka iwe, angejitokeza tu mbele ya ulimwengu wote kuwajulisha wote kuwa yeye yuko. Lakini, angefanya hivyo hakungekuwa na haja ya imani. “Tena Yesu kamwambia, ‘kwa kuwa umeniona, umeamini; heri wale ambao hawakuniona na wameamini” (Yohana 20:29).

Hiyo haimaanishi ya kuwa hakuna idhibati ya kuweko kwa Mungu. Biblia inasema, “Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga zatangaza kazi za mikono yake. Siku baada ya siku zamimina hotuba zake; usiku baada ya usiku zaonyesha ufahamu. Hakuna hotuba au lugha ambayo haisikiki. Sauti zao hutapakaa duniani kote, maneno yao mpaka mwisho wa dunia” (Zaburi 19:1-4). Ukitazama nyota, ukijaribu kufahamu kina cha anga, na kutazama maajabu ya kiasili, huku ukiona urembo wa kutua kwa jua - haya yote yanaashiria kuweko kwa Mungu muumbaji. Kuna ushahidi wakuweko kwa Mungu ndani ya mioyo yetu. Mhubiri 3:11 inatuambia, “….ameweka pia umilele ndani ya mioyo ya wanadamu…” Kuna kitu ndani yetu kinachotujulisha ya kuwa kuna kitu zaidi baada ya maisha haya tunayoishi na mwingine zaidi yetu nje ya dunia hii. Hata tukipuuza bado kuna uwepo wa Mungu maishani mwetu. Biblia inatuonya ya kuwa kuna wengine watakuwapo watakaokataa kuwepo kwa Mungu, “Mjinga amesema moyoni mwake hakuna Mungu” (Zaburi 14:1). Kwa kuwa zaidi ya asilimia 98 ya watu wa tamaduni mbali mbali katika vizazi vilivyopita ndani ya mabara yote duniani ni waumini wa kuwepo kwa Mungu wa aina Fulani – lazima kuwe kuna mtu ama kitu Fulani kinachohisi na kusababisha imani hii.

Kuongezea, kuna maoni mbali mbali ambayo hutumika kuthibitishia pia. Maoni ya kwanza yasema kwa kuwa Mungu ni kile ambacho zaidi yake hakuna. Basi uwezekano wa kuwepo kwake ni mwingi. Na kama Mungu hayuko basi hakungekuwa na ambacho zaidi yake hakuna. Maoni ya pili ni kwamba kwa kuwa ulimwengu unaonyesha kazi nzuri ya ustadi iliyofanyika basi lazima kuweko na aliyeifanya. Kila kitu kina fanya kazi vyema kwa wakati wake na kwa kipimo mwafaka. Kama hewa yetu ingeharibika tu kidogo viumbe vyote vingekufa.

Maoni ya tatu ni kwamba kwa chochote kufanyika lazima kuweko na mwenye au chenye kusababisha. Kwa vile ulimwengu upo lazima kuwe na aliyeusababisha uweko na huyo ndiye Mungu. Maoni ya nne ni kwamba katika kila utamaduni, mila na desturi za watu duniani kuna aina Fulani ya mfumo wa sheria ya kuelekeza; yenye kutambua mema na mabaya. Kuua, uongo, wizi na uchafu wa kitabia ni mambo yanayokataliwa ulimwenguni kote. Hali hii ya kutambua meme na mabaya ilitoka wapi Kama si kwa Mungu Mtakatifu?

Biblia inatuambia, watu watakataa ukweli wa kuweko kwa Mungu na kuamini roho za uongo. Warumi 1:25 inasema, “walibadilisha ukweli wa Mungu na kutumikia uongo hata kuiabudu na kuitumikia miungu waliyoiumba kwa mikono yao kinyume na Mungu aliyewaumba –ambaye daima husifiwa. Amina.” Biblia pia inasema, watu hawana sababu ya kutomwamini Mungu, “Kwa kuwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu siri za uwepo wake – Nguvu zake za milele na utisho wake umethibitika na kufahamika kutokana na yale aliyoyatenda kwa hivyo wanadamu hawana kisingizio” (Warumi 1:20).

Watu husema hawamwamini mungu kwa sababu si kisayansi ama hakuna kithibitisho cha kuweko kwake. Sababu halisi ni kwamba kwa kukubali yuko,mtu anahitajika kuwajibika mbele zake na kuomba msamaha (Warumi 3:23; 6:23). Kama Mungu yuko basi tunawajibika kwa matendo yetu. Kama hayuko, basi tunaweza kufanya mapenzi yetu wenyewe bila kujali hukumu. Huenda ikawa hii ndiyo sababu ya watu wengine kushikilia mawazo ya kuwa dunia ilifanyika tu kwa njia ya vitu tofauti tofauti kubadilika umbo polepole kupitia mabadiliko ya kimazingira ili waepukane na ukweli wa kuna Mungu muumbaji wa yote. Mungu yuko na kila mmoja anajua hivyo. Mwenye kubishana ni mbishani tu lakini huwa hata yeye anajua yuko.

Je, nitajuaje kuwa Mungu yuko? Najua Mungu yuko kwa kuwa nazungumza naye kila siku. Simsikii masikioni akinijibu lakini ninahisi uwepo wake, nahisi kuongoza kwake, najua upendo wake ninatamani neema yake.Mambo yaliyotendeka maishani mwangu hayana maelezo mengine ila Mungu. Mungu ameniokoa kimiujiza na kuyabadilisha maisha yangu mpaka sasa nimebaki tu kumtukuza. Maelezo haya yote hayawezi kumfanya mtu anayetaka kukataa kuwepo kwa Mungu akubali. Muhimu ni kumkubali kwa imani (Waebrania 11:6). Imani kwa Mungu si bure kama kubahatisha gizani bali ni sawa na kutembea salama ndani ya chumba chenye nuru ambamo asilimia 90 ya watu waliomo wamesimama.


Swali: "Ninawezaje kuwa mwana wa Mungu?"

Jibu: “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12).

“Lazima uzaliwe mara ya pili”
Wakati alitembelewa na kiongozi wa dini, Nikodemo, Yesu hakumwakikishia mbunguni papo hapo. Badala, Kristo alisema, “Amini, amini, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana3:3).

wakati mtu anapozaliwa mara ya kwanza, anarithi ile hali ya dhambi ambayo yatokana na kutotii kwa Adamu katika bustani mwa Edeni. Motto haitaji kufunzwa na mtu yeyote kutenda dhambi. Kimaumbile anaifuata ile tamaa ya dhambi, nayo inamwelekeza kudanganya, kuiba, na kuchukia. Badala ya kuwa mwana wa Mungu, ni mototo wa kutotii na wa ghadhabu.

“Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika tama za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili nay a nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine” (Waefeso 2:1-3).

Kama watoto wa ghadhabu, tunastahili kutenganishwa na Mungu jahannam. Shukrani kubwa kwa Mungu kwa sababu ya ujumbe ufuatao ambao wasema, “Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yatu;alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema” (Waefeso 2:4-5).

Je! Tumefanywa hai pamoja na Kristo/kuzaliwa mara ya pili/kufanyika wana wa Mungu namna gani? Lazima tumpokee Yesu!

Mpokee Yesu
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12).

Ufahamu huu wazi waeleza jinzi ya kufanyika mwana wa Mungu. Lazima tumpokee Yesu kwa kumwamini. Tunastahili kuamini nini juu ya Yesu?

Kwanza, lazima tutambue kwamba Yesu ni mwana wa Mungu milele ambaye alikuwa mwanadamu. Alizaliwa kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu na bikra Mariamu, Yesu hakurithi hali ya dhambi kutoka kwa Adamu. Kwa hivyo, anaitwa Adamu wa pili (1Wakorintho 15:22). Huku kwa kutotiii kwa Adamu kulileta laana ya dhambi ulimwengu, maishia makamilifu ya Yesu yanaweza kufunika yale ya dhambi. Itikio letu lazima liwe la kutubu (igeuke dhambi), kwamini maisha Yake makamilifu yatutakaze.

Pili, lazima tuwe na imani kwa Yesu kama mwokozi. Mpango wa Mungu ulikuwa kusulubisha mwanawe mkamilifu msalabani kulipa adhabu tuliyohistahili kwa ajili ya dhambi zetu: kifo. Kifo cha Yesu kinawaweka huru wale wote wanaompokea kutoka kwa nguvu ya dhambi.

Mwisho, latumfuate Yeso kama Bwana. Baada ya kumfufua Yesu kama mshindi wa dhambi na mauti, Mungu alimpa mamlaka yote (Waefeso 1:20-23). Yesu anawaongoza wale wote wanaompokea; na atawahukumu wale wote wanaomkataa (Matendo Ya Mitume 10:42).

Kwa nehema ya Mungu ambayo inatusaidia kutubu na kuwa na imani katika Mwokozi na Bwana, tumezaliwa maisha mapya kama wana wa Mungu. Ni kwa wale pekee watakao mpokea Yesu- sio kujua tu kuhusu Yeye pekee bali kumtegemea kwa wokovu, kunyenyekea kwake kama mkuu wetu, na kumpenda kama dhamani yetu kuu- itakufanya kuwa mwana wa Mungu.

Fanyika mwana wa Mungu
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13)

Kama vile hatukuchangia kitu chochote kwa kuzaliwa kwetu kwa mwili wa kawaida, vile vile hatuwezi kuwa katika jamii ya Mungu kwa nguvu zetu au kwa matendo yetu mazuri au kufanyia imani yetu mazingaombwe. Vile aya hapo juu zinasema, Mungu ndiye “aliwapa uwezo” kulingana na mapenzi yake ya nehema. “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu” (1Yohana 3:1). Kwa hivyo mwana wa Mungu hana kitu cha kujivunia, bali kuvunia kuwa ndani ya Yesu (Waefeso 2:8-9).

Mto hukua ili awe kama wazazi wake. Vile vile, Mungu anataka watoto wake zaidi na zaidi kama Yesu Kristo. Ingawa ni mbinguni pekee tutakuwa wakamilifu, mwana wa Mungu hawezi kuwa na mazoea, ya kuendelea kutenda dhambi bila kutubu. “Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, walaa yeye asiyempenda ndugu yake” (1 Yohana 3:7-10). 

Usifanye makosa; mtoto wa Mungu hawezi “kanwa” kwa kutenda dhambi. Lakini kwa Yule anayeendelea kutenda dhambi (kwa mfano, anaendelea kufurahia dhambi bila kusikia maagizo ya kumfuata Kristo na Neno lake) yaonyesha kwamba hakuwai zaliwa mara ya pili. Yesu alisema kuhusu watu kama hao, “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tama za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda” (Yohana 8:44). Watoto wa Mungu, kwa upande mwingine, hawatamani tama za dhambi bali watamani kujua, upendo na utukufu wa Baba yao.

Taji ya kuwa mtoto wa Mungu haipimiki. Kama mtoto wa Mungu, sisi tuko sehemu ya jamii yake (kanisa), tumeaidiwa makao mbinguni, na kupewa uwezo wa kumsongea Mungu katika maombi kama Baba (Waefeso 2:19; 1Petero 1:3-6; Warumi 8:15).

Itikia mwito wa Mungu wa kutubu dhambi na kumwamini Kristo. Kuwa mwana wa Mungu leo!

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.




Swali: "Biblia inasema nini juu ya kushirikiana katika ngono kabla kuoana?"

Jibu: 
Pamoja na matendo mengine ya uchafu, kufanya kitendo cha mapenzi kabla kuoana kumekatazwa katika maandiko (matendo 15:20; warumi 1:29; wakorintho wa kwanza 5:1; 6:13, 7:2; 10;8; wakorintho wa pili 12:21; wagalatia 5:19; waefeso 5:3; wakolosai 3:5; wathesalonike 4:3; yuda7). Biblia inasisitiza kuepuka kitendo hicho kabla ya ndoa.hii ina maana ya kuwa ni dhambi kama ya uzinifu kwa kuwa hujaunganishwa na unayefanya naye kitendo hicho. Mapenzi baina ya mume na mke waliooana ndiyo mapenzi yanayokubalika mbele za Mungu (waebrania 13:4).

Kushirikiana katika ngono kabla ndoa kumeenea sana kwa sababu nyingi. Mapenzi yanastarehesha. Mungu aliyaumba hivyo. Anawataka wanaume na wanawake wafurahie kitendo cha ngono (ndani ya ndoa). Hata hivyo, lengo la msingi la ngono si starehe bali kuzaana tukaongezeke. Hivyo tunazuiwa kufanya kitendo cha ngono kabla ndoa ili tusijipatie watoto tusiowatarajia. Kama jambo hili lingezingatiwa, magonjwa ya zinaa na wamama wasioolewa na kuavya mimba na kadhalika kungepungua. Kujizuia kunaokoa maisha, kunalinda watoto wachanga na kuleta ladha halisi ya ngono pamoja na heshima kwa Mungu.



Swali: "Nimeweka imani yangu kwa Yesu … sasa ni fanyeje?"


Jibu: Hongera! Umefanya uamuzi wa kubadilisha maisha! Huenda ikawa unauliza, “sasa ni fanye nini?Nianze vipi safari yangu na Mungu?” Hatua tano zilizo orodheshwa hapo chini zitakupatia muongozo kutoka kwa Bibilia. Iwapo una maswali safarini mwako,tafadhali tembelea http://jifunzenauelimike.blogspot.com/
.



1. Hakikisha unaelewa maana ya wokovu.



1 Yohana 5:13 anatuambia,” Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna uzima wa milele. Mungu anataka tuelewe maana ya wokovu.Mungu anataka tuwe na ujasiri wa kufahamu kwa kweli kwamba tumeokoka. Kwa ufupi tu,wacha tuviendee vipengele muhimu vya wokovu:



(a) Sote tumefanya dhambi.Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu (Warumi 3:23).



(b) Kwasababu ya dhambi zetu,tunastahili kuadhibiwa kwa kutengwa milele na Mungu (Warumi 6:23).



(c) Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu (Warumi 5:8; 2 Wakorintho 5:21).Yesu alitufia pahali petu,kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili. Kufufuka kwake kulidhihirisha yakuwa kifo chake Yesu kilitosha kutulipia dhambi zetu.



(d) Mungu hutoa msamaha na wokovu kwa wote wale wamuaminio Yesu – kwa kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zetu (Yohana 3:16; Warumi 5:1; Warumi 8:1).



Hizo ndizo habari za wokovu! Ikiwa umeweka imani yako kwa Yesu kama mwokozi wako, umeokoka! Dhambi zako zote zimesamehewa na Mungu ana ahidi kutokuacha wala kutokutenga (Warumi 8:38;Mathayo 28:20).Kumbuka,wokovu wako uko salama ndani ya Yesu Kristo (Yohana 10:28-29). Ukiwa unamuamini Yesu pekee kama mwokozi wako, unaweza kuwa na uhakika yakuwa utaishi milele na Mungu mbinguni!



2. Tafuta Kanisa Zuri linalo fundisha Bibilia.



Usilifikirie Kanisa kama jengo.Kanisa ni watu. Ni muhimu sana kwa wamuaminio Yesu kristo kushirikiana mmoja na mwengine. Hiyo ndiyo sababu ya kwanza muhimu ya Kanisa. Sasa kwa kuwa umeweka imani yako kwa Yesu Kristo, tunakuhimiza vilivyo kutafuta Kanisa linalo amini mafundisho ya Bibilia katika eneo lako na uzungumze na Mchungaji. Mfahamishe upya wa imani yako katika Yesu Kristo.



Sababu ya pili ya Kanisa, ni kufundisha Bibilia.Unaweza kujifundisha jinsi yakuyatumia maagizo ya Mungu katika maisha yako. Kulielewa Bibilia ni ufunguo wa kuishi katika ushindi na nguvu/ uthabiti katika maisha ya kikristo. 2Timotheo 3:16-17 yasema “kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao,na kwa kuwaongoza,na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”



Sababu ya tatu ya Kanisa ni kuabudu.Kuabudu ni kumshukuru Mungu kwa yote aliyo fanya!Mungu ametuokoa. Mungu anatupenda.Mungu anatutimizia mahitaji yetu. Mungu anatuongoza na kutuelekeza. Je ni kwanini tusingemshukuru? Mungu ni mtakatifu, mwenye haki,upendo,huruma na amejaa neema.Ufunuo wa Yohana 4:11 asema, “umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”



3. Jitengee mda kila siku wa kutafakari juu za Mungu.



Ni muhimu sana kwetu kuwa na mda wa kutafakari juu za Mungu kila siku. Wengine huuita” wakati wa kutafakari, wengine huuita wakati wa “kujitoa” kwasababu ni wakati tunapo jitolea kwa Mungu. Wngine hupendelea wakati wa asubuhi na wengine jioni. Haijalishi unauitaje wakati huu ama ni lini hujitoa. Kinacho stahili ni kwamba uwe na wakati na Mungu mara kwa mara. Ni matendo gani yanadhihirisha wakati wetu na Mungu?



(a) Maombi. Maombi ni hali ya kuzungumza na Mungu. Kuongea na Mungu kuhusu hali zako na shida zako.Muulize Mungu akupe hekima na muongozo. Muulize Mungu akutane na mahitaji yako. Mwambie Mungu ni kwa jinsi gani unampenda na ni kwa kiwango gani unamshukuru kwa yale yote anayo kutendeaHiyo ndiyo maana halisi ya maombi.



(b) Kusoma Bibilia.Zaidi ya kufundishwa Bibilia kanisani,katika shule ya Jumapili, na au kwa mafundisho ya Bibilia - unahitaji kujisomea Bibilia mwenyewe. Bibilia iko na kila kitu unacho hitaji kujua ili kukuwezesha kuishi maisha ya kikristo yenye ushindi. Ina muongozo wa kiungu katika hali yakufanya maamuzi ya hekima, katika hali ya kujua mapenzi ya Mungu, katika hali ya kuwahudumia wengine, na katika hali ya kukua kiroho. Bibilia ni neno la Mungu kwetu sisi. Bibilia ni muongozo muhimu wa Mungu katika hali ya kuishi maisha yanayo mpendeza ye (Mungu) na kututosheleza sisi.



4. Jenga uhusiano na watu watakao kusaidia kiroho



1Wakorintho 15:33 yasema, “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” Bibilia iko na tahadhari kuhusu ushawishi “mbaya” watu wanaweza kuwa nao juu yetu. Kutumia wakati na wale ambao wanajihusisha katika vitendo hivyo. Tabia za wale ambao tuko nao zitatuambukiza. Hii ndiyo sababu yakuwa ni muhimu tutangamane na watu wanao mpenda Bwana na wana wajibika kwake.



Jaribu kutafuta rafiki mmoja au wawili, labda kwa kanisa yako, ambao wanaweza kukusaidia na kukutia changamoto (Waebrania 3:13;10:24). Waulize rafiki zako wakuajibishe kuhusu wakati wako wa kutafakari, matendo yako na mwenendo wako na Mungu. Uliza kama unaweza kuwafanyia hivyo pia. Hii haimaanishi yakuwa uwachane na marafiki zako wote ambao hawajamjua Yesu Kristo kama mwokozi wao. Endelea kuwa rafiki yao na uwapende. Kwa ufupi wafahamishe yakuwa Yesu amebadilisha maisha yako na huwezi kuyafanya tena yote, yale uliyo kuwa ukiyafanya. Muulize Mungu akupe nafasi ya kumshiriki Yesu pamoja na marafiki zako.



5. Batizwa (Ubatizwe)



Watu wengi wanakosa kufahamu maana ya ubatizo. Neno “ Kubatiza” inamaanisha kuzamisha au kutosa majini. Ubatizo ndiyo njia ya kibibilia ya kujitambulisha hadharani imani yako mpya ndani ya Kristo na jukumu lako la kumfuata yeye. Kitendo cha kuzamishwa ndani ya maji inamaanisha kuzikwa pamoja na Kristo. Kitendo cha kutoka ndani ya yale maji inadhihirisha kufufuka kwa Kristo. Kubatizwa ni kujitambulisha wewe mwenyewe na kifo cha Yesu,maziko na ufufuo (Warumi 6:3-4).



Ubatizo sio ukuokoao.Ubatizo haukuondolei dhambi zako. Ubatizo ni hatua tu ya utiifu, hali ya kujitambulisha hadharani kuhusu imani yako ndani ya Kristo pekee kwa wokovu. Ubatizo ni muhimu kwasababu ni hatua ya utiifu-hadharani ukijitambulisha imani yako ndani ya Kristo na jukumu lako kwake yeye. Kama uko tayari kubatizwa,zungumza na Mchungaji.





Swali: "Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?"


Jibu: Matendo 13:38 yasema, “Basi naijulikane kwenu, ndugu zangu ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi.”

Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji?

Neno “Samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo nakulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, ku achilia, kufutilia mbali deni. Tunapo kosea mtu, huuliza msamaha wao ili tukarudishe uhusiano. Msamaha haupeanwi kwa sababu mtu anastahili kusamehewa. Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.

Bibilia inatuambia yakwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 asema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8 asema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46; Yohana 3:36).

Msamaha-Je, ni upate vipi?

Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye ari ya kutusamehe dhambi zetu! 2Petro 3:9 asema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo alitoa kwa ajili ya msamaha wetu.

Adhabu ya haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..” Mauti ya milele ndiyo ndiyo tuliyopokea kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba kwa kuchukua adhabu tuliyo stahili-mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. “Yesu alikufa msalabani, akichukua adhabu tuliyo stahili!Kama Mungu, kifo chake Yesu kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 asema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, uko na hisia za kuudhi za kila mara zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu ku epukika?Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia deni ili tukapate kusamehewa. Unacho stahili ni kumuuliza Mungu akusamehe kupitia kwake Yesu, ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina habari hii ya ajab, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”

Msamaha-Je, ni jambo lililo rahisi?

Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu bila kupitia kwa YESU KRISTO. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weak imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu/ya ajabu na kwa msamaha! Amina.”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa?


Q:

I'm not into hard-core pornography, but I don't see anything wrong with enjoying some of the sexy magazines you can get on almost any newsstand. My wife doesn't know I do this, so don't use my name.

A:

If you’re really convinced there isn’t anything wrong with this, then why don’t you want your wife to find out? The reason is obvious: You know she’d be offended and deeply hurt if she knew about it.
After all, when you were married you made a solemn vow—not just to each other or the people at your wedding, but to God. In that vow you promised to be faithful to each other and to love each other exclusively, as long as you both are alive. Why break that vow by allowing lust to overtake you—even if it’s only for an airbrushed image in a tawdry magazine? The Bible could not be clearer: “Among you there must not be even a hint of sexual immorality, or of any kind of impurity” (Ephesians 5:3).
I urge you to be honest about this, and to turn from it—decisively and forcefully. Don’t dabble with it; don’t go near places where you’ll be tempted to obtain it; avoid anything on the internet that even hints of it. Paul’s advice to his young friend Timothy applies to you as well: “Flee from all this, and pursue righteousness, godliness, faith, love, endurance and gentleness” (1 Timothy 6:11).
The most important thing you need to do, however, is to turn to Jesus Christ, confessing your sins to Him and asking Him to come into your heart and life. You need His forgiveness, and you also need His strength to resist temptation. Then—with God’s help—recommit yourself to your marriage and put into practice the vows you once made.

At the Billy Graham Evangelistic Association we receive many letters from people who have been trapped by pornography over the internet. The internet can be used for great good—but it also can be used for great evil, and the widespread availability of pornography over the internet may be its greatest evil.
The first step is to realize that this is sin in God’s eyes. It isn’t just a bad habit, nor is it only something that appeals to your lusts or your craving for excitement. It is sin—and you must not excuse it or deny it or say that it doesn’t really matter. It is sin—and the Bible warns that “after desire has conceived, it gives birth to sin; and sin, when it is full-grown, gives birth to death” (James 1:15).
This is why I urge you to turn to Jesus Christ and open your heart and life to Him. He doesn’t love your sin—but He does love you, and He wants to come into your life and take away your sins and begin to change you from within. Commit your life to Him, and then ask Him to fill you and replace everything that is evil or wrong with His goodness and purity.
Then it is critical that you take practical steps to fight this habit. Get a program for your computer that will filter out unwanted sites—and use it. Move your computer into a place where others can see what you are doing. Block or remove those television channels from your subscription. In addition, share your problem with a trusted friend, spouse, or pastor who can pray with you and hold you accountable for what you watch.
Only Jesus Christ can transform your life—God’s Word says that in Him we are a new creation (2 Corinthians 5:17). If you would like to receive Jesus Christ as your Savior by faith, you can do that right now by genuinely praying a prayer like this: 
“O God, I am a sinner. I’m sorry for my sin; please forgive me. I want to turn away from my sin. I believe Jesus Christ is Your Son. I believe He died on the cross for my sin, was buried, and You raised Him to life on the third day. I want Him to come into my heart and to take control of my life. I choose to trust Him as my Savior and follow Him as my Lord from this day forward. In Jesus’ Name I pray. Amen.”