Swali: "Nimeweka imani yangu kwa Yesu … sasa ni
fanyeje?"
Jibu: Hongera! Umefanya
uamuzi wa kubadilisha maisha! Huenda ikawa unauliza, “sasa ni fanye nini?Nianze
vipi safari yangu na Mungu?” Hatua tano zilizo orodheshwa hapo chini
zitakupatia muongozo kutoka kwa Bibilia. Iwapo una maswali safarini
mwako,tafadhali tembelea http://jifunzenauelimike.blogspot.com/
.
1. Hakikisha unaelewa maana ya
wokovu.
1 Yohana 5:13 anatuambia,” Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna
uzima wa milele. Mungu anataka tuelewe maana ya wokovu.Mungu anataka tuwe na
ujasiri wa kufahamu kwa kweli kwamba tumeokoka. Kwa ufupi tu,wacha tuviendee
vipengele muhimu vya wokovu:
(a) Sote tumefanya dhambi.Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu
(Warumi 3:23).
(b) Kwasababu ya dhambi zetu,tunastahili kuadhibiwa kwa kutengwa milele na
Mungu (Warumi 6:23).
(c) Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu (Warumi 5:8; 2 Wakorintho
5:21).Yesu alitufia pahali petu,kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili.
Kufufuka kwake kulidhihirisha yakuwa kifo chake Yesu kilitosha kutulipia dhambi
zetu.
(d) Mungu hutoa msamaha na wokovu kwa wote wale wamuaminio Yesu – kwa kuamini
kifo chake kama malipo ya dhambi zetu (Yohana 3:16; Warumi 5:1; Warumi 8:1).
Hizo ndizo habari za wokovu! Ikiwa umeweka imani yako kwa Yesu kama mwokozi
wako, umeokoka! Dhambi zako zote zimesamehewa na Mungu ana ahidi kutokuacha
wala kutokutenga (Warumi 8:38;Mathayo 28:20).Kumbuka,wokovu wako uko salama
ndani ya Yesu Kristo (Yohana 10:28-29). Ukiwa unamuamini Yesu pekee kama
mwokozi wako, unaweza kuwa na uhakika yakuwa utaishi milele na Mungu mbinguni!
2. Tafuta Kanisa Zuri linalo
fundisha Bibilia.
Usilifikirie Kanisa kama jengo.Kanisa ni watu. Ni muhimu sana kwa wamuaminio
Yesu kristo kushirikiana mmoja na mwengine. Hiyo ndiyo sababu ya kwanza muhimu
ya Kanisa. Sasa kwa kuwa umeweka imani yako kwa Yesu Kristo, tunakuhimiza
vilivyo kutafuta Kanisa linalo amini mafundisho ya Bibilia katika eneo lako na
uzungumze na Mchungaji. Mfahamishe upya wa imani yako katika Yesu Kristo.
Sababu ya pili ya Kanisa, ni kufundisha Bibilia.Unaweza kujifundisha jinsi
yakuyatumia maagizo ya Mungu katika maisha yako. Kulielewa Bibilia ni ufunguo
wa kuishi katika ushindi na nguvu/ uthabiti katika maisha ya kikristo.
2Timotheo 3:16-17 yasema “kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa
mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao,na kwa kuwaongoza,na kwa
kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate
kutenda kila tendo jema.”
Sababu ya tatu ya Kanisa ni kuabudu.Kuabudu ni kumshukuru Mungu kwa yote aliyo
fanya!Mungu ametuokoa. Mungu anatupenda.Mungu anatutimizia mahitaji yetu. Mungu
anatuongoza na kutuelekeza. Je ni kwanini tusingemshukuru? Mungu ni mtakatifu,
mwenye haki,upendo,huruma na amejaa neema.Ufunuo wa Yohana 4:11 asema,
“umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na
uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya mapenzi yako
vilikuwako, navyo vikaumbwa.”
3. Jitengee mda kila siku wa
kutafakari juu za Mungu.
Ni muhimu sana kwetu kuwa na mda wa kutafakari juu za Mungu kila siku. Wengine
huuita” wakati wa kutafakari, wengine huuita wakati wa “kujitoa” kwasababu ni
wakati tunapo jitolea kwa Mungu. Wngine hupendelea wakati wa asubuhi na wengine
jioni. Haijalishi unauitaje wakati huu ama ni lini hujitoa. Kinacho stahili ni
kwamba uwe na wakati na Mungu mara kwa mara. Ni matendo gani yanadhihirisha
wakati wetu na Mungu?
(a) Maombi. Maombi ni hali ya kuzungumza na Mungu. Kuongea na Mungu kuhusu hali
zako na shida zako.Muulize Mungu akupe hekima na muongozo. Muulize Mungu
akutane na mahitaji yako. Mwambie Mungu ni kwa jinsi gani unampenda na ni kwa
kiwango gani unamshukuru kwa yale yote anayo kutendeaHiyo ndiyo maana halisi ya
maombi.
(b) Kusoma Bibilia.Zaidi ya kufundishwa Bibilia kanisani,katika shule ya
Jumapili, na au kwa mafundisho ya Bibilia - unahitaji kujisomea Bibilia
mwenyewe. Bibilia iko na kila kitu unacho hitaji kujua ili kukuwezesha kuishi
maisha ya kikristo yenye ushindi. Ina muongozo wa kiungu katika hali yakufanya
maamuzi ya hekima, katika hali ya kujua mapenzi ya Mungu, katika hali ya
kuwahudumia wengine, na katika hali ya kukua kiroho. Bibilia ni neno la Mungu
kwetu sisi. Bibilia ni muongozo muhimu wa Mungu katika hali ya kuishi maisha
yanayo mpendeza ye (Mungu) na kututosheleza sisi.
4. Jenga uhusiano na watu
watakao kusaidia kiroho
1Wakorintho 15:33 yasema, “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia
njema.” Bibilia iko na tahadhari kuhusu ushawishi “mbaya” watu wanaweza kuwa
nao juu yetu. Kutumia wakati na wale ambao wanajihusisha katika vitendo hivyo.
Tabia za wale ambao tuko nao zitatuambukiza. Hii ndiyo sababu yakuwa ni muhimu
tutangamane na watu wanao mpenda Bwana na wana wajibika kwake.
Jaribu kutafuta rafiki mmoja au wawili, labda kwa kanisa yako, ambao wanaweza
kukusaidia na kukutia changamoto (Waebrania 3:13;10:24). Waulize rafiki zako
wakuajibishe kuhusu wakati wako wa kutafakari, matendo yako na mwenendo wako na
Mungu. Uliza kama unaweza kuwafanyia hivyo pia. Hii haimaanishi yakuwa uwachane
na marafiki zako wote ambao hawajamjua Yesu Kristo kama mwokozi wao. Endelea
kuwa rafiki yao na uwapende. Kwa ufupi wafahamishe yakuwa Yesu amebadilisha
maisha yako na huwezi kuyafanya tena yote, yale uliyo kuwa ukiyafanya. Muulize
Mungu akupe nafasi ya kumshiriki Yesu pamoja na marafiki zako.
5. Batizwa (Ubatizwe)
Watu wengi wanakosa kufahamu maana ya ubatizo. Neno “ Kubatiza” inamaanisha
kuzamisha au kutosa majini. Ubatizo ndiyo njia ya kibibilia ya kujitambulisha
hadharani imani yako mpya ndani ya Kristo na jukumu lako la kumfuata yeye.
Kitendo cha kuzamishwa ndani ya maji inamaanisha kuzikwa pamoja na Kristo.
Kitendo cha kutoka ndani ya yale maji inadhihirisha kufufuka kwa Kristo.
Kubatizwa ni kujitambulisha wewe mwenyewe na kifo cha Yesu,maziko na ufufuo
(Warumi 6:3-4).
Ubatizo sio ukuokoao.Ubatizo haukuondolei dhambi zako. Ubatizo ni hatua tu ya
utiifu, hali ya kujitambulisha hadharani kuhusu imani yako ndani ya Kristo
pekee kwa wokovu. Ubatizo ni muhimu kwasababu ni hatua ya utiifu-hadharani ukijitambulisha
imani yako ndani ya Kristo na jukumu lako kwake yeye. Kama uko tayari
kubatizwa,zungumza na Mchungaji.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours