Articles by "WOKOVU"
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo WOKOVU. Onyesha machapisho yote

“Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi
bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika
mwili, ninaishi kwa imani ya Mungu, aliyenipenda na kujitoa
kwa ajili yangu.” (Wagalatia 2:20).
Katika mstari huu, Paulo anasema kwamba alisulubiwa na sasa anaishi. Paulo anamaanisha kwamba alikufa na Yesu Kristo na sasa anaishi kwa utukufu wake, yaani Yesu anaishi ndani yake.
Katika mstari huu tunaona maana ya kuokoka. Wakati mtu anaokoka, jambo fulani kubwa hufanyika kwake. Ule utu wake wa kale hufa na badala yake kiumbe kipya hufanyika. “Mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya” (2 Wakorintho 5:17).
Hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema. Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu” (Waefeso 2:5-6).
Wakati Yesu Kristo alipokufa aliwachukua watu wake pamoja naye kaburini. Walikufa pamoja naye: “mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena” (Warumi 6:6). Wakati tunaokoka tunaunganishwa na Kristo. Utu wa kale hufa.
Katika mstari huu, Paulo anaendelea kueleza hali ya mtu ambaye amezaliwa mara ya pili, yaani mtu ambaye ni kiumbe kipya. Paulo anasema kuhusu mtu ambaye ameokoka, “Kristo anaishi ndani yake.” Huu ni ukweli kwa kila mtu ambaye ameokoka, kwamba Kristo anaishi ndani yake. Mtu ambaye ameokoka huwa anaishi chini ya mwongozo na utawala wa Yesu Kristo na anaishi maisha yake kwa nguvu za Yesu Kristo. “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13); “Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu” (Wakolosai 1:29).
Hii ndiyo sababu mtu ambaye amezaliwa upya husema “Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo” (Warumi 15:18).
Hivi ndivyo mstari wa Wagalatia 2:20 unamaanisha. Kristo anaishi ndani yetu, Kristo anatuongoza na Kristo anatupatia nguvu. Hii ndiyo sababu alikufa ili watu wake waishi kwa imani ndani yake: “Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu
Kwa hivyo kile Paulo anasema hapa ni kwamba mtu akiokoka, Kristo huja na kukaa ndani yake na kuanzia wakati huo mtu huyo anaishi maisha ya imani ndani ya Kristo. Kristo anaishi ndani ya watu wake na huwapa mwongozo, uwezo na nguvu. Mtu ambaye ameokoka hupokea haya yote kwa imani.




THE STORY OF JESUS:  2 Chronicles 29-32
“He will not turn his face from you if you return to him.” (2 Chronicles 30:9)
I have met some people who were convinced God could not forgive them.
Satan loves to reinforce this lie, and many Christians believe it.
But what do we see in these stories of the kings of Israel.?
What do we see throughout the whole bible, as far as God’s mercy goes?
Yes, there are stories of consequences and punishments.
But again and again we see a God Who wants to forgive, wants to restore.
All of these stories are summarized in Jesus: God in the flesh dying for us.
God will not turn away anyone that turns to Him humility and repentance.
Jesus fellowshipped with sinners, but the ‘religious’ missed out on it.
They refused to come to Him for mercy, because they didn’t think they needed it.
If you think you are too sinful to be forgiven, then you are the perfect candidate.
Join the club of unworthy, immoral, so-called unforgiveable sinners.
As Jesus hangs on the cross and sees me, with all my sins and failures…
He says, “Father, forgive them, for they do not know what they are doing.” (Luke 23:34)

What do you sense the Lord saying to you?
PRAYER
Lord, thank You for reminding me that You will not turn Your face from me when I come before You!
Mpendwa, unapomtumikia Mungu hatakuacha, “Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika; tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu” Isaya 65:13-14. ni vema basi kumtumika Mungu bila kuchoka.

Ee Mungu Baba nipe Neema za kukutumikia daima. Amina






Kutoka 23: 25-29

1. Atabariki Chakula Chako
2. Atabariki Maji yako
3. Atakuondolea ugonjwa katikati yako
4. Hapatakuwa na Mwenye Kuharibu Mimba
5. Ataondoa Utasa
6. Hesabu za siku zako ataitimiza
7. Atatuma Utiisho wake mbele yako
8. Atawafadhaisha maadui wote wakufikirio
9. Adui zako watakuonyesha maungo yao yaani watadhalilika.
10. Atapeleka mavu mbele yako; watakao mfukuza Mhivi, na Mkaanani na Mhiti wote watoke mbele yako(Mhivi,Mkaanani na mhiti ni tawala za shetani)
Kutoka 23:25-29 ''Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.''

Je unamtumikia MUNGU kwa nini?
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuhubiri.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuishi maisha matakatifu.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa matoleo yao kwenye kazi ya MUNGU.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuombea watumishi na Kanisa n.k
Je wewe unamtumikia MUNGU kwa nini?
Mwisho tambua kwamba Ukimtumikia YESU KRISTO hakika MUNGU atakuheshimu.
Yohana 12: 26 ''Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba (MUNGU) atamheshimu. ''
MUNGU akubariki sana, kama hujampa YESU Maisha yako basi fanya hivyo leo maana saa ya wokovu ni sasa na Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu pia zingatia kwamba hakuna uzima wa Milele kwingine kokote nje ya BWANA YESU {Yohana 14:6}


MUNGU AKUBARIKI SANA.


Faida ya Kuokoka
Swali: "Je, inamaanisha nini kumkubali Yesu kama mwokozi wako?"

Jibu: 
Je, umeshawahi kumkubali Yesu kama mwokozi wako? kabla hujajibu, niruhusu nikueleze swali hili. Ili kwakuweza kulielewa swali hili vizuri, ni sharti mwanzo umwelewe vizuri “Yesu Kristo,’’ “Kibinafsi” na “Mwokozi.’’

Yesu Kristo ni nani? Watu wengi humtambua Yesu Kristo kama mtu mzuri, Mwalimu Mkuu, au hata pia Nabii wa Mungu. Haya maelezo huenda yakawa ni kweli kabisa kuhusu Yesu, lakini hayaelezei vizuri yeye ni nani. Bibilia inatuambia yakwamba Yesu ni Mungu katika mwili, Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Tazama Yohana 1:1, 14). Mungu alikuja ulimwenguni kutufundisha, kutuponya, kuturekebisha, kutusamehe-na kufa kwa ajili yetu! Yesu Kristo ni Mungu, Muumbaji, Mungu Mkuu. Je umemkubali huyu Yesu?

Je, Mkombozi ni nini na kwanini tunahitaji Mkombozi? Bibilia inatwambia yakwamba sote tumefanya dhambi, sote tumetenda maovu (Warumi 3:10-18). Kwa wajibu wa dhambi zetu, basi twastahili hasira za Mungu na pia hukumu. Adhabu ya pekee kwa kufanya dhambi kinyume chake asiye kuwa na mwisho na Mungu wa milele ni adhabu isiyokuwa na mwisho au mipaka (Warumi 6:23; Ufunuo wa Yohana 20:11-15). Hii ndio sababu tunahitaji Mkombozi!

Yesu Kristo, alikuja duniani na akatufia pahali petu. Kifo chake Yesu, kama Mungu katika mwili, ilikuwa ni malipo yasiyokuwa na mwisho kwa ajili ya dhambi zetu (2 Wakorintho 5:21). Yesu alikufa ili kutulipia mshahara wa dhambi zetu (Warumi 5:8). Yesu alitulipia deni ili tukaweze kuwa na uhuru. Kufufuka kwake Yesu katika wafu kulidhihirisha yakwamba kifo chake kilitosha kulipa mshahara wa dhambi zetu. Hii ndiyo sababu yakuwa Yesu Kristo ndiye Mkombozi tu wa pekee (Yohana14:6; Matendo 4:12)! Je, unamwamini Yesu kama mwokozi wako?

Je, Yesu ni Mwokozi wako “Wa Kibinafsi’’? Watu wengi huchukulia yakwamba ukristo ni kuhudhuria kanisa, Kutoa makafara, kutofanya dhambi Fulani. Hiyo siyo Ukristo. Ukristo wa kweli ni ule uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Kumkubali Yesu kibinafsi kama mwokozi wako inamaanisha kuweka imani yako kibinafsi kwake na kumwamini yeye. Hakuna aokokaye kupitia imani ya wengine. Hakuna asamehewaye kwa kutenda matendo aina Fulani. Njia ya pekee ya wokovu ni kumkubali Yesu kibinafsi kama mwokozi wa maisha yako, kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zako, na kufufuka kwake kama hakikisho kwako la uzima wa milele (Yohana3:16). Je, Yesu kibinafsi ni Mwokozi wako?

Kama ungetaka kumkubali Yesu Kristo kibinafsi kama Mwokozi wako, Hebu yaseme maneno haya kwa Mungu. Kumbuka kwa kuomba ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kuwezako kukuokoa toka dhambini. Ombi hili ni kwa kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyostahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ninamkubali Yesu kibinafsi kama Mwokozi wangu! Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha-karama ya uzima wa milele! Amina!’’

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.







jibu: Bibilia inaonyesha njia ya wazi ya uzimani.Mwanzo ni sharti tutambue yakwamba tumetenda dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu,ambayo yanafanya tustahili adhabu.Kwa kuwa dhambi zetu ziko kinyume kabisa na Mungu aliye uzima wa milele,basi ni adhabu ya milele pekee itoshayo. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).

Hata hivyo Yesu Kristo asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:23), mwana wa Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8). Yesu Kristo alikufa msalabani (Yohana 19:31-42), kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili (2Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1Wakorintho 15:1-4), kudhihirisha ushindi juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu” (1Petro 1:3).

Kwa imani ni sharti tuungame dhambi zetu na tumrejee Kristo kwa ajili ya wokovu (Matendo 3:19). Tukiweka imani yetu kwake, kwa kuamini kifo chake msalabani kama malipo ya dhambi zetu,tutasamehewa na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa sababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Imani pekee katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli ya pekee ya uzimani! “Kwa maana nimeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).

Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako,tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumuelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu,najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Nina ziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu /ya ajabu na kwa msamaha - karama ya uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa?


Swali: "Nimeweka imani yangu kwa Yesu … sasa ni fanyeje?"


Jibu: Hongera! Umefanya uamuzi wa kubadilisha maisha! Huenda ikawa unauliza, “sasa ni fanye nini?Nianze vipi safari yangu na Mungu?” Hatua tano zilizo orodheshwa hapo chini zitakupatia muongozo kutoka kwa Bibilia. Iwapo una maswali safarini mwako,tafadhali tembelea http://jifunzenauelimike.blogspot.com/
.



1. Hakikisha unaelewa maana ya wokovu.



1 Yohana 5:13 anatuambia,” Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna uzima wa milele. Mungu anataka tuelewe maana ya wokovu.Mungu anataka tuwe na ujasiri wa kufahamu kwa kweli kwamba tumeokoka. Kwa ufupi tu,wacha tuviendee vipengele muhimu vya wokovu:



(a) Sote tumefanya dhambi.Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu (Warumi 3:23).



(b) Kwasababu ya dhambi zetu,tunastahili kuadhibiwa kwa kutengwa milele na Mungu (Warumi 6:23).



(c) Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu (Warumi 5:8; 2 Wakorintho 5:21).Yesu alitufia pahali petu,kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili. Kufufuka kwake kulidhihirisha yakuwa kifo chake Yesu kilitosha kutulipia dhambi zetu.



(d) Mungu hutoa msamaha na wokovu kwa wote wale wamuaminio Yesu – kwa kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zetu (Yohana 3:16; Warumi 5:1; Warumi 8:1).



Hizo ndizo habari za wokovu! Ikiwa umeweka imani yako kwa Yesu kama mwokozi wako, umeokoka! Dhambi zako zote zimesamehewa na Mungu ana ahidi kutokuacha wala kutokutenga (Warumi 8:38;Mathayo 28:20).Kumbuka,wokovu wako uko salama ndani ya Yesu Kristo (Yohana 10:28-29). Ukiwa unamuamini Yesu pekee kama mwokozi wako, unaweza kuwa na uhakika yakuwa utaishi milele na Mungu mbinguni!



2. Tafuta Kanisa Zuri linalo fundisha Bibilia.



Usilifikirie Kanisa kama jengo.Kanisa ni watu. Ni muhimu sana kwa wamuaminio Yesu kristo kushirikiana mmoja na mwengine. Hiyo ndiyo sababu ya kwanza muhimu ya Kanisa. Sasa kwa kuwa umeweka imani yako kwa Yesu Kristo, tunakuhimiza vilivyo kutafuta Kanisa linalo amini mafundisho ya Bibilia katika eneo lako na uzungumze na Mchungaji. Mfahamishe upya wa imani yako katika Yesu Kristo.



Sababu ya pili ya Kanisa, ni kufundisha Bibilia.Unaweza kujifundisha jinsi yakuyatumia maagizo ya Mungu katika maisha yako. Kulielewa Bibilia ni ufunguo wa kuishi katika ushindi na nguvu/ uthabiti katika maisha ya kikristo. 2Timotheo 3:16-17 yasema “kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao,na kwa kuwaongoza,na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”



Sababu ya tatu ya Kanisa ni kuabudu.Kuabudu ni kumshukuru Mungu kwa yote aliyo fanya!Mungu ametuokoa. Mungu anatupenda.Mungu anatutimizia mahitaji yetu. Mungu anatuongoza na kutuelekeza. Je ni kwanini tusingemshukuru? Mungu ni mtakatifu, mwenye haki,upendo,huruma na amejaa neema.Ufunuo wa Yohana 4:11 asema, “umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”



3. Jitengee mda kila siku wa kutafakari juu za Mungu.



Ni muhimu sana kwetu kuwa na mda wa kutafakari juu za Mungu kila siku. Wengine huuita” wakati wa kutafakari, wengine huuita wakati wa “kujitoa” kwasababu ni wakati tunapo jitolea kwa Mungu. Wngine hupendelea wakati wa asubuhi na wengine jioni. Haijalishi unauitaje wakati huu ama ni lini hujitoa. Kinacho stahili ni kwamba uwe na wakati na Mungu mara kwa mara. Ni matendo gani yanadhihirisha wakati wetu na Mungu?



(a) Maombi. Maombi ni hali ya kuzungumza na Mungu. Kuongea na Mungu kuhusu hali zako na shida zako.Muulize Mungu akupe hekima na muongozo. Muulize Mungu akutane na mahitaji yako. Mwambie Mungu ni kwa jinsi gani unampenda na ni kwa kiwango gani unamshukuru kwa yale yote anayo kutendeaHiyo ndiyo maana halisi ya maombi.



(b) Kusoma Bibilia.Zaidi ya kufundishwa Bibilia kanisani,katika shule ya Jumapili, na au kwa mafundisho ya Bibilia - unahitaji kujisomea Bibilia mwenyewe. Bibilia iko na kila kitu unacho hitaji kujua ili kukuwezesha kuishi maisha ya kikristo yenye ushindi. Ina muongozo wa kiungu katika hali yakufanya maamuzi ya hekima, katika hali ya kujua mapenzi ya Mungu, katika hali ya kuwahudumia wengine, na katika hali ya kukua kiroho. Bibilia ni neno la Mungu kwetu sisi. Bibilia ni muongozo muhimu wa Mungu katika hali ya kuishi maisha yanayo mpendeza ye (Mungu) na kututosheleza sisi.



4. Jenga uhusiano na watu watakao kusaidia kiroho



1Wakorintho 15:33 yasema, “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” Bibilia iko na tahadhari kuhusu ushawishi “mbaya” watu wanaweza kuwa nao juu yetu. Kutumia wakati na wale ambao wanajihusisha katika vitendo hivyo. Tabia za wale ambao tuko nao zitatuambukiza. Hii ndiyo sababu yakuwa ni muhimu tutangamane na watu wanao mpenda Bwana na wana wajibika kwake.



Jaribu kutafuta rafiki mmoja au wawili, labda kwa kanisa yako, ambao wanaweza kukusaidia na kukutia changamoto (Waebrania 3:13;10:24). Waulize rafiki zako wakuajibishe kuhusu wakati wako wa kutafakari, matendo yako na mwenendo wako na Mungu. Uliza kama unaweza kuwafanyia hivyo pia. Hii haimaanishi yakuwa uwachane na marafiki zako wote ambao hawajamjua Yesu Kristo kama mwokozi wao. Endelea kuwa rafiki yao na uwapende. Kwa ufupi wafahamishe yakuwa Yesu amebadilisha maisha yako na huwezi kuyafanya tena yote, yale uliyo kuwa ukiyafanya. Muulize Mungu akupe nafasi ya kumshiriki Yesu pamoja na marafiki zako.



5. Batizwa (Ubatizwe)



Watu wengi wanakosa kufahamu maana ya ubatizo. Neno “ Kubatiza” inamaanisha kuzamisha au kutosa majini. Ubatizo ndiyo njia ya kibibilia ya kujitambulisha hadharani imani yako mpya ndani ya Kristo na jukumu lako la kumfuata yeye. Kitendo cha kuzamishwa ndani ya maji inamaanisha kuzikwa pamoja na Kristo. Kitendo cha kutoka ndani ya yale maji inadhihirisha kufufuka kwa Kristo. Kubatizwa ni kujitambulisha wewe mwenyewe na kifo cha Yesu,maziko na ufufuo (Warumi 6:3-4).



Ubatizo sio ukuokoao.Ubatizo haukuondolei dhambi zako. Ubatizo ni hatua tu ya utiifu, hali ya kujitambulisha hadharani kuhusu imani yako ndani ya Kristo pekee kwa wokovu. Ubatizo ni muhimu kwasababu ni hatua ya utiifu-hadharani ukijitambulisha imani yako ndani ya Kristo na jukumu lako kwake yeye. Kama uko tayari kubatizwa,zungumza na Mchungaji.





Tangu unapoomba sala ile ya kumpokea BWANA YESU awe Bwana na mwokozi wa maisha yako (sala ya toba), kuna mambo mengi yanatokea maishani mwako, ila huwezi ukayaona kwa macho, yote yanafanyika katika ulimwengu wa roho ambayo macho ya kawaida hayawezi kuona. Kwanza historia yako yote ya nyuma inafutwa na unaanza maisha mapya pamoja na Mungu, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya ” (2korintho 5:17).
Imeandikwa wazi kabisa katika kitabu cha Waefeso 2:19 ya kuwa; “Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu”.
Unapata neema hii ya Mungu, na sasa unakuwa raia wa Mbinguni – biblia inakuambia tangu sasa wewe si mgeni wala mpitaji katika Ufalme wa Mungu – bali wewe ni mwenyeji pamoja na watakatifu wengi waliomo katika nyumba ya Mungu!
Nia ya Roho Mtakatifu kukupa nafasi ya kusoma ukurasa huu, ni kukufahamisha angalau kwa kiasi fulani juu ya umuhimu wa kutubu dhambi zako, na kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako.
Ukisoma ukurasa huu utakusaidia kujua kitu gani kinatokea unapo mpokea Bwana Yesu na mambo muhimu ya kufanya katika maisha hayo mapya ya Ufalme wa Mungu.
Matokeo ya Kumpokea Bwana Yesu
  •      Unasamehewa dhambi zako zote!
“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu…. Aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani …” (Wakolosai 2:13,14).
“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” (1Yohana 1:9).
  •      Unahamishwa toka katika ufalme wa shetani na kuingizwa katika Ufalme wa Mungu.
“Naye alituokoa katika nguvu za giza, na akatuhamisha na kutuingiza katika    Ufalme wa mwana wa pendo lake;” Wakolosai 1:13.
Kuna falme mbili zinazopingana na kila mtu ni raia katika mojawapo wa falme hizi. Kuokoka ni kuondolewa katika ufalme wa giza (shetani) na kuhamishiwa katika Ufalme wa Mungu. Unakubali  kutubu na kumwelekea Mungu si tu unasamehewa dhambi lakini pia unahamishwa na kuingizwa katika Ufalme wa Bwana Yesu (mwana wa pendo la Mungu) ukiwa katika Ufalme wa Mungu huna haja tena na msaada wa shetani katika maisha yako. Hirizi, utabiri wa nyota, mazindiko, ibada za mizimu na ibada za kimila huvihitaji tena. Ulipotubu umebadili msimamo na mwelekeo wako hivyo unaviondoa vitu hivi katika maisha yako maana wewe si raia wa ufalme wa shetani hata kautii na kuutumikia. Yesu ndiye mfalme wako na anawajibika kukulinda.


  •     Jina lako linaandikwa mbinguni!
“…furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni” (Luka 10:20).
“Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake” (Ufunuo 3:5).
  •      Unakuwa mwanfunzi wa Yesu.
“Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu.” Mathayo 28:19
  •      Unakuwa kiumbe kipya!
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya” (2Wakorintho 5:17).
“Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiri, bali kiumbe kipya” (Wagalatia 6:14,15).
“Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu, mkavae utu mpya ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” (Waefeso 4:22-24).
  •      Umekuwa mtoto wa Mungu!
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu (Yohana 1:12,13).
“Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo… Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo” (1Yohana 1:1,2).
  •       Malaika wanakuzunguka hata kama huwaoni!
“Je! hao wote (malaika) si roho watumikao, waliotumwa kuwahudumia wale watakaorithi wokovu? (Waebrania 1:14).
“Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe” (Zaburi 91:11,12)
  •      Unakuwa makao ya Kristo na Mungu!
“Yesu akajibu, akamwambia, mtu akinipenda atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake” (Yohana 14:23)
“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu” (Wagalatia 2:20).
“Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Waefeso 2:22).
  •      Roho Mtakatifu yumo ndani yako sasa!
“Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa roho wake anayekaa ndani yenu” (Warumi 8:11).
“Au hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? (1Wakorintho 6:19).
  •      Una mamlaka juu ya shetani na kazi zake tangu sasa!
“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru” (Luka 10:19)
“Na ishara hii zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo …. Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya” (Marko 16:17,18).
“Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia” (Yakobo 4:7).
  •      Utafufuliwa au kunyakuliwa Yesu akija kulichukua kanisa maana unao uzima wa milele!
“Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima” (1Yohana 5:12).
“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele” (1Wathesalonike 4:16,17).
“Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu …. (Ufunuo 20:6
  • Unahesabiwa haki na Mungu.
Kuhesabiwa haki maana yake ni kuonekana kuwa huna hatia mbele za Mungu. Huna kesi, hivyo una kibali mbele zake.
“kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema Yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu Yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki Yake, kwa sababu kwa ustahimili Wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. Alifanya hivyo ili kuonyesha haki Yake wakati huu, ili Yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu.” Warumi 3:23-26.
Haya ni baadhi tu ya maneno mengi mazuri ambayo yamo katika biblia yanayoeleza kilichotokea ulipookoka. Nakupa ushauri ya kuwa uyasome mara kwa mara pamoja na mengine yaliyomo katika biblia ili upate kujijua wewe sasa ni nani mbele za Mungu na   za shetani baada ya kuokoka.





YOHANA 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu ,hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele”
 Warumi 10:9 “Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chacko ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu uataokoka”


 Huenda mpendwa msomaji wangu hujaokoka na unataka kuokoka. Sasa kabla hujafanya maamuzi ya kuokoka ngoja kwa kifupi nikueleze nini maana ya kuokoka ili uweze kujua ni maamuzi ya aina gani unayoyafanya.



Kuokoka kwa kifupi maana yake ni kumkaribisha YESU katika maisha yako kwa kumruhusu achukue nafasi ya  utawala katika maisha yako. Unamruhusu atawale kwa kumkiri kwa kinywa chako na kuamini katika moyo wako, ya kwamba hakika yeye ni Bwana na Mungu alimfufua sikuya tatu katika wafu.


Kuokoka siyo kuchanganyikiwa, kupotea, ujinga au kufeli katika maisha. Unapoamua kuokoka unakuwa umempa Mungu nafasi ya;

* Kukujulisha kusudi la yeye kukuleta duniani.

*Kukujulisha mawazo na njia zake za kukufanikisha katika mambo yote.
*Unakuwa umejihakikishia uzima wa milele maadam ukiishi katika mapenzi ya Mungu.

*Mwisho unakuwa umempa Mungu nafasi ya kushughulika na maisha yako, afya yako, usalama wako,Uponyaji nk.

Sasa baada ya haya naamini unaelewa aina ya maamuzi unayotaka kufanya. Kama uko tayari kuokoka sema maneno yafuatayo kwa Imani

Sema “Bwana Yesu,  ninakuja mbele zako, ninakiri ya kuwa mimi ni mwenye dhambi, naamini kweli ulikufa na kufufuka ili nipate kuokoka, naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizotenda, kwa kujua au kutokujua naomba ulifute jina langu kwenye Kitabu cha hukumu naomba uliandike jina langu kwenye kitabu cha Uzima unitakase kwa Damu yako, nibatize kwa Roho wako Mtakatifu na kwa Moto na kwa Lugha Mpya. 

Nami nayakabidhi maisha yangu kwako uyatawale na ufanyike Bwana wa maisha yangu.  Amen. 

Baada ya sala hiyo, nikupongeze kwa kuwa umefanya maamuzi bora zaidi maishani mwako. Unatakiwa kufanya yafuatayo:-


*Tafuta mtu yeyote unayefahamiana naye ameokoka halafu mjulishe uamuzi wako pia.
*Kama hauna kanisa unalosali, basi nenda kanisa lolote linaloamini wokovu pia kisha waambie juu ya uamuzi wako.
*Jenga mazoea ya kusoma neno la Mungu kila siku na kuomba pia. Kadri unavyohudhuria kanisani utajifunza zaidi juu ya kuukulia wokuvu.
*Mwisho naomba pia nijulishe juu ya uamuzi wako kupitia anuani zangu ili nimtukuze Mungu.
Ubarikiwe sana.


calvinpetro10@gmail.com