YOHANA 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu ,hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele”
 Warumi 10:9 “Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chacko ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu uataokoka”


 Huenda mpendwa msomaji wangu hujaokoka na unataka kuokoka. Sasa kabla hujafanya maamuzi ya kuokoka ngoja kwa kifupi nikueleze nini maana ya kuokoka ili uweze kujua ni maamuzi ya aina gani unayoyafanya.



Kuokoka kwa kifupi maana yake ni kumkaribisha YESU katika maisha yako kwa kumruhusu achukue nafasi ya  utawala katika maisha yako. Unamruhusu atawale kwa kumkiri kwa kinywa chako na kuamini katika moyo wako, ya kwamba hakika yeye ni Bwana na Mungu alimfufua sikuya tatu katika wafu.


Kuokoka siyo kuchanganyikiwa, kupotea, ujinga au kufeli katika maisha. Unapoamua kuokoka unakuwa umempa Mungu nafasi ya;

* Kukujulisha kusudi la yeye kukuleta duniani.

*Kukujulisha mawazo na njia zake za kukufanikisha katika mambo yote.
*Unakuwa umejihakikishia uzima wa milele maadam ukiishi katika mapenzi ya Mungu.

*Mwisho unakuwa umempa Mungu nafasi ya kushughulika na maisha yako, afya yako, usalama wako,Uponyaji nk.

Sasa baada ya haya naamini unaelewa aina ya maamuzi unayotaka kufanya. Kama uko tayari kuokoka sema maneno yafuatayo kwa Imani

Sema “Bwana Yesu,  ninakuja mbele zako, ninakiri ya kuwa mimi ni mwenye dhambi, naamini kweli ulikufa na kufufuka ili nipate kuokoka, naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizotenda, kwa kujua au kutokujua naomba ulifute jina langu kwenye Kitabu cha hukumu naomba uliandike jina langu kwenye kitabu cha Uzima unitakase kwa Damu yako, nibatize kwa Roho wako Mtakatifu na kwa Moto na kwa Lugha Mpya. 

Nami nayakabidhi maisha yangu kwako uyatawale na ufanyike Bwana wa maisha yangu.  Amen. 

Baada ya sala hiyo, nikupongeze kwa kuwa umefanya maamuzi bora zaidi maishani mwako. Unatakiwa kufanya yafuatayo:-


*Tafuta mtu yeyote unayefahamiana naye ameokoka halafu mjulishe uamuzi wako pia.
*Kama hauna kanisa unalosali, basi nenda kanisa lolote linaloamini wokovu pia kisha waambie juu ya uamuzi wako.
*Jenga mazoea ya kusoma neno la Mungu kila siku na kuomba pia. Kadri unavyohudhuria kanisani utajifunza zaidi juu ya kuukulia wokuvu.
*Mwisho naomba pia nijulishe juu ya uamuzi wako kupitia anuani zangu ili nimtukuze Mungu.
Ubarikiwe sana.


calvinpetro10@gmail.com




Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours