Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa babaye bali mke
mwenye busara mtu hupewa na Bwana’. Nianze kwa kusema kuoa au kuolewa ni mpango
kamili wa Mungu. Zipo sababu nyingi za kwa nini unahitaji mke au mume Moja
unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana, mbili ni kwa sababu zinaa (1 Wakorintho
7:20) na tatu unapopata mke unakuwa umepata msaidizi na mlinzi.
Kibiblia mke /mme mwenye busara mtu
hupata kutoka kwa Bwana, maana yake Mungu ndiye anayehusika na kumpa mtu
mke/mme. Mungu pekee ndiye anayejua nani ana busara ya kukaa na fulani halafu
ndiyo anayekupa huyo mtu. Suala la kumpata mwenzi ambaye hakika ni wa
mapenzi ya Mungu kwa mtu husika, imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa vijana na
pia wale ambao bado hawajaoa au kuolewa.
Lengo la kitabu hiki ni;
*kuwasaidia vijana wengi ambao bado
hawajaoa au kuolewa kufanya maamuzi sahihi.
*Kuwapa maarifa wale ambao wanafuatwa
na vijana wengi kwa lengo la kutaka kuwaoa, nini wafanye pindi wanapofuatwa na
vijana wengi.
*Kuwapa uhakika / uthibitisho wale
ambao tayari wameshafanya maamuzi haya na tayari wana wachumba kwamba wachumba
hao wanatokana na Mungu au la.
*Kuwafariji na kutoa mwongozo kwa
wale ambao huenda hamna anayejitokeza kutaka kuwaoa, wanaokataliwa na wale
ambao wamechelewa kuolewa halafu wao wanafikiri ni laana.
*Kutoa mwongozo kwa wazazi,
wachungaji, walezi, viongozi wa makundi ya kidini kuwasaidia vijana wao katika
kufanya maamuzi haya makubwa.
*Kukusaidia kuzipinga hila zote za
shetani katika safari hii ya maamuzi.
Kabla ya kuzitaja njia, ndani ya kitabu
hicho nimetaja kwanza misingi unayotakiwa kuijua kabla ya kuzijua hizo njia
nayo ni;
*Kwa kila jambo kuna majira yake
hivyo hata wewe kuoa au kuolewa kwako kuna wakati wako maalumu.
*Mungu hatumii njia au mfumo wa aina
moja katika kukujulisha wewe mwenzi wako.
*Mungu anavyo vigezo vya kwake ya
kukupa mke au mme ambavyo si lazima viendane na vigezo vya kwako.
*Si kila mke au mme hutoka kwa Mungu.
*Mungu anapoamua kukupa wewe mke au
mme anakuwa ameangalia mbali kuliko wewe unavyofikiria.
*Usimuombe Mungu akujulishe mke au
mme wako wakati ndani yako umeshajichagulia wa kwako.
*Ni vema uwe umekomaa na umekua
kiakili, kiufahamu, na kiroho kwanza kabla ya kufanya maamuzi kama haya na
hujaokoka fanya maamuzi ya kuokoka maana ni kwa faida yako mwenyewe.
*Ni vema ukatambua ya kuwa mwenzi
wako si lazima atoke kanisa lako, shule au chuo ulichosoma au kazini kwako nk.
Zifuatazo ni njia za kibiblia, ambazo
hakika zimewasaidia wengi kuwajua na kuwapata wenzi wao wa maisha;
ü Kwa kumcha Mungu, (
kumtii Mungu ).
ü Kwa sauti ya Mungu
mwenyewe.
ü Amani ya Kristo.
ü Upendo wa ki –Mungu ( wa
Dhati ).
ü Mafunuo ya ki-Mungu.
ü Kwa kuyatenda mapenzi ya
Mungu.
ü Kulijua kusudi la Mungu
katika maisha yako.
ü Kuomba sawasawa na
mapenzi ya Mungu.
ü Wazazi
/walezi/wachungaji/kiongozi wako katika kundi lenu.
Bwana Mungu akubariki na akutangulie
katika safari hii ya maamuzi makubwa katika maisha yako.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours