Hakikisha kila siku unapata muda wa kuzungumza na Mungu.
Je! Utawezaje kuzungumza na Mungu? Fuata haya maelekezo yafuatayo;
- Tenga muda maalumu wa kusoma neno la Mungu pamoja na maombi. Hapa unatakiwa
utafute sehemu ambayo ni kimya na isiyo na watu. Pia unapaswa uwe wewe pekeyako
kwa maana huu ni wakati wako binafsi wa kuongea na Mungu.
- Andaa vifafa utakavyo vitumia katika kuongea kwako na Mungu. Chukua note book
(daftari), kalamu, Biblia yako, na ikibidi radio ndogo au muziki kwa ajili ya
kusikiliza nyimbo za taratibu za kuabudu.
Muda huu ni wako wewe na Mungu; sahau yote uliyoyaacha huko nyumbani, kazini,
n.k. Tumia fursa hii kusoma neno la Mungu, kumwabudu Mungu, pamoja na kuomba.
Najua kila kitu chaweza kuwa kigumu mwanzoni, lakini unaweza ukaanza kwa
kutumia dakika kumi kila siku ukiwa PEKE YAKO alafu utaona jinsi Mungu
anavyozidi kukuwezesha siku baada ya siku.
Hakikisha unaheshimu
ratiba yako siku zote. Endapo ukiona muda wa mchana unakubana; basi tafuta
nafasi usiku ambayo itakupa faragha na Mungu. Jambo hili unaweza ukalifanya
nyumbani, kazini, hata mahali po pote pale unapoona unapata nafasi ya kuwa peke
yako na Mungu katika sehemu yenye utulivu.
Siku zote neno la Mungu linaweza kukupa jambo jipya usilolifahamu. Je! Wapenda
kuyafurahia matunda ya kuongea binafsi na Mungu? Jibu lake ni hili:
TENDEA KAZI KILA KITU AMBACHO MUNGU AMESEMA NAWE. Katika hatua hii hapa
panahitajika kitu kinachoitwa UTII. Maana ya UTII ni kutekeleza kila kitu hata
kama wewe binafsi unaona nafsi yako haitaki. Kutii maana yake ni kutekeleza.
Basi endapo neno la Mungu likikutaka kutubu au kubadili mwenendo wako; wewe tii
kila kitu ambacho Mungu amesema nawe. Ukizingatia hayo utaona kila siku imani
yako na ufahamu wako juu ya neno la Mungu unaongezeka.
ZINGATIA KWAMBA: Ukristo pasipo maombi ni BURE. Biblia Takatifu inatuambia
kwamba:
"Lakini Yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu,
akaomba." (Luka 5:16)
Yesu alikuwa na desturi ya kujitenga na watu ili apate faragha ya kuomba.
Tukisoma Biblia ya Kiingereza inasema: "So He Himself often withdrew into
the wilderness and prayed." (Luke 5:16) Neno "...OFTEN..." linamaanisha
kuwa tendo hilo Yesu alikuwa analifanya kila mara (yaani ilikuwa kawaida yake
kufanya hiyo - kujitenga na watu kwa ajili ya kupata ufaragha wa maombi). Je!
Wewe wadhani Ukristo wako pasipo maombi utaweza kumshinda Shetani?
Badilika sasa; jitahidi kila siku upate muda wako binafsi ukiwa pekeyako
faragha kwa kuongea na Mungu. Japokuwa unaweza ukawa na desturi ya kulijadili
neno la Mungu ukiwa na watu mbali mbali; lakini fahamu kuwa unapaswa pia kuwa
na muda wako binafsi wa kuongea na Mungu kila siku ukiwa wewe peke yako na
Mungu tu. Ukizingatia hayo utaona mabadiliko makubwa sana katika imani yako.
Fanya sasa nawe utabarikiwa.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours