Articles by "MAHUSIANO"
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAHUSIANO. Onyesha machapisho yote


Je, unafikiri mume au mke wako ni mgumu kuishi naye? Je, unamcha mungu kuliko kujipendeza mwenyewe? Abigaili hakuwa na kanisa. Abigaili hakuwa na Biblia. Abigaili hakuwa amebatizwa na Roho Mtakatifu. Lakini basi kinyume chake, Abigaili alikuwa na mume tu aliyekuwa hana adabu, tena mwovu, tena mkorofi, aliyeitwa Nabali.

Lakini Abigaili ALIMCHA Mungu. Na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso.

Katika 1 Samweli 25 tunasoma juu ya Nabali. Kondoo na mbuzi wa Nabali walikuwa na usalama wakati wote walipokaa chini ya ulinzi wa watumishi wa Daudi. Baadaye Daudi alipoomba Nabali awape watumishi wake msaada wa vyakula, Nabali akawatukana tu. Mara moja Daudi aliamua kumwua Nabali – lakini mtumishi mmoja wa Nabali aliweza kumwambia Abigaili mambo hayo.

Alifanyaje Abigaili? Je, alifurahia tukio hilo? Je, aliwaza, “Hii sasa ni fursa yangu kwa Mungu ya kuniondoa toka kwa mume huyu! Sasa nitakuwa huru kutokana na mume huyu mkorofi! Bado mimi ni mrembo – kwa nini niolewe na mume kama huyu? Abigaili alifanyaje sasa ili awe huru kutokana na mume wake mwovu? Hakuna chochote! Yeye hakupaswa kusema wala kufanya lolote lile! Yeye angeweza kutulia TU pale na kumwacha Daudi aje pamoja na watu wake kumwua mumewe Nabali! Na wewe ungefanyaje?

Lakini Abigaili ALIMCHA Mungu! Hakujipendeza. Hakujitumikia. Alitaka kumpendeza Mungu na kumtumikia! Hakujifikiria yeye mwenyewe, au ajiokoe mwenyewe kutokana na hali hiyo ngumu. Hapana. Yeye alifikiria tu kumsaidia Daudi asilete hukumu juu yake kwa kujilipiza kisasi mwenyewe na kumwua mumewe. Alimwamini Mungu. Kwa hiyo alinyenyekea chini ya mikono ya Mungu na hakufikiri juu ya faraja yake mwenyewe au hali yake ngumu wala hakutafuta njia ya kutoroka kutoka katika mazingira yake ngumu. Na wewe?

Aliamini kuwa kila kitu kilikuwa mikononi mwake Mungu, na kwamba iwapo mumewe inampasa kufa, basi huo ulikuwa ni wakati wake Mungu mwenyewe na wala sio kwa mkono wa mwanadamu.

Hivyo Abigaili alifanyaje? Yeye aliandaa zawadi ya vyakula kwa ajili ya Daudi na hao watu wake Daudi alioandamana nao. Abigael akaondoka na kumfuatilia Daudi hukohuko njiani, “Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, … akainama mpaka nchi. Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, JUU YANGU MIMI NA UWE UOVU; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako.”

Kumbe, Abigaili alikuwa yu radhi kuyatoa maisha yake kwa ajili ya mumewe mwovu! Kwa kuwa alimwamini Mungu, alitaka kumwokoa mumewe, na pia Daudi mwenyewe kutokana na hali ya kujilipiza kisasi. Abigaili hakujitafutia mlango au njia ya kutoka ili awe huru kutokana kwa mumewe mwovu. Na wewe?

Aliamini kuwa kila kitu kilikuwa mikononi mwake Mungu. Ndoa yake ili kuwa mikononi mwa Mungu. Na alikataa kufanya cho chote kubadilisha hali hiyo ya maisha yake!

Je, mumeo au mkeo ni mtu mgumu sana hata unafikiri ungeshindwa kuendelea kuishi naye? Jaribu kufikiria hali ilikuwaje kwa mwanamke kuishi na mume kama Nabali!

Je, wewe ni mwamini? Je, unayo Biblia? Je, unakiamini kilichoandikwa ndani ya Biblia? Unampenda Mungu na unaamini kuwa yeye yuko pamoja nawe katika mazingira yoyote yale? Je, unatafuta kumpendeza yeye au kujipendeza wewe mwenyewe?

Je, umepatwa na ubaridi au ugumu dhidi ya mumeo au mkeo kwa sababu unajisikia kuwa yeye ni mtu mgumu? Je, unamshughulikia kwa dharau na chuki? Yawezekana unataka kuniambia, “Lakini…” Lakini nini? Unataka kusemaje hapa? Unatakaje kujipa haki wewe mwenyewe – hapa hatuongelei juu ya dhambi kubwa, lakini ni kuhusu kile unachokifanya pale unapojisikia kuwa mumeo au mke wako ni mtu mgumu kwako.

Je, unatafuta njia ya kuikwepa hali unayoipitia kuliko kuitafuta njia ya Mungu katika hali hiyo? Yesu ndiyo njia. Tabia yake ndiyo njia na uzima. Kama umeingiwa na ubaridi au umekuwa mgumu juu ya mumeo au mke wako, na ikiwa wewe ni mkristo, usimlaumu – sio mapenzi ya Mungu kwako uwe baridi au mgumu bali huo ni uchaguzi wako mwenyewe. Usimlaumu MTU yeyote. Utubu badala ya kuuachilia moyo wako uwe mgumu. Jinyenyekeze mwenyewe chini ya mkono wa Mungu wenye nguvu na upokee neema izidiyo – ambayo itakubadilisha WEWE kwanza, na kisha umpende mumeo, mpende mkeo.

Abigaili hakuwa na Biblia isemayo kuwa, “mke ajinyenyekeze kwa mumewe”, wala hakuwa na Biblia inayosema, “waume wapendeni wake zenu”. Hakuwa na Biblia inayowaambia waumini wanaojikuta kwenye hali ngumu, , ‘Neema yangu YAKUTOSHA; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.’ (2 Wakor. 12:9). Je, wewe unaamini mstari huu? Je utalipokea neno hili? Abigaili aliishi maisha ya namna hiyo. Je, wewe unaamini kuwa mume wako au mkeo ni mtu mgumu mno au ni mgumu kupita kiasi kwako? Lakini sikiliza neno la Mungu lisemavyo, “Lakini hutujalia sisi neema ILIYOZIDI; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.” (Yakobo 4:6).

Ikiwa utapungukiwa na neema ya Mungu katika mahusiano yako, waweza kupata sababu toka katika mistari hii ya neno ka Mungu.

Waweza kujisomea vitabu vingi vihusuvyo ndoa, waweza pia kwenda kuhudhuria semina nyingi zihusuzo ndoa, lakini kama humwendei Mungu na kujinyenyekeza mwenyewe mbele zake kwanza, hakuna hata jambo moja kati ya hayo ufanyayo yatakayo kusaidia.

Daudi alimwambia Abigaeli, ‘ubarikiwe wewe’! Nawe pia utabarikiwa, na utafanyika kuwa baraka kwa wengine nyumbani mwako ikiwa unampenda Kristo na kumtumikia kuliko kujipendeza mwenyewe tu, ikiwa unamfuata Yeye na ‘kuipoteza nafisi yako’ kwa ajili Yake kuliko kujaribu kujiokoa maisha yako kwa kujaribu kuikimbia hali ngumu au kulalamika kuhusu hali hiyo, na kuwa mgumu na mwenye uchungu.

Kumfuata Kristo Yesu na kujikana mwenyewe kutayafanya “machungu” kuwa “matamu” katika maisha yetu. “Kujitwika msalaba wako” haimaanishi kubeba mzigo nzito! Inamaanisha kujikana mwenyewe na kumchagua Yesu na njia yake, na huku kunaleta MABADILIKO katika maisha yako. Kama neno la Mungu linavyosema, “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito”, na tena, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni NIRA YANGU, mjifunze KWANGU; kwa kuwa mimi ni MPOLE na MNYENYEKEVU wa moyo; nanyi mtapata RAHA nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni LAINI, na mzigo wangu ni MWEPESI. (1 Yoh. 5:3; Mathayo 11:28-30).

Abigaeli hakujaribu kumbadilisha mumewe, alikabidhi uhai wake mikononi mwa Mungu na alikuwa anaridhia hukumu ya mumewe imwangukie yeye. Ikiwa Abigael angeweza kufanya hayo na kuwa kama hivyo nyakati za Agano la Kale, je, haitupasi sisi kuonyesha hata upendo mkuu na dhabihu katika mahusiano yetu sisi kwa sisi – sisi ambao tumeipokea neema na upendo wa Mungu kupitia Yesu Kristo ili kwamba uzima wake upate kudhihirishwa katika maisha yetu.

Inawezekana kabisa neno hilo siyo neno kwa wote, hata hivyo inawezekana ni neno kwa wengine.

Mungu alibariki neno lake kwa mioyo yetu.
 © David Stamen 2019 somabiblia.com


Je unaona kama mke wako hakuheshimu? Anahitaji upendo toka kwako. Je mume wako haonyeshi  upendo? Anahitaji heshima toka kwako.
Jinsi wewe na mwenzi wako mnavyotendeana kulingana na kila mmoja anavyohitaji, ndivyo jitihada zenu zitakapoleta matunda na kila mmoja atazidi kutiwa moyo kuendelea kutenda  mazuri kwa mwenzake na kupeelekea kuboresha ndoa yenu. Sasa ili kufanikisha hili kila mmoja wenu lazima ajue kuozungumza lugha ya upendo na heshima kwa mwenzake.
Zitazame tofauti zenu kama mtaji na sio tatizo
Tofauti kati yako na mwenzi wako haimaanishi kuwa mmoja wenu hayuko sahihi. Muombe Mungu aweze kukusaidia kuzikubali tofauti kati yenu na kukuwezesha kuzitumia kusaidiana na kufaidiana. Kumbuka mbele za Mungu wote ni sawa na mna thamani sana.
Muone mwenzi wako kuwa ni mtu mwenye nia njema
Kama mwanadamu mwingine mwenzi wako pia anaweza akafanya mambo yanayoonekana kama ubinafsi. Ni muhimu kuwa na imani kuwa mwenzi wako ana nia njema juu yako hata katika nyakati anaposhindwa kuonyesha upendo na heshima juu yako. Kumbuka kuwa ndani ya moyo wake mwenzi wako anakupenda na hapendi kukuudhi. Muombe Mungu akuwezeshe kumuona mwenzi wako kama yeye anavyomuona.
Chunga maneno yako
Maneno unayoongea yanaonyesha yaliyomo ndani ya moyo wako. Hivyo muombe Mungu aujaze moyo wako upendo na heshima kila siku, na muombe Roho mtakatifu kuifanya upya akili yako ili mawazo yako yawe mema yatakayokupelekea kuongea maneno mema yenye upendo. Kuwa mwangalifu nay ale unayoyasema kwa mwenzi wako na jinsi unavyoyachukulia yale mwenzi wako anayoyasema. Epuka kutumia maneno ambayo yatamuudhi mwenzi wako. Sikiliza kabla ya kujibu na fikiri kwanza kabya ya kuongea. Hakikisha unaongea kwa sauti nzuri ya upole na upendo na pia lugha ya mwili iwe ya upendo na upole pia. Nia kuongea maneno yanayojenga, ya kweli, yenye msamaha, ya kushukuru, ya kiMungu na yenye kutia moyo.
Tambua lugha ya mawasiliano ya mwenzi wako
Wanawake na wanaume wanatofauti kubwa sana ya lugha ya mawasiliano kati yao. Itambue lugha ya mawasiliano ya mwenzi wako, usiwe na hisia tu bali hakikisha unaielewa vyema ili kuepuka migogoro inayotokana na kutokuelewana au tafsiri isiyo sahihi. Sikiliza kwa makini, uliza pale unapokuwa na wasiwasi na azimia kujifunza na kuifahamu lugha ya mawasiliano ya mwrnzi wako. Kumbuka kutokuelewana kwa lugha ya mawasiliano na jinsi ya kuwasiliana hakumaanishi ndoa yenu ni mbaya, bali kunaonyesha tofauti ya matarajio na namna ya kuwasiliana. Jaribuni kwa pamoja kwa msaada wa Mungu kukabiliana na hali hii kwa upendo na maelewano.
Samehe
Tegemea msaada wa Mungu katika kukuwezesha kumsamehe mwenzi wako pale anapokukosea, mara zote. Kumbuka kuwa Mungu amekusamehe makosa yako na hivyo onyesha msamaha kwa mwenzi wako. Pale unapopata msamaha kwa mwenzi wako baada ya kumkosea tambua kuwa kuna uwezekano wa kuhitaji muda wa kuponya jeraha la moyo wake, kuwa muelewa na onyesha kuwa kweli umekubali kosa lako na upo tayari kurekebisha.
Timiza mahitaji ya muhimu ya mwenzi wako
Hakikisha unatumia uwezo wako kuhakikisha unatimiza mahitaji muhimu ya mke wako ya kuwa karibu naye, kuwa muwazi, kumuelewa, kumthamini, kumtunza na kumjali. Anahitaji uwe karibu naye katika hali zote, kuwa muwazi kwake na kushirikiana naye katika mawazo na mipango yako, kumsikiliza bila kujaribu kumbadilisha, kusuluhisha matatizo kwa pamoja, kumheshimu na kila wakati kumhakikishia upendo wako kwake.
Hakikisha unatumia uwezo wako kuhakikisha unatimiza mahitaji muhimu ya mume wako ya uongozi, mahusiano na kimwili. Tambua hitaji lake la kuongoza na usijaribu kuudharau uongozi wake, sikiliza kwa makini mawazo yake na ushauri, thamini hitaji lake la kuwa karibu na wewe na kuwa rafiki yake katika hali zote, na uwe tayari kwa hitaji la kimwili bila vipingamizi.
Tambua kuwa Mungu pekee ndiye anayeweza kutimiza kila hitaji la mwanadamu. Hivyo mwenzi wako anaposhindwa kutimiza baadhi ya mahitaji yako usikasirike wala  kuumia sana. Badala yake mwendee Mungu.
Angalia nia yako
Usitumie vitendo au lugha ya upendo na heshima kama njia ya kumfanya mwenzi wako kufanya kile unaachokitaka. Muombe Mungu akuwezeshe kuwa na nia safi kila wakati ili uweze kufanya jambo jema kwa nia njema na kwa wakati unaofaa, kumfurahisha Mungu na pia mwenzi wako. Onyesha upendo ha heshima kwa mwenzi wako bila kutarajia chochote kama malipo.
Chagua lililo jema bila kuangalia mwenzi wako anasema nini
Hata kama mwenzi wako haonyeshi ushirikiano kwa jitihada zako za kuonyesha upendo na heshima wewe endelea kufanya hivyo kwa moyo wa kupenda. Mungu atazilipa jitihada zako kwa kukubariki. Tamabua kuwa kwa kumwonyesha mwenzi wako upendo na heshima unakuwa unamtumikia Mungu na kumheshimu, hivyo endelea kufanya yaliyo mema bila kujali mwenzi wako anafanya nini. Mungu anaona na atabariki juhudi na jitihada zako.


Mchungaji Dk Peter Mitimingi

SIFA ZA MSICHANA ILI AWEZE KUOLEWA!


Katika agano la kale ili msichana aweze kuolewa ilikuwa lazima awe na sifa zifuatazo:

1. UZURI WA USO WAKE (“Naye yule msichana alikuwa mzuri sana uso wake)
2. AWE NI MSICHANA BIKIRA (bikira, wala mwanamume hajamjua bado).
3. AWE MSICHANA CHAPA KAZI ZA MIKONO (akashuka kisimani, akajaza mtungi wake, akapanda.”)

Mwanzo 24:16“Naye yule msichana alikuwa mzuri sana uso wake, bikira, wala mwanamume hajamjua bado; akashuka kisimani, akajaza mtungi wake, akapanda.”

Katika ziku hizo sifa kuu za msichana zilikuwa zinaangaliwa katika maeneo haya matatu:

Wadada mpo hapooo!!


 WACHUMBA WASIFANYE MIPANGO WALA MIRADI YA KIPESA KATIKA KIPINDI CHA UCHUMBA MPAKA WATAKAPOKUWA WAMEOANA TAYARI.


1. Msichange na kununua gari lenu mkiwa wachumba

2. Msichange na kununua shamba, kiwanja au nyumba yenu mkiwa wachumba.
3. Msianzishe biashara ya pamoja mkiwa wachumba.
4. Msikopeshane kiwango kikubwa cha pesa mkiwa wachumba.
5. Msishirikiane kukopa kiwango kikubwa Bank au kwenye taasisi za fedha mkiwa wachumba.
6. Haishauriwi kabisa kwa watu ambao ni wachumba kushirikiana kifedh na mipango iliyotajwa hapo juu wakati wakiwa ni wachumba. Mambo hayo hapo juu yanapaswa yafanywe na watu ambao tayari ni wanandoa.
7. Uchumba sio ndoa, hauna "garantee" wala hauna mashiko. Unaweza kuvunjika dakika yoyote ile na kama mlikuwa mmesha wekeza kila mmoja kwa mwenzake kwa kuamini kwamba si mtakuja kuoana, uzoefu unaonyesha kwamba mara nyingi mmoja kati ya wachumba hao ambaye mali ilikuwa imeandikishwa kwa jina lake huishia na mali ile na kumdhurumu mwenzake bila kujali kwamba mali hizo walikuwa wamechanga wote wawili wakati ule wa mapenzi moto moto na kuacha jeraha na maumivu makubwa sana kwa mmoja aliyedhurumiwa kitu ambacho kama hakitashughulikiwa vizuri katika ushauri "counseling" huweza kuleta athari za kimahusiano kwa mchumba atakayefuata na hata mwanandoa atakaye oana naye ataumizwa kwasababu ya lile jeraha la kudhurumiwa ambalo mchumba alitoka nalo kule.



 MAMBO YA VIJANA KUJITAYARISHA KINYUME NA MATARAJIO: (The unexpected)

Utachukua hatua gani kama jambo hili litajitokeza katika ndoa yako Baada ya Kuona? 
1. Unagundua kuwa hauwezi kupata watoto.
2. Mwenza wako anaugua na kuumwa sana.
3. Anakosa kazi au amefirisika sana.
4. Mnahitajika kuhamia katika makazi ambayo ni ya hadhi ya chini sana. 
5. Analazimmika huhamia katika nchi au mji hatarishi.
6. Anakumbwa na hali ngumu sana ya kiuchumi.
7. Kifo cha mtoto.
8. Ukagundua kuwa mwenza wako sio mwaminifu kwako.
9. Mwenza wako amepoteza kiungo fulani.
10. Unakuja kubaini kumbe mwenza wako anajihusisha na shughuli haramu kama:
• Ujambazi
• Uchawi
• Kuuza madawa ya kulevya
• Kununua na kuuza viungo vya binadamu nk.



UMUHIMU WA WANANDOA KUTUMIA MUDA PAMOJA NA KUWEKA MIKAKATI - TIME SPENT TOGETHER

1. Ni kwanjia gani mtatumia muda pamoja
2. Muda wa mke na mume wawili tu
3. Muda wa mke mume na watoto.
4. Muda wa mume na watoto tu
5. Muda wa mke na watoto tu.
6. Muda wa watoto peke yao tu.
7. Muda wa mume, mke, watoto wao na watoto wengine.
Ni muhimu sana kutenga muda kama huu wa kuwa na "time together" na mwenzi wako na familia yako kwa ujumla. 
Mara nyingi unahitaji kupanga na sio kusubiria nafasi ijitokeze maana huenda isijitokeze nafasi kama hiyo maana mambo ni mengi na yote yanahitaji pesa hivyo inahitaji kuamua na kujipanga na kulazimisha vinginevyo haitawezekana.
 KWA HUDUMA ZA USHAURI WASILIANA NAMI


Counseling Psychologist - Dr. Mitimingi - 0713 183 939

1. Huweza Kufungua Milango ya uasherati kwa Wachumba

Inaweza kupelekea kwenye maisha ya uasherati kati yenu kwasababu mtakuwa mmetumia muda mwingi kuwa pamoja na kujihalalishia uhalali wa kushiriki tendo la ndoa na kujiona tayari mmeshazoenana na kujihisi ni kama mke na mume tayari.


2. Inaweza kupunguza kasi na kiwango chenu katika mambo ya Mungu. 

Kukaa sana katika uchumba kupita kiasi kutaweza kushushaa kiwango chenu cha mambo ya kimungu kwasababu mtapeleka nguvu kubwa ya vipaumbele vyenu na muda wenu kwenye mambo ya mahusiano kuliko kupeleka kwa Mungu.

3. Inanyonya kwa kiwango kikubwa sana nguvu za kihisia kati yenu. (It is emotionally demanding).

• Muda mwingi unakuwa unamuwaza mchumba wako.

• Huna uhakika huko aliko kama yupo salama?

• Hakuna wengine walio msogelea na kutaka kukupindua.

• Kutaka kujua yupo wapi sasa, anafanya nini, nk.
• Inachukua mawazo yako kwa sehemu kubwa sana na wakati mwingine hata kazi zako hauzifanyi vuzuri.
• Sasa inapokuwa ni kwa muda mrefu inaweza kukunyonya sana kiwango cha hisia zako.


4. Inaweza kupelekea mawazo yasiyofaa na ya upinzani kutoka kwa ndugu zenu, jamaa na marafiki.

• Uchumba unapokaa kwa muda mrefu sana kupita kiasi unawafanya wanandugu kuanzisha maneno maneno ambayo yanaweza kuharibu na kila kitu katika mahusiano hayo.

• Kuna msemo wa kiswahili unasema kuwa "bata ukimchunguza sana huwezi kumla" kama mmekaa katika uchumba kwa muda mrefu sana, inaweza kuwafanya wanandugu kumfuatilia mchumba wako kwa ukaribu kwa muda mrefu na kuanza kugundua vikasoro vidogo vidogo ambavyo hata kama vilikuwa vinaweza kurekebishika wao wanavishikia bando na kusema huwezi kuoana na yule kwasababu ya hivyo vikasoro kasoro,

5. Inaweza kusababisha uchumba kuvunjika kabla ya kuoana.

• Kukaa katika mahusiano ya uchumba kwa muda mrefu kunaweza kupelekea hata uchumba wenyewe kuvynjika.

• Kukaa katika uchumba muda mrefu kunaweza kuwafanya hata ile shauku mliyokuwa nayo ya kuoana iweze kwisha kabisa na kuwafanya mjikute mkivunja na uchumba wenyewe.

6. Italeta majeraha makubwa sana baina yenu hasa baada ya uchumba kuvunjika kutakuwa na majuto na maumivu sana kwasababu Zifuatazo: 

• Kupotezeana muda miongoni mwenu.

• Kupoteza pesa na vitu mbalimabli mlivyopeana wakati wa uchumba (loss of resources).

• Maumivu ya kumwaga siri zako hata zile za ndani kabisa ambazo usingependa mtu mwingine azijue, sasa unakuwa huna uhakika kama hatamweleza mtu mwingine huko nje.
• Aibu kwa ndugu, jamaa na marafiki na jamii kwa ujumla na kujiona kuwa wameshindwa (failure to the public image).
• Hupelekea historia mbaya (bad records) kwa wachumba watakao fuata na hasa kama uchumba ujao hautafanikiwa pia.


7. Kuendesha Uchumba Wa Muda Mrefu Ni Gharama Kubwa.

• Safari za mara kwa mara kwaajili ya kuonana na mchumba wako.

• Mitoko "outing" za mara kwa mara pamoja na mchumba wako.

• Mawasiliano ya kila dakika na mchumba wako.
• Kutumiana zawadi za mara kwa mara na mchumba wako.
KWA HUDUMA ZA USHAURI WASILIANA NAMI




Counseling Psychologist - Dr. Mitimingi - 0713 18 39 39

Haikuanzishwa na wanadamu bali mungu ndiye aliyeanzisha taasisi hii… imeanzishwa na mungu ambaye ni roho, uwe na uhakika haiwezi kuendeshwa kwa kutegemea akili, hekima na maarifa ya wanasaikolojia, washauri wa mahusino nakadhalika.
Kama ni ndoa lazima kwanza msingi wake uwe imara; na msingi sahihi wa ndoa imara na ya kudumu lazima uwe mungu ambaye ni roho; lazima msingi wa ndoa ya uhakika uwe neno la mungu!
Ndoa si taasisi ya hisia, hisia zinakuja baadaye cha kwanza ni kuwa na msingi sahihi wa mungu na neno lake kuhusu ndoa na mahusiano kwa ujumla!
Hawa washauri wa mahusiano ni waburudishaji tu; hawawezi kukupa kanuni za kweli za kukufanya uwe na ndoa ya ushindi, bali wataishia kukutia moyo, wao ni sawa na pampu inayopuliza hewa kwenye puto lenye tundu.

Hawawezi kuona tundu bali juhudi zao zitagonga mwamba baada ya muda mfupi sana.

Kama ndoa ni wazo la mungu, na si wazo la adamu, uwe na uhakika adamu anahitaji wazo la mungu kukaa na kumfurahia hawa wake aliyeletewa na mungu… adamu akimtafuta hawa kwa mbinu na kanuni zake anazojua, hawezi kuthibitika…ni rahisi namna hiyo!
Kwa Waoaji“Ninajua Kati Ya Tabia Ya Mungu Ni KUCHUNGULIA KWENYE MOYO WA MTU, Kisha AKIONA HAJA YA MOYO WAKO ILIYO SAWA NA MAPENZI YAKE Anachukua Hatua KUKUPA HAJA YA MOYO WAKO…. Kwa Mtaji Huu, Naamini Kabisa Kwamba Mungu ALIUONA UHITAJI WA ADAMU Kuhitaji MSAIDIZI TENA WA KUFANANA NAYE, Ambaye Atakuwa NYAMA KATIKA NYAMA ZAKE NA MFUPA KATIKA MIFUPA YAKE… 

Adamu Alikuwa Na PICHA YA MWANAMKE NDANI YAKE [Aina, Tabia, Hata Rangi Na Mwonekano] HATA KABLA MUNGU HAJAMTENGENEZEA MKE Na Ndiyo Maana ALIPOTOKA USINGIZINI [kwenye Operation] BILA KUAMBIWA NA YEYOTE ALIWEZA KUMTAMBUA MKEWE…. Akajua Kwamba NI NYAMA KATIKA NYAMA ZAKE NA MFUPA KATIKA MIFUPA YAKE, NA AKAMWITA MWANAMKE… Katika Hili HAKUKUWA NA KUBAHATISHA:

Adamu Alijua Na Kufahamu Kuhusu MKEWE [Aliyemtarajia] Kiasi Kwamba Alipozinduka Na Kumkuta Pale HAIKUMPA SHIDA KUMFAHAMU…. Kila Nikiona VIJANA WENZANGU WA KIUME “HAMJUI” Mke Mnayemhitaji, NABAKI NA MSHANGAO; Ndani Yako TAYARI Unayo Picha Ya MKE Unayemhitaji… HUO NDO MTAJI WA KWANZA NA WA MUHIMU…. Kuanzia Hapo Unaweza Sasa KUANZA KUOMBA MBELE ZA MUNGU Ukimsihi AKUKUTANISHE Na Huyo MWANAMKE WA NDOTO ZAKO…. Kama HUNA PICHA KABISA NDANI YAKO; MUNGU HANA PA KUANZIA KUKUSAIDIA… Mungu Anashughulika Na Yale UYAONAYO NAFSINI MWAKO… If You Have the Inner Picture of Her, You Can Have Her…. Kama HAKUNA, Basi HAKUNA”
What Do You Say Mecktilder Mchomvu?? I Believe It Is a Divine Solution,
Hekima Ya Mwalimu,
Mwl D.C.K





Kumbuka upendo wako wa kwanza kwa mkeo. Kumbuka yule binti uliyekuwa unakosa usingizi kwa ajili yake, ulivyokuwa unapita pita karibu na kwao ili walau umuone moyo wako utulie. Uliyekuwa huwezi kulala kabla hujaisikia sauti yake. Kumbuka jinsi moyo ulivyokuwa unadunda siku ya kwanza kumueleza ya moyoni na jinsi gani ulivyojaa furaha alipokubali kuwa nawe siku zote za maisha yako.
 
Je kwanini leo hii unamuona hafai tena? Leo hii msichana aliyekuwa mpenzi wa moyo wako unamtendea visivyo tena bila hata kujali? Je ule upendo wa kwanza umeenda wapi? Amka katika usingizi wako, huyo mkeo ndiye yule yule binti uliyekuwa huambiwi wala husikii juu yake, uliyeapa kumlinda, kumfurahisha na kuwa naye siku zote za maisha yako.

Chukua dakika chache ufikirie mwanzo wa penzi lenu, na pia andika kabisa vitu ambavyo ulikuwa unamfanyia na uso wake unachanua kwa furaha. Sasa azimia kuyafanya hayo yote kuanzia sasa. Hata kama kuna uzito ndani yako, jisukume kutenda na hakika hutajuta. Usiangalie amefanya nini na amekosa nini bali angalia ule upendo wako wa kwanza na dhamiria kuurudisha upya katika ndoa yako.

Nakwambia ukifanya hivi utakuja kunishuhudia jinsi furaha ya ndoa ilivyoongezeka mara dufu.


1PETRO 4:8,   1WAKORINTHO 13:1-13


Uko wapi ule upendo wako wa kwanza kwa mumeo. Kumbuka jinsi gani ulivyojaa furaha baada ya kijana uliyempenda kukuvalisha pete ua uchumba na kuja kwa wazazi wako kutoa mahari? Unakumbuka jinsi gani ulivyokuwa umejiandaa kumpenda na kumtii mumeo siku zote za maisha yako. Mwanzoni ulikuwa unaona raha kumhudumia mumeo na kumfurahisha lakini kwanini sikuhizi imekuwa ni kama msalaba kwako?

Chukua muda ufikirie jinsi gani ulikuwa unajibidisha kupata muda wa kuwa na mwenzio siku hizi uko busy na watoto na marafiki basi. Ule upendo wa kummtendea mema kila siku umeenda wapi? Haijalishi amekuumiza kiasi gani, uliapa kumpenda, na hakika upendo hugeuza hata moyo wa chuma.

Kuanzia leo dhamiria kumtendea matendo ya upendo, kumuonyesha upendo hata asipostahili kabisa na utaona furaha itakavyozidi katika ndoa yako na amani kutawala daima. Upendo hufunika wingi wa dhambi na hauhesabu mabaya.

1PETRO 4:8,   1WAKORINTHO 13:1-13 









Wapendwa leo nimejisikia kuongea na wanandoa wote. Maadamu uliamua mwenyewe kuolewa, mumeo ulimpenda bila kulazimishwa na una Roho mtakatifu kamwe usinene mabaya juu ya ndoa yako wala kuikatia ndoa yako tamaa. Ni ukweli usiopingika kuwa kwenye ndoa utapita hatua mbalimbali, utapanda milima na kushuka mabonde na utalia na kucheka lakini mwisho wa siku lazima iwe ushindi.

Kuna matatizo yatatokea ndani ya ndoa sababu ya tofauti zenu, mengine sababu ya ujinga na kutokuelewa na mengine ni shetani kwa 100% maana hayana maelezo. Katika yote hayo msingi wa ushindi ni maombi, kuchukuliana na kusamehe. Mambo haya matatu ni msingi mkuu sana wa ndoa yako. Kamwe usiruhusu kiburi, kisasi au kinyogo kuchipuka ndani ya ndoa yako. Haijalishi mwenzio amekosea kiasi gani na haijalishi ameomba msamaha au la..una jukumu la kumuombea, kumchukulia na kumsamehe na juu ya yote kumtii. Pale unapoona panahitaji kuongea kaa naye muongee mfikie muafaka.

Usipende kabisa narudia usipende kabisa kutatua matatizo yako na mumeo kwa kumwambia mtu mwingine. Jitahidi kujifunza kuongea na mumeo hadi kufikia muafaka ili mambo ya ndoa yenu yawe yenu wawili tu. Mwingine ni Mungu. Kila unapomzungumza mumeo mzungumze kwa mema na sifa kede kede mengine mapungufu mwambie Yesu. Maneno huumba so jenga tabia ya kumsema vizuri mumeo kuanzia ukiwa mwenyewe hadi mbele za watu. Mheshimu mumeo hata unapokuwa mwenyewe yani mawazoni mwako.

My dear ndoa ukiyonayo ndio hiyo hiyo hakuna kubadili wala kuanza upya so una kila sababu ya kuhakikisha inakuwa yenye furaha na amani no matter what. Hata pale unapoona kama it will never be jua kuwa it will be na usikate tamaa kabisa. Kwa miaka yangu 9 ya ndoa nimeona mengi na kupitia mengi na katika yote nimejifunza we can choose to be happy or to dwell in the negatives. Si kwa uweza wala nguvu bali ni kwa Roho wa Mungu. Tuna msaidizi ambaye yupo nasi kila mahali, msaidizi anayetafuta kutuona wenye furaha daima. Msaidizi ambaye yupo kukusaidia katika kila eneo kwenye ndoa yako.



Akina Dada Wanapenda Sana Kuolewa; Lakini Ni Wachache Sana Wanajua Namna Ya Kukaa MKAO WA KUOLEWA, Na Pia Namna Ya Kuchambua Kati Ya MWANAUME MUOAJI NA MWANAUME MUONJAJI!

Maua Yana Tabia Ya KUJIFUNGA, Lakini Yanajua Pia Muda Sahihi Wa KUCHANUA Na Kutoa HARUFU Inayowavutia NYUKI; Lakini Cha Ajabu Akina Dada Wa Digitali HAMJUI Haya, Mnazidiwa AKILI NA MAUA… Hii Ni Hatari Sana!

Ninapozungumzia Muda Wa UA KUCHANUA NA KUTOA HARUFU INAYOVUTIA NYUKI; Namaanisha Uwezo Wa Kutambua MAJIRA SAHIHI YA WEWE DADA KUOLEWA NA KUHAMA TOKA KWENYE KUNDI LA “MAUA YALIYOJIFUNGA” Yaani USICHANA Kuingia Kwenye Maua Yanayoingia Kwenye “UCHAVUSHAJI” Yaani Kuwa Mke, Mama Nakadhalika!

Nyuki Hawawezi Kuruka Kuja Kwenye UA LILILOJIFUNGA (Mdada Aliyekaa Mkao Wa KUTOONESHA DALILI ZA KUWA MKE), Bali Nyuki Huwa Wanaruka Kuelekea Kwenye MAUA YALIYOCHANUA NA YENYE HARUFU YA KUVUTIA!

Kama Dada, Kama Unaona Muda Wako Wa Kuolewa ULIOKUSUDIA Umekaribia, ANZA “KUCHANUA” Anza Kujenga Tabia Za Mke Na Si SISTA DUU Anayetafuta Mme.
Nyuki Wote Wanajua MAUA YALIYOCHANUA NA YENYE HARUFU NZURI; Vivyo Hivyo Kwa WANAUME WAOAJI, NAO WANAJUA BINTI GANI ANAFAA KUWA MKE!

Tabia Na Mfumo Wa Kuwa Mke HAUJENGWI NDANI YA NDOA; Unajengwa Ukiwa Bado Peke Yako, Unaanza KUPUNGUZA TABIA ZISIZOHITAJIKA KWENYE NDOA AMBAZO MABINTI WA KAWAIDA HUWA WANAKUWA NAZO.
Unaanza Kujenga Tabia Ya Kuwa Mama Mwenye Nyumba, Jifunze Kuwa Katika Namna Ya Mke Apaswavyo Kuwa.
Ukikaa Kwenye UHALISIA WA MKE ATAKIWAVYO KUWA; NYUKI WATAONA NA WATAKUJA, Halafu Wewe Ndiwe Utakayekuwa Na Kazi Ya KUCHAGUA YUPI KATI YAO NI MUOAJI NA YUPI KATI YAO NI MUONJAJI!

Kila Mwanadada Aliyekusudia Kuolewa Anaweza Kuolewa, Lakini Ni Lazima Uwe Na UFAHAMU WA KUTOSHA Kuhusu MKE Apaswavyokuwa Kabla Hauja-Attract Attention Ya Waoaji.

Mungu Awasaidie Akina Dada Wenye Nia Ya Dhati Ya Kuolewa Na Kuwa Na Miji Yenu!




Swali: "Ninawezaje kujitayarisha kwa ndoa?"
Jibu: Mtu kujitayarisha kwa ndoa kibibilia ni sawa na kujitahidi katika maisha. Kuna kanuni ambayo inastatahili kuongoza sehemu zote za maisha yetu kama Wakristo ambao tumeokoka: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote” (Mathayo 22:37). Hii si amri ya mzaa. Ndio nguzo ya katikati ya maisha yetu kama Wakristo. Ni kuchagua kumtazamia Mungu na neno lake kwa moyo wetu wote ili nafsi zetu na akili zetu zijazwe na mambo ambayo yanamfurahisha Mungu.

Uhusiano tukonao na Mungu kupitia kwa Yesu Kristo ndio unaweka uhusiano wote katika mtazamo. Uhusiano wa ndoa umejengwa juu ya mfano wa Kristo kwa Kanisa lake (Waefeso 5:22-33). Kila sehemu ya maisha yetu inaongozwa na bidii yetu kama Wakristo kuishi kulingana na amri na sheria za Mungu. Utiifu wetu kwa Mungu na neno lake unatuami kutimiza majukumu yetu ambayo tumepewa na Mungu katika ndoa na neno lake. Na jukumu la kila Mkristo ambaye ameokoka ni kumtukuza Mungu kwa mambo yote  (1Wakorintho10:31).

Ili tujitayarishe kwa ndoa, tutembea kadiri na mwito wetu katika Kristo Yesu, na tuwe na ushirika wa karibu na Mungu kupitia kwa neno lake (2 Timotheo 3:16-17), tazamia utiifu katika mambo yote. Hakuna mpango rahisi wa kujifunza kutembea kwa utiifu kwa Mungu. Ni chaguo ambalo ni lazima tulifanye kila siku tuweke kando mitazamo ya kiulimwengu na badala yake tumufuate Mungu.

Kutembea kadri na namna Yesu alitembea na kujitoa kwa unyenyekevu kwa njia moja peke, njia peke ya kweli na maisha peke siku baada ya siku, wakati hadi wakati. Huko ndiko kujiandaa kila Mkristo anastahili kujitayarisha kwa zawadi ambayo twaiita ndoa
Mtu ambaye amekomaa kiroho na anatembea na Mungu amejitayarisha kwa ndoa kuliko kitu kingine kile. 

Ndoa huitaji jitiada, hisia, unyenyekevu, upendo na heshima. Hizi tabia kila mara zajidhihirisha kwa mtu ambaye ako na uhusiano wa karibu na Mungu. Unapojitayarisha kwa ndoa, tazamia kumruhusu Mungu akuchonge na akufinyange uwe mume au mke anayetaka uwe (Warumi 12:1-2). Ukinyenyekea kwake, atakuwezesha uwe tayari kwa ndoa wakati siku hiyo ya ajabu ikiwadia.





Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa babaye bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana’. Nianze kwa kusema kuoa au kuolewa ni mpango kamili wa Mungu. Zipo sababu nyingi za kwa nini unahitaji mke au mume Moja unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana, mbili ni kwa sababu zinaa (1 Wakorintho 7:20) na tatu unapopata mke unakuwa umepata msaidizi na mlinzi.

Kibiblia mke /mme mwenye busara mtu hupata kutoka kwa Bwana, maana yake Mungu ndiye anayehusika na kumpa mtu mke/mme. Mungu pekee ndiye anayejua nani ana busara ya kukaa na fulani halafu ndiyo anayekupa huyo mtu. Suala la kumpata mwenzi ambaye hakika ni wa mapenzi ya Mungu kwa mtu husika, imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa vijana na pia wale ambao bado hawajaoa au kuolewa.
Lengo la kitabu hiki ni;

*kuwasaidia vijana wengi ambao bado hawajaoa au kuolewa kufanya maamuzi sahihi.

*Kuwapa maarifa wale ambao wanafuatwa na vijana wengi kwa lengo la kutaka kuwaoa, nini wafanye pindi wanapofuatwa na vijana wengi.

*Kuwapa uhakika / uthibitisho wale ambao tayari wameshafanya maamuzi haya na tayari wana wachumba kwamba wachumba hao wanatokana na Mungu au la.

*Kuwafariji na kutoa mwongozo kwa wale ambao huenda hamna anayejitokeza kutaka kuwaoa, wanaokataliwa na wale ambao wamechelewa kuolewa halafu wao wanafikiri ni laana.

*Kutoa mwongozo kwa wazazi, wachungaji, walezi, viongozi wa makundi ya kidini kuwasaidia vijana wao katika kufanya maamuzi haya makubwa.

*Kukusaidia kuzipinga hila zote za shetani katika safari hii ya maamuzi.

Kabla ya kuzitaja njia, ndani ya kitabu hicho nimetaja kwanza misingi unayotakiwa kuijua kabla ya kuzijua hizo njia nayo ni;

*Kwa kila jambo kuna majira yake hivyo hata wewe kuoa au kuolewa kwako kuna wakati wako maalumu.

*Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wako.

*Mungu anavyo vigezo vya kwake ya kukupa mke au mme ambavyo si lazima viendane na vigezo vya kwako.

*Si kila mke au mme hutoka kwa Mungu.
*Mungu anapoamua kukupa wewe mke au mme anakuwa ameangalia mbali kuliko wewe unavyofikiria.

*Usimuombe Mungu akujulishe mke au mme wako wakati ndani yako umeshajichagulia wa kwako.

*Ni vema uwe umekomaa na umekua kiakili, kiufahamu, na kiroho kwanza kabla ya kufanya maamuzi kama haya na hujaokoka fanya maamuzi ya kuokoka maana ni kwa faida yako mwenyewe.

*Ni vema ukatambua ya kuwa mwenzi wako si lazima atoke kanisa lako, shule au chuo ulichosoma au kazini kwako nk.

Zifuatazo ni njia za kibiblia, ambazo hakika zimewasaidia wengi kuwajua na kuwapata wenzi wao wa maisha;

  ü  Kwa kumcha Mungu, ( kumtii Mungu ).
  ü  Kwa sauti ya Mungu mwenyewe.
  ü  Amani ya Kristo.
  ü  Upendo wa ki –Mungu ( wa Dhati ).
  ü  Mafunuo ya ki-Mungu.
  ü  Kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu.
  ü  Kulijua kusudi la Mungu katika maisha yako.
  ü  Kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.
  ü  Wazazi /walezi/wachungaji/kiongozi wako katika kundi lenu.

Bwana Mungu akubariki na akutangulie katika safari hii ya maamuzi makubwa katika maisha yako.