Wapendwa leo nimejisikia kuongea na
wanandoa wote. Maadamu uliamua mwenyewe kuolewa, mumeo ulimpenda bila
kulazimishwa na una Roho mtakatifu kamwe usinene mabaya juu ya ndoa yako wala
kuikatia ndoa yako tamaa. Ni ukweli usiopingika kuwa kwenye ndoa utapita hatua
mbalimbali, utapanda milima na kushuka mabonde na utalia na kucheka lakini
mwisho wa siku lazima iwe ushindi.
Kuna matatizo yatatokea ndani ya ndoa
sababu ya tofauti zenu, mengine sababu ya ujinga na kutokuelewa na mengine ni
shetani kwa 100% maana hayana maelezo. Katika yote hayo msingi wa ushindi ni
maombi, kuchukuliana na kusamehe. Mambo haya matatu ni msingi mkuu sana wa ndoa
yako. Kamwe usiruhusu kiburi, kisasi au kinyogo kuchipuka ndani ya ndoa yako.
Haijalishi mwenzio amekosea kiasi gani na haijalishi ameomba msamaha au la..una
jukumu la kumuombea, kumchukulia na kumsamehe na juu ya yote kumtii. Pale unapoona
panahitaji kuongea kaa naye muongee mfikie muafaka.
Usipende kabisa narudia usipende
kabisa kutatua matatizo yako na mumeo kwa kumwambia mtu mwingine. Jitahidi
kujifunza kuongea na mumeo hadi kufikia muafaka ili mambo ya ndoa yenu yawe
yenu wawili tu. Mwingine ni Mungu. Kila unapomzungumza mumeo mzungumze kwa mema
na sifa kede kede mengine mapungufu mwambie Yesu. Maneno huumba so jenga tabia
ya kumsema vizuri mumeo kuanzia ukiwa mwenyewe hadi mbele za watu. Mheshimu
mumeo hata unapokuwa mwenyewe yani mawazoni mwako.
My dear ndoa ukiyonayo ndio hiyo hiyo
hakuna kubadili wala kuanza upya so una kila sababu ya kuhakikisha inakuwa
yenye furaha na amani no matter what. Hata pale unapoona kama it will never be
jua kuwa it will be na usikate tamaa kabisa. Kwa miaka yangu 9 ya ndoa nimeona
mengi na kupitia mengi na katika yote nimejifunza we can choose to be happy or
to dwell in the negatives. Si kwa uweza wala nguvu bali ni kwa Roho wa Mungu.
Tuna msaidizi ambaye yupo nasi kila mahali, msaidizi anayetafuta kutuona wenye
furaha daima. Msaidizi ambaye yupo kukusaidia katika kila eneo kwenye ndoa
yako.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours