Uko wapi ule upendo wako wa kwanza kwa mumeo. Kumbuka jinsi gani ulivyojaa furaha baada ya kijana uliyempenda kukuvalisha pete ua uchumba na kuja kwa wazazi wako kutoa mahari? Unakumbuka jinsi gani ulivyokuwa umejiandaa kumpenda na kumtii mumeo siku zote za maisha yako. Mwanzoni ulikuwa unaona raha kumhudumia mumeo na kumfurahisha lakini kwanini sikuhizi imekuwa ni kama msalaba kwako?

Chukua muda ufikirie jinsi gani ulikuwa unajibidisha kupata muda wa kuwa na mwenzio siku hizi uko busy na watoto na marafiki basi. Ule upendo wa kummtendea mema kila siku umeenda wapi? Haijalishi amekuumiza kiasi gani, uliapa kumpenda, na hakika upendo hugeuza hata moyo wa chuma.

Kuanzia leo dhamiria kumtendea matendo ya upendo, kumuonyesha upendo hata asipostahili kabisa na utaona furaha itakavyozidi katika ndoa yako na amani kutawala daima. Upendo hufunika wingi wa dhambi na hauhesabu mabaya.

1PETRO 4:8,   1WAKORINTHO 13:1-13 








Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours