Haikuanzishwa na wanadamu bali mungu ndiye aliyeanzisha
taasisi hii… imeanzishwa na mungu ambaye ni roho, uwe na uhakika haiwezi
kuendeshwa kwa kutegemea akili, hekima na maarifa ya wanasaikolojia, washauri
wa mahusino nakadhalika.
Kama ni ndoa lazima kwanza msingi wake uwe imara; na msingi
sahihi wa ndoa imara na ya kudumu lazima uwe mungu ambaye ni roho; lazima
msingi wa ndoa ya uhakika uwe neno la mungu!
Ndoa si taasisi ya hisia, hisia zinakuja baadaye cha kwanza
ni kuwa na msingi sahihi wa mungu na neno lake kuhusu ndoa na mahusiano kwa
ujumla!
Hawa washauri wa mahusiano ni waburudishaji tu; hawawezi kukupa
kanuni za kweli za kukufanya uwe na ndoa ya ushindi, bali wataishia kukutia
moyo, wao ni sawa na pampu inayopuliza hewa kwenye puto lenye tundu.
Hawawezi kuona tundu bali juhudi zao zitagonga mwamba baada ya muda mfupi sana.
Kama ndoa ni wazo la mungu, na si wazo la adamu, uwe na
uhakika adamu anahitaji wazo la mungu kukaa na kumfurahia hawa wake aliyeletewa
na mungu… adamu akimtafuta hawa kwa mbinu na kanuni zake anazojua, hawezi
kuthibitika…ni rahisi namna hiyo!
Post A Comment:
0 comments so far,add yours