Kila jambo maishani
lina kanuni zake. Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya
kushirikiana na Mungu.
1.
MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA
YAKO.
UPENDO WA MUNGU
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,
hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima
wa milele. Yohana 3:16
MPANGO WA MUNGU KWAKO
Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe
nao tele. Yohana 10:10
Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo?
Ni kwa sababu . . .
2.
MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI. Dhambi zake zimemtenga na Mungu.Kwa hiyo hajui
upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.
MWANADAMU NI MWENYE
DHAMBI
Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na
kupungukiwa na utukufu wa Mungu.Warumi 3:23
Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la
kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu.
Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi. Mtu
anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.
MWANADAMU AMETENGANA
NA MUNGU
Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu
wenu. Isaya 59:2
Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati
yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu
kwa nija nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi.
Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .
3.
YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI. Alikufa kwa ajili yetu ili
tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
ALIKUFA ILI ATULETE
KWA MUNGU
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa
ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1
Petro 3:18
YESU YU HAI
Kristo alikufa kwa ojili ya dhambi zetu, kama
yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu,
kama yanenavyojil maandiko.1 Wakorintho 15:3,4
YESU NDIYE NJIA YA
PEKEE
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na
uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.Yohana 14:6
Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na
Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe
daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.
Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo
kumjua maishani mwako . . .
4.
INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na
mpango wa Mungu kwa maisha yako.
UNAMPOKEA KRISTO KWA
IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.Yohana 1:12
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya
imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa
matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.Waefeso 2:8,9
INAKUPASA KUMKARIBISHA
YESU, MAISHANI MWAKO
Tazama, nasimama milangoni, nabisha, mtu
akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .
Kumpokea Yesu Kristo ni:
1.
Kujua wewe ni mwenye
dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
2.
Kumtegemea Mungu kwa
kukusamehe kabisa.
3.
Kumkaribisha Yesu Kristo
atawale maisha yako kwa imani, ili uwe kama anavyopenda.
Je, ni picha gani aliye mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambaye ungependa awe mfano
wa maisha yako?
Yafuatayo ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea
Kristo ndani ya maisha yako?
UNAWEZA KUMPOKEA
KRISTO SASA
Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika
sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.
Bwana Yesu Kristo,
ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha
yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya
dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba
uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe
kama upendavyo wewe. Amin.
Je, sala hii ni sawa na haja ya moyo wako?
Kama sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi
omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.
YESU YUMO MAISHANI MWAKO
Sasa, je, umemkaribisha Yesu maishani mwako?
Unajuaje?
Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20.
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je,
si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako?
Mungu ameahidi kwanba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.
ALIYE NA YESU, ANAO
UZIMA WA MILELE
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa
uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwana. Yeye aliye naye Mwana, anao huo
uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo
hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa
Mungu. 1 Yohana 5:11-13
Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi
katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa.
(Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.
USIYATEGEMEE MAWAZO YA
MOYO WAKO.
Unaweza kujisikia leo unalfuraha kisha kesho
ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani
mwako. Waebrania 13:8.
- Ukweli wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.
- Tunaunganishwa na uwezo wa ukweli kwa imani.
- Tunapotii ukweli, hali ya kujisikia ya moyo (maoni)
huongozwa vyema.
- Tunamtegea Mungu na ukweli wake wala sio hali ya
kujisikia ya moyo.
Tukifanya dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.
Basi, usitegemee mawazo yako, bali utegemee
ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.
KWA KUWA SASA
UMEMPOKEA YESU
Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi
yametokea.
1.
Yesu ameingia katika
maisha yako. (Ufunuo 3:20)
2.
Umesamehewa dhambi zako.
(Wakolosai 1:14)
3.
Umefanyika kuwa mwana wa
Mungu. (Yohana 1:12)
4.
Utazidi kujua makusudi
ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)
Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko
kumpokea Yesu katika maisha yako?
Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa
kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu
kwa maombi.
Tuombe tukiwa huru.
Na sasa je?
JINSI YA KUKUA KIROHO
Kama mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho
ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:
1.
Zungumza na Mungu kwa
maombi (Yohana 15:7)
2.
Soma Neno la Mungu
(Matendo 17:11)
3.
Uwe mwaminifu kwa Mungu
(Yohana 14:21)
4.
Mshuhudie Kristo kwa
matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)
5.
Umtumaini Mungu kwa kila
jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)
6.
Umruhusu Roho Mtakatifu
akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)
NI MUHIMU KWA WAKRISTO
KUSHIRIKIANA
Biblia inatuambia kukusanyika pamoja
(Waebrania 10:25)
Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi
zikirundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na
kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke
yako.
Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea
Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.
Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia
kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours