jibu: Bibilia
inaonyesha njia ya wazi ya uzimani.Mwanzo ni sharti tutambue yakwamba tumetenda
dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na
utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi
Mungu,ambayo yanafanya tustahili adhabu.Kwa kuwa dhambi zetu ziko kinyume
kabisa na Mungu aliye uzima wa milele,basi ni adhabu ya milele pekee itoshayo.
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele
katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Hata hivyo
Yesu Kristo asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:23), mwana wa Mungu alifanyika kuwa
mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu. “Bali Mungu aonyesha
pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili
yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8). Yesu Kristo alikufa
msalabani (Yohana 19:31-42), kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili
(2Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1Wakorintho
15:1-4), kudhihirisha ushindi juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi
alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu
Kristo katika wafu” (1Petro 1:3).
Kwa imani
ni sharti tuungame dhambi zetu na tumrejee Kristo kwa ajili ya wokovu (Matendo
3:19). Tukiweka imani yetu kwake, kwa kuamini kifo chake msalabani kama malipo
ya dhambi zetu,tutasamehewa na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. “Kwa maana
jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa
sababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako
ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Imani pekee
katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli ya pekee
ya uzimani! “Kwa maana nimeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo
haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye
yoyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa
unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako,tazama mfano huu wa
maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile
haitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini.
Ombi hili ni njia ya kumuelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa
kukupea wokovu. “Mungu,najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na
ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa
kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Nina ziacha dhambi zangu na ninaweka imani
yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu /ya ajabu na kwa msamaha
- karama ya uzima wa milele! Amina!”
Je,
umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa?
Post A Comment:
0 comments so far,add yours