Swali: "Je,
kuna Mungu? Je, kuna ushahidi wa kuthibitisha kuweko kwa Mungu?"
Jibu: Je, kuna Mungu? Ninaona
ni jambo la kusisimua ya kwamba umakini mwingi umepawa mjadala huu. Katika
takwimu zetu hivi sasa zasema ya kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watu duniani
wanaamimi kuweko kwa Mungu au Mamlaka ya kiwango cha juu. Jukumu linabaki kwa
wenye kuamini kuthibitisha ukweli wa kuweko kwake. Mimi nafikiri ingewapasa
wale hawaamini watuthibitishie.
Kuweko kwa Mungu hakuwezi kutothibitishwa wala kuthibitishwa. Bibilia inasema
inatupasa kukubali kwa imani kuwa Mungu yuko, “Na pasipo imani haiwezekani mtu
kumpendeza Mungu, kwa kuwa kila ajaye kwake sharti aamini kuwa yuko na ya kuwa
huwapa vitu wale wamtafutao kwa bidii” (Waebrania 11:6). Kama Mungu alingetaka
iwe, angejitokeza tu mbele ya ulimwengu wote kuwajulisha wote kuwa yeye yuko.
Lakini, angefanya hivyo hakungekuwa na haja ya imani. “Tena Yesu kamwambia,
‘kwa kuwa umeniona, umeamini; heri wale ambao hawakuniona na wameamini” (Yohana
20:29).
Hiyo haimaanishi ya kuwa hakuna idhibati ya kuweko kwa Mungu. Biblia inasema,
“Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga zatangaza kazi za mikono yake. Siku
baada ya siku zamimina hotuba zake; usiku baada ya usiku zaonyesha ufahamu.
Hakuna hotuba au lugha ambayo haisikiki. Sauti zao hutapakaa duniani kote,
maneno yao mpaka mwisho wa dunia” (Zaburi 19:1-4). Ukitazama nyota, ukijaribu
kufahamu kina cha anga, na kutazama maajabu ya kiasili, huku ukiona urembo wa
kutua kwa jua - haya yote yanaashiria kuweko kwa Mungu muumbaji. Kuna ushahidi
wakuweko kwa Mungu ndani ya mioyo yetu. Mhubiri 3:11 inatuambia, “….ameweka pia
umilele ndani ya mioyo ya wanadamu…” Kuna kitu ndani yetu kinachotujulisha ya
kuwa kuna kitu zaidi baada ya maisha haya tunayoishi na mwingine zaidi yetu nje
ya dunia hii. Hata tukipuuza bado kuna uwepo wa Mungu maishani mwetu. Biblia
inatuonya ya kuwa kuna wengine watakuwapo watakaokataa kuwepo kwa Mungu,
“Mjinga amesema moyoni mwake hakuna Mungu” (Zaburi 14:1). Kwa kuwa zaidi ya
asilimia 98 ya watu wa tamaduni mbali mbali katika vizazi vilivyopita ndani ya
mabara yote duniani ni waumini wa kuwepo kwa Mungu wa aina Fulani – lazima kuwe
kuna mtu ama kitu Fulani kinachohisi na kusababisha imani hii.
Kuongezea, kuna maoni mbali mbali ambayo hutumika kuthibitishia pia. Maoni ya
kwanza yasema kwa kuwa Mungu ni kile ambacho zaidi yake hakuna. Basi uwezekano wa
kuwepo kwake ni mwingi. Na kama Mungu hayuko basi hakungekuwa na ambacho zaidi
yake hakuna. Maoni ya pili ni kwamba kwa kuwa ulimwengu unaonyesha kazi nzuri
ya ustadi iliyofanyika basi lazima kuweko na aliyeifanya. Kila kitu kina fanya
kazi vyema kwa wakati wake na kwa kipimo mwafaka. Kama hewa yetu ingeharibika
tu kidogo viumbe vyote vingekufa.
Maoni ya tatu ni kwamba kwa chochote kufanyika lazima kuweko na mwenye au
chenye kusababisha. Kwa vile ulimwengu upo lazima kuwe na aliyeusababisha uweko
na huyo ndiye Mungu. Maoni ya nne ni kwamba katika kila utamaduni, mila na
desturi za watu duniani kuna aina Fulani ya mfumo wa sheria ya kuelekeza; yenye
kutambua mema na mabaya. Kuua, uongo, wizi na uchafu wa kitabia ni mambo
yanayokataliwa ulimwenguni kote. Hali hii ya kutambua meme na mabaya ilitoka
wapi Kama si kwa Mungu Mtakatifu?
Biblia inatuambia, watu watakataa ukweli wa kuweko kwa Mungu na kuamini roho za
uongo. Warumi 1:25 inasema, “walibadilisha ukweli wa Mungu na kutumikia uongo
hata kuiabudu na kuitumikia miungu waliyoiumba kwa mikono yao kinyume na Mungu
aliyewaumba –ambaye daima husifiwa. Amina.” Biblia pia inasema, watu hawana
sababu ya kutomwamini Mungu, “Kwa kuwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu siri za
uwepo wake – Nguvu zake za milele na utisho wake umethibitika na kufahamika
kutokana na yale aliyoyatenda kwa hivyo wanadamu hawana kisingizio” (Warumi
1:20).
Watu husema hawamwamini mungu kwa sababu si kisayansi ama hakuna kithibitisho
cha kuweko kwake. Sababu halisi ni kwamba kwa kukubali yuko,mtu anahitajika
kuwajibika mbele zake na kuomba msamaha (Warumi 3:23; 6:23). Kama Mungu yuko
basi tunawajibika kwa matendo yetu. Kama hayuko, basi tunaweza kufanya mapenzi
yetu wenyewe bila kujali hukumu. Huenda ikawa hii ndiyo sababu ya watu wengine
kushikilia mawazo ya kuwa dunia ilifanyika tu kwa njia ya vitu tofauti tofauti
kubadilika umbo polepole kupitia mabadiliko ya kimazingira ili waepukane na
ukweli wa kuna Mungu muumbaji wa yote. Mungu yuko na kila mmoja anajua hivyo.
Mwenye kubishana ni mbishani tu lakini huwa hata yeye anajua yuko.
Je, nitajuaje kuwa Mungu yuko? Najua Mungu yuko kwa kuwa nazungumza naye kila
siku. Simsikii masikioni akinijibu lakini ninahisi uwepo wake, nahisi kuongoza
kwake, najua upendo wake ninatamani neema yake.Mambo yaliyotendeka maishani
mwangu hayana maelezo mengine ila Mungu. Mungu ameniokoa kimiujiza na
kuyabadilisha maisha yangu mpaka sasa nimebaki tu kumtukuza. Maelezo haya yote
hayawezi kumfanya mtu anayetaka kukataa kuwepo kwa Mungu akubali. Muhimu ni
kumkubali kwa imani (Waebrania 11:6). Imani kwa Mungu si bure kama kubahatisha
gizani bali ni sawa na kutembea salama ndani ya chumba chenye nuru ambamo
asilimia 90 ya watu waliomo wamesimama.
Ni kweli mbingu ipo Mungu akubariki!
JibuFuta