“Nimesulubiwa
pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi
bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika
mwili, ninaishi kwa imani ya Mungu, aliyenipenda na kujitoa
kwa ajili yangu.” (Wagalatia 2:20).
bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika
mwili, ninaishi kwa imani ya Mungu, aliyenipenda na kujitoa
kwa ajili yangu.” (Wagalatia 2:20).
Katika mstari huu, Paulo anasema
kwamba alisulubiwa na sasa anaishi. Paulo anamaanisha kwamba alikufa na Yesu
Kristo na sasa anaishi kwa utukufu wake, yaani Yesu anaishi ndani yake.
Katika mstari huu tunaona maana ya
kuokoka. Wakati mtu anaokoka, jambo fulani kubwa hufanyika kwake. Ule utu wake
wa kale hufa na badala yake kiumbe kipya hufanyika. “Mtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya” (2 Wakorintho 5:17).
“Hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa
yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema.
Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu
wa roho katika Kristo Yesu” (Waefeso 2:5-6).
Wakati Yesu Kristo alipokufa
aliwachukua watu wake pamoja naye kaburini. Walikufa pamoja naye: “mkijua
neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa
dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena” (Warumi 6:6). Wakati
tunaokoka tunaunganishwa na Kristo. Utu wa kale hufa.
Katika mstari huu, Paulo anaendelea
kueleza hali ya mtu ambaye amezaliwa mara ya pili, yaani mtu ambaye ni kiumbe
kipya. Paulo anasema kuhusu mtu ambaye ameokoka, “Kristo anaishi ndani yake.”
Huu ni ukweli kwa kila mtu ambaye ameokoka, kwamba Kristo anaishi ndani yake.
Mtu ambaye ameokoka huwa anaishi chini ya mwongozo na utawala wa Yesu Kristo na
anaishi maisha yake kwa nguvu za Yesu Kristo. “Nayaweza mambo yote katika yeye
anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13); “Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo,
nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa
nguvu” (Wakolosai 1:29).
Hii ndiyo sababu mtu ambaye amezaliwa
upya husema “Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu,
Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo” (Warumi 15:18).
Hivi ndivyo mstari wa Wagalatia 2:20 unamaanisha. Kristo
anaishi ndani yetu, Kristo anatuongoza na Kristo anatupatia nguvu. Hii ndiyo
sababu alikufa ili watu wake waishi kwa imani ndani yake: “Nimesulubiwa pamoja na Kristo;
lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio
nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda,
akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu”
Kwa hivyo kile Paulo anasema hapa ni
kwamba mtu akiokoka, Kristo huja na kukaa ndani yake na kuanzia wakati huo mtu
huyo anaishi maisha ya imani ndani ya Kristo. Kristo anaishi ndani ya watu wake
na huwapa mwongozo, uwezo na nguvu. Mtu ambaye ameokoka hupokea haya yote kwa
imani.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours