Swali: "Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa
Mungu?"
Jibu: Matendo 13:38 yasema, “Basi naijulikane kwenu, ndugu zangu ya kuwa
kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi.”
Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji?
Neno “Samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo nakulifanya kutokuwa na mawaa
yoyote, ku achilia, kufutilia mbali deni. Tunapo kosea mtu, huuliza msamaha wao
ili tukarudishe uhusiano. Msamaha haupeanwi kwa sababu mtu anastahili
kusamehewa. Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo,
huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha
mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.
Bibilia inatuambia yakwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya
dhambi. Mhubiri 7:20 asema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa
duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8 asema, “Tukisema
kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi
zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo,
tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa,
tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu
(Mathayo 25:46; Yohana 3:36).
Msamaha-Je, ni upate vipi?
Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye ari ya kutusamehe dhambi
zetu! 2Petro 3:9 asema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee,
bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo alitoa kwa
ajili ya msamaha wetu.
Adhabu ya haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya
kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni
mauti…..” Mauti ya milele ndiyo ndiyo tuliyopokea kama mshahara wa dhambi zetu.
Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo
(Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba kwa kuchukua adhabu tuliyo
stahili-mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya
kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
“Yesu alikufa msalabani, akichukua adhabu tuliyo stahili!Kama Mungu, kifo chake
Yesu kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 asema, “Naye
ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa
dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu
ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na
kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni
kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, uko na hisia za kuudhi za kila mara
zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu ku epukika?Msamaha wa dhambi zako upo
ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso1:7 yasema,
“katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi,
sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia deni ili tukapate kusamehewa.
Unacho stahili ni kumuuliza Mungu akusamehe kupitia kwake Yesu, ukiamini
yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina
habari hii ya ajab, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali
ulimwengu uokolewe katika yeye.”
Msamaha-Je, ni jambo lililo rahisi?
Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu bila kupitia kwa YESU
KRISTO. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa
imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo
kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza
kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni
kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Ombi hili ni
njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea
msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili
adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini
yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weak imani yangu kwako
ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu/ya ajabu na kwa msamaha! Amina.”
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa?
Post A Comment:
0 comments so far,add yours