Swali: "Ina
maana gani Yesu kuwa Mwana wa Mungu?"
Jibu: Yesu si Mwana wa Mungu
kulingana na ubaba wa kawaida wa binadamu. Mungu hakuoa na kupata mwana wa
kiume. Mungu hakufanya tendo la ndoa na Mariamu, na pamoja naye kuzaa mtoto wa
kiume. Yesu ni Mungu katika hali kwamba ni Mungu anajithirihisha kama mwili.
(Yohana 1:1, 14) Yesu ni mwana wa Mungu kwa dhana kwamba Mariamu alipata mimba
kupitia Roho Mtakatifu. Luka 1:35 yasema, “Malaika akajibu akamwambia, Roho
Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama
kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa
Mungu.”
Wakati wa kujaribiwa kwake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kuhani mkuu alimtaka
Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana
wa Mungu” (Mathayo 26:63). “Yesu akamwambia wewe umesema,’ Yesu akamwambia,
wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi
mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Mathayo 26:64)
viongozi wa Kiyahudi walimdhania kwa kukufuru (Mathayo 26:65-66). Baadaye mbele
ya Pilato, “Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo
amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu” Yohana 19:7) ni kwa
nini makisio yake kuwa Mwana wa Mungu yachukuliwe kuwa kufuru na astahili
hukumu ya kifo? Wayahudi wilielewa vizuri sana chenye Yesu alimaanisha kwa
maneno haya “Mwana wa Mungu” kuwa Mwana wa Mungu ni kuwa hali moja na Mungu.
Mwana wa Mungu “wa Mungu” kusema uko katika hali sawa na Mungu-hakika kuwa
Mungu- kulikuwa sawa na kukufuru kwa viongozi wa Kiyahudi; kwa hivyo walimtaka
Yesu auwawe, kulingana na Mambo ya Nyakati 24:15. Waebrania 1:3 inadhihirisha
haya wazi, “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake, akiisha kufanya utakaso wa
dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”
Mfano mwingine unaweza patikana katika Yohana 17:12 mahali Yuda anaelezwa kama
mwana wa “upotevu”? jina upotevu lamaanisha “uharibivu” Yuda hakuwa mwana wa
uharibivu, lakini mambo hayo ndio ya kutambulisha maisha ya Yuda. Yuda
anadhihirisha upotevu. Vile vile Yesu mwana wa Mungu. Ni Mungu anajidhihirisha
(Yohana 1:1,14).
Post A Comment:
0 comments so far,add yours