Swali:
"Je, Yesu ni Mungu? Je, Yesu alitoa madai ya kuwa yeye ni Mungu?"
Jibu: Yesu hakunakiliwa
mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi
ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika
Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili
linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa
wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni
mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi
ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo
hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya
kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na
Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu
akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena
kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59).
Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe YESU kama haingekuwa ya kuwa alisikika
akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?
Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika
mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28
inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake
mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo.
Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe.
Kwa hivyo Yesu ni Mungu!
Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana
20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi
kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1).
Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na
Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya
ufalme wako.”
Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu
Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa
(Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa
kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile
malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu
ni Mungu.
Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa
kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu
pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia
dhambi za ulimwengu wote (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke
kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours