BWANA
YESU atukuzwe.
Karibu
tujifunze.
Neno
'' KUPENDA''limekuwa msamiati mgumu sana kwa vijana wa leo, shetani amefanikiwa
kwa asilimia 90 kuwanasa vijana wengi na kuwaangusha katika dhambi, akitumia
msamiati huu NAKUPENDA.
2
Timotheo 2:22 '' Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na
upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi. ''
-Kwa
Wasichana Kusumbuliwa Na Vijana Wasio Na Hofu Ya MUNGU Limekuwa Ni Jambo La
Kawaida. Kwao Ni Kama Vile Usivyoweza Kuwazuia Ndege Wasiruke Juu Ya Kichwa
Chako. Lakini Licha Ya Hayo Mimi Naamini Kila Msichana Anaweza Kuwazuia Ndege
Hao Wasijenge Viota Kwenye Nywele Zake. Dada Najua Umeshindwa Kuwazuia Ndege
Kuruka Juu Ya Kichwa Chako Lakini Naamini Unaweza Kuwazuia Ndege Hao Kujenga
Kiota Kwenye Kichwa Chako, Shika Utakatifu Na Utunze Wokovu Wa BWANA YESU Kama
Pesa.
-Mabinti
jizuieni na uasherati, jizuieni maana nyie ndio mara nyingi mnafuatwa. upendo
hauko katika ngono.
1
Kor 5:10 Biblia inasema ''Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii,
au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana
hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.''
-Wazinzi
na wenye kutamani tunao katika mazingira yetu iwe ni nyumbani au ni kazini
lakini ni jukumu lako binti kukataa kutumiwa kama chombo cha kujifurahishia
wadhalimu. Kataa dhambi ya uzinzi, ogopa dhambi ya uzinzi, ikimbie dhambi ya
uzinzi na usifanye dhambi ya uzinzi.
BWANA
YESU Anakupenda Sana Na Hataki Ukose Uzima Wa Milele Kwa Sababu Ya Hao Ndege
Wanaoruka Juu Ya Kichwa.
Ufunuo
21:8 '' Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na
wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa
liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.''
-Kumbe
katika watakaopelekwa jehanamu na wazinzi wamo.
-shetani
analeta kila mitindo ya mavazi na mapambo ili tu kuwanasa vijana katika dhambi
ya uasherati.
-Uzinzi
ni moja ya dhambi zinazowakosesha wengi.
-Nduguyangu,
uzinzi wa muda mfupi unaweza kukupeleka kabisa jehanamu kama hukupata nafasi ya
kutubu, na sio wote wanaopata nafasi ya kutubu na kugeuka.
-Uzinzi
na uasherati ni dhambi ving'ang'anizi na ndio maana shetani huitumia sana ili
kuwaangamiza maelfu ya vijana, uzinzi unamfanya shetani anapata nafasi ya
kukutawala.
ndugu
kupitia ujumbe huu nakuomba badilika. Na kama umeona imekuwa ngumu mweleze
mchungaji wako akusaidie na kukuombea maana wengi hadi wana majini mahaba.
Mithali
6:32-33 '' Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo
litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala
fedheha yake haitafutika. ''
-Mvulana
Leo Akimwambia Msichana "NAKUPENDA" Maana Yake Hasa Ni "
NATAMANI KITU, SIO WEWE MWENYEWE BALI KITU KUTOKA KWAKO, SIWEZI KUNGOJA, NATAKA
KUWA NACHO SASA HIVI, BILA KUCHELEWA. SI KITU NINI ITAKAYOTUKIA BAADAE.
NINAANGALIA WAKATI HUU, NINAYO HAJA KWAKO ILI KUZITULIZA TAMAA ZANGU, WEWE NI
CHOMBO TU CHA KUNIFIKISHA KWENYE SHABAHA YANGU, NATAKA KUWA NA WEWE MUDA
HUU"
Hiyo
Ndio Maana Ya Neno "Nakupenda" Kwa Maisha Ya Leo Kwa Vijana Wengi.
Maana Halisi Ya Kijana Kama Huyo Ni Hii "NINAJIPENDA MIMI MWENYEWE PEKE
YANGU TU, KWA SHABAHA HIYO NAMTUMIA MSICHANA KUKAMILISHA KUJIPENDA
KWANGU".
Wasichana
Wengi Nao Hujikuta Wakiingia Kwenye Upendo Huu Feki Na Kuingia Dhambini.
Ndugu
Zangu Tambueni Neno Hili Kwamba MUNGU Atawahukumu Adhabu Ya Jehanamu Wazinzi Na
Waasherati, Waebrania 13:4 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe
safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu. '',
BWANA
MUNGU Anawaonya Wanadamu Kila Leo Ili Waache Uovu Huu. Dhambi Hii Ndio
Ilisababisha Sodoma Na Gomora Kugeuka Matanuru Ya Moto Na Kuwateketeza Wanadamu
Wote Isipokuwa Lutu Na Familia Yake
1
Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili
wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. ''
Upendo
Wa Kweli Haukamiliki Isipokuwa Katika Ndoa Takatifu Mlioingia Bila Dhambi. Kwa
Hiyo Mvulana Asitaje Lile Neno Kubwa La Kusema "NAKUPENDA" Kwa
Msichana Asipokuwa Na Nia Ya Kufunga Nae Ndoa Tena Asiseme Neno Hilo Huku Akiwa
Na Mpango Wa Kufunga Ndoa Miaka 10 Ijayo Bali Miezi Kadhaa Ijayo.
Yakobo
4:4 ''Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa
MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa
MUNGU.''Wazinzi ni adui wa MUNGU, Ukianguka kwenye dhambi ya uasherati au
uzinzi kwa sababu tu ulidanganyika na neno ''nakupenda'' basi wewe unakuwa adui
wa MUNGU hadi utakapotubu.
Kijana
na kiume au wa kike tambua kwamba wewe ni wa thamani sana mbele za MUNGU, Tunza
uthamani wako na mwili wako bila kufanya uasherati.
Maombi
yangu MUNGU akupe kinga kwa kila hatari iliyo mbele yako, akupe baraka kwa kila
jambo jema unaloliwaza na kulipanga kwa ajili ya maisha yako ya baadae yakiwemo
maisha ya ndoa, BWANA akupe jibu katika ombi lako la kumpata mwenzi wa maisha
mwenye hofu ya MUNGU, BWANA YESU akupe tabasamu kwa kila chozi unalolia
ukimuomba akupe mme/mke mwema, akujalie afya njema, furaha,amani na upendo.
Nguvu ya MUNGU likasimame na wewe katika magumu unayopitia hadi ushindi wako na
maadui zako kuanzia walio ndani hadi walio nje kwa jina la YESU KRISTO
washindwe.
BWANA
YESU akuondoe kwenye maagano ya ukoo na mizimu yanayokuzuia kuoa au kuolewa.
MUNGU akawafunge waliokufunga,wawe mateka waliokufanya mateka,wateseke wao
waliokutesa,waliokufungia uchumi wafungwe wao.
Kwa
sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa
mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni
anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU
akubariki sana.
Ni
mimi ndugu yako
Peter
M Mabula
Maisha
ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU
akubariki sana uliyesoma somo hili.
Barikiwa kwa fundisho zuri lenye kubariki
JibuFuta