Kutunza ujana, ndoa, uzee au wokovu wako ni wajibu wa mtu
mwenyewe. Ni kweli Mungu anatutunza na anayosememu kubwa katika kila
rika la maisha yetu; lakini amempa mwanadamu ufahamu na utashi na anao wajibu
wa kufanya ili kujitunza.
Ili kuutunza ujana wako ni lazima ujue na uyazingatie mambo
muhimu yafuatayo:
1. NIZIJUE
CHANGAMOTO ZINAZO KABILI KIJANA.
i) Kwenda na Wakati–Biblia
inaagiza kuukomboa wakati-Waefeso 5:15-16 Ni changamoto
kwetu na ni fursa kutumia nguvu ya msalama kuishinda
hii
kawaida ya Dunia hususani vijana kuvutwa katika kwenda na
wakati. Kijana huvutwa na kushawishika kwenda sawa na wakati katika
maeneo mengi. Kijana anavutwa na kuvaa, kusuka, kunyoa, kutembea,
kusema, kutenda sawa na wakati, hata kumiliki vitu vinavyoendana na kuendana na
wakati. Dunia inavyotuvuta katika kwenda na wakati, Biblia inatuagiza kuukomboa
wakati. Kuukomboa wakati ni kutumia vizuri wakati tuliopewa kama
fursa ya pekee. Wakati wa Ujana ni wa kuwekeza vitu vya rohoni na mwili,
komboa wakati.
a) Komboa wakati Ki-Elimu: Usipoteze
wakati kwa mambo yasiyokuhusu, mfano kijana mwanafunzi Soma kwa bidii ni wakati
wake, siku ikiisha jiulize umeongeza nini ki-elimu? Usiishi kiholeholela tu
fursa hiyo inapita.
b) Komboa wakati Ki-Uchumi: Usipoteze
wakati kwa matumizi ya kipuuzi, fasheni za mavazi, mitindo ya nywele, hata
kijiko huna, wewe unavaa tu. Komboa wakati ukijua kuna kuoa na kuolewa lazima
ujipange mapema. Siku ikiisha, wiki, mwezi, mwaka Jiulize umeongeza nini
kiuchumi? Kumbuka kuna miaka saba ya shibe na miaka saba ya njaa lazima
uishi kwa adabu/hekima, siku zijazo huna nguvu ya kuwekeza kama UJANANI.
c) Komboa wakati
Kiroho: Usipoteze wakati Kiroho, tumia fursa hii vizuri. Siku inapoisha,
wiki, mwezi, mwaka, kijana jiulize umeongeza nini Kiroho. Umeongeza
nini ufahamu katika Neno la Mungu, Umeongeza nini Maombi, Umeongeza nini
utumishi wako wakati huu una nguvu, usiishi kiholela. Wekeza vitu vya Ki-Mungu
ndani yako, funga na kuomba, soma neno, tumika kadri uwezavyo. Ukifika uhitaji
yamkini hata huwezi kuomba sana unaakiba ya kutosha ya Maombi/Neno la kusimamia
kupita kipindi hicho.
d) Komboa wakati-tumia vizuri fursa ya
kuwa kijana - 1Nyakat 12:32 Kwa kufanya mambo yakupasayo kufanya wakati
huu (ujanani) kila eneo. Wakati ujao ukifika hata ukitaka
kurudidarasani akili haitunzi tena kumbukumbu kama leo na majukum
yataongezeka, ukitaka kubeba zege huwezi huna nguvu kama leo, Kiroho
vivyo hivyo, ukisoma Neno ufahamu unachoka haraka, kufunga huwezi
tena. Uwe na akili zijue nyakati.
ii) Tamaa za Ujanani – 2Tim 2:22, Mith
27:2, 1Kor 6:18a, Wimbo 3:5
Ni changamoto kwetu na ni fursa kuonesha nguvu ya msalaba
kutiisha mwili.
Kijana anavutwa sana na tamaa za ujanani na hizi zinamkumba
kijana si kwa sababu hayuko kiroho hapana, zinamkumba kwa vile ni
kijana. Changamoto hii tunaipata wote, vijana waliookoka na
wasiookoka ila tofauti yetu ni katika kuzi-hundle Kijana aliyeokoka anazitiisha
na asiyeokoka anazitii tamaa hizi.
Biblia imetaja moja kwa moja kuwa ni tamaa za ujanani na
zinawakumba vijana wote na lazima kuzitiisha zisubiri wakati [NDOA].
NI MUHIMU KUYAJUA,
KUYAELEWA NA KUZINGATIA MAMBO 4 YAFUATAYO: -
a) Uhai wa milango ya fahamu kwa
kijana ni tofauti na rika nyinginezo.
Milango ya fahamu ni Macho, Maskio, Pua, Mdomo, Ngozi-inauhai
[active].
b) Uhai wa hisia za mwili kwa kijana
ni tofauti na rika nyingine. Unatokana na mabadiliko ya mwili yaliwekwa na
Mungu mwenyewe.
c) Upo Uhusiano wa karibu kati
ya Hisia za mwili wa kijana na Tamaa za ujanani, hili lazima kijana alijue ili ajilinde.
d) a, b, na c hapo juu,
zinatusaidia kujua sababu ya Mungu kutuagiza watu Kukimbia tamaa za
Ujanani, tusichochee mapenzi mpaka Ndoa.
iii) Inaagiza kwa msisitizo kusema zikimbieni
tamaa za ujanani/mwili. Tumeongea na vijana wengi walioanguka hawakupanga
kuzini. Ila wamezembea katika kulitii Neno la Mungu badala ya kukimbia wao
wanakaa, wanaleta hoja, wanakemea, wanaomba, wanapinga mwisho wa siku
wanajikuta chini, kwa ukaidi wao kwa Neno la Mungu. Biblia haikushindwa kusema
kemea, ombea, pinga ila imesema KIMBIA.
iv) Usichochee mapenzi, usizichochee hisia za
mwili/matakwa ya
mwili.
v) Milango ya fahamu ikichochewa
inazalishahisia katika mwili;
vi) Hisia/Msisimko wa Mwili wa kijana
ukichochewa unazalisha uhitaji;
vii) Uhitaji wa Kimapenzi ukichochewa
unazalishaTamaa za Mwili;
j) Tamaa za Mwili/Ujanani zenye msukumo mkali
kutaka kukidhi uhitaji zikichochewa zinalet anguko, mauti; Kijana hatua hii
hakumbuki wokovu, huduma, aibu, magonjwa yanayotokana na zinaa-Kaswende,
kisonono wala Ukimwi. Hakumbuki mimba au watoto wasiotarajiwa. Anahaha kutaka
kukidhi uhitaji wa mfalme/malkia wake tu, ni hatari.
k) Mauti inazaliwa kutokana na Tamaa
iliyopembejewa na Kijana. Kuna Kijana alizilea hatua tulizojifunza hapo juu,
hakuchukua hatua za Kiroho kuutiisha mwili akajikuta anabaka-wadada na wakaka
wote wanabaka japo hapo tunamuona kaka amebaka – 2SAMWELI 13:1-22. Biblia
inasema wazi unaingamiza nafsi yako mwenyewe-Mithali 6:32.
Kuyalea na Kuyachekea mambo hayo juu ndipo unaskia anguko,
Kijana anayeheshimiwa na Mungu na watu anajikuta amezini. Unapokosa subra
na kuparamia unalala na mke au mume wa mtu kiuumbaji. Kimsingi kila mtu
ameumbiwa mume au mke wake – Mwanzo 2:22.
iii) Vichocheo vya mapenzi/tamaa za ujanani/tamaa za
mwili
Ni changamoto ya tatu inayotukabili vijana na lazima
tuishinde ili tusalimike. Ni muhimu kujua vichocheo vya mapenzi/tamaa za mwili
ili kuviepuka. Nisipojuavichocheo hivi si kiroho bali
ni ujinga unaotishia usalama wangu.
Vichocheo vifuatavyo huyaamsha mapenzi, huchochea tamaa za mwili:
-
a) Kuzitafakari/kusikilizia hisia za
mwili-Inahusisha ufahamu wenyewe
Biblia imetuagiza tuyatafakari yaliyo juu-Wafilip 4:8. Mungu
alijua tukiyatafakari ya chini yakiwemo tamaa za mwili tutachochea mapenzi.
i) Usijiulize maswali ya kipuuzi mf. ‘Hivi, tafika
kuoa au kuolewa bila kuonja? Wenzio walioonja wamekuwa watumwa wa dhambi hiyo
kujitoa ni gharama kubwa wengi wameshindwa kuilipa, usiwaze kuonja hadi NDOA.
ii) Baridi imezidi/Upweke jamani niko peke yangu.
Ulitaka uwe na nani? Haya ni majira ya Bwana yenye kusudi timilifu uwe peke
yako, wakati wa kuwa 2 na 12 watakapokuja hao wa kike na wa kiume-utakuja tu,
vumilia.
b) Kusoma makala za mapenzi [makala za
Internet, magazeti, vipeperushi, vitabu]-inahusisha macho yanayosoma makala.
·
Unashangaa
binti au kaka anasoma vitabu vya tendo la ndoa/Mapenzi.
·
Internet
Café anaenda kutazama mambo ya Ngono/Mapenzi. n.k.
Kijana huyu atakuwa salama kweli au ndio hao mwisho anabaka
mtu.
c) Kutazama mambo ya ngono au
yanayohusu ngono-inahusisha macho.
Mikanda ya x, sinema za x, picha za x hasa kwa internet na
hata ‘live’ kuna watu wanapenda kuchungulia sehemu zenye upenyo wa kufanya
hivyo. Raha yake aone tu utupu wa watu na mchezo unavyokwenda,
atapona?
d) Kushika au kushikana/kugusana-inahusisha
ngozi-Wakolosai 2:21.
·
Mkono
unaganda dk.5 dada na kaka wanasalimiana salamu yetu.
Mkono wako una chapa ya Yesu usiruhusu kujinajisi kwa kutii
mwili.
·
Vidole
vinaongea kwa kupapasa au kubonyeza au kutekenya ni uchochezi.
Vidole vyako vinachapa ya Yesu, usiruhusu kujinajisi kwa
mambo hayo.
·
Tongue Kiss/Denda
ni hatari wala mtu asijifariji kuwa salama-usionje.
Ulimi wako unachapa ya Yesu usionje uchafu [mate] subiri Ndoa
utanyonya mpaka uchoke ukitaka maana utakuwa huru katika hayo si leo.
·
Ngozi
ikiskia umeshika/kwa, unapapasa/swa, umekula denda, lazima itashtuka na
kuleta hisia ya kuvutwa katika ngono kwavile wewe ni kijana. Usiidhalilishe
Chapa ya damu ya Yesu uliogongwa siku ulipookoka, itunze.
e) Kusikiliza mambo/maneno ya
ngono au yanayohusu ngono-sikio.
Sikio lako linachapa ya Yesu usilisikizishe uchafu wowote-ni
kichocheo.
Kusikia ni sikio kupata jambo bila kukusudia lakin kusikiliza
ni kukusudia. Hata kama sikio limenasa uchafu kwa bahati mbaya hakikisha
unalitoa.
f) Kuongea mambo ya ngono
au yanayohusu ngono-inahusisha mdomo.
·
Mazungumzo
ya Mdomo ni hatari-Mithali 6:26; 7:16-18,21. Iko nguvu katika
midomo/maneno. Biblia inasema Maneno huzaa uhitaji na sura hiyo hiyo ya 6,
inashauri jiepushe na midomo ya malaya; Kwa maneno alimshinda-si kwa mtutu, si
kwa ‘hug’ wala busu ni maneno tu na akamshinda. Usiruhusu kupokea maneno hata
ya mzaha kuhusu ngono.
·
Mawasiliano
katika Simu ni vema kuangalia sana unavyoenenda.
Idadi ya “Call au Sms” mfano kutwa mara tatu unampokea
Fulani.
Simu inazidi ‘dose’ ya Panadol kutwa mara tatu yeye mara tano.!!
Muda wa “Call au Sms” mfano usiku sana au alfajiri ni
kichocheo.
Usiruhusu Simu za usiku wa manane/alfajiri hata kwa manadai
ya kuamsha ktk maombi kwa muda huo ataamsha na vingine si maombi tena!
Sauti ya “Call” kuna sauti za uchochezi mfano kulegeza,
kuguna, kutetemesha sauti, sauti kama analia na nyinginezo kwa kijana utajua
tu.
·
Mazungumzo
“Simu au Sms” yakihusu ngono ni uchochezi sana.
Mambo hayo juu hata kama mtu hajaweka neno la
kimapenzi/kimahaba ni kichocheo, Je, mazungumzo yenyewe hayo ni hatari
zaidi mara 100.
Biblia inaonya mazungumzo mabaya yanaharibu tabia njema-1Kor
15:33.
Mfano: Naskia baridi njoo basi unipe joto,
wewe umekuwa ‘heater’?
Najiona mpweke ‘lonelyness’ afadhali uje hapa
nichangamke. Kweli wewe una Baba, Mwana na Roho Mtakatifu bado mpweke?
Ukiyachekea hayo, hutaki kuyakemea, anaongeza ‘dose’ sasa
utaambiwa wazi zaidi ‘nina nyege, ni wewe wa kutoa nyege zangu’
g) Zawadi ni moja kati ya vichocheo
vya mapenzi kwa namna hii.
·
Size
ya zawadi - Ukubwa, zawadi ya thamani
kubwa. Itaua msimamo.
·
Idadi
ya zawadi - Wingi vitu
tele unapokea au mara nyingi-utalipa tu.
·
Aina
ya zawadi - Kitu gani unapokea-chupi? Zawadi
hiyo itaongea tu.
Msimamo wa Semina hii ni USITOE NA USIPOKEE ZAWADI. Tunaishi zama za uovu,
usanii na malaghai mpaka Kanisani wa kike/kiume wao wanajua kuipaka asali
nia yao ili usishtuke mapema mpaka umefika chini, zawadi ni chambo kukunasa
we. Hutaki Kanuni hii yatakayo kupata usilie.
Wachumba: Vijana hawa wako huru kutoa/kupokea zawadi ila
Kanuni ni hizo hizo hapo juu. Uchumba si Ndoa muda huo bado unaendelea
kumthibitisha Mungu, usijeishia njianiukalilia mtu na vitu vyako.
h) Picha na Mikao ya Picha kwa jinsia
mbili ni Kichocheo cha Mapenzi.
·
Picha
za nusu uchi eg. Kifua/Tumbo/Mapaja wazi au chupi/sidiri tu.
·
Picha
za utupu [mwili wote], picha hii hana nguo hata moja-ni kichocheo.
·
Picha
na Mikao yake inavunja miiko ya jinsi ya kuenenda Vijana waaminio.
‘Pouse’ la Kushikana Mabegani, Kushikana Viuno, Kushikana
Kifua mtu anajikuta ameshika matiti katika pouse la picha, Kushikana Makalio,
Kubusiana Shavu au Mdomo, Kupakatana/Kukumbatiana ni KICHOCHEO. Kijana
usikubali Kuidhalilisha Chapa ya Yesu kwa Pouse la Picha.
i) Mavazi ya Vijana wa
Kike na Kiume yanavyokuwa Kichocheo.
·
Mavazi
ya Kuonesha Nguo za Ndani-Milegezo, Vifungo wazi, Mipasuo n.k.
·
Mavazi
ya Kuonesha Maungo/Maumbile-Kubana sana inachora umbile, Kuangaza [transparent]
inaonesha viungo vyote japo kavaa, ni vichocheo.
·
Mavazi
ya Kutositiri Mwili-Nguo fupi-pensi/bukta/skert/gauni/blaus, Nguo hizi huacha
Kifua wazi, matiti nje, Kitovu nje, Tumbo nje, Kiuno nje, Kwapa nje-ndio
unakuta kijana haabudu anachungulia titi kupitia kwapa.
·
Ni
maombi yetu mavazi hayo yasivaliwe nawe unayesoma makala hii. Ni maombi
yetu uushinde mwili, endapo utakutana na mavazi hayo kazini, shuleni,
kwenye daladala, barabarani, dukani, sokoni na hata Kanisani kwa Waongofu Wapya
au Wakongwe wenye mitazamo tofauti. Utaona hatuwezi kuepuka hili moja kwa moja
kwa jamii yetu ila tumejifunza ili ukiona mavazi hayousi-‘take advantage’,
usikodolee macho mpaka mate yanatoka huna habari ni hatari kwa afya
yako, epuka.
j) Mazingira
hatarishi/njia kuu ni Kichocheo - Mithali 7:7-13a, 21-23.
Njia Kuu ni mahali pa Kificho, Gizani, Uchochoroni, Chumbani,
Ufukweni, Kuwepo wawili tu mnataka kufa maana mazingira tu ni kichocheo tosha.
Kabla ya kugusana, mabusu, zawadi, mazungumzo vyote hivyo
bado, ile kuwa wawili tu maeneo hayo ni kichocheo tosha na kinaongea kwa kasi.
Kijana mmoja mjinga yeye alizubaazubaa NJIA KUU yaliyomkuta
ni balaa.
Tunapomalizia kichocheo cha 10 cha mapenzi hebu tusome andiko
hilo.
Kijana huyu alitembea muda hatarishi kwa kijana, akakaa
mahali hatarishi, akakutana na mtu hatarishi [kahaba], akaambiwa maneno
hatarishi, akanaswa. Mithali 6; inatoaushauri kuwa jiepushe na maneno ya Malaya
n.k. ndipo sura ya 7; inaonesha kwa maneno ya ubembelezi tu kahaba akamshinda
Kijana kiulaini kabisa akaongoza njia kama Ng’ombe aendavyo machinjioni uhitaji
umeshapamba moto, mfalme amesimamisha majeshi hayarudi chini, anaona nikidhi tu
uhitaji wa mfalme nisalimike, kumbe maskini anaiangamiza nafsi yake ya
thamani-Marko 8:34-35.
Tunaishi zama za uovu makahaba wa kike/kiume wapo Kanisani
pia. Makahaba hupenda NJIA KUU soma Ezekiel 16:22-26. Ni
mahodari wa ubembelezi, kwa kiroho cha kusuasua cha kutozingatia mipaka ya
uhuru wetu, hutoki, utalainika mwenyewe na utajikuta unaongoza njia kama kijana
mjinga. Epuka mazingira hatarishi, kuna kisa kilitokea Kanisani mkesha wa
Vijana wa Maombi ya masaa 48. Kaka kamfata dada anamwambia “nina nyege na wewe
ndio wa kutoa nyege zangu” Ikiwa mkesha wa maombi kuna watu wanamawazo hayo,
je, huko njia kuu?
Umejua vichocheo 10, usichochee. Ukifanya uzembe umenaswa
hatua No.1 Mlango wa fahamu umepokea taarifa-Itoe mapema, ikiwa uko hatua No.2
ya hisia/msisimko wa mwili pambana-usipembejee, kama ni hatua No.3 ya uhitaji
usimridhie mfalme/malkia tiisha hali hiyo, usifikie hatua No.4 ya kuwaka
tamaa ni mbaya sana inapelekea hatua No.5 ya MAUTI.
2. NIJUE JINSI YA KUZIKABILI
CHANGAMOTO KWA MUJIBU WA BIBLIA
Tumeona Changamoto 3 katika Somo hili, Kwenda na
Wakati, Tamaa za Ujanani na Vichocheo. Hizi ni changamoto kali
kwetu ukitumia akili utachemsha. Ufuatao ni muongozo kidogo tu wa kukabiliana
na Changamoto hizo kwa mujibu wa Biblia:
i) Maombi-Uwe na maisha ya
maombi, ombea ujana wako siku zote-Luk 18:1;
Tabia ng’ang’anizi Funga na Kuomba na utapata upako wa
kuutiisha mwili.
ii) Neno la Mungu likae kwa wingi
ndani yako ili usafishe njia zako-Zab 119:9.
iii) Nikubali na niamue kwa dhati kuusulubisha
mwili/kuunyima matakwa yake.
·
Utu
wa kale ni wakati mwili ulipokuwa na nguvu, ukiokoka-Rum 6:6;12:1
Kama utu wa kale unakung’ang’ani jichunguze pengine hujauvua
vizuri- funga na kuomba utoke-Math 17:21. Umvae Kristo-Rumi 13:13-14.
·
Kuishi
kinyume na mwili na tamaa zake na mawazo yake-Galatia 5:24.
·
Paulo
aliamua kutesa mwili, wewe na mimi je? 1Kor
9:27; Marko 8:34-35;
Ukitaka kuiponya nafsi ati mwili unahaha, mfalme amesimamisha
majeshi au malkia anahaha acha niiponye nafsi yangu kwa kukidhi uhitaji huu,
maskini unaingamiza nafsi yako wala huiponyi kama unavyodhani. Na ukiamua
kuiangamiza nafsi yako kwa ajili ya Kristo UNAIPONYA. AMEN.
iv) Nijitenge na ubaya wa kila namna yaani ubaya
wote-1Thesalonike 5:22.
Tangu mwanzo wa somo hili tumeutaja ubaya mwingi tu na
tumeujua EPUKA.
·
Kujiepusha
na marafiki wabaya iwe waaminio/wasioamini-2Kor 6:14-18.
·
Kujiepusha
na mazungumzo–Mith 18:7;1Tim 5:20;1Kor 15:33; Kol2:20-21.
·
Kujiepusha
na Elimu na Hekima ya Ulimwengu huu ambayo ni upuuzi kwa Mungu-Efeso 4:13-14;
Rumi 16:19 2Tim 2:11-22; 2Kor 10:5; Yakobo 3:17.
Elimu ya jumla ni nyingi moja wapo ni huwezi kuokoka duniani.
Elimu ya Kristo inasema wazi watakatifu walipo Duniani ndio waliobora-Zab 16:3.
Elimu iliyotawala ulimwengu huu inayogusa vijana na baadhi wa
Kanisani wameipokea na kuiamini, maana yake hawaamini nguvu ya msalaba ni: -
Huwezi kuishi KIJANA mwenye afya bila kufanya mapenzi kabla
ya ndoa!!
Huwezi kuoa au kuolewa BIKRA kwa karne hii ‘Mary type’ hakuna
leo!!!
Vijana wamepokea Elimu ya Kwanza ikazalisha Elimu ya Pili,
ona juu. -Shetani anajua wakipokea tu Elimu hizi na kuziamini zitawakatilia
mbali. -Watakata tamaa ya kujitunza kwamba sawa na bure, na wengi wamenasa.
-Kumpata Bikra mwenzio huwezi, bora na wewe jichanganye; wamenasa. -Kufika
hadi Ndoa ukiwa BIKRA haiwezekan ananesha vichocheo, ananasa. Kwa nini
ung’ang’ane na Elimu ya Dunia na kuamini na wewe si wa dunia?
Elimu ya Kristo iliyosema yasiyowezekana kwa wanadamu kwa
Mungu yote yanawezekana mbona hiyo huiamini na kuitumia ili ukaishi.
Elimu ya Kristo iliyosema mwili si kwa zinaa pia siijui-1Kor
6:13.
Nikijawa na Neno la Mungu [Elimu ya Kristo] nitashinda-Zab
119:10.
v) Nijue kuwa niliumbwa Kutenda Mema
nisijifariji kuutii mwili/elimu-Efes 2:10
Kwa vile niliumbiwa utakatifu Biblia inanitarajia nijizuie
-1Kor 9:25.
vi) Mtazamo wa Mungu kwangu Kijana ni tofauti
kabisa na ninavyodhani.
·
Rika
ya ujana natarajiwa kumkumbuka/kumuabudu Mungu Mhubiri 12:1.
·
Nizo
nguvu si za ugali na maharage bali za kumshinda muovu-1Yoh 2:13-14.
·
Kwanini
Mbingu zinaona kijana nina nguvu na nimemshinda muovu?
·
Ninauwezo
wa Kufunga siku nyingi, kuomba kwa muda mrefu bila kuchoka,
·
Kusoma/kujifunza
na kutafakari Neno la Mungu na kuliweka moyoni,
·
Kutumika
kwa nguvu zangu zote hata sina muda wa kupoteza ila kukomboa.
·
Nguvu
za Kiroho zinapatikana katika hayo hapo juu, adui atakupataje?
Nguvu za
Kiroho zinakusaidia kuushinda mwili, changamoto, dunia n.k.
Nguvu za
Kiroho zinakuweka karibu na Mungu na adui lazima akukimbie
Nguvu za
Kiroho zinakupa ufahamu wa kumjua Mungu na Neno lake.
Nguvu
za Kiroho zinanipa uwezo wa kumuamini Mungu si wanadamu.
Nguvu
katika Roho Mtakatifu na kuwa chini ya uongozi wa Mungu.
Nawaandikia ninyi vijana kwasababu mnazo nguvu, hata
nguvu za kimwili tulizopewa pamoja na kutusaidia kiuchumi, elimu pia zipo
kutusaidia kupata nguvu za Kiroho. Kijana usile mwaka mzima funga, omba kwa
afya Kiroho/mwili.
Tangu siku za Yohana Mbatizaj Ufalme wa Mungu unapatikana…. Math
11:12.
Ili upate vitu vya Ufalme wa Mungu lazima uwe na Nguvu si
kilegelege hivyo.
Ili kuteka kitu lazima umfunge mwenye nguvu, na ufalme ni
hivyo kama mwili unanguvu utiishwe, hekima za dunia zitiishwe ili uteke vya
ufalme-Math 12:29.
Ili uje upate mke/mume mwema aliyejaa nguvu hizo lazima uwe
na nguvu.
Ili upate Baraka za Ki-Mungu hata kwa maisha ya kimwili
lazima uwe na nguvu.
Kwahivyo, unahitaji nguvu ili kuutunza Ujana wako si kwa
ulegelege. Nikizembea katika kutafuta nguvu nikajikuta nimezini yapo MADHARA
yake.
3.ZIJUE BAADHI YA MADHARA [20] YA KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA
i) Kumtenda Mungu dhambi
[Yusufu]–Mwanzo 39:6-9; Rumi 8:6-8; 1Kor 6:15-20.
ii) Kuharibu ushuhuda [Wokovu
unatukanwa] – [aibu] Mithali 6: 32 – 33.
iii) Kufungua Mlango wa mapepo/kupokea maroho ya
unayezini nae – 1Kor 6:16.
iv) Kuishi na Hatia Moyoni hasa dhambi isipotubiwa
– [fedheha] Mithali 6:32-33.
v) Kuishi na Majuto maishani maana
kumbukumbu haifutiki – 1Kor 6:18 – 20. Dhambi hii inafanyika juu ya mwili wako
ndio maana haifutiki. Toba ya Kweli Mungu atasamehe na kusahau-Ebrania 8:12,
lakini wewe hutosahau kamwe.
vi) Kujichukia na Kumchukia sana mtu uliyeanguka
naye, misisimko yote itaisha-2Samweli 13:1-22. Kuna kisa cha kusikitisha cha
Kijana Amnoni na Tamari.
vii) Kuwa hatarini kuingia katika
anguko tena-kwa mwili kudai haki yake kwa
Kasi maana umechokozwa. Utaingiwa na roho ya
kutoshiba-Ezekiel 16:28-30a.
viii) Kuua nguvu ya kujizuia, kuudhibiti na kuuweza
mwili- 1Kor 6:13; 9:25. Ndipo mambo ya kuchua/kupiga punyeto [masterbation]
yanapoingia Kanisani, malkia na wafalme bandia wanaponunuliwa na vijana kwa
matumizi machafu. Kuchua, kutumia malkia/wafalme bandia ni ukahaba
tosha-Ezekiel 16:15-17.
ix) Kuwaumiza wazazi wako na Kanisa la Mungu wewe
ni kiungo – 1Kor 12:12-26. Tunaudhaifu katika mapambano maana kiungo wewe
umejeruhiwa na nafasi yako inaupungufu, pia tunaposimama kama Kanisa unatutia
doa/dosari.
x) Kutoaminika kwa Mungu,
Wazazi, Kanisa na Kutojiamini-Maombolezo 1:8a.
xi) Kupata Mimba/Watoto wasiotarajiwa; wote
kaka/dada mnapata mimba/watot. Ni aibu sana ukiwa Kanisani
kupata/kutia mimba/watoto wasiotarajiwa.
xii) Kupata magonjwa ya Zinaa
Kaswende, Kisonono, Gonoria, Ukimwi n.k.
Ni aibu kijana wa Kanisani kupata magonjwa ya
zinaa akiwa Kanisani.
xiii) Kuua ndoto zako. Ukishapata
mimba/mtoto/ukimwi ndoto zinaishia hapo.
Ndoto ya wengi ni kuoa au kuolewa akiwa bikra,
asilale na mtu kabla ya ndoa.
Utaiua ndoto hii nzuri ya Ki-Mungu inayotaka kila mtu awe na
mke/mume wake mwenyewe 1Wakor 7:2; Ilikusudiwa hivyo tangu awali-Efeso 2:10.
xiv) Kulipa gharama kubwa ya kurudi katika nafasi
yako kiroho na kimwili pia.
Kihuduma kurudisha viwango ni gharama kubwa, masomo kuanza
tena ni gharama kubwa, kwa wazazi/jamii kukupokea kama mwanzo ni ngumu. Na
BIKRA hiyo ndio utalipa gharama ya kukubali matokeo maana hairudi si kwa kijana
wa kiume au wa kike uki-unsealed hakuna muujiza wa ‘resealed’.
xv) Kuchakaza maumbile yako wavulana/wasichana–Wimbo Bora
8:8,9,10.
Malkia-uke unaukuta[bikra] kwa kulala na mvulana tu
ukuta unaondoka-8:8.
Ukuta ukitunzwa hadi ndoa ni heshima na furaha kwa Wazazi na
Kanisa-8:9.
Ukuta ukitunzwa hadi ndoa ni heshima na kibali cha ziada kwa
‘mr’ wako-8:10.
Inatisha sana ukuta kuondoshwa binti akiwa ameokoka na yupo
Kanisani. Dada ambaye umeokoka huna UKUTA utunze UKUTA wa Roho
Mtakatifu sasa. Na endapo utaolewa ukiwa umejitunza kwa jinsi hii kwa maumbile
ya uke ‘mr’ wako atajua umejitunza hata kama UKUTA haupo. Miaka yako
katika WOKOVU ifanane na hali halisi ya Malkia wako. Sio Miaka 5 ya
Wokovu lakini Malkia anaonesha ni Muongofu Mpya wamiezi 5 tu ya baada ya
kuchumbiwa-AIBU!
Mfalme-uume unaharibiwa na wanawake/kupata jeraha-Mith
31:3; 6:32-33.
Kibinaadamu wakaka wanadhani wako salama kwa vile hawana alama ya wazi.
Ki-Mungu Biblia inaonesha wazi kuwa wafalme wanaharibiwa na wanawake na kuna
jeraha lisilofutika na kuvunjiwa heshima kwa kaka aliyezini. Kaka anatoka akili
kila anavyozini na alama Mungu aliyoiweka kwa
mfalme used haifutiki. Mungu anatutaka wote wakaka
na wadada tuwe BIKRA na INAWEZEKANA. Maswali ya wewe mzima yaulizwe kote kote
si kwa dada tu. Biblia imetoa ‘Gender Balance’ juu ya hili na kuonesha madhara
na matokeo ya kaka kuzini >Kutoka akili – aziniye na mwanamke hana akili
kabisa, anaingamiza nafsi. >Jeraha na fedheha haitofutika – Mithali 6:32-33;
20 – 26; 7:1-15; 21-23. >Haifutiki moyoni maana hufanyika juu ya mwili wako
wote – 1 Kor 6:18 – 20. >Ni kweli kuwa kwa toba ya kweli Mungu
atasamehe/atasahau-Ebrania 8:12. >Wewe hutosahau kamwe tendo hilo hata kama
ni dk 5 tu, maana linahusisha >>Moyo wako wote, Akili zako zote, Nguvu
zako zote na Mwili wako wote. Na Inasikitisha kijana kuanza ngono
akiwa tayari ameokoka na yupo Kanisani.
Nakupa pole unayejifariji kufanya dhambi hii ukidhani
hawapo tena MABIKRA. Dhana hiyo haikuanza leo tangu waandishi wa makala hii
tukiwa ‘single’ dhana ilivuma hawapo mabikra kumbe tupo na tukaoana tukiwa
BIKRA kaka na dada. Na tumekutana na wanandoa wengi waliooana wakiwa BIKRA kaka
na dada. Mabikra hawatakoma katika nchi maana katika kila jambo la Ki-Mungu
masalia wataendelea kuwepo hata uovu uzidi sana. Kaka kuwa
wa Kwanza kwa DADA na Dada kuwa wa Kwanza kwa
kaka SIKU YA NDOA ni Jambo la Ki-Mungu. Ni Muhimu kuishi maisha ya
uaminifu kamwe usijifariji kwa dhana hiyo potofu.
Ni wote tunapaswa kujilinda na kujitunza hadi NDOA –
Mithali 5:1-5; 9:13-16. Sio Malkia watunzwe, Wafalme waharibiwe hakuna fundisho
hilo katika Biblia. Dhambi ni dhambi kwa wote, misisimko ya mwili ni wote,
uzembe wa kuutii mwili badala ya kuutiisha mnafanya wote, kwanini BIKRA awe
dada tu? Tunatamani tunapomaliza kipengele hiki cha kuchakaza
maumbile ufunguke. Usiulize maswali ya upuuzi kwa mchumba wako, “Vipi dada wewe
ni mzima” nawewe je, kaka ni mzima? Au unataka kuvuna usipopanda? Hakuna Kanuni
hiyo kwenye Biblia-Wagalatia 6:7; Wakolosai 3:25. Umeondosha kuta za wasichana
tele tena mpaka upo Kanisani, inafika kuoa unataka mzima atoke wapi? Kuna
wenzio kuliko wewe ulipoondosha kuta 5 wao wameondosha 15. Ukipata
mchumba/mke mzima ni neema tu usiifanye ni Kanuni ya
kusimamia. Ikiwa umeomba na umempenda kwa dhati maswali yanatoka
wapi? Upendo hustiri wingi dhambi 1Pet 4:8, Upendo una adabu-1Kor 13:5. Upendo
wako vipi?
Mkazo huu ukuguse moyoni kaka/dada bikra muendelee
kujitunza, uthamani wa Ubikra wako ni mtaji mkubwa kwa hatima yako ni zaidi ya
fedha/dhahabu. Mungu amekuokoa, amekuwahiUSIICHEZEE NEEMA HIYO wengi
wanaililia, jiombee sana huku ukizingatia yale mambo ya mwanzo wa somo ili
kujilinda.
xvi) Kaka
kupoteza mbegu za uzazi-unatoa wakati sio, kwa mtu siye, mahali sio.
Dada naye anapokea
mbegu za uzazi-wakati sio, kwa mtu siye, mahali sio.
Wakati muafaka ni
Ndoa, mtu sahihi ni Mwenzi wako, uchochoro huo sio.
xvii) Kaka/Dada
wote kupoteza nguvu kwa kutumia kwa ngono hiyo-Mith 31:31
Nguvu ambayo
ingetumika kwenda kushuhudia inatumika katika ngono.
xviii) Dhambi hii
ikilelewa na kijana mwisho hupelekea kutamani wake/waume
za watu. Kawaida ya uovu unakua, hukuweza kumuogopa Mungu na
ukafanya ngono na wanafunzi wenzio Sekondari au vijana wenzio wadogo Kanisani
mwisho unaona wake/waume za watu wote sawa tu na hao. Kijana unaanza
kumendea wake/waume za watu kwa kutotunza ujana wak.
Biblia imeonya vikali hapa, usidhani uko salama ni
hatari-Mith 6:27-29. Inaonesha kuwa makali ya moto yatakuwa kifuani mwako,
hauko salama. Wengin sawa na baba/mama yako unapata laana kuona
utupu-Walawi 18:7
Vijana wengine huona ni bahati kuwa na mke/mume wa mtu hiyo
ni balaa, nuksi, mkosi huo, kwanini uone sawa ku-share na mtu? Walawi 18:16;20.
xix) Madhara ya Dhambi hii kwa Kijana hata
akiingia katika Ndoa ni:
·
Dada
atapata aibu kwani mumewe atajua kuwa hukutulia Kanisani alitulia siku chache
karibu na kuolewa na pengine akawa na mimba isiyo ya ‘mr’.
·
Dada
kutoaminiwa na mumewe na kuishi kwa mashaka katika Ndoa.
·
Kaka
naye ikibainika hakutulia Kanisani mkewe hatomuamini ni hatari.
·
Mume/Mke
kuua nguvu ya mguso wa upendo wa mvuto kwa T. Ndoa.
·
Kwa
kuwa amezoea ku-sex na malkia/wafalme wengine Kanisani/nje.
xx) Kufungua Mlango wa Adui kukuhubiri nani
zaidi kati ya mafataki na ndoa.
Kuvutwa kumbukumbu ya ‘sex’ ya kabla ya Ndoa kupambanishwa na
ndani ya Ndoa. Ni rahisi sana kugundua nani zaidi kwa vile Tendo ni
lile lile ila tofauti ni kabla ya Ndoa ni HARAMU na Ndani ya Ndoa ni HALALI.
Sasa ukizoea dhambi hii Kanisani tena kwa siri, hakuna toba ya kweli,
haujatengwa iabishwe, haijulikani kwetu ila mwili wako unajua ni HATARI.
Unaweza kuoa/kuolewa na mume mzuri/mke mzuri tu lakini tatizo
likawa hakidhi uhitaji wa kimapenzi kwa namna ya mwili wako ulivyouzoesha kabla
ya kuoa/kuolewa hili tayari ni tatizo kubwa linalotikisa NDOA.
Tunapomalizia madhara hayo ishirini [20] kati ya mengi ya
kufanya mapenzi kabla ya Ndoa; tunakusihi wewe
ambaye hujaguswa na hujagusaUsijaribu na mwenye Ukuta wa
Roho MtakatifuUsitende dhambi tena. Wote tuipate THAWABU ya wanaovumilia
hadi mwisho-Mathayo 24:13.
4. HITIMISHO
i) Ishi ukijua kuwa
umekufa kwa dhambi unaishi kwa roho-Warumi 8:5-10;
Na ukiishi kwa roho hautazitimiza kamwe tamaa za
mwili/ujanani-Gala 5:16.
ii) Ishi kwa tahadhari sana huku
ukijiangalia usianguke – 1Kor 10:12-13.
iii) Usijiamini kupita kiasi [over confidence] kwa
kigezo cha andiko Rumi 6:2-11.
Kuna watu wamejiamini kupita kiasi kwa andiko hili, busu
maiti mara inafufuka.
iv) Ishi kama mtumwa wa Mungu uko huru lakini huko
huru- 1Pet 2:16; Rum 6:12-14.
Kijana wewe ni mtumwa wa Mungu na Yesu ni Bwana wako mipaka
ni lazima.
Mipaka katika Mavazi, Marafiki, Mazungumzo, matendo,
mahusiano, masaidiano, muda, mikutano [mahali pa kuwepo], mawasiliano kwa
ujumla, Mipaka kwa mwenendo mzima hasa kwa jinsia 2 hizi tofauti-ni hatari
kugandana kama ruba, ni hatari kufatana kama kumbikumbi, ni hatari kuambatana
gizani sisi ni wa nuruni. Mungu akupe neema ya kushinda mwili unaokuvuta huko
na uweke mipaka kila eneo kwa damu ya Yesu na kuhakikisha huvuki wigo huo ili
UTUNZE UJANA WAKO na Utumishi wako usilaumiwe kwa kusababisha mwenyewe tuhuma
hizo. Vyanzo vya Vijana wengi kulaumiwa hata kama hatujafanya jambo
ni KUKOSA MIPAKA. Kuutumia vibaya uhuru wetu na undugu wetu katika
Kristo ila wewe usiwe hao.
v) Ishi kwa kufuata hekima ya Mungu si
wanadamu – Yakobo 3:17; Rumi 16:19b.
vi) Subiri wakati wa Bwana [Ndoa] – Mith 6:20; 26;
7:1-5; 21:27; Mhubiri 3:1. Usijidhalilishe kwa mtu asiye wako,
mara Mfalme ‘anamatege’ au ‘anamaganda’ yatanadiwa mji
mzima. Malkia ‘anamakovu’ anayaona fataki. Mtu aliyewako hata akute
mapungufu atakupokea jinsi ulivyo maana amepewa na Bwana. Subiri Ndoa.
vii) Jizoeshe kuliishi Neno la Mungu ili uwe na
adabu neno huadibisha- 2Tim 3:16.
Biblia inasema wazi neno hutuadibisha, hututia adabu ya
kuongea, kutenda n.k.
viii) Inawezekana kabisa kutunza ujana wako hadi
ndoa–Marko 10:27; Matha 19:26.
Yasioyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yote yanawezekana,
AMEN.
**MWISHO**
Nawezaje kupata soft copy?
JibuFutaNinashukuru sana kwa ujumbe huu mzuri sana. Mungu aibariki kazi ya mikono yako.
JibuFuta...somo zuri sana
JibuFutaMungu atusaidie tuweze kuyafanyia kazi.