Je wewe ni mtu mwenye furaha? Au hofu na hatia
huondoa furaha yako yote? Je,ungetamani
kuondoa hatia yako, lakini kwa njia
gani? Huenda unajiuliza , je, nitakuwa mwenye furaha tena?.
Ninayo habari
njema kwa ajili yako. Kuna mtu mmoja awezae kukusudia , kusamehe dhambi
zako , na kukupa furaha ya daima. Jina
lake ni Yesu. Ngoja nikuambie habari zake.
Mungu ndiye huyo mmoja aliyeumba
ulimwengu . Vyote aliviumba ulimwenguni. Alikuumba wewe na mimi.
Mungu akupenda . yeye humpenda kila
mmoja ulimwengu. Mungu atupenda sabna hata alimtuma Yesu mwanae pekee
ulimwenguni. Yesu alipokuwa hapa Duniani aliponya wagonjwa; aliwafariji wenye
huzuni. Alifungua macho vipofu . Aliwafundisha watu mambo mengi. Tusome habari katika Biblia.
Yesu alitutaka tuelewe upendo mkubwa
alio nao Baba yake kwa ajili yako na mimi. Alisema hadithi hii iliyoelezea
upendo huo nao Baba yake. Mtu mmoja
aliishi mjini kwa furaha na wana wake wawili alidhani yote ni salama . Siku
moja , mmoja wa wana wake aliasi na kumwambia, spendi mji huu, nataka kufuata
njia yangu mwenyewe na kuondoka. Nigawie urithi wangu. Baba aliuzunika sana , lakini alimpa
fedha na kumruhusu aende . Alijiuliza,
je, nitamwona mwanangu tena? Kwa nini mwana alikuwa muasi hivyo?
Mwana alienda mbali na kujifurahisha
kwa hela yake na rafiki zake. Alifuja fedha zake na kufanya mabaya mengi.
Alidhani amepata wakati mzuri hata kwa ghafla fedha zake ziliisha na rafiki
zake walimwacha. Kisha walimwaacha yeye pekee na ailjiona mwenye hatia
sana je, angefanya nini?
Alimwendea mkulima alimpeleka kuchunga
nguruwe. Hakupewa chakula cha kutosha. Alikuwa na njaa sana hivyo alitamani
kula chakula cha nguruwe . Alianza kufikilia maovu yote aliyofanya na jinsi
alivyomtendea Baba yake. Alizidi kupata
uchungu zaidi.
Siku moja ,alikumbuka Baba yake jinsi
alivyokuwa mwenye upendo na jisi alivyopendwa alipokuwa nyumbani. Alifikiri je,
ningerudi kwa Baba yangu baada ya
kumtendea haya yote? Je, bado angenipenda ? sistaili kuwa mwana wake. Ikiwa angenipokea ningekuwa tu kama mjakazi
wake nyumbani kwake.
Kwa ghafla alisismama na kuanza safari
ya kurudi nyumbani kwa Baba yake . Angeona kama Baba yake bado angempenda . Baba alitamani mwana wake tangu alipotoka.
Alijiuliza , je, mwana wangu atarudi tena?
Baadaye siku moja alimwona mtu yuko mbali
anakuja. je, anaweza kuwa mwanangu? Alimkimbilia na kumkaribisha nyumbani kwa
mikono ya ukarimu. Alisema , mwanangu huyu alipotea lakini sasa amepatikana.
Sisi sote tumekuwa kama huyu mwana , sote tumetoka kwa Baba yetu mbinguni. Tumeharibu
muda na mema yote ambayo ametupa . Tumefanya maovu na kumwasi leo, Baba yetu wa Mbinguni anatutaka tumrudie .
Anatungojea kwa mikono ya ukarimu . Je,
tunaelewa upendo alio nao Yesu kwa ajili yetu? Baada ya kufundisha hapa
Duniani kwa miaka mitatu , aliwaacha
watu waovu kumpingilia misumari msalabani. Aliona maumivu na kuachwa alipokuwa
anakufa na kumwaga Damu yake kama Sadaka kwa ajili ya dhambi za Dunia yote.
Tunapokwenda kwa Baba , tunamwomba
atusamehe Dhambi yetu. Atuonapo tumehuzunikia Dhambi zetu kwa Damu yake
aliyomwaga . Jinsi gani njia hii ilivyo
ya ajabu. Yesu amekuwa Mwokozi wetu. Tumezaliwa upya na kuwa mtu mpya. Uzima
unayo njia mpya . Yesu amebadilisha hatia
na hofu yetu kwa furaha na shangwe.
MWOKOZI KWA AJILI YAKO
Post A Comment:
0 comments so far,add yours