*NA MWL CHRISTOPHER E.A.
MWAKASEGE*
*TAREHE 6 SEPT 2016*.
*SIKU YA 3*
*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI
UPATE ULICHOPOTEZA*
*SUMMARY*
Bwana Yesu afiwe, leo ni siku
yetu kama ni siku ya kwanza unahudhiria semina hii tumekwenda mbali kidogo.
Sina namna ya kurudi nyuma ila jitahidi upande kanda za kuanzia siku ya kwanza.
Sikiliza na kusikiliza, hata kama ulikuwepo huwezi daka chote kwa muda mmoja,
chukua cd sikiliza tena na tena.
_Waefeso 5:15-17 ‘’ Basi
angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu
wenye hekima; *MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU*. Kwa sababu
hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana’’._
>>Muda umepewa jukumu
kubwa sana kubeba maisha ya mtu, na ukitaka kufupisha maisha ya mtu unatumia
unafupisha muda wa huyo mtu.
*VIBEBEO VYA MUDA*
>>Jana tuliangalia
kibebeo cha kwanza cha muda ambacho ni *FIKRA* na leo nataka tuangalie kibebeo
cha pili
*SHERIA*
Daniel 7:25 ‘’ _Naye atanena
maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu;
*naye ataazimu kubadili majira na sheria*; nao watatiwa mikononi mwake kwa
wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.’’_
*JAMBO LA 1* *Uimara wa hali
watakatifu kusimamia kusudi la Mungu, unategemea muda uliobebwa na sheria
inayotumika wakati huo.
*Waefeso 1:3-4* Kwa mujibu wa
mstari huu wa waefeso ni kuwa mtakatifu ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi.
Paulo anasema alitengwa tangu
tumboni mwa mama yake, na kutengwa ina maana ya kuset aside kwa kusudi Fulani
la Mungu.
Ile Muungu kukuleta hapa
duniani ina maana kunakuwa na kusudi la kazi Fulani ambayo anakuwa kakuleta
hapa duniani. Na kusudi maana yake ni sababu ya kuwepo. Ukisoma Mhubiri
3:1b biblia inasema *kuwa kila jambo lina wakati wake na kusudi chini ya
mbingu*. Maana yake ni kuwa kila kitu uwepo wake unakuwa umefungwa na kusudi
maalamu ambalo Mungu kapanga.
*Matendo ya mitume 13:36* Kwa
maana Daudi, akiisha kulitumikia *shauri la Mungu katika kizazi chake*,
alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. Daudi alikuwa tayari
kalitumikia kusudi la Mungu wake kwa kizazi chake. Shauri maana yake ni kusudi
yaani lengo la Mungu wake naye akalala.
Kwa maana hiyo hali ya
utakatifu ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi na ndio maana biblia inatuambia kuwa
Mungu alimtenga Yeremia tangu akiwa tumboni mwa mama yake .Mungu akitaka
utembee kwenye kusudi lake ina maana atakuzuia kufanya kitu kilicho nje ya
kusudi lake na damu ya Yesu itasimama kama ukuta kukuzuia kutokufanya hilo
jambo unalokusudia kulifanya. Na atahakikisha anaondoa fikra zozote ambazo
zinataka kuingilia kati hilo kusudi la Mungu.
*JAMBO LA 2* *Majira na sheria
yanapofanya kazi kwa pamoja vinakuwa ni uwanja wa mapambano ya kiroho na ya
kimaisha,kati yako na waliotofauti na wewe kimisimamo au kifikra*
Wakolosai 4:5 ‘’ Enendeni kwa
hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.
Biblia inasema mwende kwa
hekima kwa watu walionje ya kusudi au wale ulio nao tofauti kimisimamo ya
Mungu. Na uwanja utakaokuwa unapambana nao ni uwanja wa wakati. Katika Daniel
7:25 shetani alikusudia kubadilisha majira na sheria ili aweze kuwadhoofisha watakatifu
ili wasiweze kusimamia kusudi la Bwana.
>>Mungu hakupanga tuishi
nae mbinguni milele bali alipanga tuishi nae hapa hapa duniani na ndio maana
Yesu alisema naenda kuwandalia makao ina maana hayakuwepo na haya makao ni ya
muda. Yahana aliona kuwa mji mpya Yerusalemu unashuka toka juu na aliona na
nchi mpya kwa maana hiyo hii iliyopo inaondoka na hiyo mpya inakuja ili
kuendeleza maisha ya wanadamu ambayo Mungu anakusudia kuwepo hapa duniani.
>>Suala la Roho
Mtakakatifu kukusaidia kuishi hapa duniani, usijisahau sana kuwa unakuwa na
mawazo tu ya kwenda mbinguni na tusahau namna bora ya kuishi hapa duniani.
Maana shetani anatumia sana hio fursa ya watu kuwaza tu kwenda mbinguni na
kusahau namna ya kuishi bora hapa duniani kwa nyakati hizi.
>>Sheria ni kibebeo cha
muda na shetani anapobadili majira na sheria lengo lake ni kuwadhoofisha
watakatifu ili wapoteze kuona umuhimu wa muda, majira na sheria.
>>Kwa mfano unaoa au
unaolewa na mwenzio ina maana kila mtu anakuwa fikra zake na muda wake kwa hiyo
mkiingia ndani ya ndoa kuna lango lingine la muda linafunguliwa na sheria mpya
ya ndoa inakuwa inawafunga hakuna kutengana hadi kifo. Kwa hiyo msipokuwa makini
kusaidiana kifikra yaani mwenzio akiwa pole pole na wewe hujui namna ya
kumsaidia na yeye aweze kuchangamka unakuta na wewe unaanza kwenda kwa slow
motion sawa na mwenzio. Na unaanza kusingizia shetani kumbe sababu kubwa ni
Fikra zenu.
>>Hata katika hali ya
kawaida watu wawilia au watatu wanakubaliana kufanya Biashara kwa pamoja alafu
huku kila mtu anamuda wake na fikra zake, mwanzoni wataenda vizuri ila baada ya
muda utaanza kuona wanaacha kuelewana na mwisho wanakuja kuvunja hata
hiyo biashara yao, na sababu kubwa ni kutokujua namna ya kuharmonize (kuweka
sawa) Fikra zao ili waweze kutembea katika muda mmoja. Na hili jambo huwezi
fanya tu ni hadi kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Pia huwa nawaambia sana
Vijana kabla hawajaanzisha huduma wacheki kwanza sheria itakayokuwa inaongoza
huduma yao maana wasipojua, itawasumbua sana kuendelea mbele.
*JAMBO LA 3* *Ukibadilisha
sheria unabadilisha na wakati uliobeba aina Fulani ya wakati na maisha
yanabadilika ili kuweza kuendana na sheria iliyobadilishwa*
>>Ikiwa sheria
ikibadilika na muda usipobadilika kunaanza kuwa na ugumu wa kuendana pamoja na
muda uliopo. Sheria inaweza kukusaidia uweze kuishi kwa muda ulioko au
uliobadilishwa kutokana na sheria hiyo.
*JAMBO LA 4* *Sheria kuwa
kibebeo cha muda kinaunganisha muda na maeneo mengine yafuatayo*
a)Amri…Ordinance
b) Hukumu..Judgement
c) Agano… Covenant
d) Agizo ….Decree
e)Haki ….Justice
Haya maneno katika Lugha ya
kiingereza yanakuwa na maana tofauti tofauti kwa kulingana na tafsiri ya Biblia
kama ni King James, Amplified, NIV, NLT.etc
*Kazi ya Sheria ni kulinda aina
Fulani ya maisha* Hukumu inazuia muda na ndio maana ukitokea mgogoro au ugomvi
uwe na uhakika kuwa shetani anataka kakuiibia huo muda maana unakuta kila kitu
kinastop.
*MFANO
WA MABADILIKO YA MUDA NA SHERIA KATIKA KIPINDI CHA (HAMANI, MODERKAI, AHUSERO
NA ESTA)*
*Sheria ya kwanza* *Esta 3:1-8*
hapa tunaona kuingizwa kwa sheria inayotaka watu wote kumsujudia Hamani. Na
hapa tunaona kuwa watu wanapokuwa kwenye taifa Fulani wanakuwa chini ya muda na
sheria husika. Hii sheria ya kumsujudia mtu wayahudi hawakuwa nayo na
ndio maana Mordekai alikataa maana alijua mtu wa kumsujudia ni Mungu peke yake.
Endapo angekubali kumsujudia Hamani tayari angekuwa anatembea kwenye muda
mwingine.
*Sheria ya Pili* Esta 3:9-10 ‘’
Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta
kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika
hazina ya mfalme. Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin
Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.
>>Sheria hii ilikuja na
ilikuwa ni tarehe 13 December yaani mwezi Adari. Maana kwa wayahudi mwezi Adari
ni mwezi wa 12 na lengo la sheria hii kuweza kuwabana akina Mordekai na
wenzake.Sheria Yoyote huwa inaweka pressure juu ya muda wako.
*Sheria ya tatu* *Esta 4;9-11*
Basi Hathaki akaja, akamwambia Esta maneno ya Mordekai. Ndipo Esta akasema na
Hathaki, akamtuma tena kwa Mordeka. kusema, Watumwa wote wa mfalme wanajua
sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume
au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, *kuna sheria
moja kwake*, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya
dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku
thelathini.
>>Ukiangalia mstari wa 10
unaonaesha kuwa sheria hii ilikuja kumbana sana Esta na kumdhoofisha hali yake
kabisa. Na Lengo la Esta kuolewa ilikuwa ni kulisimamia kusudia la
Bwana , na kuolewa ilikuwa ni njia tu ili awepo mtu wa kiyahudi kwa wakati huo
ili aweze kulisimamisha kusudi la Bwana. Upande wa pili wanayajua sana haya
mambo (nguvu za giza) na huwa wanawahi sheria ili kuweza kuwabana watakatifu
wasiweze kutembea juu ya muda ambao ndio unabeba kusudi la Bwana.
>>Hapo Esta alikuwa
anasema si Suala la Kwenda kwa mfalme Ahusero bali ni sheria, na Esta alipokuwa
anaomba maombi yafanyike ni ili yaweze kurejesha muda ili aweze kushughulika na
sheria. Na asingeweza kushughulika na sheria ikiwa yuko nje ya muda. Kwa hiyo
kurudishwa kwa muda wake yaani na ile position yake ingemsaidia kuweza
kubadilisha sheria.
>>Ugomvi au mgogoro
unapotokea unaua thamani ya muda katikati ya wagombanao. Maana vita hustopisha
maendeleo maana watu watakuwa wanasema ngoja kwanza tumalize mgogoro ndipo
tuendelee. Na kwa hali hiyo shetani anakuwa anakuibia muda wako na kuna mambo yake
anayokuwa anayapitisha wakati ndio mnagombana na baada ya mgogoro kuisha
unakuta kuna mambo mengi sana yamebadilika.
*ZINGATIA HILI* *_Shetani
anapokuletea ugomvi lengo lake ni kukuibia muda wako kuwa usahau mambo mengine.
Na ukiona hali hiyo mwambie shetani kuwa hatapata huo muda wako na katikati ya
vita beba bunduki na jembe pia, usiombee mgogoro au vita tu bali ombea na mambo
mengine_*
Ukiibiwa muda unaibiwa na
maisha pia.
*Warumi 8:1-2* *``` Sasa, basi,
hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya
Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya
dhambi na mauti.```*
>>Mwekezaji akija
kuwekeza haijalishi shida zetu zikoje mtalazimika kuzibadili tu ili aweze
kuwekeza hapo kwenu. Maombi ya Esta kwa Mungu yalikuwa ya kuomba, muda
wake urudi na Mungu alirudisha sheria.
Yale maombi ya Esta yaligeuza
kabisa maisha kwa wakati ule kuanzia tarehe ile ile ya 13 December, waandishi
wale wale walioandika sheria ndio walele wale waliorekebisha na ile ile sheria
iliyotaka kuwaua wayahudi iliwaua wale wale akina Hamani.
>>Kuna nguvu sana ya
maombi hata katika kipindi cha Daniel maombi yake yalitunza sana muda wake na
Mungu akamsaidia na Pia maombi ya Esta yalirudisha muda wake ukaruishwa.
>>Shetani alipokuwa
anazuia maombi ya Daniel ili aweze kumdoofisha na siku 30 alikuwa anataka
kupitisha baadhi ya mambo kwa spidi kubwa sana na ndio maana Daniel
aling’ang’ana sana na Mungu na Mungu aliingilia kati sheria hiyo iliyokuwepo.
>>Wana wa Israel wangejua
hii siri ya kujua namna ya kutangua sheria hizi wangerudishiwa na muda wao
maana wangeomba kwa Mungu ili ashughulike na sheria hiyo na wasingekaa miaka
400 utumwani na wangeomba Mungu na Mungu angefupisha dhiki. Maana Mungu anafupisha
muda na baada ya hapo dhiki inakoma.
>>Sijui unapitia sheria
gani, au upo katika mazingira yapi,, Yuko Yesu atakayekusaidia na kukuvusha.
Mlango wa Benki haufungwi na askari bali hufungwa na muda. Yaani ikifika saa
kumi unafungwa na wanaandika *door closed* lakini kama una uhusiano na manager
utampigia simu hata baada ya muda kupita na manager anamuambia askari afungue
huo mlango hata kama muda umepita unaingia ndani.
>>Yesu ni Zaidi ya
manager wa benki na ukimuomba hata kama kuna sheria yeye yuko juu ya sheria na
atakusaidia. Hata kama uko kwenye dhiki usigombane na dhiki bali shughulika na
muda kwa sababu ukishughulika na muda maana utafupisha hiyo dhiki.
*Baada ya hapo tuliomba sana na
Nguvu kubwa sana ya Mungu ilitushukia pale uwanjani. Barikiwa sana na Mungu*.
Tembelea http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
Endelea kutufuatilia Jifunze
Na Uelimike kila siku kwa mafundisho yanayoendelea Jijini Arusha
Post A Comment:
0 comments so far,add yours