Mwalimu Christopher Mwakasege
Siku ya pili ya semina kutoka Ollotu, Mbeya Mjini
Tarehe 11 Oktoba 2016
SOMO;NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO.
kama unatusikiliza kwa mara ya kwanza mimi naitwa mwalimu Christopher mwakasege nikifundisha kutoka Mbeya semina yenye kichwa kinachosema "NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO"karibu tushirikiane kwa pamoja.
Jana nilikwambia namna ambavyo nilipata shida wakati nimeokoka na naskia kiu ndani yangu ya kumtumikia Mungu na mara kwa mara nilipata kumsikia Mungu akizungumza nami kwa njia ya ndoto juu ya Utumishi alioweka ndani yangu.
Ilinipa shida sana na nikaamua kutafuta zaidi mafundisho juu ya ndoto sehemu mbali mbali toka katika vitabu vya kidini na vile vya kidunia LAKINI havikunisaidia sana mpaka ROHO MTAKATIFU ALIPOANZA KUNIFUNDISHA.
Na nilikwambia somo kama hili halikua katika mipango yangu ya kufundisha ingawa nimekua nikijifunza kwa muda mrefu sana tangu miaka ya 80 nilipoitwa kwenye huduma LAKINI MUNGU AKASEMA NAMI NIPATE KUFUNDISHA kwa watu ingawa kabla ilikua vigumu sana kufundisha kutokana na mwitikio wa watu lakini nilikua najaribu kumfundisha mtu mmoja mmoja au baadhi ya watu ambao walikua wanashida Na wanaota ndoto lakini hawapati majibu au tafsiri ya ndoto hizo.
Pia wakati naanza huduma nilikua na kiu mno ya kumtumikia Mungu na ilitokea ndani yangu hali ya kutaka kuacha kazi serikalini nikamtumikie Mungu kiasi cha kwamba sa nyingine naingia ofisini na kazi zipo lakini sijisikii kufanya ila nataka nikahubiri au kuombea wagonjwa na saa nyingine nilikua nikienda hospitalini kwa rafiki angu na kumwambia kama unaona kuna mgonjwa na ugonjwa wake sio wa matibabu ya kiganga nipo nje namsubiri nipate kumuombe.
KUNA SIKU wakati wa usiku nikaota ndoto ambayo niko ng'ambo ya mto na kuna watu wengine wako upande wa pili lakini kuna wigo wamewekewa hawaruhusiwi kuvuka apo alafu ghafla nikamuona mtu amevaa nguo nyeusi mwili mzma na amejifunga kitambaa cheusi akiniambia vuka tu nenda upande wa pili...vuka tu...vuka tu...Nami nikawa namjibu siwezi kuvuka mpaka nimeona pakukanyaga...halafu badae likatokea jiwe nikasema sasa naweza kuvuka na nilipovuka nikakuta nipo kwenye chumba kikubwa pekeangu halafu kuna nyoka mkubwa usawa wa urefu wangu afu chumba icho kimefungwa sioni pakutoka baada ya mda fulani nikaona kuna mtu ametokea na kuvunja ukuta wa kile chumba na nikapita.
Nilipoamka nikajua kuwa haikuwa mpango wa Mungu mimi kuacha kazi muda huo.
Bwana Yesu asifiwe!!kwa hiyo sio kila msukumo wa kuacha kazi na kumtumika Mungu unatoka kwa Mungu saa nyingine unatoka kwa shetani na ndiyo maana unatakiwa ujifunze kutofautisha msukumo toka kwa Mungu na ule toka kwa adui.
ZINGATIA JAMBO HILI;
Shetani akishindwa kukuzuia kuanza safari atakuzuia kuendelea na safari.
Hebu tusogee mbele kidogo;Jana tuliangalia Jambo la kwanza ambalo unatakiwa kujua kuhusu ndoto linalosema ;USIIDHARAU WALA KUIPUUZIA NDOTO ULIYOOTA MAANA NDOTO NI LANGO MOJAWAPO LA KIROHO AMBALO MUNGU NA shetani WANALITUMIA KUMFIKIA MWANADAMU.
JAMBO LA PILI;
ambalo nataka tujifunze siku ya leo ni kwamba VIJUE VYANZO VYA NDOTO NA KUVIOMBEA IPASAVYO.
VYANZO VYA NDOTO;
1)NDOTO KUTOKA KWA MUNGU.
Daniel 2:21-28, Matendo 2:17
Kumbuka jambo hili sio kila ndoto unayoota imetoka kwa shetani wala sio kila ndoto unayoota imetoka kwa Mungu.
2)SHETANI AU NDOTO KUTOKA KWA SHETANI.
Shetani nae anaouwezo wa kuleta ndoto.
Kumbukumbu 13:1-4 Usifurahie tu matendo ya mtumishi cheki na matunda yake.usifurahie tu miujiza ya mtumishi angalia matokeo ya miujiza hiyo..kama ni yanakutenga na Mungu na kukusogeza karibu zaidi na mtumishi uwe na uhakika sio utumishi toka kwa Mungu.
3)NDOTO KUTOKA KWENYE MAZINGIRA YA SHUGHULI NYINGI.
-Mhubiri 5;3
4)NDOTO KUTOKA KWENYE HALI YA KIROHO YA MAHALI ULIPOLALA.
-Mwanzo 28:10-19, Mwanzo 13:2-4.
-Yakobo aliota ndoto mahali alipolala palipokua na madhabau aliyoijenga babu yake mzee ibrahimu kama tunavojua ibrahimu alikua na tabia ya kumjengea Mungu aliyehai madhabau maeneo mbalimbali.
-Betheli ni eneo ambalo lilikua na madhabau ya Mungu aliyehai kwa hiyo liliunganishwa na mbingu ndiyo maana Yakobo aliota ndoto akiona malaika wakipenda na kushuka.
KUMBUKA;kujua kwako chanzo cha ndoto ni muhimu sana katika kukusaidia katika kuomba juu ya jambo hilo.
Sasa uyo ni yakobo alilala mahali ambapo paliunganishwa na mbingu umewahi jiuliza umelala sehemu yenye umiliki au maagano na miungu mingine.
HEBU TUANGALIE CHANZO KIMOJA KIMOJA NA NAMNA YA KUOMBA.
1. NDOTO KUTOKA KWA MUNGU.
Omba Mungu akusaidie kusikia kama kile kitu kimetoka kwa Mungu. (Omba upate kusikia na kuelewa kama kweli jambo hilo limetoka kwa Mungu)
-Ayubu 33:14-15
-Mwanzo 41;1,4,5,32
Unapoona ndoto inajirudia mara mbili ni kwasababu neno hilo Mungu amerithibitisha na atalitimiza upesi. Pia tambua ndani kuna muda uliomo ndani ya ndoto.
-Daniel4:27-33.
🔸Farao alipewa miaka saba.
🔸Nebukadneza alipewa ndoto yenye miezi kumi na mbili ndani yake.
🔸Mke wa pilato aliota ndoto ambayo ilikua chini ya masaa kumi na mbili.
2) CHANZO KUTOKA KWA SHETANI.
-Kumbukumbu 13:1-4,kutoka 12:21-23
Ombi;Jifunze kuomba langi la ndoto katika ulimwengu wa roho lifunikwe na damu ya Yesu.
3) CHANZO CHA SHUGHULI NYINGI.
-Luka 8:5-15.
kama umewahi ota unapita njia kuna miba basi katika jambo hili utapata kujua maana yake.
-Maisha ya mwanadamu yameumbwa na yameratibiwa katika ulimwengu wa roho na Mungu hata kabla ya kutokea.
-Haitoshi tu utembee kwenye njia na Bwana Bali hadi atua ziongozwe na Bwana.
OMBI;jifunze kumwomba Mungu akupangilie siku na aongoze siku yako.
4) CHANZO CHA NNE;HALI YA KIROHO YA MAHALI UNAPOLALA.
OMBI: Jifunze kuombea hali ya kiroho ya mahali unapolala.
Yakobo alilala kwenye ardhi ambayo inamilikiwa na Mungu.kuna maeneo au nyumba ambazo zina milikiwa na miungu na mapepo.
Biblia inaeleza wazi sehemu yoyote ambayo ni ukiwa au haijakaliwa na mtu kwa mda mrefu inakua makazi ya mapepo na majini alafu nawe unaingia umo unaanza kuabudu na kuishi bila kuombea eneo hilo kwanza ghafla unashangaa wanakwambia aisee mbona umeingia nyumbani kwetu.
Mungu alipo tufundisha mambo haya tumekua tukiomba kila mahali tunapolala ata kama tumefika na kuchoka sana.
Kuna mwaka nilipata kushiriki katika mkutano wa uchumi marekani na ulikua unafanyika mahali ambapo ni jirani na kijiji ambacho kina kampuni ya HOLLYWOOD..Na tukapangiwa hoteli yenye jina la Hollywood njee ya ile hoteli mtaani kuna mambo yalikua yanafanyika ambayo sio ya kimungu.nikamuuliza Roho mtakatifu naombaje juu ya eneo hili akanambia usiombee chochote ila JIFUNIKE KWA DAMU YA YESU.
WARUMI 8;26
Swali;Umejuaje Chanzo cha ndoto na unaombaje juu ya chanzo cha ndoto husika.
Jibu;WARUMI 8:26__Roho mwenyewe hutusaidia udhaifu wetu maana hatujui kuomba jinsi ipasavyo.
KABLA YA KUOMBA; OMBA NAMNA YA KUOMBEA JAMBO.
Omba Mungu akupe namna ya kuombea jambo. Omba kwa kunena kwa lugha.
KUMBUKA;Udhaifu wetu haupo katika kuomba upo katika kuomba jinsi ipasavyo.
Ndio maana unatakiwa ujazwe Roho mtakatifu na apete kukupa kunena kaa lugha iliuweze kuomba.
SIKU YA TATU
TAR 12 Oktoba 2016
SUMMARY
1. Usidharau wala kupuuzia ndoto uliyoota maana ni lango mojawapo la Kiroho
2. Vijue vyanzo vya ndoto na jua kuombea ipasavyo , Kabl sijasema jambo la tatu nataka nikuambie jambo moja kwanza kwa kitu kilichoko mbele.
Ukisoma habari za Rahabu utashangaa maana huwanajiuliza Maswali mengi sana kwanini Mungu alikubali kuingia gharama zoote hizo za kuibomoa Yeriko lakini Yeye alikuwa anamhitaji mtu mmoja tu Rahabu na Ukisoma Kitabu cha Waebrania unaona kinasema Rahabu Yule kahaba. Sasa kwanini kisingekaa kimya maana baada ya kuchukuliwa na wana wa Israel hakuwa kahaba tena. Lakini lengo lake kuu kutuonesha kuwa *haijalishi shetani amekufanya kitu gani au kakuchafua kiasi gani thamani yako ni damu ya Yesu msalabani. Haijalishi ni ukuta gani uko katika maisha yako , Yupo Mungu anaeweza kubomoa ukuta na kukuweka huru atika maisha yako. Maana thamani yako ni damu ya Yesu kumwagika. Mungu atatumia kila mtu kuhakikisha kuwa anakuokoa, na Mungu atabomoa kila ukuta kwakoni ukuta wa umasikini au wa kujikatia tamaa, au wa umasikini ataubomoa kabisa, atakuweka huru.
Kwa sababu ya Rahabu, ndugu zake wote walipona, Mungu alichagua kahaba kwa ajili ya kuwachapa injili ili wapate kujua kuwa liko Tumaini kwa Mungu. Na ukisoma biblia utoana (Yoshua 6:23) ikisema Rahabu baada ya kuokolewa alikaa nje ya matuo ya Israel lakini Joshua alipokuja alimuweka katikati ya Israel mpaka leo. (Yoshua 6:25) na ukisoma Mathayo 1:5 utaona Rahabu akiingia katika ukoo wa Yesu.
Fahamu hili Kama mbele yako ni kuzuri sana kunakuwa na vita yako kubwa sana
Ukisoma habari za Paulo kabla ya kuitwa Paulo alikuwa anaitwa Sauli, Baadae alikuja kuwa mhubiri mkubwa sana wa injili. Na mara ya kwanza alitumia Torati kupinga injili lakini baada ya kuokoka alitumia Torati ile ile kuhubiri injili. Fahamu hili yuko Mungu anayeweza kugeuza mambo yote usijidharau jipe tumaini kwa Bwana.
Tuendelee na somo
3. Ngo’a kilichopandikizwa na shetani ndani yako kwa njia ya ndoto na upate kuondoa na madhara yake Ayubu 4:12-16 ‘’ Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu. Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena
Ayubu 33:14-15 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;¬
Daniel 7:1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo
>>Katika Ayubu anazungumzia juu ya ndoto na maono ya usiku. Mahali pengine kwenye biblia wametumia maono, lakini ni ndoto. Na aliposema katika usingizi kitandani maana yake ni ndoto
>>Kwa kusoma mistari hii mistari unaona vitu kama vine hivi.
1 Alipata neno katika mawazo yake ‘’ Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake’’Ayubu 4:12
2 Iligusa na kusikia kwake Kama umekuwa msomaji wa habari za ndoto, na utajua kuwa lango la ndoto lipo kwenye nafsi. Na Biblia inazungumzia sikio la ndani.
3 Hapa utaona mstari wa 14 Hofu ilimuangukia na Roho ya hofu ilimuingia ndani yake. Kwa hiyo ndoto ndiyo iliyoingiza wazo ambalo hakuwa nalo katika maisha yake yaani wazo la hofu. Ndoto iligusa mifupa yake na mifupa yake na akaanza kupata matatizo. Na kama ni wewe umepewa jukumu la kumbadilisha mtu huyu inatakiwa ushughulike na vitu vyote vinne.
Ngoja nikuletee shuhuda chache
Nilikuwa Dar es Salaam mwaka Fulani. Na nilikuwa karibu na hospitali moja ivi na nilishuka kwenye gari, huwa si mara nyingi nashuka kwenye gari nikiwa maeneo ninayofahamika. Kwa sababu siku moja kule Arusha nilikwenda dukani na lilikuwa ni duka Kubwa, lakini Mke wangu akaniambia utaweza nikamwambia ndiyo, nikaenda hapo dukani nikawa na Sukuma Toroli na nahitaji kununua vitu, ghafla watu wakaniona na wakaanza kunifuata, sasa hamna kitu kigumu kama unataka kununua vitu na kuna watu wanakusimamia kwa nyuma. Basi kila mtu hapo anahitaji maombi. Na siku moja nimeenda benki ghafla Wafanyakazi wa pale wote wakaweka Temporary closed kwa sababu nao wanahitaji maombi. Si maisha mepesi sana kuishi kama hivyo maana utatamini uishi kama wengine ila ukionekana tu kila mtu anahitaji maombi.
Sasa nilipokuwa nje ya gari langu nilimouna mama mmoja na binti yake na binti yake alikuwa anachechemea mguu. Na walikuwa wameniona niliposimama basi wakaja, Yule mama alisema tumekuona na tulitaka tuje kukusalimia. Nikamuuliza wana shida gani pale hospitali, Binti akaniambia kuwa ameumia kwenye ndoto. Kwa sababu aliota ndoto usiku kuwa analikuwa anapiga mpira na akaumia na alipoamka akaona kweli mguu wake umeumia. Basi nikafanya nao maombi pale na baada ya Maombi alikuwa mzima kabisa kama hajawahi kuumwa kabisa. Na maombi niliyoyafanya ni ya kung’oa madhara yaliyoletwa na ndoto. Na tusingefanya yale maombi hakika ile hali ingemsumbua kwa muda mrefu sana.
>>Pia kuna mwingine aliniandika kuwa huwa anaota ndoto kuwa anaangukia kwenye shimo moja lina maji lingine halina maji na kuna mguu mmoja tu ambao ndio unatangulia yaani kuteleza kuingia kwenye shimo na baada ya muda kidogo ule mguu wake ulileta kidonda.
>>Mwingine kaniandika hapa, kasema hivi niko kanisani naombewa na Mume wangu akaja kuniparua macho, na baada ya hapo macho yangu yalianza kuniuma sana kama yanataka kung’oka na baada ya muda tena mume wangu alinifukuza na hataki hata uniona.
Isaya 29:8 Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
Waebrania 12:22-24 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
Katika Ebrania ndiyo tunasoma maana kamili ya mlima Sayuni, kwa sbabu mlima Sayuni ni mdogo sana kuliko hata mlima Rungwe lakini mlima Sayani unaongelewa hapa ni na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili¬_na sasa ukiona katika Isaya unaona kuwa mtu huyu alikuwa ameota ndoto kama anakula, lakini alipoamka alikuwa kama hana kitu. Kwa hiyo ndoto ya mtu huyu pia iligusa viungo vyake na nafsi.Hivi ndivyo alivyoshetani akitaka kuanzisha vita huwa anapita kwenye ndoto na baada ya hapo unakuta mtu anaanza kuwa na hasira na neno la Mungu bila sababu.
Na watu hawa ambao shetani kawabana, inakuwa shida sana kwao kulisikia neno la Bwana. Na kama si Mungu kulilinda kanisa lake huyu mtu aliyeingiliwa na shetani kupitia ndoto na akapandikiza vitu vibaya sana na hasira kali sana, na asipoombewa vizuri anaweza fanya kitu kibaya sana.
Msichana mmoja alinitafuta sana baada ya kuoka akawa anasema baba naomba unisamehe, nikamuuliza kwanini, akasema niliingia mkataba na shetani ili nikuue. Akasema siku moja niliingia hotelini ulipkuwepo na Wafanyakazi wa hoteli hawakunigundua nilikuwekea sumu kwenye chakula ambayo ingekuua kwa dakika tano tu. Na baada ya kula tuliona hata hamjafa na tulikimbia. Na hatukuishia hapo siku moja tulijua gari uanendesha wewe mwenyewe na tukaenda katika kizuizi kimoja cha barabara ambacho askari wapo ili watuombee lifti na baada ya hapo tuweze kulipindua gari. Basi tulipofika mahali pale askari wakatusimamisha wakawa wanawaombea lifti hao wadada lakini askari alisema mzee kwa kuwa mmejaa basi endeleeni. Ukweli ni kuwa tulikuwa wawili tu, lakini Mungu alituongezea malaika na tulionekana kamatumejaa.
Kama si Mungu kutulinda wangekuwa wanatufanya mambo mabaya sana. Siku moja nilikuwa kwenye mkutano (semina) sehemu nyingine na nilipokuwa nataka kuachilia Baraka Roho mtakatifu akasema ngoja kwanza waite hao watu au waombee rehema maana baraka hizi zitageuka laana kwao. Kwa sababu walikuwa wanatamka maneno magumu kwa ajili yangu na mke wangu.
Pia siku nyingine kwenye semina niliona malaika kaja na upanga, na watu walikuwa na hasira na mimi na Malaika akasema nimekuja ili niwamalize au uwombee rehema, basi nikawaita mbele. Wakaanza kujitokeza mmoja mmoja na niliona malaika ananiambia bado wawili nao nikaita tena wakaja kwa nao na ndipo malaika akatoweka.
Hivi vitu ni halisi kabisa. Sasa nataka tuangalie vitu vichache ili tuweze kuomba hapa.
1 Lazima uombe toba kwa kusababisha lango la ndoto kufunguka na shetani kupita hapo kwenye ndoto.
Kutokujua sheria sio sababu ya wewe kuvunja sheria.
Toba inafanya mambo mawili makubwa, 1. na inakupa uhalali kisheria 2. Inampa Mungu uhalali wa kukupigania. Ni sawa na ndege ya marekani ikienda kuokoa watu, na itaokoa watu wotewa marekani na nafsi ikibaki ndipo itaokoa na watu wengine.
Damu ya Yesu kupitia toba unayoifanya ndiyo inakupa uhalali wa wewe kusaidiwa na Mungu.
2 Ng’oa Roho iliyoingia kwako.
katika Isaya tumeona Roho ya Hasira, na katika Ayubu ni Roho ya hofu. Na nataka kutahadharisha watu hapa kuwa usipambane na watumishi wake kwenye nafasi walizonazo kwa Mungu, gharama yake ni kubwa sana.
3 Omba uponyaji wa madahara yaliyotokea.
Kama ni mifupa ombea mifupa, na Yule aliyeomba kuwa ombewe maana nyoka aliyemng’ata alikuwa kamuachia sumu. Na tulipoomba alitapika sumu (kitu cheupe)
4 Kama hujaokoka okoka hii ni kwa usalama wako
Wokovu unampa Mungu uhalali wa kuja kwako na ndio maana Yesu alikufa msalabani ili aweze kukukomboa na kukuokoa kwa hiyo ni muhimu sana kuokoka.
Tulipokuwa Kigoma siku ya kwanza nikawaambia kuwa Yesu sio wa wakristo na Biblia sio ya wakristo. Si unajua Kigoma watu wengi sio wakristo. Kwa hiyo nilipowaambia hivyo wakawawananishangaa, biblia inasemaje katika Yohana 3:16 ni kuwa Mungu aliupenda ulimwengu,ina maana Yesu ni watu wote na ukimuamini ndio unakuwa mkristo. Biblia nayo ni manual (Mwongozo) ambayo Mungu kama muumbaji katuwekea ili tujue namna ya kuishi hapa duniani kama Yeyeyanavyotaka.
Ukishaokoka unapata mahali pa kukulea kiroho na pia kusanyika na wenzio sio baada ya kuokoka unakuwa unakaa peke yako peke yako. . sasa utaelewa maana yake nini Nuhu alihubiri kwa miaka 120 na alipata watu nane tu. Na hatuoni biblia ikisema mkristo bali ni watu wliomuamini ndio waliokoka.
5 Kama umeokoka basi Mungu akupe neno lake la kukusaidia kusafisha njiailiyochafuliwa na ndoto
Neno la Mungu ni nuru, nit aa maisha mwetu, neno la Mungu ni pumzi yake kwa ajili ya kutuongoza maisha yetu.
Baada ya hapo mwalimu aliomba, na hasa kwa watu waliopata shida kupitia ndoto. Ili kuona live semina semina hizi tembelea;
Christopher and Diana Mwakasege Mana Ministry
FACEBOOK
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/
Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
Website
www.mwakasege.org na kama umeokoka kupitia mafundisho haya soma somo la Utangulizi katika link hii http://www.mwakasege.org/mafundisho/hongera/utangulizi.htm
Post A Comment:
0 comments so far,add yours