Popote palipo na ushindi lazima
kuwe na nguvu iliyotumika katika kuleta ushindi ule.Nguvu ile inaweza kuwa
nguvu ya kifkra ,silaha,maneno na ibada.Ukristo mpaka ulipo hapa leo na ulivyo
leo hii si kwamba umefika fika tu ,kuna nguvu kubwa ilitumika katika
kuueneza,wengi walisimama kuupinga,na hata wengi waliumizwa ,kwa kuteswa
na kuuwawa kwa vifo vya kutisha.
Kwa mfano, ukifuatilia historia
utaona kuwa Yakobo yule mkubwa aliuawa kwa kukatwa kichwa na herode
mfalme(rejea mdo 12:1-2) ,mtume Petro aliuawa kwa kusurubiwa miguu juu , kichwa
chini na Kaisaria Nero mwaka 67 B.K na mtume paulo aliuawa kwa
kukatwa kichwa na kaisaria Nero mwaka wa 65 B.K na wengine wengine waliofuatia
kutokana na utawala dharimu wa Kirumi.Hata hivyo nguvu ya kushinda iliyokuwemo
ndani ya Mitume ilikuwa kubwa sana kuriko hofu na changamoto zilizokuwa
zinazunguka huduma zao.Mtume paulo anaeleza mateso mengi aliyapata kutokana na
kujitahidi kwake kuieneza injili,anasema kuwa “Lakini,ndugu zangu,nataka
mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yametokea zaidi kwa kuieneza
injili.hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo,miongoni mwa
askari,na kwa wengine wote pia” Wafilipi 1:12 pia katika ,2kor 11:23-27
“katika taabu kuzidi sana ;katika vifungo kuzidi sana ;katika mapigo kupita
kiasi,na katika mauti mara nyingi.Kwa Wayahudi mara tano nalipata
mapigo arobaini kasoro moja.mara tatu nalipigwa na bakora;mara moja
nalipigwa kwa mawe;mara tatu nalivunjikiwa na jahazi;kuchwa kucha nimepata
kukaa kilindini;katika kusafiri mara nyingi;hatari za mito;hatari za
wanyang’anyi;hatari kwa taifa langu;hatari kwa mataifa mengine;hatari za
mijini;hatari za jangwani;hatari za baharini;hatari kwa ndugu za uongo;katika
taabu na masumbufu;katika kukesha mara nyingi;katika njaa na kiu;katika kufunga
mara nyingi;katika baridi na kuwa uchi”.Paulo anadhihirisha pia kuwa
utendaji wake wa kazi ulikuwa unatokana na nguvu iliyokuwemo ndani
yake,ukisoma,Kol 1:29.
Kwahiyo katika safari ya maisha
lazima kila mwanadamu ajenge nguvu ya kushinda kwani bila hivyo atajikuta
ameondolewa katika ulimwengu kama mwanasayansi Charles Darwin aliyeleta hoja ya
“survive for the fittest” yaani “ishi kwa uzuri/uimara” akidai ya kuwa, uzuri
au uimara wa mtu ndio unaomwezesha aendelee kuishi duniani kwasababu utamsaidia
kujipatia mahitaji yake ya mhimu ya kumwezesha aendelee kuwa hai.
Kuna
msemo wa kiswahili husema kuwa “ukiona vyaelea, jua vimeundwa” maana yake nini?
Hii inatuonyesha kuwa kila kitu tunachokiona humu duniani kuna nguvu fulani
ilitumika ili kukitengeneza, hata Mungu alipokuwa anaumba duniani ,hakuitokeza
tu,alitumia nguvu ya kinywa kuweza kuiumba.
Tukumbuke
kuwa, Adamu baada ya kutenda lile kosa la kula tunda katika bustani ya edeni, alipewa
jukumu la kufanya kazi ili aweze kuishi duniani,nalo ni la kutumia nguvu,baada
ya kuambiwa kuwa “atakula kwa jasho lake(Mwanzo 3:17-19)”.
Nguvu ile ndiyo
inayomwezesha mwanadamu kufanya kazi, wanasaikolojia wanaiita ile
nguvu”libido”.
Katika safari ya maisha
tumekuwa tukipitia maisha ya aina mbalimbali, lakini yamegawanyika katika
sehemu mbili ambazo ni masha ya kushinda na maisha ya kushindwa.
Tunaweza kujiuliza kwanini
wakati mwingine tunashinda na kwanini wakati mwingine tumekuwa
tukishindwa huenda ni jambo lile lile? Au tunaweza kujiuliza kwanini
watu wengine wamekuwa mbele yetu katika mambo mbalimbali ya kimaisha?
Nguvu ya kushinda
ni uwezo unaomwezesha mtu ili aweze kushinda anapokuwa anatembea katika dunia
hii akipitia maisha mbalimbali.Maisha yetu yamegawanyika katika sehemu kuu
mbili ,sehemu ya kwanza ni maisha ya furaha baada ya ushindi na upendo na
maisha ya huzuni baada ya kushindwa kutokana na ugonjwa ,kifo,ajari.
Kumbuka kuwa uwezo wa kushinda
umekaa ndani ya akili ya mtu mwenyewe, mwanafalsafa mmoja alisema kuwa “kiwango
cha mafanikio ya mtu kinapimwa au kinajengwa katika fikra za mtu” maana yake,
jinsi mtu anavyowaza ndivyo atakavyofanikiwa. Ninaweza kusemakuwa, aina ya
mafanikio na kiwango cha mafanikio aliyonayo mtu ni matokeo ya fikra na juhudi
za mtu katika kuyawaza yale mafanikio na kujitahidi kuyapigania mpaka kuyapata.
Yapo mambo
mengi yanayochangia kuunda nguvu ya kushinda kama yakifuatwa.
Jambo la kwanza na kubwa
kuriko yote ni, Neema ya Mungu maishani mwa mtu, tunaweza
kuzania ya kuwa baada ya mwanadamu kuondolewa katika bustani ya edeni
akapewa jukumu la kutafuta mahitaji yake kwa nguvu zake, huenda Mugu alimwacha
mwanadamu pekee yake asimsaidie hata kidogo,lakini ukweli ni kwamba bado Mungu
amekuwa akiachilia nguvu zake kwa mwandamu ili kumsaidia katika harakati zake
za kujitafutia mahitaji yake.
Mtume Paulo katika kitabu
cha Waraka wa pili kwa wakorintho sura ya kumi na tano mstari wa kumi, anasema
kuwa ameweza kufanikiwa kupita hata mitume waliomtangulia kutokana na neema ya
Mungu inayoizunguka huduma yake “Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa
hivi nilivyo;na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure,bali nalizidi sana
kufanya kazi kupita wao wote;wala si mimi ,bali ni neema ya Mungu pamoja nami”.1Kor
15:10.
Hapa
ninaposema neema ya Mungu ninamaanisha nguvu ya uwezo anayopewa mtu na Mungu au
miungu kutokana na kufuata taratibu za ibada au kutokana na upendo wa Mungu au
miungu. Kuna wakati mwingine tunaweza kuwashuhudia marafiki zetu wakifanikiwa
sana au waking’ara sana tukashindwa kuelewa kuwa ni kwa sababu gani.Lakini hii
ndiyo neema ya Mungu au miungu ,kumbuka, hata shetani naye ana neema yake
anayoiachilia kwa watu wanaomwabudu kama anavyomwambia Bwana wetu Yesu Kristo
katika Luka4:6- 7 akisema “Ibilisi akamwambia ,nitakupa wewe enzi
hii yote,na fahari yake ,kwa kuwa imo mikononi mwangu,nami humpa ye yote kama
nipendavyo.Basi ,wewe ukisujudia mbele yangu yote yatakuwa yako”.
Kwa hiyo si kwamba tunapoona
watu wanafanikiwa tunazania huenda ni kwasabu ya uwezo wao wa kufikiria au
juhuda zao ,la, bali ni nguvu fulani iliyonyuma yao.Ndiyo maana leo
tunasikia mara Freemasons na wengine mara wanaenda kwa waganga wa kienyeji, na
wengine kuombewa, yote haya ni kwa ajiri ya kutafuta usaidizi wa Mungu au
miungu.Kumbuka kuwa uwezo wa mwanadamu unampaka au unamwisho.Kuna mwanafalsafa
mwingine alisema kuwa “maisha ya mwandamu yako chini ya uangalizi au usimamizi
wa Mungu,miungu”.Labda niweke sawa hapa kuwa ,kwa kila mtu ipo neema
ambayo Mungu huiachilia kwake ili kumsaidia kudumu katika dunia hii au kushinda
upinzani unaojitokeza katika maisha yake,kinachotofautiana ,ni aina ya neema
,kiwango cha utendaji wa ile neema na jinsi mtu anavyoitumia ile neema.
Hili nilieleze kwa
kukumbusha kuwa, wakati ukiwa bado uko darasani au kazini kwako, kwanini
kuna wanafunzi wenzetu wamekuwa wakiwa na uwezo mkubwa kimasomo na
hata tukitumia nguvu nyingi sana lakini bado hatuwezi kufikia uwezo wao. Lakini
makazini tunaweza kujiuliza juu ya uwezo wa wafanyakazi wenzetu
,wapo wamekuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi na kuzisaidia taasisi au
makampuni kuweza kukua kwa haraka sana.Lakini kibiashara tunaweza kujiuliza
kwanini biashara za watu wengine zinakuwa kwa kasi sana na zetu zinakuwa kwa
kasi kidogo au inatokeaje mtu kukubalika kwa watu na mwingine kukataliwa na
watu?
Hapa
ndipo tunapoongelea neema ya Mungu, inakupa nguvu ya kufanikisha jambo Fulani
kwa wakati Fulani kwa kukupa kibali mbele za watu kwa kazi unayoifanya au kuzidisha
juhudi yako ya kupigania mafanikio.Kuna mtu mmoja alisema hivi “uweza na
utajiri wa mwanadamu ni matunda ya neema ya Mungu”.
.Mfano tunaona viongozi,
wasanii, wachezaji na wafanyabiashara waking’aa, si kwa juhudi zao tu bali kwa
ile neema ya Mungu inayoandamana nao.
Kwahiyo kwa
kifupi “mwanadamu amekuwa vile alivyo kutokana na kiwango na aina ya neema
inayomzunguka”
.
Jambo la pili ni mtazamo.Mtazamo
ni jinsi unavyowaza na kuhisi juu ya kitu Fulani.Watu wengi wameshindwa
kutimiza ndoto zao au kufikia katika mafanikio ambayo wamekuwa wakiyaota
kutokana na mitazamo yao juu ya hayo mafanikio, hii inaweza kuwa ni kutokana na
mapito wanayopitia ,mfano wakati mwingine tumekuwa tuna ndoto nyingi sana
lakini kutokana na maisha magumu au changamoto tunazokumbana nazo tumefikia
kipindi tumekata tamaa.
Lakini pia mazingira ya
kuyafikia hayo mafanikio yamekuwa yakichangia watu kukata tamaa.Kulingana na
ugumu ulioko mbele ya safari ya mafanikio tunayoyaendea yamekuwa yakitufanya
tubadili mitazamo yetu. mfano, wanafunzi wengi wanaacha kusoma masomo ya
sayansi kutokana na kusikia kuwa ni magumu na watu ambavyo wamekuwa wakiyasema.
au kutokana na kuwa kuna kazi zingine ukisoma unapata kazi moja kwa moja, watu
wengine wameacha kusomea kozi ambazo wanazipenda kwasababu ya hofu ya
ajira.Mwanasaikolojia Wiliam James anaseama ,kuwa, “wanadamu wanaweza
kugeuza maisha yao ,kwa kugeuza mitazamo ya akili zao”.Mitazamo yetu
inatakiwa kuendana na ndoto zetu au kule tunakotaka kufika.
Kwahiyo
jinsi unavyowaza na kujisikia juu ya mafanikio ndivyo utakavyokuwa. Ingawa
kunaweza kuwa na ukinzani lakini mtazamo wako juu ya yale mafanikio yatakufanya
ufikie mafanikio.Kumbuka kuwa, changamoto si kwamba inakutuzuia tusiweze
kufikie mafanikio yetu ,bali inapunguza kasi yetu kuelekea mafanikio ,ni sawa
na milima na mabonde ,hayaizuii gari kuendelea na safari bali yanapunguza kasi
kuelekea nwisho wa safari.
Mtazamo wa
mafanikio unakupa nguvu ya kuendelea kupigania mafanikio na pia unakufanya
uvumilie.
Tatu, kubali
kubadilika,katika safari ya kuelekea katika mafanikio unatakiwa wakati
mwingine kuwa kama kinyonga ,ninaposema kubadilika si manisha kuondoka au
kuacha njia uliyokuwa unaipita bali pia kuboresha ile njia .Kwa mfano kama
ulikuwa unafanya kazi kwa masaa sita lakini unaona kabisa kuwa masaa hayo
hayatoshi kukufanya ufanikiwe unatakiwa kuongeza masaa mengine,mfano uanze
kufanya kwa masaa tisa.Kwa mwanafunzi kama ulikuwa unatenga muda wa masaa
mawili kwa ajili ya kujisomea unapaswa kuongeza lisaa moja.Kwa mwombaji kama
ulikuwa unaomba mara mbili kwa siku unatakiwa kuongeza iwe mara tatu kwa siku
au kama ulikuwa unafunga kwa masaa kumi na mbili unatakiwa kufunga kwa masaa
ishirini na nne. si hivyo tu, unaweza ukatafute njia nzingine za kuongeza
kipato,mfano kama wewe ni mwalimu,unaweza ukaanzisha kilimo au ufugaji wa kuku.
Unaweza kuanzisha kampuni wakati ukiwa umeajiriwa, lengo ni kukuza kipato
chako.
Ubunifu
unatuwezesha kushinda changamoto mbalimbali tunazokumbana nazo katika safari
yetu ya maisha.
Nne ,kutumia fursa,Katika
maisha ,watu wengi wamekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao kutokana na sababu
ya kwamba wameshindwa kutumia fursa zinazokuja mbele yao.Kwa mfano watu wengi
wanalia leo hii kwasababu ya kuchezea fursa ya kupata elimu,kwa kuacha shule au
kuacha kujituma katika masomo na hatimaye kushindwa mitihani au kuendekeza
tabia zisizofaa na hatimaye kufukuzwa shule.Siku moja nikiwa sehemu moja jijini
Arusha nikinyolewa,kinyozi aliyekuwa akininyoa alikuwa akilalamika sana kwa
kudai kuwa anajuta kwa kukataa kusoma kutokana na ushawishi wa rafiki
zake,wakaendekeza madawa ya kulevya. Lakini leo hii anatamani apate mtu
atakayemwambia arudi shuleni, atafurahi sana na ataenda kujituma ili atimize
ndoto zake.
Katika maisha zipo fursa nyingi
zinazojitokeza katika maisha yetu, kama ,fursa za elimu,ajira na fursa za
kutumia mali asili.
Katika nchi nyingi za Afrika, kuna
tatizo kubwa la serikali kushindwa kutumia fursa zilizopo ili kukuza kipato cha
nchi kwa mfano katika taifa letu la Tanzania kuna tatizo kubwa la kushindwa
kutumia fursa za mali asili kama madini, gesi na misitu. Ndiyo maana kipato cha
nchi kimekuwa kidogo kiasi cha kwamba kuifanya serikali kutegemea kukopa kwenye
benki za duniani au nchi za magharibi ili kupata pesa za bajeti.
Ukiangalia nchi nyingi za ulaya
ziliweza kuendelea kwa kasi sana kutokana na kutumia fursa zilizokuwa mbele yao
,hasa ardhi kwa kilimo na ufugaji ,karne ya tano baada ya kuanguka kwa utawala
wa Rumi.Walifanya kazi kwa bidii na kwa ushindani sana,tofauti na nchi zetu za
Afrika ,leo hii ingawa watu ni maskini ,lakini hawajitumi kabisa katika
kazi,uvivu na uzembe kazini ni mkumbwa.Wengi wetu tunapenda starehe tu
kuriko kazi utazania tuko peponi.
Lakini pia, Wakati,
Mwanadamu hupita katika nyakati za aina mbalimbalia kama inavyosema katika
mhubiri 3:1-8 imeandikwa”Kwa kila kila jambo kuna majira yake, na wakati wa
kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa ,na wakati wa kufa;wakati wa
kupanda,na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;wakati wa kuua,na wakati wa
kupoza;wakati wakubomoa na wakatiwa kujenga;wakati wa kulia na wakati wa
kucheka;wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza…..wakati wa kutafuta na
wakati wa kupoteza…”.
Kwa maana hiyo kuna wakati
tumekuwa tukishindwa kutokana na sababu ya kuwa tupo katika wakati wa
kushindwa. Inawezekana usinielewe vyema lakini ukikaa chini na kutafakari
utaelewa,j iulize kwanini kuna wakati biashara yako ilichangangaya,ukafurahi
sana ,lakini kwanini kuna wakati biashara yako ilikwama ukaanza kuhuzunika
,ukitaka kutafuta hata mchawi.Kwanini inafikia kipindi tunakwama katika mambo
yetu tunayoyafanya?j ibu ni kwamba ,wakati.
Zaidi
,Uvumilivu,Uvumilivu ni kitendo cha kuwa na subira au kustahimili
ukinzani anaokumbana nao mtu.Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa, safari ya
maisha ni safari inayochangayikana na changamoto,kwahiyo kama unataka kushinda
lazima uzishinde changamoto.Ninaweza kusema kuwa “katika kila hatua moja
unayotaka kuvuka ya kimaisha ili uingie hatua nyingine ya kimaisha unatakiwa
kutegemea kukutana na changamoto”.
Unapovuka changamoto moja si
kwamba ndio umekuwa salama unatakiwa kujua kuwa unapovuka changamoto moja
kuingia hatua nyingine ya mafanikio,kuna changamoto nyingine katika hatua
hiyo,kwa hiyo jiandae kuikabili.Kwa kifupi ,katika kila hatua ya maisha ipo
changamoto yake.D.k Robert H.Schuller anatufundisha kuwa “wakati mgumu huwa
haudumu bali watu wagumu au wenye nguvu ndio wanaodumu”.Kwa hiyo katika maisha
changamoto utakutana nazo tu,lakini weka katika akili yako kuwa,hiyo changamoto
haitadumu milele,ipo siku itazimika kama mshumaa.Walter Chrysler ,yeye anasema
kuwa “siri ya mafanikio ni kuwa na shauku”.
Kwahiyo shauku yetu juu ya
mafanikio inatakiwa kuzidi kuwa kubwa hata tunapokutana na mapingamizi ya kila
namna.Hapo mwanzo tumeona kuwa Mtume Paulo alikutana na changamoto za
kila namna ,hata hivyo hakukata tamaa,hii inatokana na shauku yake
ya kuieneza injili na kukamilisha huduma yake.Anasema kuwa aanendelea kukaza
mwendo ,bila kuangalia ya jana ,ila yeye anayachuchumilia yaliyo
mbele(Wafilipi 3:12-13).
Na,Uthubutu, watu
wengi wanashidwa kuvuka hatua moja ya mafaniko kwenda mbele kutokana na kujaza
maneno ya “siwezi” ndani ya fikra zao.Hiii inatokana na hofu kubwa iliyojaa
ndani ya mioyo yao.Watu wengi hutamani kujua ngazi zote wanazopaswa
kuzipanda,lakini Mkuu Martin Luther King jr mwanafalsafa na mwanaharakati wa
watu weusi amerika anasema kuwa “chukua hatua ya kwanza kwa imani,si lazima
uone ngazi zote,chukua tu hatua ya kwanza”.Methali ya wachina inasema kuwa
“safari ya maili elfu,huanza kwa hatua moja”.Kwahiyo lazima tushinde hofu
inayotuzuia kuanza kwani bila kuanza hatuwezi kufika tunakotaka kufika. Rais wa
kwanza wa Afrika Kusini kutokana na kuhangaika kwingi na hatimaye kushinda,
alisema kuwa “Nimejifunza kwamba, ujasiri si kwamba haukuwa na hofu ndani yake,
lakini shangwe ndani yake.Mtu shujaa si kwamba hana hofu, bali ni Yule
anayeishinda hofu”.
Kwahiyo
tunapotaka kuchukua hatua na mazingira yetu yanayotuzunguka yanatudokeza kuwa,
hatuwezi si kwamba tukate tamaa bali tutafute namna ya kuanza, hata kama ni kwa
unyonge sana. Unapoanzisha kitu Fulani si lazima kiwe kimetimilika kwa asilimia
mia,bali hicho ambacho hakijakamilika kinawezakuwa mtaji wakukupeleka katika
kitu kilichokamilika.Mfano; unapotaka kuanzisha biashara Fulani ,si lazima uwe
umekamilika kila kona,hiyo hiyo biashara nyonge inaweza kuwa mtaji wa kupata
biashara kubwa.Mfano siku moja katika kipindi cha televisheni cha klauds fm
kinachoitwa “siz kitaa” kuna bwana mmoja alisimulia namna ambavyo aliweza
kupata mafanikio makubwa(kuwa na kiwanda),anasema kuwa alianza kwa
magunia matano tu ya mpunga,lakini baada ya jitihada kubwa ,sasa anakiwanda.
Hivyo,
katika kile ulichonacho unaweza kukitumia kuwa mtaji wa kukufanya ufike pale
ambapo umekuwa ukiota.Watu wengi wameshindwa kufika katika mafanikio ambayo
huyatamani kwasababu ya kushindwa kutumia mitaji waliyonayo kwa kuona kuwa ni
midogo sana, mfano kujenga nyumba.
Nakumbuka
baba yangu mzazi alipokuwa akishauriwa kujenga nyumba, alikataa sana kwa kudai
kuwa hana pesa, kwani yeye alitaka apate pesa ya kujenga moja kwa moja na si
kidogo kidogo, kipindi hicho mimi nilikuwa bado mdogo sana.Lakini baada ya mama
yangu kuamua kuanza ujenzi yeye kama yeye, naye ameamua kuungana naye, ingawa
kidogo kidogo, kutokana na kuwa na pesa kidogo, hata hivyo hivi sasa wako
mbioni kumaliza ujenzi wote.
Kama
ulikuwa hufahamu, nikudokeze siri hii, mara nyingi unapoanzisha jambo, ndipo
hata akili ya namna ya kuliendeleza huja na hata milango hufunguka kwa ajiri ya
kufanikisha jambo hilo.
Rais marafu sana wa sasa
duniani, nikimaanisha Baraka Obama alisema kuwa,”mabadiliko hayatakuja kama
tukisubiri wakati mwingine au watu wengine, sisi ndio tuliosubiriwa kwa ajiri
ya hayo, sisi ndio mabadiliko tunayoyatafuta”
Nihitimishe
kwa kusema kuwa kila mtu anao utajiri wa mafanikio na
nguvu,inategemea ni jinsi gani anautumia huo utajiri na kwa namna gani ili kupata
matokeo chanya.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours