Bwana Yesu asifiwe milele!
Jambo la 4 kati ya “Mambo
unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”
ni hili:
“Ikiwa umeota ndoto ambayo
tafsiri yake huijui ufanyeje?”
1. OMBA MUNGU AKUPE UFAHAMU JUU
YA NDOTO! UFAHAMU HUU JUU YA NDOTO, UKIUPATA TOKA KWA MUNGU KATIKA KRISTO YESU,
UTAKUSAIDIA WEWE NA WATU WENGINE PIA!
Biblia inatueleza ya kuwa:
“Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto” (Daniel 1:17).
Kufuatana na Wakolosai 1:9,
Mtume Paulo akiongozwa na Roho Mtakatifu aliwaombea wakristo waliokuwepo
Kolosai wakati ule, wajazwe “maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na
ufahamu wa rohoni”.
Naamini hata katika nyakati za
sasa, Roho Mtakatifu yupo tayari kutuongoza tujazwe “ufahamu wa rohoni”.
Naamini ufahamu huu wa rohoni unahusu pia ufahamu juu ya ndoto!
2. USITAFUTE TAFSIRI YA NDOTO
TOKA KWA MTU YE YOTE TU UNAYEDHANI ANAWEZA KUKUSAIDIA!
Kitabu cha Mwanzo 40:8 tunasoma
swali hili: “Kufasiri si kazi ya Mungu” Hayo yalikuwa maneno ya Yusufu
akiwahakikishia “Mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri”, juu ya upatikanaji
wa tafsiri juu ya ndoto walizokuwa wameota!
Farao alipoota ndoto zake mbili
mfululizo zilizofanana, tena kwa usiku mmoja (Mwanzo 41:1 – 7), alitafuta
tafsiri ya ndoto zile mahali ambapo hakutakiwa kutafuta!
Farao alitafuta wapi kwanza juu
ya tafsiri zake za ndoto alizoota usiku ule? Biblia inasema: “Farao akapeleka
watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima
walioko…akawahadithia ndoto zake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria…” (Mwanzo
41:8).
Ni mpaka alipotafutwa Yusufu
aliyekuwa gerezani wakati ule, ili amtafsirie Farao ndoto zake. Yusufu
akamwambia Farao: “Si mimi, Mungu atampa Farao majibu ya amani” (Mwanzo 41:16).
Ni wazi ufahamu aliokuwa nao
Yusufu juu ya ndoto, ulikuwa mkubwa kuliko wa waganga na wachawi wote waliokuwa
nchini Misri wakati ule!
Mfalme Nebukadreza aliona jambo
kama hili kwa Danieli, alipomlinganisha na waganga na wachawi waliokuwa kwenye
himaya yake alipokuwa anatawala.
Biblia inatueleza ya kuwa:
“Danieli…alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto” na alifaa “mara kumi
zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake” (Danieli 1:17,20).
Ni kweli kuna mtu ambaye
anaweza kukupa tafsiri ya ndoto yako, lakini asiweze kukupa ujumbe uliomo
katika ndoto hiyo! Kupewa tafsiri ya ndoto, bila kupewa ujumbe unaoambatana na
ndoto hiyo; ni sawa na kula chakula na ukashiba huku hakina virutubisho kwa afya
yako.
3. OMBA MUNGU AKUPE KUJUA
UJUMBE ULIOMO KWENYE NDOTO ULIYOOTA, ILI USIISHIE KUPATA TAFSIRI YA NDOTO BILA
KUJUA UJUMBE WAKE!
Ukisoma kitabu cha Danieli 4:4
– 18, utaona ya kuwa kiu aliyokuwa nayo mfalme Nebukadreza, ilikuwa ni kujua
tafsiri ya ndoto aliyoota, na si ujumbe uliokuwa ndani ya ndoto kwa ajili yake!
Lakini Danieli alimpa mfalme
Nebukadreza vyote viwili – tafsiri ya ndoto (Danieli 4:20 – 26), na ujumbe
uliokuwemo kwenye ndoto ile kwa ajili yake (Danieli 4:27).
Na kwa sababu mfalme Nebukadreza
alitaka tafsiri ya ndoto, na si ujumbe wa ndoto, alijikuta akipuuzia na
kutokutilia maanani ujumbe wa ndoto aliopewa, wala hakuufuatilia! Na matokeo
yake ni maisha ya mateso ya miaka saba, kwa ajili yake, na kwa ajili ya familia
yake, na kwa ajili ya serikali ya ufalme wake.
Unapoendelea kutafakari juu ya
jambo hili, ni vizuri nikujulishe pia yafuatayo:
(i) Kuna ndoto ambazo zimebeba
vitu vinavyohitaji tafsiri ili uweze kupata ujumbe uliomo ndani yake. Mfano wa
ndoto kama hizi tunaupata katika Mwanzo 40:5 – 23.
(ii) Kuna ndoto ambazo zimebeba
vitu ambavyo maana yake iko wazi, na kwa ajili hiyo havihitaji tafsiri yake,
ili kuupata ujumbe uliomo ndani yake. Soma mfano wake katika Mathayo 1:18 – 24.
(iii) Kuna ndoto ambazo zina
ujumbe peke yake, bila kubeba vitu vyovyote zaidi ndani yake. Soma mfano wake
katika Mathayo 2:12,22 na Mwanzo 31:24,29.
(iv) Mfasiri sahihi wa ndoto na
ujumbe uliomo ndani yake ni Mungu tunayemwabudu katika Kristo Yesu; bila kujali
chanzo cha ndoto uliyoota!
4. UWE NA NENO LA BIBLIA LA
KUTOSHA NDANI YAKO – TENA KATIKA HEKIMA YOTE!
Wakolosai 3:16 inasema hivi:
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana
na kuonyana…”
Kwa nini jambo hili ni la
muhimu katika kutafsiri ndoto na kupata ujumbe uliomo ndani yake? Hii ni kwa
sababu kufuatana na Ayubu 33:14,15 – ndoto ni neno katika picha!
Na kwa kuwa “kusikia huja kwa
neno la Kristo” (Warumi 10:17), basi ujue bila neno la Kristo ndani yako huwezi
“kusikia” ujumbe uliomo ndani ya ndoto – hata kama unajua tafsiri ya ndoto
hiyo!
Hebu tuangalie mfano juu ya
Biblia inasema nini kuhusu tafsiri ya ndoto zinazohusu madarasa, au kusoma, au
kufanya mitihani; na ujumbe uliomo ndani yake.
Ukisoma kitabu cha Danieli 1: 3
– 20 unaweza kujifunza yafuatayo juu ya ndoto hizo:
(i) Maandalizi yanahitajika kwa
ajili ya hatua iliyo mbele yako, au hatua unayotaka Mungu akupe unapoomba
katika maombi yako.
(ii) Kuota “shule” au “chuo”
maana yake maandalizi ya hatua fulani iliyo mbele yako yanahitaji utaratibu
maalumu.
(iii) Kuota “shule” au “chuo”
ulichowahi kusoma zamani, ina maana kwamba kuna jambo lililotokea hapo
ulilotakiwa “kuvuka” – lakini hukuweza kuvuka, na kwa hiyo kuna eneo limekwama
kwenye maisha yako.
(iv) Watu mlio nao darasani
katika ndoto ina maana watu mlio ngazi moja ya kimaandalizi.
(v) Kuota ndoto uko darasani na
watu uliowahi kusoma nao zamani au unaota unarudia darasa, au unarudia mtihani
– ina maana umekwama mahali kimaisha na unahitaji maandalizi ili kuvuka hapo.
(vi) Ukiota hukai darasani
wakati wengine wako darasani; au hukai kwenye mtihani wakati wengine wanafanya
mitihani – ina maana huna utulivu unaotakiwa uwe nao ili uweze kujiandaa vyema
kwa hatua iliyo mbele yako.
(vii) Ukiota unafanya mtihani –
ujue: au unapita mahali kimaisha ambapo unapimwa kiwango chako ulichofikia
kimaandalizi; au mbele yako kuna kuja kipimo kwa ajili ya kujua ikiwa umefikia
kiwango kinachotakiwa kwa wewe kuingizwa hatua nyingine ya maisha.
(viii) Ukiota unaota unasoma,
na ukaona na somo unalosoma, au ukaota unafanya mtihani na ukaona somo la
mtihani huo – ina maana unaonyeshwa aina ya, au eneo la – maandalizi
unalotakiwa kulifuatilia kimaandalizi.
Kumbuka – huu ni mfano tu wa
kutafsiri ndoto na kupata ujumbe uliomo ndani yake kwa kutumia neno la biblia.
Mungu aendelee kukubariki
unapoendelea kujifunza somo hili la ndoto.
Mimi nimeota nipo mazingira ya shule ambayo ni mageni kwangu na nisiku ya mtihani, mwaliMwanayegawa mtihani alishawahi nifundisha O level, wakIla Mimiati mwalimu anagawa mtihani nilibarikiwa na haha ndogo kwahiyo nilitoka nikatafute choo maana ni mgeni mazingira Yale, nilitafuta bila mafanikio nikagundua muda wa mtihani unaenda nikarudi hivyohivo darasani lakini nilipofika niliona wenzangu wameshaanza mtihani na Mimi Mwalimu kanizuia kuingia, nikastuka, nisaidie tafsiri ya hii ndoto mwalimu ikiwa utafanikiwa kuiona ili nijue namna ya kufanya maana sio mlango wa kupitia kwenye maisha yangu
JibuFuta