Hakuna jambo linaumiza kama kusalitiwa na mtu uliyempenda na ukamuamini
mfano mzazi, mke, mume, mchumba, mtoto, kaka, dada au rafiki wa karibu. Maumivu
yake huwa ni makali sana na huweza chukua muda mrefu sana kupona.
ZAB. 55:6-7, 12-13
“Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningerukia mbali na
kustarehe. Ningekwenda zangu mbali,
Ningetua jangwani. Kwa maana aliyetukana
si adui; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye;
Kama ndivyo, ningejificha asinione.
Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.”
Unaweza jaribiwa kurudisha kisasi au kumchukia huyo mtu kabisa. Lakini
biblia inatukumbusha kuwa Yesu naye alijaribiwa kama sisi lakini hakutenda
dhambi.
EBR. 4:15
“Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu
ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila
kufanya dhambi.”
Hivyo unapokuwa umesalitiwa na ndugu, mwendee Yesu yeye awezaye kuponya
mioyo iliyojeruhiwa na kukupa moyo wa msamaha na kuachilia. Yesu alisalitiwa na
mtu wake wa karibu, anajua maumivu ya usaliti na pekee ndiye awezaye
kukuondolea maumivu hayo na kuuponya moyo wako. Usijaribu kutafuta suluhisho
mwenyewe maana hutalipata, mkabidhi Yesu, lia mbele zake na hapo furaha yake
itakuwa nguvu yako.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours