Kijana unatakiwa ujitambue, ujielewe wewe ni nani na una kusudi gani katika maisha yako, Kupata uelewa wa kutosha juu ya kipindi cha ujana na umuhimu wake, Kuelewa changamoto zilizopo katika kipindi cha ujana na namna ya kuzishinda, Kujenga shauku, nia na kiu kwa kijana ili uweze kuishi maisha yenye mwelekeo na uweze kutimiza maono yako ukiwasaidia na wengine kumjua Mungu na maisha yako kwa ujumla wake, Kuwekeza uthamani na nguvu ya kipindi cha ujana kwa mtazamo wa Ufalme wa Mungu.

Yesu amefundisha katika Mathayo 6:33 kuwa tunapaswa kuutafuta kwanza Ufalme wa Mungu na haki yako, yaani wewe kama kijana unatakiwa kutoa kipaumbele, kuwekeza kwa nguvu zako zote katika kuutafuta Ufalme wa Mungu lakini ni muhimu kujua kuwa ni vigumu sana kukitafuta kitu usichokijua ndio maana ni muhimu sana kuujua kwanza.
Lakini kabla ya kufika mbali napenda pia kukusaidia kujenga msimamo katika fikra zako juu ya Ufahamu wa namna Mungu anavyokutazama kama kijana ili utakaposikia jambo lolote lisilolingana na mtazamo huu basi ujue ni maamuzi gani unapaswa kuyachukua.

Ni muhimu kujua namna Mungu anavyokutazama ili utakavyotazamwa na ulimwengu uwe na msimamo wenye nidhamu katika maamuzi yako, hii inategemeana na kama umeamua kusimama katika upande wa Mungu na kujitambua. Kumbuka upo Ufalme wa giza na Ufalme wa Nuru na ni Wajibu wako kuchagua upande upi wa kuutumikia na mimi binafsi nakushauri kuwa mchague Yesu Kristo aliye Mfalme wa wafalme wote, mkubali na umpokee na umfanye kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako na kama unahitaji msaada zaidi tumia mawasiliano yetu.

Waamuzi 6:12
Unamkumbuka Gedioni au ulishawahi kusoma habari zake, au je, ulishawahi kumsikia? Kama bado soma Waamuzi 6, na kama tayari tafakari tena kwa upya habari zake. Wakati wana wa Israeli wamefanya maovu, mara baada ya kukaa kwa Furaha na amani kipindi cha nabii mke alieyeitwa Debora, kwa kusahau ukuu wa Mungu wana wa Israeli wakarudia uovu wako. Ndipo Waamuzi 6:1 inapoanzia na kwasababu hiyo alitakikana mtu wa kuwatoa tena wana wa Israeli toka katika mikono ya maadui zao wamidiani.
Ndipo kuanzia msitari wa 11, tunaona malaika wa Bwana akaenda kuongea na Gidioni akiwa anapepeta ngano yako na hivi ndivyo malaika alimwambia, “…BWANA yu pamoja nawe ee shujaa.” Kumbuka kipindi hiki Gidioni alikuwa bado kijana mdogo na kwa namna yoyote ile isingekuwa rahisi kwake kujiona ni shujaa kama malaika alivyomuita. Kimsingi, Mungu alimuona kuwa yeye ni shujaa pamoja na ujana wake kwa maana ushujaa wake usingetokana na umbo la mwili wake bali na kuwa na  mahusiano mazuri na Mungu wake.
Kijana, wewe ni shujaa na ushujaa wako hautokani na:
·         Elimu yako
·         Ukoo wako
·         Nguvu za mwilini mwako
·         Mali na fedha ulizonazo
·         Umaarufu ulionao
·         Wala historia nzuri au mbaya ya maisha yako, hapana.

Wafilipi 4:19
Kijana, unayaweza mambo yote ndani ya Kristo, unayaweza mambo yote katika wewe akutiae nguvu Yesu Krsito.
Mafanikio yako na ujasiri wako ni huu, kwamba katika Kristo Yesu wewe unaweza kufanya jambo lolote. Kuyaweza mambo yote katika Kristo kuna uhusiano na nguvu zake tu na wala sio ukoo wako, familia uliyozaliwa au mambo magumu yaliyotokea kwako Wafilipi 4:19. Ni Mungu anaekupenda na kukuwazia mema siku zako zote za maisha yako, huu ndio uhakika wa mafanikio yako na kushinda kwako bila kujali wewe ni nani. Huenda wazazi au ndugu au marafiki wanakubeza na kukudharau kuwa huna kitu, uchaguzi ni wako, aidha uwasikilize hao ambao mwisho wao ni siku chache zinazohesabika au uamue leo kuishi kwa kutii na kulifuata Neno la Mungu. Zaburi 119:9.

Ujasiri na ushujaa wako umefichwa ndani ya kujitambua katika Mungu, yaani kumjua Mungu katika mahusiano yako wewe na Yesu na kujijua wewe ni nani kwa kadri Mungu anavyokufunulia katika Kristo, thamani yako pia imefichwa huko, Mungu anakuona na anakuita wewe kuwa ni shujaa kwa sababu anauona ushujaa ndani yako unaotokana na wewe mwenyewe. Waamuzi 6 Soma habari za Gidion
 Kwa lugha nyingine, si kwa uweza wala si kwa nguvu zako wewe ni shujaa bali kwa nguvu na uweza wa Mungu mwenyewe katika Roho Mtakatifu unaokufanya wewe kuwa shujaa. Najua, kutokana na historia za maisha ya vijana wengi, inaweza isiwe rahisi sana kukubali ukweli huu kwamba wao ni mashujaa au kwamba wao ni wenye hekima.
Pamoja na kukataa huku bado nasisitiza kuwa wewe kijana unaesoma hapa ni shujaa na anayesema na kutaka hayo ni Mungu, mimi nimerudia tu kukukumbusha kuwa wewe umetajwa na Mungu wako kuwa wewe ni shujaa. Ni mashujaa tu wanaoweza kufanya mambo makubwa na ya ajabu na wengi wao ndio wameandikwa katika vitabu vya historian na wewe hata kama hujaandikwa bado, fahamu kuwa umechorwa kwenye kitanga cha mkono wa Mungu ambaye ndiye mratibu wa historia zote.

Ni kutokana na uhalisia huo huo, ndiyo maana hata Gidioni mwenyewe haikuwa rahisi kwake kukubali alipoitwa na malaika. Angalia jibu lake baada ya malaika kumuita wewe ni shujaa, Gidioni akamwambia malaika kuwa kama ni kweli Bwana yuko pamoja nae mbona mambo mabaya yanawatokea? Na pia yako wapi matendo makuu ya Mungu kati kati yao? Na wewe unaweza ukajiuliza pia au kumuuliza Mungu, kama ni kweli Mungu anakupenda kwanini umezaliwa kwenye familia.

Kwa ujumla wake, Mungu anakutazama wewe kijana katika sifa au pande tatu:

1.      Kila kijana ana nguvu
2.      Kila kijana anao uwezo wa kumshinda shetani katika Kristo

3.      Ukiwa kijana ndio wakati pekee ambao Neno la Mungu linaweza kupata nafasi nzuri ya kukaa ndani ya moyo wako.



Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours