1Yohana 2:14
“
Nimewaandikia
ninyi,vijana kwa sababu mna nguvu,na neno la Mungu linakaa ndani yenu ,nanyi
mmeshinda yule mwovu.”Mungu anao mtazamo wake binafsi
juu ya kila kundi la watu chini ya jua,.Na kila kundi mfano wa
wamama,wajane,watoto,vijana kuna mambo fulani ambayo Mungu anatarajia kila
kundi litatekekleza. Mungu anazungumza na vijana na kusema nimewaandikia ninyi
vijana kwa sababu moja mna nguvu,mbili neno la Mungu linakaa ndani yenu, na
tatu mmemshinda yule mwovu.
Nguvu
zinazozungumziwa hapa ni nguvu,uweza wa Mungu wa kukusaidia kutekeleza maagizo
yake. Na kwa sababu hiyo basi kuna matarajio ya Mungu kwa hao vijana. Sasa
lengo la ujumbe huu mfupi ni kukueleza nini Mungu anatarajia/anategemea kwamba
utafanya sawasawa na nafasi aliyokupa mbele zake na uwezo aliokupa. Matarajio
ya Mungu kwa vijana ni kama ifuatavyo:
VIJANA WAUTEKE UFALME WAKE.
Mathayo
11:12 “Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana
kwa nguvu,nao wenye nguvu wauteka”. Biblia inapozungumzia ufalme wa Mungu
inazungumzia habari za utawala wa Mungu . Hivyo ni matarajio ya Mungu kwamba
popote pale vijana walipo basi watatengeneza mzazingira ya Mungu kutawala
katika maeneno waliyopo iwe darasani, Chuoni, Kazini, Kanisani nk na hii ni kwa
sababu wana nguvu.Sikiliza vijana wana nguvu na ufalme unapatikana kwa
nguvu,maana yake Mungu anatarajia vijana watumie nguvu zao kuuteka ufalme wake
na kuurusu uchukue utawala duniani.
VIJANA
WAREJESHE URITHI NA MALI ZA WANA WA MUNGU ZILIZOTEKWA.
Mwanzo
14:13-16. “…Akawapa silaha vijana wake,walozaliwa katika nyumba yake,watu mia
tatu na kumi na nane,akawafuata mpaka Dani”. Hizi ni habari za Ibrahamu
aliyeenda kumuokoa nduguye Lutu baada ya kuwa ametekwa.Ili kurejesha urithi wao
na mali zao ilimbidi Ibrahimu atumie nguvu kazi ya vijana. Na hivyo hata leo
Mungu anatarajia kwamba vijana wasimame kwenye nafasi zao na kupambana kwa
ajili ya afya,ulinzi, uchumi,uponyaji,mafanikio ya watu wake. Hebu jipe dakika
moja halafu tazama jinsi shetani anavyotesa watu na kudhulumu afya zao, ujana
wao, ndoa zao ,uchumi wao nk.Ni nani watakaorejesha hali nzuri, urithi huu kwa
wana wa Mungu , ni Mungu kupitia Vijana.
VIJANA
WASIKOSEE KATIKA KUFANYA MAAMUZI YA KUOA AU KUOLEWA.
Mithali 5:18
“Chemichemi yako ibarikiwe;nawe umfurahie mke wa ujana wako”.Sikiliza Mungu
anataka ndoa yako iwe ni ndoa ya mafanikio na ya furaha, maana yake ni ndoa
ambayo hautaijutia kwamba kwa nini nilimuoa au kuolewa na huyu mtu.Sasa ili
ndoa yako iwe ni ya furaha na amani, ni lazima huyo mwenzi wako umpate kwa
uongozi wa Mungu mwenyewe.
Sasa mtazamo
wa Mungu kwa vijana ni huu vijana hawatakosea kufanya haya maamuzi kwa sababu
tayari Neno la Kristo limejaa kwa wingi ndani yao.Kumbuka neno la Kristo ni taa
ya miguu yangu.
VIJANA WAWE
WASULUHISHI WA MATATIZO KATIKA JAMII NA TAIFA.
Mithali
1:4 “Kuwapa wajinga werevu,na kijana maarifa na hadhari”. Leo ndani ya kanisa,
jamii tunayoishi na katika taifa kwa ujumla yapo matatizo mbalimbali ya
kiroho,kiuchumi,kijamii,kiafya,kimwili,kibiashara,kindoa nk. Sasa Mungu
anatarajia vijana ndio watumike kusuluhisha matatizo haya mbalimbali katika
jamii kwa sababu ya wingi wa neno la Kristo ndani yao. Hii ina maana mtu mwenye
neno la Kristo kwa wingi ndani yake basi maana yake ana upeo mkubwa wa kuelewa
mipango na njia za Mungu za kuwatoa watu wake kwenye matatizo yanayowakabili.
Hivyo tumia fursa hiyo kutatua matatizo hayo na kusuluhisha kwa sababu ya Kujua
mawazo na njia za Mungu za kuwatoa watu wake kwenye shida walizonazo.
VIJANA
WALITUMIKIE KUSUDI LAKE LA KUHUBIRI HABARI NJEMA.
Mathayo
28:19 “Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa
jina la baba na la mwana na la Roho Mtakatifu”. Sikiliza kwa sababu ya nguvu
ambayo Mungu amewekeza kwa vijana basi ni matarajio yake kwamba wewe kama
kijana utatumika kuwaeleza watu wengine habari njema za Yesu Kristo ziletazo
amani. Ni matarajio yake kwamba vijana watapita nyumba kwa nyumba , mtaa hadi
mtaa wawaambie wengine kuhusu huyu Yesu, wakiwafungua waliofungwa na kuutangaza
mwaka wa Bwana uliokubalika. Naamini haya matarajio matano ya Mungu kwako kama
kijana mwenzangu basi yatakusaidi sasa kukaa kwenye nafasi yako ili Mungu
ajivunie kuwa na kijana kma wewe.
Amani
ya Kristo na iwe pamoja nanyi.
Ndimi
katika utumishi huu Patrick Sanga.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours