LENGO LA SOMO.
 
Kujifunza namna ya kutumia  Damu ya Yesu katika kutatua matatizo ya kurithi.
Kila siku Mungu atakuwa anaongeza kitu ndani yako ili uwezo kuitumia Damu ya Yesu kwa ajili ya kuchukua hatua ili kuomba.
Kwa hiyo tutakuwa tunajifunza na kuomba hapa ili kuweka kwenye matendo kile tunachojifunza.
Kwa hiyo tutakuwa tunajifunza hapa na itakusaidia kuomba kwa ajili yako na mtu mwingine.
Hamna sababu ya kusoma shule kama huna mpango wa kutumia unachosoma ina maana unapoteza muda kama hutatumia hicho ulichojifunza hapa. Mungu kakuleta mahali hapa chini ya Mwalimu ina maana unatakiwa kujifunza ili utumie maarifa haya.  Kwa sababu umepata hii nafasi itumie vizuri kujifunza na kuweka kwenye matendo kile ulichojifunza.
 
MTIRIRIKO WA SIKU YA LEO WAKATI TUNAWEKA MSINGI NATAKA TUANGALIE POINT KADHAA HAPA
1. Kurithi ni kitendo cha kupokea kitu kwa kuwa umechaguliwa uwe mrithi wa hicho kitu.
Maana kurithi si kwa kila mtu maana tunapewa kurithi na mtu mwingine.
Waebrania 1:1-2
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Hujiweki kuwa mrithi bali unawekwa yaani umechaguliwa kuwa mrithi wa hicho kitu ulichopewa kurithi. Kwa hiyo kama unasumbuliwa na matatizo ya kurithi  ina maana huko umechaguliwa wewe kuwa mrithi na ndio maana hayo mambo yamekupata.
Biblia inatuambia kuwa Mungu alimuweka mwana awe mrithi wa yote na anazungumza na ulimwengu kupitia Yesu katika zamani hizi kwa sababu Yesu ni mrithi wa Yote.

2.  KURITHI NI KITENDO CHA KUPEWA KITU KIWE CHAKO KAMA MRITHI, KITU AMBACHO KILIKUWA CHA MWINGINE.
Waebrania 1:3-4
Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri Jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.
Hapa utapata picha kuwa Jina la Yesu halikuwa Jina la Yesu bali lilikuwa Jina la Baba yake yaani jina la kurithi. Kwa sababu baba alimpa mtoto kama urithi.
Yohana 17:11
Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Yesu anasema kuwa baba hili Jina sio langu ni la kwako ulilonipa kama urithi. Kwa sababu huwezi kurithi kitu cha kwako Kama Jina la Yesu ni bora kuliko la malaika. Kwa maana hiyo huwezi kurithi jina la kwako ina maana lilikuwa la mtu mwingine.
Yohana 17:6
Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.
Hapa tunaona Jina ambalo ametudhihirishia ni jina la Yesu.
Yohana 10:25
Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa Jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia.
Ina maana Jina la Yesu lilikuwa la Baba yake.
Yohana 5:43
Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
Hapa Yesu anasema kuwa hili jina nimerithi kwa baba yangu kwa kazi maalumu, na sababu moja yapo ya kupewa jina la kwa sababu ya urithi.
Hii ni muhimu kujua ili uweze kushughulika na kitu cha kurithi kwa sababu kitu cha kurithi hujipi wewe mwenyewe.Ina maana unachaguliwa na mtu fulani. Na yule anayewapa urithi na akishwapa inakuwa halali katika ulimwengu wa roho na mwili. Na ndio maana hata Yesu aliporithi Jina Yesu tunamjua kuwa ni Yesu.
Kuna sababu ya Yesu kusema hilo jina sio lake kwa sababu kuna nguvu katika Jina la Yesu kwa kule lilikotoka. Kwa maana hiyo hata matatizo ya kurithi hayatokani na mtu mwenye matatizo maana chanzo chake ni nguvu iliyoko nyuma ya matatizo ya kurithi.  Maana chanzo sio wewe na yako kwako kihalali na sio rahisi kupangua kiurahisi
Kwa hiyo fuatilia kwa karibu kwenye maandiko. Mbinguni utaenda ila kina vitu katika maisha haya vitakwama. Na kuna wengine wanaweza enda vizuri katika maisha haya maana unaweza ukakosa mbingu usipopata msaada utakwama hata kwenda mbinguni kwa sababu tu ya vitu/ matatizo ya kurithi.

3. INGAWA DAMU YA YESU NI DAMU YA AGANO JIPYA. LAKINI INA UHALALI MBELE ZA MUNGU KWA AJILI YA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA KURITHI
Luka 22:20
Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.
Yesu alisema Kikombe hiki ni agano Jipya katika Damu yangu
Waebrania 9:15
Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Nataka utazame kidogo, Yesu alisema Damu hii ni damu yangu katika agano Jipya. Ina maana ina uhalali wa kutatua matatizo yako hata ya zamani kwa sababu Kupitia mauti ya Yesu ni kwa ajili ya kumsaidia mtu ambaye amebanwa na kufungwa yaani kukomboa makosa ya agano la kwanza (maagano mengine yoyote). Kwa hiyo usifungike tu kuwa Damu ya Yesu ni ya agano jipya tu. Maana yake inashugulika na maagano mengine yoyote. Ina maana makosa yaliyotanguliwa kufanyika Damu ya Yesu inakusaidia kushugulika  katika kurithi kwako na uweze pata urithi katika Kristo Yesu.
Kama una matatizo ya kurithi na yamekuletea shida kwa sababu jina lako lilitajwa huko (Zamani). Na kwa maana hiyo hata wewe utapata shida kwa sababu ya agano hilo. Lakini Damu ya Yesu ya thamani yaani ubora na ukiona ubora ina maana kuna ushindani. Na kwa maana hiyo unaweza kupangua kila kitu(Hakuna damu nyingine yenye ubora kama Damu ya Yesu). Hata kama kungekuwa na TBS ya Kiroho wangeona Damu ya Yesu ni bora kuweka maagano yote. Na ndio maana agano jipya na bora kwa sababu ya Damu iliyotumika.
Kwa maana hiyo ahadi zinakuwa bora katika agano jipya kwa sababu ya Damu ya Yesu. Damu ya Yesu ina uwezo mkubwa kwa sababu inaweza kufanya mambo makubwa sana.
Damu ya Yesu imepewa uhalali yaani ina uhalali wa kisheria kutoka kwa Mungu.  Na ndio maana ikifika mahali hata kama ni jela na ikamkuta shetani hawezi kataa. Maana damu inaongea katika Waebrania 12:24.  Damu ikija jela itaita na kusema namtaka Mwakasege, Shetani atasema unamtaka Mwakasege, basi shetani ataita na kusema Mwakasege njoo hapa unatakiwa na Damu huku. Na unatoka na Damu ya Yesu inakupokea na kukusafisha, kwa sababu kuna mtu kaitumia Damu na nikatoka.
Ni rahisi sana mwanasheria wa upande mwingine na anasema kuwa hiyo damu imemwagika hivi karibuni maana tatizo lake ni la zamani na kama hajui kukutetea ina maana hutoki. Ngoja tuangalie pointi hizi mbili alafu ntaeleleza.

4. DAMU YA YESU USIYOITUMIA HAINA FAIDA KWAKO.

5. DAMU YA YESU USIYOITUMIA NAE MUNGU HAITUMII.

1Wakorintho 5:7
Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
Pasaka wetu amekwisha kutolewa na kwa maana hiyo Yesu ni Sadaka. Na kwa maana hiyo Pasaka ni jina la Sadaka.
Kutoka 12:21-23
Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.
Kutoka 12:12-13
Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.
Sasa nisikilize itakusaidia. Damu ya Yesu ni damu ya Pasaka. Na maana Pasaka sio sikukuu tu bali ni sadaka kwanza ndipo baadae ndio ilikuwa kuwa sikukuu maana Mungu alisema fanyeni hivi kwa ukumbusho wa tendo hili katika vizazi vyenu vyote. Ina maana wachinje kondoo.
Yule kondoo aliyechukuliwa alikuwa na damu ndani yake na biblia inasema achinjwe na damu iwekwe kwenye bakuri. Na haisemi ni kiasi gani (size ya bakuri) kwa hiyo bakuri inaweza ikajaa na ikamwagikia chini. Na walikuwa wanatakiwa kuchukia hisopo na kichovya na kupiga juu ya kizingiti cha juu na miimo ya milango maana hiyo ndio ilikuwa ishara.  Kwa hiyo damu iliyoko kwenye bakuli sio ishara na damu iliyoko kwenye kondoo sio ishara. Na Mungu anasema nitakapoiona hiyo damu ipi? Iliyo katika kizingiti cha juu na miimo ya mlango.
Alisema nikiona hiyo damu
👉Ntaihukumu miungu ya Misri.
👉Ntwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misiri wa wanyama na wa wanadamu.
👉Ntamzuia mharibu asiwaharibu.
Na damu iliyokuwa juu ya mlango ilikuwa ni kidogo sana. Damu iliyoko ndani ya bakuli na kondoo haina msaada kwao. Maana unaweza ukawa na damu ya Yesu na isikusaidie maana Mungu alitaka watumie ile damu kwa imani.
Kwa hiyo tumia damu kwa imani, maana imani bila matendo imekufa. Kwa hiyo unatakiwa sana kufuatilia kwa umakini sana matumizi yake kwa maana ukikwama hapo huwezi fanikiwa.
Kwa hiyo unaposoma habari za Mashahidi watatu – Baba, Neno na Roho (wa mbinguni).
Damu, Roho na Maji (mashahidi wa duniani).
Roho mtakatifu yuko pande mbili. Damu usiyoitumia duniani haikusaidii mbinguni na kwa maana hiyo huwezi okoka baada ta kufa it will be too late. Kwa sababu Damu ya Yesu ilimwagika upande huu ili uitumie upande huu.
Unaweza mtumia Yesu na usitumie Damu yake na ukakwama maana unaweza mtumia kondoo na sio damu yake. Kwa hiyo fuatilia Damu ya Yesu ili imani yako iweze kusimama kutumia katika mambo ya kurithi.
Maana mtu anaweza kukuombea na ukapona na usijue formula yake je ukikwama, unaanza kumtafuta yeye kama hayupo utafanyeje?.
Ni sawa na mama anayeacha maziwa kwa ajili ya mtoto mdogo nyumbani. Kila siku ndio unatengeneza maziwa na kumwachia msichana wa kazi.  Na kazi yake ni kumpa maziwa mtoto maana yeye hajui kutengeneza, sasa ghafla huonekani nyumbani siku 2 uwe na uhakika kuwa  msichana anajua tu kumpa maziwa. Na kama haupo atatafuta kila aina ya maziwa na kumpa, lakini si katika ule mchanganyiko unaotakiwa.
Na ni sawa tukatangaza kuwa kuna maombi ya kuombea matatizo ya kurithi  na watu wakaja tukaomba na wakafunguliwa, na wakashangilia lakini kesho ukikwama au mtu mwingine amekuja na hiyo shida unaanza kusema Ngoja tumtafute Mwakasege au tusubiri semina au tumtafute mchungaji mahali alipo. Na unaweza kutana na mtu mwingine akasema anhaa ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya hii kitu unadanganywa tu. Hilo neno lina nafasi yake lakini usije ukafutia vitu vingi hapo kwa sababu Watu wengi waliokoka wanapata shida na hawajui kutoka na wakati wanajua huo mstari.na wamekwama kwa sababu wametumia mstari vibaya.
Ndio maana nakufundisha sasa ili ujue maana kazi ya mwalimu ni kuwasaidia kuwa wajue kuendesha gari na sio kila siku kuwa abiria kila siku. Hii ni kazi ya mwalimu kuwe na madereva wengi.
Ndio mwana ukiwa Mwalimu usiwe na wivu, ukiwa na wivu hufai kuwa Mwalimu. Kama unafikiri natania kawatafute waaalimu waliofundisha darasa la pili. Wanafunzi waliowafundisha sasa ni mameneja na wakubwa sana. Lakini mwalimu yuko pale pale na raha yake ni kuwaona wanafunzi wake wamefanikiwa.
Sasa kama kila mtu atakimbilia Chuo kikuu nani ataweka msingi wa darasa la kwanza maana ni muhimu, kwa sababu ndio unafanya hata wanafunzi wanakuwa wazuri chuo kikuu kwa sababu walipewa msingi mzuri darasa la kwanza.

6.  MUDA AMBAO TATIZO HILO LIMEKUWEPO SI KIKWAZO MBELE YA UWEZA WA DAMU YA YESU
 Kutoka 12:41-42
Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri. Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.
Kama damu ya kondoo na Mungu aliweka neno na ilishughulikia shida utumwa wa wana wa Israel kwa miaka 430. Si zaidi sana damu ya Yesu.
Watu wengi wanakata tamaa na kuona mambo ya kurithi ni kama sehemu ya maisha yao. Kwa sababu wameomba sana na hawajatoka na wengine hawajui hata wafanyeje. Na hata akienda hospital  anaomba kupunguziwa maumivu na sio  kupona.
Hawa watu (Wana wa Israeli) walikaa miaka 430 na ingekuwa rahisi kutoka maana kilichowapeleka ni njaa na ilidumu miaka 7. Sasa kwanini walikaa miaka 400. Kitu gani kiliwazuia wakati Yusufu kafa si wangeondoka? Maana hata mzee Yakobo alipokufa walienda kumzika Kanani na walirudi tena Misri. Haukuwa utumwa wa kawaida kwao, ndio maana biblia inasema Misri nyumba ya utumwa.
Ufunuo 13:8
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Tega  sikio hapo na sikia na kusikia huo mstari. Ina maana kuna kitu cha zaidi cha kusikiliza hapo. Hapo tunajua kuwa ni habari za Yesu, na alichinjwa msalabani.
Na Mungu hapa anataka kutuambia kuwa Damu ya Yesu inaweza shughulikia  hata tatizo ambalo Lipo tangu kuweka misingi ya Dunia.
Damu ilimwagika msalabani. Na inaweza shugulika na tatizo hilo hata mwanzo. Kwani unapo okoka ina maana unafanywa kuwa mwana wa Mungu. Ina maana unapelekwa hata katika kipindi cha adamu mwanzo kabisa na kufuta ile shida yaani dhambi ya kurithi. Sasa Kwanini usiipeke hata kwenye mambo mengine imani hiyo uliyoamini wakati unaokoka.
Kuna mtu alikuwa anakemea kitu cha kurithi na kikaja kitu cha kutisha (pepo) likaja na kusema tumekaa kwenye hii familia  kwa miaka 600. Wewe mtu wa juzi hapa Unataka kutupeleka wapi. Yule mtu aliiinuka  na akaacha kuomba. Unajua kwa nini alishindwa? ni kwa sababu alikuwa hana huu mstari wa 8 wa ufunuo 13 na angesema kuwa nani ana umri mkubwa kati yako shetani na Yesu.
Haijalishi hili tatizo limedumu kwa muda gani.  Ila jua kuwa Damu ya Yesu inaweza kukutoa katika tatizo hilo la kurithi unalopitia.


Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours