Na Mchungaji Peter Mitimingi

SABABU YA KWANZA

Tatizo la Udongo.
Wainjilisti walio wengi wana mbegu nzuri (neno la Mungu), lakini udongo au ardhi wanayokwenda kupanda hiyo mbegu ndio unakuwa haujaandaliwa kupokea mbegu.
Mathayo 13:3 - 9

3 Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. 
4 Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; 
5 nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;
6 na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. 
9 Mwenye masikio na asikie.

.............................................................................
1. Kabla ya kwenda kupanda mbegu, udongo unaokwenda kuupanda umeandaliwa kwa kiasi gani?
Umeombea wale unaotaka kwenda kuwahubiria neno la Mungu.
Umeshughulikia mkuu wa anga wa eneo unalotaka kwenda kufanyia uinjilisti.
Mathayo 12:29 
Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.
2. Mbegu uliyo nayo ni nzima au imeliwa na wadudu?
Unalijua neno la Mungu kwa usahihi kabla ya kwenda kuwapelekea wengine?
Ukiamini mafundisho potofu utapotosha watu katika uinjilisti.
Mfano wa Kijana aliyejifanya msomi kijijini walipookota kopo la dawa wakamuomba awaambie inatibu nini na yeye kumbe hajui kingereza akajifanya anawasomea na kuwatafsilia kuwa ni dawa inatibu magonjwa mbalimbali ya watoto. Walipo nyweshwa watoto, wengi walikufa. Kumbe ilikuwa ni dawa ya kuulia wadudu wa mashambani.
3. Mazao yatakayo patikana kuna utaratibu mahususi wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo?
4. Maghala ya kuhifadhia mazao yapo safi na yanafaa kuhifadhia mazao?
5. Maghala ni makanisa ya kupokelea hao watu wanaokuja kwa Yesu yapo vizuri kiasi cha kuwa sehemu muafaka na salama kwa kupokea mazao (waongofu wapya) kutoka katika mavuno ya shamba la Bwana?
6. Makanisa mengi hayajaandaliwa kwajili ya kupokea waongofu wapya na kuwasaidia kujisikia kwamba wapo mahali sahihi ndani ya kanisa.
7. Wakristo wachanga wanapokuja kwa Bwana hawapewi ushirikiano wa kutosha na makanisa ili kuwafanya waone wapo mahali salama wanapopaswa wakae wakomae na kudumu.
8. Waganga/wachawi wakiokoka wakija kanisani kila mtu anawatenga kwamba hawataki kusogeleana na wachawi au waganga.
9. Makahaba wakiokoka wanawake wa kanisani wanawatenga na kuwaogopa eti watachukua waume zao.
10. Wavuta madawa na bangi wakiokoka na kuja kanisani wanatengwa na kunyanyapaliwa eti wataiba vitu vya watu kanisani.
11. Maghala mengi (Makanisa hayana mfumo mzuri wala mtaala wa mafundisho maalumu ya kuukulia wokovu.

12. Kila mtu akiokoka anachanganywa na wale wa zamani na maisha yanaendelea kiasi kwamba hawa wapya wanakuwa hawaelewi mambo mengi maana hawajapatiwa mafunzo ya wokovu ya kuukulia wokovu.
13. Hakuna shule duniani ambayo huwa ina weka wanafunzi kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu kwenye chumba kimoja. Lakini madarasa mengi ya makanisani mwetu tunawachanganya watu wote kuanzia aliyeokoka miaka ya 47 mpaka anayeokoka leo wote wanakaa chumba kimoja.
Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours