Na Mchungaji Peter Mitimingi. |
SADAKA INAYOCHOMA MOYO NDIYO YENYE MATOKEO MAKUBWA
SINDANO INAYOUMA SANA NDIYO INAYOPONYA UGONJWA.
Utangulizi:
1. Utawezaje kujua kuwa sadaka niliotoa inathamani kubwa mbele za Mungu?
2. Moja wapo ya kipimo cha kujua kwama sadaka uliotoa inathamani au haina thamani kubwa mbele za Mungu, ni kuangalia kiwango cha mguso wa maumivu kinachobakia baada ya kuitoa sadaka hiyo.
3. Ukiona unatoa sadaka ambayo hata husikii kuumia kwa namna yeyote huenda utakuwa umetoa sadaka ambayo ipo mbali sana na moyo wako.
4. Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya sadaka yako na moyo wako.
Mathayo 6:21
Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
5. Wachawi na waganga Wanajua siri ya sadaka inayochoma moyo.
Wachawi wanataka sadaka ya mtu ambaye ni wakaribu sana na wewe:
• Kafara ya Baba mzazi
• Mama Mzazi
• Mtoto Yule umpendaye
• Mke Yule umpendaye.
• Ukipeleka sadaka ya mtu hata kama ni wakaribu lakini humpendi, utasikia kwamba sadaka hii imekataliwa na mizimu kumbe ni kwasababu haiugusi moyo wako.
• Mfano:
Binti wa Rufiji aliyetakiwa atolewe kama mchango na mama yeke kwenye kikao cha wachawi.
MUNGU ANATAKA SADAKA YA ISAKA SIO SADAKA YA ISHMAILI;
MAFUNDISHO YA KULIKUZA NA KULIKOMAZA KANISA
Mwanzo 22:2 - 3
2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako. 3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
1. Ingawa wote walikuwa ni watoto lakini Mungu alimchagua Isaka na Sio Ishmail.
2. Watu wengi wapo tayari kumtolea bwana lakini sio sadaka ya Isaka bali sadaka ya Ishmaili (second hand offering).
3. Mara nyingi Mungu anapoitaka sadaka ya Isaka huwa anaihitaji wakati ambapo na wewe pia unakuwa na uhitaji nayo sana kuliko wakati mwingine wowote.
4. Mungu huwa anaihitaji sadaka ya Isaka wakati wa kiangazi ikiwa ndio macho yako yote yameelekezwa hapo hapo na Bwana naye anagusa hapo hapo.
5. Inaweza kuwa zote ni sadaka Mungu anataka ile iliyonona ambayo wewe unaipeda zaidi.
SADAKA YA ISAKA MARA NYINGI HUWA INAPIGA KELELE KWA SAUTI KUU IKIJITETEA ISITOLEWE
Mwanzo 22:7
7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
Mara nyingi unapotaka kutoa sadaka ya Isaka huwa inapiga kelele kwa sauti kuu ikijitetea isitolewe:
Mfano:
1. Angalia madeni uliyonayo
2. Pesa Ulizonazo hazitoshi
3. Angalia una majukumu muhimu hujatekeleza
4. Maliza kwanza hili na hili utakuja kutoa baadaye ukishafanikiwa.
5. Wewe kipato chako sio kikubwa waachie wenye pesa nyingi ndio watatoa.
6. Hata Mungu anakujua kuwa wewe ni masikini usiye na kitu.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours