SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE
UWANJA WA TANGAMANO TANGA 6 JUNE 2017
SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.
Siku ya Pili.
Hakikisha unapata DVD au CD na kusikiliza na kusikiliza na utaona unapata kitu cha kukusaidia.
MAMBO YA KUZINGATIA
1.Katika ndoto unawezafanya agano na Mungu.
Katika biblia neno ndoto kuna mahali limetumika kama Njozi au maono ya usiku lakini maana yake ni Ndoto.
Tunaona Ibrahimu aliongea na Mungu kwenye ndoto.
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu. Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viunoy vyako ndiye atakayekurithi. Akamleta nje, akasema, Tazamay sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki. Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,MWA. 15:1-6, 18 SUV
Pia tunaona katika mstari wa 18 Bwana alifanya agano na Ibrahim katika ndoto.
Agano walilofunga katika ndoto liliwafanya wana wa Israel kuishi misri miaka 400.
Na waliomba waondolewe uchungu wa kazi lakini Mungu aliliangalia agano ndio maana utasema Mwl mbona biblia inasema ombeni lolote? “ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”YOHANA. 15:7.
Lakini nakuambia omba kwa kufuata agano maana kuna tofauti ya maombi ya mtu wa chekechea au primary na secondary na maombi ya University.
Mungu ametoa nafasi ya kumsikiliza kila mtu maana kila mtu kwa ngazi yake karuhusiwa kuomba. Sasa Biblia inasema “tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”1 Yohana 5:14b
Ndio maana nakuambia omba kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Kwa5 kila jambo lina utaratibu wake. Huwezi endesha gari kwa utaratibu wa Marekani ukiwa hapa Tanzania lazima ufuate taratibu wa hapa Tanzania
2.Kukujulisha kuwepo kwa agano
Habari za Yokobo kuota Ndoto.
10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.
12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.
13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.14 Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mwanzo 28 :14
15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Mungu hakufunga agano na Yakobo bali alifunga na Ibrahim babu wa Yakobo na alimuambia Yakobo kuwa nitakuwa Mungu wako. Maana yake kuna mahusiano tumekubaliana na baba yako yanayotaka nikufuatilie katika maisha yako.
Yakobo alikuwa hamuamini Mungu na ndio maana alisema “Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”
Alisema hivyo kwa kuwa hajawa bado my personal God na tunaona hapa njia ya ndoto ilimjulisha kuwa Mungu alifunga agano na baba yake. Ndio maana alisema Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako
3.Unaweza kukumbushwa kwa njia ya Ndoto juu ya kuwepo kwa agano linalohusu
Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka. Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.
MWANZO. 31:10-13
Mungu anamkubusha kwa njia ya ndoto kuwa kuna agano linalokuhusu na anamwambia kuwa ni Mungu wa Bethel na kulikuwa na alama kuwa maana kulikuwa na jiwe na akalala.
Halikuwa jiwe na kawaida maana alipolala na Mungu alijifunua na ukifikiri natania jaribu kuchukua jiwe na uweke kama mto uone kama utalala. Ndio maana unaona hilo hilo jiwe Yakobo alimina mafuta na akaweka kama nguzo ili iwe alama ya nadhiri yake.
_Akasafiri Israeli, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa. Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.
MWANZO. 46:1-5.
Alitoa sadaka kwa Mungu wa baba yake nat kama wewe umetoa sadaka kwa Mungu wa baba yako unakuwa unaamsha agano lililopo na kama unaenda nyumbani kwenu ujue atakutembelea kwa njia ya ndoto.
Na Mungu alisema nae kwenye ndoto na alimkumbusha kuwa niko pamoja na wewe.
Na alipotoa sadaka ina maana alikuwa anahitaji msaada na kwa sababu alikuwa na agano na Mungu.
_Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.
ZABURI. 50:5 _
Kwa hiyo agano huwa linafanywa kwa sadaka.
- Atakujulisha ujumbe wa agano lilopo.
Kwa ishara au wazi wazi.
Na ukitaka kutafsiri Ndoto za kwako hakikisha unasoma biblia maana mwenye kutafsiri Ndoto ni Mungu. Na tafsiri ya Mungu ipo kwenye biblia.
Mifano.
Nabukedneza aliota mti mkubwa una ndege na chini kuna wanyama.. na akasema ukatwe.
Ukiona namna hiyo Mungu anasema na wewe kwenye ndoto kuwa kuna agano Lipo. Maana agano haliwezi kukuruhusu ufanikiwe zaidi ya kiwango kilicho kwenye agano.
Watu wanaotumia “vigoda” ina maana ni kiti cha enzi.
Kwa hiyo katika ndoto utaona.. na damu inatumika kuzungumza na miungu maana dhambi iliua mawasiliano na Mungu katika agano la kale Mungu aliruhusu damu za wanyama na ndege ili ziongee.
Biblia inasema damu ni uhai sasa ukitumia damu ya mbuzi kwenye agano utakuwa unaona mbuzi kwenye ndoto zako kama unaomba Mungu akutoe ulipokwama. Ina maana mbuzi ndio ilitolewa sadaka kwa ajili yako ndio maana Mungu anakusisitiza kuwa fuatilia hiyo alama ili uipangue kwa kutumia damu ya Yesu .
Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili;
basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?Waebrania 9:13- 14
Kama ni sadaka ya jogoo utaona jogoo katika Ndoto zako utaona jogoo kila ukiomba Mungu akufanikishe.
Haijalishi umefungwa kiasi gani Mungu atakuja kukufungua. Kama alivyomfungua punda aliyepandwa na Yesu.
Kuna watu wanaota ndoto wako njia panda na hawajavuka hapo katika biblia katika njia panda kuna kiapo.
21 Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.
Ezekieli 21 :21
22 Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome. 23 Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe.
Ezekieli 21 :23
Ukiona namna hiyo ujue kuna kiapo hapo mambo hayo yapo kwenye biblia.
Kusikia huja kwa neno la Kristo maana lazima usome biblia maana kusikia huja kwa neno la Kristo.
Kuna watu wanaota wanafunga ndoa kwenye Ndoto. Angalia vizuri hiyo Ndoto sio nzuri
Mwaka wa 1984 niliota ndoto upinde wa mvua na ulikuja mara nyingi nikitembea na nao unatembea.
Pia niliona katika nyumba yetu upo juu na umeishia mbinguni. Na nilianza kuomba na kusoma biblia na nakagundua.
Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi. MWANZO. 9:12-17
Kwa hiyo upinde ni alama ya agano.
Mungu alisema muulize mama yako. Na bahati nzuri mama yangu alikuja kunitembelea kwetu .
Na mama aliniambia alipokuwa anasoma kule Tosamaganga katika shule ya Wakatoliki aliyokuwa anasoma walitaka asomee usista maana walimpenda.
Mama yangu alikuwa anataka kuolewa maana angesomea usista asingeolewa. Kwa hiyo alienda porini na kuanza kuomba kwa Mungu maombi ya nadhiri. Na alisema watoto nitakao zaa hao nimekupa Mungu watumie ila mimi niolewe.
Basi nikaelewa Mungu aliniambia kuwa kabla hujazaliwa wewe ulikabidhiwa kwangu.
Na nilijua kuwa kuna agano ila sio maisha mepesi maana inabid niishi kwa kufauata agano.
Namshukuru Mungu aliyeniongoza kunipeleka kwenye biblia. Na nikaelewa.
Kama unaota ndoto na mtu aliyekufa nyumbani kwenu angalia vizuri. Na ukiota Ndoto unavaa mavazi au bibi Harusi ina maana umeolewa kwenye ulimwengu wa roho check vizuri.
Mbaya sana ukiota ndoto unazini ni mbaya sana. Mtu mmoja alisema anazini na mnyama maana yake unatengwa na jamii na mauti.
Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.
Kutoka 22:19
Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27:21
Na mwingine alisema anazini na mtoto wake ina maana utatengwa na jamii.
20 Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :20
Unahitaji kujua namna ya kutoka mahali hapo unapoota Ndoto za namna hiyo kwa njia ya neno Mungu ( neno kukunasua mahali ulipokwama)
Mwingine aliota Ndoto kazini na mtu kwenye ndoto na baada ya muda ndoa yake ilipata shida.
Mwingine aliota Pete ya ndoa imekatika ina maana agano limevunjwa na baada ya miez 6 mume wake alihama chumbani.(hakuomba mapema na alipata madhara)
Mwingine aliota nyoka kapita tumboni kwake baada ya hapo ndoa yake ikafa. Na nyoka ina maana ni miungu ya ukoo
Ukiota ndoto za aina hiyo uwe na uwe speed kuomba na kufutilia
Kuota unazini kwenye ndoto sio sahihi haijalishi unamfahamu huyo mtu unayezini nae au humfahamu ila sio ndoto nzuri hata kidogo Angalia pia alama iliyopo hapo unapoota mfano umeona gauni la harusi limechanika.
Sauli alishika vazi la samwel lilichanika.
_27 Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka.28 Basi Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.
1 Samweli 15 :28_
Yesu aliposema damu ya agano “Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.Luka 22:20”
Tumia damu ya Yesu kupangua vitu vibaya vilvyoletwa na ndoto
5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,
Ufunuo wa Yohana 1 :5
basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?Waebrania 9:14
Niliposikia hili somo la Ndoto miaka ya nyuma Mungu aliponifundisha . Nilisikia sana kumshukuru Mungu maana ilikuwa ni neema . Na endelea kumshukuru Mungu kwa kuweka wazi mambo haya ya Ndoto.
Ndio maana naimba wimbo wa ni salama rohoni mwangu kwa sababu ya neema ya Mungu iliyofunguliwa sasa inayotupa kujua mambo haya kwa uwazi.
Baada ya hapo yalifanyika maombi sana kwa ajili ya watu waliopata shida kwenye ndoto na Mungu aliwafungua sana watu wake.
Ubarikiweeee na Bwana Yesu tuonane tena kesho..
==Glory to God Glory to God==
Post A Comment:
0 comments so far,add yours