Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Mithali 29:18

Je, ni ndoto ipi Mungu ameweka moyoni mwako? Siulizi ikiwa una ndoto – Najua ipo, kwa maana Mungu huwekeza ndoto ndani yetu. Nimeona watu wakifanyia ndoto zao mambo tofauti. Wengine huficha ndoto zao moyoni ili wasikashifiwe na wengine.

Watu wengine huzitupilia ndoto zao ili wasizifikirie tena, na wengine huachana na ndoto zao kwa vile ni ngumu kuzishikilia.
Ikiwa utaanza kuishi kwa ajili ya ndoto yako, kuna mambo mawili ningependa ukumbuke. Kwanza kabisa, yafaa upate maono kamili kwa ndoto hiyo, na jambo la pili unafaa kuweka maono yako mbele ya ndoto hiyo kila mara.

Lakini kuwa na maono hakumaanishi kwamba itajitokeza tu. Mungu ana haja na safari ya maono yako hadi mwisho wake.

Mtume Paulo katika Wafilipi 4:11-13 alisema kwamba amejifunza kuridhika katika hali zote kiasi cha kwamba hangesumbuliwa na hali yoyote ile. Hii ni kusema kwamba hakusumbuliwa na hali yoyote ile aliyokuwa ndani yake – Kila mara alitazamia kuona kule alikuwa anaelekea.

Basi kama Paulo, tunafaa kuwa na usawa kati ya kuridhika na kufuatilia ndoto zetu. La muhimu ni hili, jifunze kufurahia pale uliko huku ukiendelea kusonga mbele kufikia ndoto zako.
Ikiwa una ndoto au maono, jifunze kuyaweka mbele. Ikiwa itasaidia, andika chini. Kumbuka kwamba, Mungu atakusaidia kuishi kuafikia ndoto yako, hatua baada ya ingine, siku baada ya siku.


OMBI LA KUANZA SIKU
Ewe Yesu, hata kama sihisi kufanya lolote na maisha yanajaribu kunifanya nikate tamaa, ninaamini una mpango mwema kwa maisha yangu. Ninakuamini unisaidie kuafikia ndoto yangu badala ya kuziamini hali zangu.






Author: Joyce Meyer

Share To:
Magpress

Bila jina

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours