Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda,
atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya
makao kwake. Yohana 14:23
Maisha yetu yana shughuli nyingi na vizuizi vingi.Ni
rahisi sana kushikika katika shughuli, wasiwasi na majukumu hadi tukasahau kile
kilicho cha muhimu zaidi.
Kuna hadithi fupi ya kupendeza mwishoni mwa Luka 2
wakati Maria na Yusufu walimpeleka Yesu Yerusalemu kwa pasaka akiwa na umri wa
miaka 12. Baada ya sherehe walianza safari kurudi nyumbani wakidhani kwamba yupo
nao.
Nami najiuliza, ni mara ngapi tunadhani Mungu yupo nasi
ili hali tumeenenda katika shughuli zetu wenyewe.
Sasa jambo la kushangaza ni hili; Maria na Yusufu
walikuwa wamesafiri siku nzima pasipo kutambua kuwa Yesu hakuwa nao na
iliwachukua siku tatu kumpata. Siku tatu! Sasa ujumbe hapa ni huu; ni rahisi
sana kwetu kuupoteza uwepo wa Mungu kuliko kuupata tena tunapoupoteza.
Inafaa tuwe waangalifu kusalia katika uwepo wa Mungu.
Tunapofanya hivyo, Mungu hupata maskani mioyoni mwetu.
Hii huanza kwa kuwa watiifu kwa neno la Mungu. Njia
moja ya kuonyesha ukomavu wa kiroho ni kuachana na tabia ambazo hazimpendezi
Mungu, hii huonyesha kwamba unayajali yale anayofikiria.
Hii inamaanisha unakuwa mkarimu kwa watu, unajifundisha
kusamehe, unaachana na migogoro na unaishi kwa amani. Tunapojifunza kuwa makini
na maneno yetu, kumshukuru Mungu na kuwainua wengine, tutazidi kuwa katika
uwepo wa Mungu siku nzima.
OMBI
LA KUANZA SIKU
Baba, asante kwa kufanya moyo wangu makao yako.
Ninahitaji uwepo wako leo. Nisaidie nikuheshimu kwa mawazo na maneno yangu, na
kuwa wa Baraka kwa wale walio karibu name.
Author: Joyce Meyer
Post A Comment:
0 comments so far,add yours