Hivyo
watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo
ninyi kwa ninyi. Yohana 13:35.
Kama wakristo, tumeitwa
kuwaonyesha wengine upendo. Kama vile maandiko yanasema, ulimwengu utajua
kwamba sisi ni wafuasi wa Yesu mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (Yohana 13:35).
Watu wengi hupenda upendo
kana kwamba ni hisia tu, lakini ni zaidi ya hisia tu. Upendo halisi hudhihirika
katika matendo.
Matendo haya hayapaswi
kuwa magumu na yakutuchosa. Njia moja ya kuonyesha upendo wa Kristo ni kupitia
njia rahisi ajabu.
Kwa mfano, kumpa mtu
zawadi kidogo, au kupata muda wa kuongea na mtu aliyeshoshwa moyo.
Au kumpatia kapu la
chakula kwa mama asiye na mume anayengángána kuwapa wanawe chakula.
Kuonyesha upendo kwa weza
kuwa halisi kama kumpa tabasamu mtu unayempita njiani, kwenye maduka au chumba
cha mkutano.
Kuna njia nyingi za
kuuonyesha upendo wa Kristo. Unapomuonyesha mtu yeyote yule upendo wa Kristo,
kunawezesha kuufanya moyo wake mwepesi, na kwa muda kidogo, naye pia ataanza
kutafuta nafasi za kuwaonyesha wengine upendo.
Kwa hivyo sherehekea
upendo huu na umuache Mungu akuongoze. Je, anakunenea kumhusu mtu yeyote leo?
Ningependa upendo wangu
kwa Yesu udhihirike katika namna ninayoonyesha wengine upendo – hata wale walio
wagumu wa kupendwa. Ikiwa nitaweza kuufanya moyo mgumu kuwa mwepesi kupitia
upendo wa Mungu, huenda moyo huo pia ukaifanya mioyo mingine mepesi, na upendo
wa Mungu utazidi na kuzidi. Na baada ya muda tutakuwa na mapinduzi ya upendo.
OMBI
LA KUANZA SIKU
Mungu, ningependa upendo
wako udhihirike wazi katika namna ninavyoonyesha wegine upendo. Nionyeshe njia
za kuweza kuonyesha upendo huo kwa yeyote na kwa kila mtu utayenikutanisha
naye.
Author: Joyce Meyer
Source: https://tv.joycemeyer.org
Post A Comment:
0 comments so far,add yours