Iyohana 2:14
Kila
kundi katika kanisa, jamii na hata nchi Mungu amelipa nafasi na wajibu wake
maalumu wa kutekeleza. Pia Mungu anao mtazamo wake binafsi na matarajio yake
kwa hayo makundi mbali
mbali ndani ya nchi. Vijana, watoto, wababa, wazee, wanawake, viongozi wote /
yote yana mtazamo wake mbele za Mungu. Ukimuuliza Mungu nini mtazamo wako kwa
vijana, atakujibu soma vizuri IYohana 2:14 maana yake
Mungu anawatazama vijana kama watu wenye nguvu, watu ambao neno la Mungu
linakaa ndani yao na pia wamemshinda mwovu.
Sasa ukirudi mazingira halisi
unaona kwa asilimia kubwa vijana wengi hawako kwenye nafasi ambazo
Mungu aliwakusudia. Lengo la somo hili ni:-
Kueleza
sababu za kwa nini vijana wengi hawajakaa katika nafasi zao.–
Kumweleza
kijana mambo ya kujiepusha nayo ili aweze kukaa kwenye nafasi yake.–
Kumpa
kijana maarifa yatakayomsaidia kurejea kwenye nafasi yake na ili aweze
kutekeleza matarajio ya Mungu kwake. Zaidi ujumbe huu umekusudia kulenga
na kuelewesha vijana waliokoka, nazungumza na vijana waliookoka
maana hawa ndio ambao Mungu amewatamkia maneno haya au kuwa namtazamo huu juu
yao. Zipo sababu nyingi lakini hizi zifuatazo ni za msingi na
zimesababisha wengi kuishi maisha nje ya kusudi la Mungu na kufa bila
kutekeleza matarajio ya Mungu kwao sababu hizo ni:-
Moja
vijana wengi hawajajazwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Biblia
inasema katika matendo ya Mitume 1:8 kwamba “lakini mtapokea nguvu, akiisha
kuwajia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu
katika Yerusalemu, na katika uyahudi wote, na samaria, na hata
mwisho wa nchi”. Hivyo vijana wengi hawajakaa katika nafasi zao kwasababu
wengi wa vijana leo makanisani hawajajazwa nguvu za Roho Mtakatifu
si kwamba Mungu hataki kuwajaza lakini shida ipo kwa vijana wenyewe
wengine kutotaka kujazwa nguvu hizo, lakini wengine hawajui nini wafanye
wajazwe nguvu za Roho Mtakatifu na wengine
wanajua lakini hawana kiu ya kujazwa nguvu hizo.
vijana
wengi hawajui namna ya kuenenda kwa Roho.
Paulo
kwa warumi anasema” kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana
wa Mungu” Warumi 8:14 na pia kwa wagatia anasema” Basi nasema enendeni
kwa Roho hamtatimiza kamwe tamaa za mwili “Gal 5:16. Kuna wengi
waliojazwa lakini si wote wanaoenenda au wanaoishi wa Roho. Vijana wengi Mungu
amewapa vitu vizuri sana ndani yao lakini kwa sababu ya
kukosa utiifu na kutoenenda kwa Roho wameshindwa kusimama kwenye
nafasi zao.
vijana
wengi wameshindwa kushirikiana na upako wa Munguuliodhihirishwa kwao.
Hili
ni tatizo kubwa kwa kweli, Mara nyingi Mungu amekuwa
akiwapa upako, nguvu au uweza wa kufanya mambo mbalimbali vijana.
Sasa si vijana wote wanaojua namna ya
kushirikiana na huo upako ambao Mungu aliwapa kwa jambo
fulani Mfano, Mungu anaweza akampa kijana upako wa kuomba
lakini kijana huyo badala ya kuomba yeye anaangalia mpira,
au ni mwanafunzi anatakiwa kusoma na Mungu ameleta upako huo sasa
yeye anaenda kuomba mambo huwa hayakai hivyo. Upako lazima utumike kwa
kusudi lile uliotumiwa. Upako wowote unaokuja kwako
unakuja kwa kusudi maalumu.
Kukosa maarifa ya Mungu.
Mungu
anasema katika Hosea 4:6 kila kipengele cha kwanza watu wangu
wanaangamia kwa kukosa maarifa na pia katika Zaburi 119:9 anasema “Jinsi gani
kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno lake”. Sasa kwa
sababu nazungumza na vijana naweza nikaweka mistari huu hivi “Vijana
wangu wanaagamizwa kwa kukosa maarifa. Maarifa yanayozungumzia hapa ni
mafundisho ya neno la Mungu.
Vijana
wengi wako tayari kuangalia mechi mbili mfululizo kuanzia saa nne
kasoro usiku hadi saa nane kwa masaa ya Kitanzania, lakini hawako
tayari kusoma Biblia kwa saa moja, wako tayari kuangalia “Movie” za kinigeria,
au za kizungu hata masaa matatu (3) lakini si kuangalia na kusikiliza
mafundisho ya Neno la Mungu. Na Biblia inasema Apendaye mafundisho hupenda
maarifa. Sasa kwa vile vijana wengi hawapendi mafundisho ndiyo maana hawako
kwenye kusudi la Mungu.
vijana
wengi bado wanaipenda dunia.
Mzee
Yohana katika 1Yohana 2:15” Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia,
mtu akiipena dunia kumpenda Baba hakupo ndani yake”. Na pia Daudi
anasema katika Zaburi 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la
wasio haki wala kusimama katika njia ya wakosaji
wala hakuketi barazani pa wenye mzaha.Ni vijana
wachache sana katika kanisa la leo ambao wako tayari kujikana nafsi
zao kwa ajili ya Mungu wengi wanapenda kupoteza muda kwa habari zisizo
za Msingi, wengi wanapenda mzaha na utani, ni vijana wachache ambao
wanaweza kuacha kuangalia mchezo kwenye TV, au akakataa kwenda
kutembea ufukweni kwa lengo la kuomba, au kusoma Neno, ninachojaribu
kusema hapa ni hiki, najua kila jambo lina wakati wake, lakini ni vijana
wachache sana waliojizuia katika mambo ya mwili kwa ajili ya kufanya yaliyo
mapenzi ya Mungu.
Vijana
wengi hawajazivaa silaha za vita.
Waefeso
6:11 Vaeni Silaha zote za Mungu, mpate kuzipinga hila za
shetani.Viajana wengi wameshindwa kumshinda mwovu kwa sababu hawazajivaa silaha
za vita. Wengine hawajui silaha za vita ni zipi? Lakini wengine wanajua lakini
hawajazivaa. Ile sura ya sita ya waefeso 6:10-18 Paulo anazungumzia silaha za
vita, ambazo ni kwlei, haki, amani, Imani, wokovu na Neno la Mungu. Sasa hizi
ni silaha na kama ni silaha zina namna zinavyovaliwa na namna zinavyotumika.
Sasa si vijana wote waliozivaa silaha, wengi hawasomi neno la Mungu, hawatendi
haki, wengi wana imani ya maneno isiyo ya Matendo.
Vijana
wengi wanaishi bila kuwa na malengo katika maisha yao / maono.
Mithali
29:18. Inasema “Pasipo maono watu huacha kujizuia bali ana heri mtu yule
aishikaye sheria”. Hivi leo ukiwauliza vijana wengi kwamba una maono
au hasa malengo gani katika maisha yako? Asilimia kubwa watakujibu sina
malengo yeyote yale.Wakati huo huo hakuna aliyeumbwa kwa
bahati mbaya Yeremia 29 :12. Kwa kila mtu Mungu analokusudi maalum
la kumuumba na pia anayo malengo na mikakati ya kumpa huyu mtu atekeleze katika
maisha yake. Sasa kwa sababu vijana wengi hawana na hawajajua hayo
malengo ndio maana wanafanya kila kinachotokea mbele yao bila
kujua kama ni kusudi la Mungu.
Naamini baada
ya kuwa umesoma ujumbe huu umepata maarifa ya kukusaidia kukaa katika nafasi
yako kama kijana kwa sababu umeshajua sababu za kutokukaa kwenye nafasi yako.
Amen, nimebarikiwa sana
JibuFuta