1. KWANINI MUNGU ANATUPA UTAJIRI MALI NA FEDHA ? 



1. ILI KUIMARISHA AGANO LAKE (UFALME WAKE)* Kumb 8:18 (12-18)

Agano la Mungu kwa siku za leo, ni Agano JIPYA. Kuimarisha Agano lake maana yake; nikuimarisha kazi ya injili ya Yesu Kristo, ili wokovu uwafikie watu wote. Tunapotoa muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalme wa Mungu, tunakuwa tumetimiza makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha agano lake” (Kumb 8:17-18)
Soma pia, Gal 3:11,23-26,29; Rum 10:13 – 15; Fillip 4:15 –19)Mali zetu si pesa tu. Mali ni kitu chochote chenye thamani na kikitumiwa vizuri, kinawezakuongeza ubora wa kitu. Kwa mfano;
a) Muda wako ni mali ya thamani sana, ukiutumia vizuri, utakuletea kipato.

b) Vipawa vyako pia ni mali, ukikitumia vizuri, kitakuletea kipato.
c) Fedha yako pia ni mali, ukiipangilia a kuitumia vizuri, itakuboreshea maisha yako.

Tunapotoa muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ilikuimarisha Ufalme wa Mungu, tunakuwa tumepanda mbegu katika ufalme wa Mungu nakwa wakati wa Mungu, zitarudi kwetu moja ikiwa imezaa 30, na nyingine itarudi imezaa 60,na nyingine 100. Hii ni kwasababu, mali zako na vipawa vyako na muda wako, ni sadakambele za Mungu.Hayo ndio makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha aganolake” (Kumb 8:17-18).
Unapotoa sadaka kama hizi kwa Mungu, toa kwa imani, yaani toa kwa kutarajia kupokea tenakutoka kwa Mungu. Usione muda wako kama unapoteza au unajitolea tu. Bali vione hivi vitukuwa ni sadaka, kwasababu kwa uhalisi, vitu hivi ni mali. Muda ni pesa; vipawa ni pesa pia,na mali zetu ni pesa. Unapotoa muda, vipawa na mali zako kwa Mungu, ona kwamba unatoasadaka. Na sadaka ni mbegu. Na mbegu ikitolewa kwa usahihi, huzaa sana (Math 13:8). 1

2.

Hivyo, toa kwa imani, yaani toa kwa kutarajia kupokea tena kutoka kwa Mungu. Usionemuda wako kama unapoteza au unajitolea tu, bali ona kwamba umetoa sadaka. Tunapotoamuda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalmewa Mungu, tunakuwa tumepanda mbegu katika ufalme wa Mungu na kwa wakati wa Mungu,zitarudi kwetu moja ikiwa imezaa 30, na nyingine 60, na nyingine 100; kama tulivyosomakatika Mathayo 13:8.
2. ILI KUVITUMIA KWA MAHITAJI YETU BINAFSI *Yoh16:24
Soma tena 1Timotheo 6:17 na   2Wakorintho 9:8 – 11

Mungu kama Baba yetu na kama Mchungaji Mwema, anajali sana mahitaji yetu na haja zetuau shauku za mioyo yetu. (vitu vitupavyo furaha na kuridhika). Ndio maana hutupa utajiri, ilitufurahie maisha. Si mapenzi ya Mungu tuwe masikini. Ndio maana Yesu alifanyika maskini(kimwili) ili kwa umasikini wake, (sisi) tupate kuwa matajiri (kimwili)” (2 Kor 8:9)

Ni mapenzi ya Mungu tupate vitu vyote vitakavyotufanya tufurahie maisha yetu duniani.Nyumba nzuri, mavazi mazuri, chakula kizuri, kazi nzuri, magari mazuri, biashara nzuri,mifugo mizuri, mashamba mazuri, mshahara mzuri, n.k. (Zab23:1- 2; Fil 4:6-7,19; Zab37:4; Zab145:17- 19)
3. ILI KUWAGAWIA WAHITAJI *2KOR 9:8-13;



Pia soma 1Timotheo 6:17-19; Waefeso 4:28 na Luka 6:38.

Tunapowapa wahitaji fedha, nguo, viatu, chakula au vitu vya aina nyingine ili kuwasaidiakimaisha, tunapata thawabu kubwa kwa Mungu. Kumsaidia mhitaji kitu, ni kumpa Mungu.Hebu soma vizuri Mathayo 25:31-40; Mathayo 10:40 – 42 na Yohana 13:20.
Mungu ametupa mali, fedha na utajiri wa namna nyingi ili tuwasaidie wahitaji na masikini,wajane na yatima, wagonjwa na walemavu. Thawabu yake ni kubwa mbele za Mungu, naMungu ataona sababu ya kukupa tena na kukuzidishia. Tena Mungu atakufanya uwenjia/mkondo wa baraka zake kwa watu wengine. Soma pia 2Kor 8:14-15, Mdo 20:35 2
 TUMTUMIKIE MUNGU KWA MALI ZETU 

Ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanyaMungu, kutufungulia madirisha na milango ya mbinguni, ili kutumwagia baraka nyingi,tunazohitaji katika mashamba, mifugo, biashara, miradi mbalimbali tuliyonayo. Pia ushirikiwetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanya Mungu azibariki familia zetu, watoto wetu, ndoa zetu na afya zetu pia, ili tuzidi kumtumikia na kuwabaraka kwa wengine pia. Baraka za Mungu zitatuzidishia mapato yetu, ili tuwe na vitu vyakutosha kutumia na hata kuwa baraka kwa wahitaji wengi.

Utoaji ni njia ya Mungu kutupa na kutujaza tunavyohitaji *1Fal 17:1-16
Mungu ndiye alieyewaka kanuni ya kupanda na kuvuna, kutoa na kupokea. Hivyo, maranyingi tunapomwomba Mungu atubariki/atujaze mahitaji yetu, anatuletea mafasi ya kutoakwanza, ili tupokee mahitaji yetu tumwombayo. Kwasababu, ndiyo kanuni ya kupokea. Niajabu, sicho tunachotegemea (kutoa wakati wewe binafsi unahitaji). Badala ya Mungukukupa moja kwa moja kitu ulichomwomba, anakuletea nafsi ya kutoa hicho hicho kidogo ulichonacho, kiwe kama mbegu, ili hatimaye upokee (uvune) kile ulichomwomba, na hata zaidi ya ulivyoomba.
Biblia pia inasema hivi katika kitabu cha Waefeso 3:20 na Wafilipi 4:15-19; kwamba, “Basi atukuzwe Mungu awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tumwombayo au kulikoyote tuyawazayo, kwa kadri ya nguvu, itendayo kazi ndani yetu” (Efe 3:20; Fil 4:15-19).
1Wafalme 17:13-16; Eliya akamwambia (yule mama mjane); usiogope (kutoa hicho kidogokilichobaki) … enenda ukafanye kwa ajili yangu (kwa maana ukinipa mimi, utakuwaumempa Mungu) na Mungu wa Isarael anasema, unga wako wala mafuta yakohayatapunguka kamwe, mpaka njaa itakapoondoka juu ya nchi. Yaani Mungu atavizidisha. Siajabu anliongezea Kama ukikubali na kutii, utakula mema ya nchi. Lakini ukikataa,utaangamia (kama wengine wanavyoangamia). (Isaya 1:19)
Si jambo rahisi kutoa wakati wewe mwenyewe umepumgukiwa au una uhitaji. Inahitajikaimani kubwa kutoa kidogo kilichobaki, ili uhitai wako ujazwe. Hivyo, usishangae sikuutakapomwomba Mungu pesa au vitu, halafu badala ya kukupa, anakuletea mhitaji ili umpe pesa au vitu, au analeta nafasi ya wewe kutoa sadaka. Kumbuka kanuni yake, huwezi kuvuna bila kupanda!
Hivyo, ukikubali na kutii, utavuna na kupata mema, tena zaidi ya ulivyotarajia. Hii ni kanuniya Mungu; ukipanda haba utavuna haba, ukipanda nyingi, utavuna nyingi. Huwezi kuvuna bila kupanda
Utoaji wa sadaka, hufungulia na kutuletea mahitaji yetu (2Wafalme 4:8-41)
Huyu mama Mshunami pamoja na mume wake, japo walikuwa ni watu wenye fedha nyingina cheo kikubwa, lakini walikuwa hawajapata mtoto, pengine kwa miaka mingi sana.Inaawezekana walishaombewa na watumishi wengi wa Mungu, lakini bado maombi yaohayakuleta muujiza waliokuwa wanausubiri kwa hamu kubwa. Kumbe ufunguo wa muujizawao, haukuwa katika maombi pekee, bali katika utoaji wao pia. Yamkini Mungu alishawapamtot wao katika ulimwengu wa kiroho, ila sadaka ndio ilikuwa inahitajika, ili kutelemshaBaraka yao ya mtoto.
Neno la Mungu linasema, Mungu akaweka mzigo ndani ya mama huyu, kumjengea NabiiElisha nyumba, ili asipate shida katika utumishi wake. Na huyu mama akamshirikishamumewe. Nao wakaiweka azma yao katika matendo. Walipotii na kufanya kile kitu ambachoMungu aliweka mioyoni mwao, kwa ajili ya Elisha mtumishi wa Mungu, ndipo muujiza waowa kupata mtoto, ukatimia.
Biblia inasema, Elisha akapewa Neno la Mungu kwa ajili ya familia hii, juu ya kupewa mtotowao (ambaye tayari alishatolewa kwao, kwa njia ya maombi, lakini ni katika ulimwengu wakiroho). Sadaka yao, iliushuhsa ule muujiza wao, kutoka rohoni, ukawa halisi katika mwili,kwasababu ya Utii wao. Sadaka ina nguvu ya kutupa mahitaji yetu.
Kwahiyo Ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali,utamfanya Mungu, kutufungulia madirisha na milango ya mbinguni, ili kutumwagia barakanyingi, tunazohitaji katika mashamba, mifugo, biashara, miradi mbalimbali tuliyonayo.Pia ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanyaMungu azibariki familia zetu, watot wetu, ndoa zetu na afya zetu pia, ili tuzidi kumtumikia nakuwa baraka kwa wengine pia. Baraka za Mungu zitatuzidishia mapato yetu, ili tuwe na vituvya kutosha kutumia na hata kuwa baraka kwa wahitaji wengi (Malaki 3:10–12, Luk 6:38) 4
                                                 Wako katika kazi ya Mungu

                                                     Mwl. Mgisa Mtebe
                                                    +255 713  497  654
                                                 mgisamtebe@ yahoo.com
                                                   www.mgisamtebe.or.tz



Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

1 comments so far,Add yours