Articles by "MWALIMU MGISA MTEBE"
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MWALIMU MGISA MTEBE. Onyesha machapisho yote

Hatua na vipengele muhimu katika kuomba 

MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU. *Rum 8:26-27 *Yoh 14:16-17
Yesu alisema Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu. Atatusaidia na kutufundisha yote, kwa maana pasipo yeye, sisi hatuwezi neno lolote. Na sisi peke yetu hatujui kuomba ipasavyo, bali yeye (Roho) ajua kutuombea kwa Mungu kama vile Mungu apendavyo. Hivyo kabla ya kuanza maombi au kusoma neno au ibada au safari au mitihani au kikao n.k. jifunze kujikabidhi kwa Roho Mtakatifu, uombe msaada wake, akupe ufanisi/ubora katika yote yakupasayo kufanya.
Tambua Utu wake, Uungu na Uweza wake.
Jikabidhi katika Nguvu ya Uongozi wake.
Tii kila Uongozi anaokupa.
FANYA TOBA NA UTAKASO. *Isa 59:1-2, Yoh 9:31, 1Yoh 1:8-9,7
Sikio la Bwana si zito kusikia wala mkono wake si mfupi kushindwa kututendea mambo tumwombayo, bali maovu yetu ndiyo yanatufarakanisha na Mungu wetu. Mungu hawasikii wenye dhambi. Hivyo chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako mbele za Mungu na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha. Mungu ni mwaminifu kutusamehe na kututakasa na uchafu wote. (Isa 1:18). Lakini, kabla hujafanya toba yako binfsi;
(i) – Kwanza, samehe wote waliokukosea, hata kama hawajaja
kukuomba msamaha. Usipowasamehe waliokukosea, na Mungu
hataweza kukusamehe wewe. (Math 6:12,14-15)
(ii) – Ndipo nawe ufanye toba yako binafsi. Na Mungu atakusamehe kabisa.
Hata kama ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe sana. (Isa 1:18, Isa 43:25)
3. MSIFU, MUABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Zab 147 na Zab 148
Msifu Bwana kwa Matendo yake makuu, mwabudu Bwana kwa uzuri wake na kwa sifa zake. Mwadhimishe Mungu kwa Tabia zake, wema wake, fadhili zake na baraka zake mbalimbali anazotutendea. Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo atakuwa tayari kukupa haja za moyo wako. Haja zetu zimefichwa nyuma ya mgomgo wa sifa. Ndio maana Neno linasema;
‘Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu na kumshukuru), naye atakupa
haja za moyo wako’ (Zab37:4).
Yesu anatuonyesha mfano; angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake imekuwa “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.” (Math 6:9). Anaanza maombi kwa kumsifu Mungu. Msifu Mungu kwa kuimba na kwa kunena/kusema/kuelezea. Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Ukifanya sifa nzuri, ya kuufurahisha moyo wake, atakupa hata na vile ambavyo hukutegemea/hukuomba.


4. MWELEZE MUNGU MAHITAJI NA HOJA ZAKO. *Wafilipi 4:6-7,19 Isa 43:26
Mweleze Mungu zile hoja zilizokusukumwa kwenda kumwomba. Nenda mbele za Mungu kama ‘kuhani’ (1Pet 2:9). Kwa unyenyekevu na heshima. Lakini kabla ya kumweleza mahitaji yako binafsi;
(i) Kwanza fanya ‘maombezi’ – ombea watu wengine; (1Tim 2:1-4)
Viongozi mbalimbali na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu, marafiki zako, wenye shida, ndugu zako, nchi yako, shule yako, shirika lenu, ofisi yenu, chama chenu, n.k. Usianze kujiombea mwenyewe tuu, zoea kuwatanguliza wengine.
(ii) Kisha fanya ‘maombi yako’– ombea haja za moyo wako. (Math 7:7-11)
Mweleze Mungu haja zako. Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli. Japo anazijua haja zetu, lakini ameagiza kuwa tumwombe ndipo atafanya. ‘aombaye hupokea’ yaani; asiyeomba, hapati. Mungu anasema tumpelekee hoja zenye nguvu (Isa 41:21). Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili upewe (pray for good things and big things)
5. FANYA MAOMBI YA VITA VYA ROHONI. *Efe 6:10-13 *2Kor 10:3-5
Baada ya kumwendea Mungu na kumweleza mahitaji yako, sasa simama kama ‘mfalme’, kwasababu wewe ni ‘mfalme’ (Ufu 5:8), tumia mamlaka yako ya kifalme, ongea na hali/hitaji ulilokuwa unaliombea, na kwa mamlaka, amuru iwe kama vile ulivyoomba/unavyotamani. Ndio maana Bwana Yesu alipokabidhiwa mamlaka yote na Mungu, naye akatukabidhi sisi (kanisa lake) “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui. Wala hakuna kitakachowadhuru” (Luk 10:19, Yer 1:10, Yak 4:7). Tuma neno lenye mamlaka katika hali/jambo ulilokuwa unaliombea, Amuru iwe vile ulivyokuwa unamwomba Mungu iwe. Kemea kila roho ya shetani inayoweza kuwa inasababisha tatizo katika swala lako.
6. OMBEA ULINZI JUU YA ULIYOYAOMBEA. *Math 6:13a
Baada ya kupiga vita vya kiroho, weka ulinzi katika yale uliyoyaombea, ili shetani na mapepo yake wasiweze kuirudia hali/jambo/mtu yule uliyemkomboa kwa maombi ya vita. Yesu alisema shetani akifukuzwa mahali, haendi mbali, anasubiri kuona kama atapata upenyo wa kuparudia mahali pale alipokuwa kwanza. (Math 12:43-45). Kwahiyo, usipoweka ulinzi, kuna uwezekano wa adui kurudi na kuliharibu zaidi lile jambo uliloliombea na kulipata.
Kumbuka, unapoomba vizuri, unapokea papo hapo (katika ulimwengu wa roho), lakini udhihirisho wake katika ulimwengu wa mwili, unaweza kuchukua muda fulani. Hivyo katika muda huo wa kusubiri, shetani anaweza akapita na kuzuia au kuharibu kile unachokisubiri kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana Yesu alitufundisha kuombea ulinzi, “tuokoe na yule mwovu” (Math 6:13a). Weka ulinzi juu ya mambo yako yote. Jengea wigo wa moto wa mbinguni (2Fal 6:16-17), Yafunike kwa damu ya Yesu na agiza malaika walinzi walinde mambo yako masaa yote. Omba hivyo kila siku. (Zab 34:7, Zab 91:9-11, Ebr 1:13-14)
MSIFU, MWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Math 6:13b
Yesu alianza maombi kwa kumsifu Mungu na kumtukuza. Na akamaliza maombi yake kwa kumtukuza Mungu tena. Akasema “kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu ni zako, sasa na hata milele” akamaliza. Kwahiyo nawe kwa kumaliza maombi yako, msifu na kumshukuru Mungu tena, kwa ukuu wake, uaminifu wake, na ahadi zake juu yetu. Ndipo ufunge maombi yako.
MUHIMU: TUMIA MAANDIKO KATIKA KUOMBA *Kol 3:16
-Katika kuomba kwako, mara zote tumia maandiko kumkumbusha Mungu ahadi zake .(Isa 43:26). Mungu analiangalia neno lake ili alitimize. Sababu pekee itakayomfanya Mungu akupe alichoomba, ni ili kulitimiza neno lake. Hivyo, baada ya kumweleza unachohitaji (kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu unayemwombea) mpe Mungu andiko/neno lake linalokupa wewe uhalali wa kuomba hicho kitu mbele zake na kupewa.
-Hata unapompinga na kumkemea shetani, baada ya kutoa amri yako dhidi yake, shetani atasubiri kusikia andiko/neno linalomnyima yeye uhalali wa kushika alichoshika. Ndio maana Yesu alimshinda shetani kwa neno la Mungu. Alisema “imeandikwa” na shetani akashindwa. “Nao wakmshinda (shetani) kwa damu ya Yesu na kwa Neno” (Ufu 12:11)
 MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI  KWA MUDA MREFU
1. CHAGUA MAHALI PAZURI PA UTULIVU. *Mk 1:35
ili uweze kuomba kwa utulivu na kwa umakini, chagua au tafuta mahali pazuri
patakapokupa utulivu katika kuomba (concentration in prayer). Ndio maana Mungu
alipenda kuongea na Musa juu ya mlima. (Kut 24:12-18). Hata Yesu alizoea kwenda
kuombea mlimani, mahali palipo mbali na vurugu za watu, alipenda kwenda mlimani.
(Math 14:22-23). Tafuta mahali patulivu; chumbani, kanisani, mlimani (Math 6:5-6)
2. CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7
Ili uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili
wako viko fresh. Usilazimishe kuomba hata kama akili yako au mwili wako umechoka sana. Kila jambo lina wakati wake. Kama umechoka sana, huo si muda wa kuomba, bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili baadaye uweze kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala shetani. Penda kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini kuongea na Mungu kwa akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri sana kwenda kuomba mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)
3. OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum 8:26-27
Mbinu nyingine nzuri ya kuomba kwa muda mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa Roho; yaani kuomba kwa kunena kwa lugha. Tunapoomba kwa akili za kibinadamu, Mungu anasikia pia, lakini maombi yako yanakuwa na mipaka / limited kwasababu akili ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni iliyo bora zaidi. (Yuda 1:20, Mk 16:17, 1Kor 14:1-4, 15-16,7)
4. OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18
Kufunga kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe makini zaidi kuongea na Mungu kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi kufanya mambo ya Mungu. Na mwili ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa kufanya mambo ya kiroho. Mbinu mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia posho yake ya chakula. Mwili ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na upenyo mzuri zaidi (Zab 35:13). Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba. Ndio maana Yesu anasema ‘mfungapo’ akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo. Inasaidia.
5. OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10
Neno la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna faida ya kuomba pamoja na rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu, inaleta hamasa na ari ya kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na waombaji wenzako. Pili; nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji mmoja anafukuza adui elfu moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili) bali elfu kumi! Shangaa! (Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya Ki-Mungu. Kadri mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.
Kwahiyo, wakati mwingine, omba na rafiki yako, unayemwamini, unayeweza kumshirikisha mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa imani, walikuwa na marafiki wa kiroho. (Prayer Partners). Kwa Mfano:-Math 17:1-9
Musa – alikuwa na Joshua, Haruni na Huri
Eliya – alikuwa na Elisha
Daniel – alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.
Yesu – alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.
Paul – alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.
Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho?
Kama huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke kujichaglia. Tulia umwombe Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu mtakayefungamanishwa naye katika roho, hata kama mmetengana kijiografia, lakini katika roho, mko na umoja mzuri wa imani. (Math 18:18-19)
6. OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.
Katika kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia kwenda mwendo mrefu. Yakupasa kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point and weak point). Wakati wa kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia mikao inayokua nguvu zaidi. Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa kupiga magoti au kwa kuegemea kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au unatembea tembea, ili kuepuka usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua mikao inayowasaidia kuomba maombi marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali wakiwa katika maombi, huwa wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni mbinu nzuri pia.
Mifano ya Mashujaa wa imani;
Ibrahim – aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)
Daniel – aliomba kwa kupiga magoti (Dan 6:10)
Paul – aliomba kwa kupiga magoti (Efe 3:14)
Yesu – aliomba kwa kulala chini (Math 26:38-39)
Eliya – aliomba kwa kukaa chini na
kuweka kichwa kati ya miguu (1Fal 18:42)
Mimi – huwa napenda kuomba kwa kutembea tembea
Naweza kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu
Nikitembea huku nikiomba.
Wewe Je? Unaujua mkao wa nguvu? Kama hujui, Tafuta kujua.
OMBA NA MUZIKI LAINI KWA KUMWABUDU MUNGU.
Muziki wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana ya kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa namna ya pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki ukapigwa, nao wakawa kama mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza lile hekalu hata makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule mbinguni, kila malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii, mpaka mpiga kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa Mungu) alipokija juu yake, naye akatabiri.
Najaribu kukuonyesha, kuna connection kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu. Kwahiyo, ukiweza kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za taratibu, utapata (experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una nguvu ya kuomba kwa muda mrefu. Kama unaweza, tengeneza kanda au CD maalum yenye nyimbo nzuri unazozipenda wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi. Utajikuta unaweza kuomba kwa muda mrefu na kwa bubujiko zuri zaidi
Mwl. Mgisa Mtebe,Bsc Economics

Mzumbe University,+255 713 497 654









Utangulizi

Mkristo ni nani?
Mkristo ni mtu aliyemwamini Yesu Kristo na kumpokea au kumfanya Bwana na Mwokozi wa maisha yake (Warumi 10:9-10). Haitoshi tu kusema, ‘Mkristo ni mtu aliyemwamini Yesu’, kwasababu Biblia inasema ‘hata shetani naye anaamini na kutetemeka pia’ lakini si mkristo (Yakobo 2:19)
Uchumi ni nini?

Uchumi ni Maarifa ya namna ya kutumia rasilimali (resources) zilizopo au chache (scarce) ili kukutana na mahitaji na matakwa mengi (needs and wants) katika maisha ya mtu/watu.
Ni mapenzi ya Mungu tuyafurahie maisha yetu aliyotupa yeyé hapa duniani kama anavyosema katika kiyabu cha Isaya 1:19 ‘mkikubali na kutii, mtakula mema ya nchi.’ Na kila kitu unachohitaji kwa ajili ya maisha mazuri ya utoshelevu, kipo hapa hapa ulipo.

Rasilimali zote tunazozihitaji kwa ajili ya Maisha mazuri ya Baraka, tunazo hapa hapa. Lakini wewe kama Mkristo, hautaweza kuyafurahia maisha aliyokuandikia Mungu, uyaishi hapa duniani, kama hutajua namna/jinsi/mbinu/kanuni za ki-Mungu za kufanikiwa kimaisha ili kukutana na mahitaji yako na matakwa yako ya kimaisha.

Tujifunza siri na kanuni za kufanikiwa kiuchumi kwa maisha ya tajiri mmoja, aliyeandikwa katika Biblia, na jinsi alivyofanikiwa sana kimaisha na kiuchumi, japo alianza maisha kwa shida na taabu. Mtu huyu tajiri anaitwa Yakobo. Habari hii utaipata katika kitabu cha Mwanzo 28:1-5; 29: 13-30; 30:25-43; 31:1-3; 32:1-18

Kwa ufupi ni kwamba:
Yakobo alipomkimbia ndugu yake Esau, alifika kwa mjomba Labani akiwa na fimbo tu, lakini baada ya kukaa huko kwa muda, alirudi katika nchi ya Baba zake akiwa tajiri mkubwa mwenye wafanyakazi 1,200 (Matuo mawili = Makundi mawili ya watu 600)  Soma Mwanzo 32:9-12. Fikiri mwenyewe,  mtu mwenye wafanyakazi 1,200 alikuwa ana wanyama wangapi? Thamanisha mali zake kwa fedha ya sasa.

Utakapokwenda kuisoma habari hii, utaona jinsi Yakobo alivyokuwa tajiri, kwa maana alikuwa na uwezo wa kutoa zawadi kwa mtu, kiasi cha punda 200, farasi 200, ngamia 200, ng’ombe 200, kondoo 200 na mbuzi 200. Utajiri huu kwa lugha ya sasa; Punda 200 (kiuchumi, hii inakadiriwa kuwa ni sawa na magari madogo ya mizigo (pickup) 16; yaani punda 12 wanaweza kubeba mzigo wa pickup 1). Kondoo 200 ni sawa na maduka 4 ya nguo, ngamia 200 ni sawa na malori madogo ya mizigo 16, farasi 200 ni sawa na pikipiki 50.

Unaweza kuona jinsi Yakobo wa Isaka alivyokuwa tajiri. Mtu anayeweza kukupa zawadi ya pikipiki 50, maduka 4 ya nguo, malori madogo 16 na magari madogo ya mizigo (pickup) 16; yeyé anabakiwa na kiasi gani cha utajiri? Na kama alianza akiwa mikono mitupu, alitumia njia gani kufikia katika mafanikio hayo ya kiuchumi? Hata mimi nataka kujua. Utashangaa kwamba, Biblia inafundisha uchumi kiasi hiki.

KANUNI ZA KIBIBLIA ZA UCHUMI MZURI

Maono - Kuona Fursa za kiuchumi
Mafanikio hayaji kwa bahati mbaya au nzuri, bali yanapangwa. Ukiona mtu amefanikiwa kiuchumi, ujue aliona kwanza fursa hiyo na akaichuchumilia na kuifuatilia mpaka akafanikiwa. Hivyo muombe Mungu akupe kuziona fursa zilizopo. Tafuta kuona mahitaji mbalimbali ya jamii, huwezi kukosa kuona fursa kadhaa za kiuchumi.

Utakapokwenda kusoma habari hizi, utagundua kwamba, mjomba Labani alikuwa tajiri mwenye shughuli mbalimbali na wafanyakazi wengi sana. Kwa muda mfupi ambao Yakobo alikaa kwa mjomba wake, aligundua kwamba, ataweza kufanikiwa kwa kujishughulisha na kazi mojawapo za mjomba, hivyo akachagua kujikita katika mifugo ya mjomba Labani. Mwanzo 29: 15-20.

Mafanikio hayaji kwa bahati mbaya au nzuri, bali yanapangwa. Lazima uwe na uwezo wa kuona fursa za kiuchumi na kujitosa humo baada ya kufanya upembuzi yakinifu. Ukiona mtu amefanikiwa kiuchumi, ujue aliona kwanza fursa hiyo na akaichuchumilia na kuifuatilia mpaka akafanikiwa. Soma Mwanzo 21:14-19 na Waefeso 1:15-19 utaona umuhimu wa kuwa na macho yanayoweza kuona vitu vilivyojificha. Hivyo muombe Mungu akupe kuziona fursa zilizopo. Tafuta kuona mahitaji mbalimbali ya jamii, huwezi kukosa kuona fursa kadhaa za kiuchumi.

Malengo mahususi – Kujua kwa hakika unataka kufika wapi
Alijua alichokuwa anataka na alikaza uso kutoyumbishwa mapaka apate anachotaka. Hii ni tabia ya kila mjasiliamali aliyefanikiwa. Lazima uwe ‘focused’ usiyumbishwe. Utaiona tabia hii ya Yakobo kwa jinsi alivyojaribiwa katika swala la kupata mke aliyemtaka. Alijua anataka mke, na sio bora mke.

Mjomba Labani alikuwa na mabinti wawili, Lea na Raheli. Aliambiwa kama anataka kumuoa Raheli, atoe mahari ya kufanya kazi kwa miaka 7. Baada ya maiaka 7 akapewa Lea badala ya Raheli. Kwa lugha rahisi, alitapeliwa au alizulumiwa. Akaambiwa, kama vado anamtaka Raheli, afanye kazi tena kwa miaka 7 ndipo atapewa Raheli.

Kama Yakobo angekuwa anataka bora mke, angeridhika na Lea, lakini kwakuwa alikuwa anamtaka Rachel, akalenga ‘kutokupumzika’ mpaka ampate Raheli, bila kuyumbishwa. Akaapinda mgongo tena kwa miaka 7 ili tu kuyafikia malengo yake, na akampata mke aliyemtaaka, Raheli !!!    Mwa 29:16-18.

Ni muhimu sana kwa mtu kuwa na makusudio ya moyo (Malengo).
Malengo hufungulia nguvu za Mungu (Msaada wa Mungu)
‘Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; na mwanga utaziangazia njia zako’ (Ayubu 22:28)
Malengo hukupa nidhamu ya kimaisha (Descipline)
‘Pasipo maono, watu huacha kujizuia (yaani hukosa nidhamu, au msimamo - huyumba-yumba)   (Mith 29:18).

Yeremia 1:5-10; Mungu alimtenga Yeremia kuwa Nabii tangu tumboni mwa mamaye, Je wewe ulitengwa uwe nani? Tafuta kujua mpango wa Mungu kwako. Usipopatia wito wako, kuna hatari ya kutofanikiwa katika baadhi ya vitu unavyohangaika kuvifaya. Mungu anabariki kazi zake, si kila kazi. Ni muhimu uutafuta uso wa Mungu ili ujue mpango wa Mungu juu ya maisha yako.  Yeremia 29:11-13,  Zaburi 32:8


Mipango Mizuri – Kuwa na njia za kukufikisha katika malengo yako
Mwanzo 30:25-36; Ili kufikia mafanikio na maisha mazuri, mtu wa Mungu si tu kwamba anahitaji kuwa na maono na malengo tu, bali pia anahitaji kuwa na mipango mizuri ya kumfikisha katika maono na malengo yake. Jiulize, ni kwa njia gani nitaweza kufikia kule ninakotamani kufika? Hizo njia utakazopata, ndio tunaita mipango.

Katika habari hii ya Yakobo, unaona anapanga kuwachukua wanyama wa mjomba na kwenda nao umbali wa siku tatu (3) na kukita kambi ya mifugo huko. Na utaona anapanga kukaa huko kwa miaka mitatu (3). Hizi namba unazoziona hapa, ni mipango madhubuti. Ni mawazo ya mtu aliyefanya uchunguzi wa eneo zuri la kuweka kambi ya mifugo na ni mawazo ya mtu aliyepiga mahesabu kuona, ni baada ya muda gani atakuwa ameweza kutengeneza faida.

Mipango mizuri itazaa matokeo mazuri. Mipango mibaya itazaa matokeo mabaya. Kwahiyo, tafuta namna ya kutengeneza mipango mizuri, ikibidi tumia wataalam wa mipango. Fanya Fisibility study  na tengeneza a good Business Plan. Yakobo alijitenga mwendo wa siku 3 na akakaa nyikani muda wa miaka mitatu. Huu ni Mpango wa Shughuli (This is a  business plan au activity plan). Baada ya miaka kadhaa, Yakobo alikuwa mtu mwenye mafanikio na utajiri mkubwa, leo tungemuita ‘Milionea’ mkubwa. Kumbuka; Mipango mizuri itazaa matokeo mazuri. Mipango mibaya itazaa matokeo mabaya.

Linaendelea…

Mwl. Mgisa Mtebe,
P. O. Box 837, Dar es Salaam.
Simu: (+255) 0713497654.
Barua pepe (Email): mgisamtebe@yahoo.com:
Tovuti (Website): www.mgisamtebe.or.tz



1. KWANINI MUNGU ANATUPA UTAJIRI MALI NA FEDHA ? 



1. ILI KUIMARISHA AGANO LAKE (UFALME WAKE)* Kumb 8:18 (12-18)

Agano la Mungu kwa siku za leo, ni Agano JIPYA. Kuimarisha Agano lake maana yake; nikuimarisha kazi ya injili ya Yesu Kristo, ili wokovu uwafikie watu wote. Tunapotoa muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalme wa Mungu, tunakuwa tumetimiza makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha agano lake” (Kumb 8:17-18)
Soma pia, Gal 3:11,23-26,29; Rum 10:13 – 15; Fillip 4:15 –19)Mali zetu si pesa tu. Mali ni kitu chochote chenye thamani na kikitumiwa vizuri, kinawezakuongeza ubora wa kitu. Kwa mfano;
a) Muda wako ni mali ya thamani sana, ukiutumia vizuri, utakuletea kipato.

b) Vipawa vyako pia ni mali, ukikitumia vizuri, kitakuletea kipato.
c) Fedha yako pia ni mali, ukiipangilia a kuitumia vizuri, itakuboreshea maisha yako.

Tunapotoa muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ilikuimarisha Ufalme wa Mungu, tunakuwa tumepanda mbegu katika ufalme wa Mungu nakwa wakati wa Mungu, zitarudi kwetu moja ikiwa imezaa 30, na nyingine itarudi imezaa 60,na nyingine 100. Hii ni kwasababu, mali zako na vipawa vyako na muda wako, ni sadakambele za Mungu.Hayo ndio makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha aganolake” (Kumb 8:17-18).
Unapotoa sadaka kama hizi kwa Mungu, toa kwa imani, yaani toa kwa kutarajia kupokea tenakutoka kwa Mungu. Usione muda wako kama unapoteza au unajitolea tu. Bali vione hivi vitukuwa ni sadaka, kwasababu kwa uhalisi, vitu hivi ni mali. Muda ni pesa; vipawa ni pesa pia,na mali zetu ni pesa. Unapotoa muda, vipawa na mali zako kwa Mungu, ona kwamba unatoasadaka. Na sadaka ni mbegu. Na mbegu ikitolewa kwa usahihi, huzaa sana (Math 13:8). 1

2.

Hivyo, toa kwa imani, yaani toa kwa kutarajia kupokea tena kutoka kwa Mungu. Usionemuda wako kama unapoteza au unajitolea tu, bali ona kwamba umetoa sadaka. Tunapotoamuda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalmewa Mungu, tunakuwa tumepanda mbegu katika ufalme wa Mungu na kwa wakati wa Mungu,zitarudi kwetu moja ikiwa imezaa 30, na nyingine 60, na nyingine 100; kama tulivyosomakatika Mathayo 13:8.
2. ILI KUVITUMIA KWA MAHITAJI YETU BINAFSI *Yoh16:24
Soma tena 1Timotheo 6:17 na   2Wakorintho 9:8 – 11

Mungu kama Baba yetu na kama Mchungaji Mwema, anajali sana mahitaji yetu na haja zetuau shauku za mioyo yetu. (vitu vitupavyo furaha na kuridhika). Ndio maana hutupa utajiri, ilitufurahie maisha. Si mapenzi ya Mungu tuwe masikini. Ndio maana Yesu alifanyika maskini(kimwili) ili kwa umasikini wake, (sisi) tupate kuwa matajiri (kimwili)” (2 Kor 8:9)

Ni mapenzi ya Mungu tupate vitu vyote vitakavyotufanya tufurahie maisha yetu duniani.Nyumba nzuri, mavazi mazuri, chakula kizuri, kazi nzuri, magari mazuri, biashara nzuri,mifugo mizuri, mashamba mazuri, mshahara mzuri, n.k. (Zab23:1- 2; Fil 4:6-7,19; Zab37:4; Zab145:17- 19)
3. ILI KUWAGAWIA WAHITAJI *2KOR 9:8-13;



Pia soma 1Timotheo 6:17-19; Waefeso 4:28 na Luka 6:38.

Tunapowapa wahitaji fedha, nguo, viatu, chakula au vitu vya aina nyingine ili kuwasaidiakimaisha, tunapata thawabu kubwa kwa Mungu. Kumsaidia mhitaji kitu, ni kumpa Mungu.Hebu soma vizuri Mathayo 25:31-40; Mathayo 10:40 – 42 na Yohana 13:20.
Mungu ametupa mali, fedha na utajiri wa namna nyingi ili tuwasaidie wahitaji na masikini,wajane na yatima, wagonjwa na walemavu. Thawabu yake ni kubwa mbele za Mungu, naMungu ataona sababu ya kukupa tena na kukuzidishia. Tena Mungu atakufanya uwenjia/mkondo wa baraka zake kwa watu wengine. Soma pia 2Kor 8:14-15, Mdo 20:35 2
 TUMTUMIKIE MUNGU KWA MALI ZETU 

Ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanyaMungu, kutufungulia madirisha na milango ya mbinguni, ili kutumwagia baraka nyingi,tunazohitaji katika mashamba, mifugo, biashara, miradi mbalimbali tuliyonayo. Pia ushirikiwetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanya Mungu azibariki familia zetu, watoto wetu, ndoa zetu na afya zetu pia, ili tuzidi kumtumikia na kuwabaraka kwa wengine pia. Baraka za Mungu zitatuzidishia mapato yetu, ili tuwe na vitu vyakutosha kutumia na hata kuwa baraka kwa wahitaji wengi.

Utoaji ni njia ya Mungu kutupa na kutujaza tunavyohitaji *1Fal 17:1-16
Mungu ndiye alieyewaka kanuni ya kupanda na kuvuna, kutoa na kupokea. Hivyo, maranyingi tunapomwomba Mungu atubariki/atujaze mahitaji yetu, anatuletea mafasi ya kutoakwanza, ili tupokee mahitaji yetu tumwombayo. Kwasababu, ndiyo kanuni ya kupokea. Niajabu, sicho tunachotegemea (kutoa wakati wewe binafsi unahitaji). Badala ya Mungukukupa moja kwa moja kitu ulichomwomba, anakuletea nafsi ya kutoa hicho hicho kidogo ulichonacho, kiwe kama mbegu, ili hatimaye upokee (uvune) kile ulichomwomba, na hata zaidi ya ulivyoomba.
Biblia pia inasema hivi katika kitabu cha Waefeso 3:20 na Wafilipi 4:15-19; kwamba, “Basi atukuzwe Mungu awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tumwombayo au kulikoyote tuyawazayo, kwa kadri ya nguvu, itendayo kazi ndani yetu” (Efe 3:20; Fil 4:15-19).
1Wafalme 17:13-16; Eliya akamwambia (yule mama mjane); usiogope (kutoa hicho kidogokilichobaki) … enenda ukafanye kwa ajili yangu (kwa maana ukinipa mimi, utakuwaumempa Mungu) na Mungu wa Isarael anasema, unga wako wala mafuta yakohayatapunguka kamwe, mpaka njaa itakapoondoka juu ya nchi. Yaani Mungu atavizidisha. Siajabu anliongezea Kama ukikubali na kutii, utakula mema ya nchi. Lakini ukikataa,utaangamia (kama wengine wanavyoangamia). (Isaya 1:19)
Si jambo rahisi kutoa wakati wewe mwenyewe umepumgukiwa au una uhitaji. Inahitajikaimani kubwa kutoa kidogo kilichobaki, ili uhitai wako ujazwe. Hivyo, usishangae sikuutakapomwomba Mungu pesa au vitu, halafu badala ya kukupa, anakuletea mhitaji ili umpe pesa au vitu, au analeta nafasi ya wewe kutoa sadaka. Kumbuka kanuni yake, huwezi kuvuna bila kupanda!
Hivyo, ukikubali na kutii, utavuna na kupata mema, tena zaidi ya ulivyotarajia. Hii ni kanuniya Mungu; ukipanda haba utavuna haba, ukipanda nyingi, utavuna nyingi. Huwezi kuvuna bila kupanda
Utoaji wa sadaka, hufungulia na kutuletea mahitaji yetu (2Wafalme 4:8-41)
Huyu mama Mshunami pamoja na mume wake, japo walikuwa ni watu wenye fedha nyingina cheo kikubwa, lakini walikuwa hawajapata mtoto, pengine kwa miaka mingi sana.Inaawezekana walishaombewa na watumishi wengi wa Mungu, lakini bado maombi yaohayakuleta muujiza waliokuwa wanausubiri kwa hamu kubwa. Kumbe ufunguo wa muujizawao, haukuwa katika maombi pekee, bali katika utoaji wao pia. Yamkini Mungu alishawapamtot wao katika ulimwengu wa kiroho, ila sadaka ndio ilikuwa inahitajika, ili kutelemshaBaraka yao ya mtoto.
Neno la Mungu linasema, Mungu akaweka mzigo ndani ya mama huyu, kumjengea NabiiElisha nyumba, ili asipate shida katika utumishi wake. Na huyu mama akamshirikishamumewe. Nao wakaiweka azma yao katika matendo. Walipotii na kufanya kile kitu ambachoMungu aliweka mioyoni mwao, kwa ajili ya Elisha mtumishi wa Mungu, ndipo muujiza waowa kupata mtoto, ukatimia.
Biblia inasema, Elisha akapewa Neno la Mungu kwa ajili ya familia hii, juu ya kupewa mtotowao (ambaye tayari alishatolewa kwao, kwa njia ya maombi, lakini ni katika ulimwengu wakiroho). Sadaka yao, iliushuhsa ule muujiza wao, kutoka rohoni, ukawa halisi katika mwili,kwasababu ya Utii wao. Sadaka ina nguvu ya kutupa mahitaji yetu.
Kwahiyo Ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali,utamfanya Mungu, kutufungulia madirisha na milango ya mbinguni, ili kutumwagia barakanyingi, tunazohitaji katika mashamba, mifugo, biashara, miradi mbalimbali tuliyonayo.Pia ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanyaMungu azibariki familia zetu, watot wetu, ndoa zetu na afya zetu pia, ili tuzidi kumtumikia nakuwa baraka kwa wengine pia. Baraka za Mungu zitatuzidishia mapato yetu, ili tuwe na vituvya kutosha kutumia na hata kuwa baraka kwa wahitaji wengi (Malaki 3:10–12, Luk 6:38) 4
                                                 Wako katika kazi ya Mungu

                                                     Mwl. Mgisa Mtebe
                                                    +255 713  497  654
                                                 mgisamtebe@ yahoo.com
                                                   www.mgisamtebe.or.tz



Tumejifunza mambo mengi sana yaliyokuhamasisha na yaliyokupiga deni uwe kiumbe wa kumsifu na kumtukuza Mungu. Tunapomsifu mtu, huwa tunaelezea yale ambayo yanamtofautisha na wengine. Hivyo basi, ufikapo katika muda wa kumsifu na kumwabudu Mungu, ujue namna ya kuifanya sifa
yako na ibada yako kwa usahihi.  
                   
Na ili kumpa Mungu sifa na ibada, ni lazima na ni muhimu sana ujue mambo ambayo yanamstahilisha Mungu wetu kusifiwa na kutukuzwa. Kwa kutumia sifa na tabia za Mungu, utaweza kumsifu na kumwabudu vizuri. Hakuna kiumbe kingine chochote kinazo zile sifa kuu tano za Mungu,
isipokuwa yeye Mungu Jehova peke yake.  
Kwahiyo, na hizo ndizo zinayomstahilisha yeye kusifiwa na viumbe wake. Katika sura ya nane, tumeshajifunza mambo yanayomstahilisha Mungu kupewa sifa. Kwakuwa sasa unayajua, basi tumia mambo hayo uendapo mbele za Mungu katika katika ibada yako ili kumsifu na kumwabudu. Unapomueleza Mungu sifa zake na tabia zake (vile alivyo) hapo unakuwa unamsifu na kumwabudu.

Tofauti ya kusifu na kuabudu
Naomba urudie kuisoma sura ya kwanza ya kitabu hiki, ambapo nimefundisha vizuri maana ya kumshukuru Mungu, kumsifu Mungu na kumwabudu Mungu. Hii itakusaidia kutofautisha mambo haya kwa nia ya kuyaelewa au kuyaelezea kwa mtu mwingine. Nilisema hivi,  
Ibaba ni kitendo cha mtu kumtukuza, kumhimidi, kumwinua, kumwadhimisha, kumshukuru na kumheshimu Mungu kwa vile alivyo na kwa yale aliyoyatenda. (Appreciation and admiration for who God is and for what He has done). Lakini haya mambo matatu, yanayofanana sana na si rahisi sana
kuyatenganisha kimaelezo au kivitendo.
                
Lakini tuendapo mbele za Mungu kwa ibada, iwe ni chumbani kwako au sebuleni kwako au kwenye gari lako au kanisani kwako, kusifu na kuabudu na kushukuru, ni mambo yanayofanyika kwa kuingliana sana. Sio sheria kwamba, hautakiwi kuchanganya sifa na kuabudu na kushukuru, hapana.
Hebu soma tena sura ya kwanza vizuri. Kati ya mengi, nilisema hivi;
                
Haya mambo matatu, kusifu, kushukuru na kuabudu, ni mambo yanayofanana sana. Inaweza ikawa vigumu kidogo kuyatenganisha kimaelezo au kivitendo. Ni ngumu kidogo, kufanya kimoja pasipo wenzake, kwasababu ni mambo yanayokwenda kwa pamoja sana. Lakini kwa tafsiri zake, yako hivi;
1. Kumshukuru Mungu;‐  Ni ile hali ya kumueleza Mungu jinsi tunavyothamini (Appreciate and Admire) wema wake, fadhili zake na baraka zake katika maisha yetu.
2. Kumsifu Mungu;  ‐ Ni kumueleza Mungu juu ya matendo yake makuu na ya ajabu aliyoyafanya. Au ni kuwaeleza wengine kuhusu matendo makuu ya Mungu aliyoyafanya katika maisha yetu au kwa watu wengine.
3. Kumwabudu Mungu; ‐ Ni kumueleza Mungu tukuzo zetu, heshima yetu na upendo wetu kwake kwasababu ya uzuri wa tabia zake kwetu. (Credentials and Characters). Kwahiyo, tuendapo mbele za Mungu kwa ibada, iwe ni chumbani kwako au sebuleni kwako au kwenye gari lako au kanisani kwako, ili kumsifu na kumwabudu na kumshukuru Mungu, uwe huru kujimimina mbele za Mungu kwa kufanya vyote vitatu, kwa namna moyo wako utakavyokuwa unaongozwa na Roho Mtakatifu. Vyote vitatu vinatengeneza ibada takatifu kwa Mungu.
Katika sura inayokuja, nimefundisha vizuri namna ya kuingia katika ibada na hata kupenya na kufika katika chumba cha ndani kabisa cha uwepo na utukufu wa Mungu; ili unapokwenda mbele za Mungu wetu, uweze kukutana na nguvu zake katika utukufu wake.  
                
Lakini hapa chini nimeziweka kwa ufupi ili kukukumbusha. Na pia nimekuongezea na mambo mengine yanayotakiwa katika kumsifu na kumtukuza Mungu. Kwahiyo, utengapo muda wa kukaa mbele za Mungu wetu kwa ibada, msifu na kumtukuza Mungu kwa mambo yafuatayo,
1. Mtukuze Mungu kwa Sifa zake za Uungu (ambazo hakuna mwingine
aliye nazo) Kwamba;
a) Jehova ni Mungu wa Milele
b) Jehova ni Mungu Mtakatifu
c) Jehova ni Mungu Aliye kila mahali
d) Jehova ni Mungu Anayejua mambo yote
e) Jehova ni Mungu Aliye na nguvu zote na anaweza kufanya mambo yote kabisa.
Nimezielezea vizuri hizi sifa za Uungu, katika sura ya kwanza. Hizi ni baadhi tu ya sifa za Mungu, sio zote. Kwa hivyo basi, pamoja na namna nyingine ambazo utajifunza kumsifu na kumwabudu Mungu, hebu uwe unamsifu Mungu kwa mambo haya au kwa sifa zake hizi pia.  
Msifu Mungu kwa;
2. Kwasababu ya Tabia zake
3. Kwasababu ya Matendo yake ya Ajabu
4. Kwasababu ya Fadhili nyingi na kuu mno
5. Kwasababu ya Ahadi zake kubwa za thamani2.   Mtukuze Mungu  kwa Tabia zake
Neno la Mungu, linatuonyesha jinsi ambavyo Mungu wetu ana tabia na kawaida nyingi nzuri ambazo kwa hizo, tunavutiwa na tunapigwa deni kumsifu na kumwabudu. Kwa mfano ; Biblia inasema kwamba, Mungu wetu amejaa Upendo, usio na mwisho. Ni Mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, sifa yake ni kuwa na rehema daima. Soma mistari ifuatayo, ili uone zaidi. Lakini kwasababu ya sifa hizi (Tabia zake), tunapigwa deni kumsifu na kumwabudu.
*Zaburi 103:8, Kutoka 34 :6,  
*Efeso 3 :18‐19, Daniel 9 :4, Ufunuo 19 :11
3. Mtukuze Mungu  kwa Matendo yake ya ajabu.
Mungu wetu ni Mungu aliyefanya mambo ambayo hakuna tena, awezaye kufanya. Kwa mfano; ndiye aliyeziumba na kuzitundika sayari zote za ulimwengu huu, bila minyororo wala nguzo. Mungu wetu ndiye anayesababisha mioyo yetu inadunda, bile kuwekewa betrii wala chaji (charge). Au ni lini ulichomeka moyo wako katika soketi ya umeme kama unavyochomeka simu yako ili kupata umeme?
       
Nina uhakika, hakuna mtu anayefanya hivyo. Sasa unadhani moyo wako unadundaje? Hizo ni kazi za ajabu za Mungu wetu.na hakuna mtu awezaye kuzifanya. Kwasababu ya matendo yake ya ajabu, Mungu wetu anastahili kusifiwa na kutukuzwa. Soma mistari ifuatayo kwa umakini. Utaweza kuona kwa uchache, jinsi maandiko yanavyoeleza juu ya matendo makuu ya Mungu.  
Haya ni maelezo ya watu wa Mungu ambao kwa kumjua Mungu, waliweza kueleza ukuu wake vizuri, ili na sisi tunaosoma maandiko yao, tunajifunza juu ya ukuu wa Mungu, uweza wa Mungu na tabia za Mungu wetu. Soma vizuri Kitabu cha Daniel 6:25‐27,  Nehemia 9:6,  Zaburi 147:1‐18,  na Zaburi sura ya 136:4‐26
4. Mtukuze Mungu  kwa Fadhili zake.
Mungu wetu ni Mungu atupaye baraka na fadhili nyingi kila siku. Fikiri wema ambao Mungu amekufanyia maishani mwako, na hata katika siku ya leo tu. Kuna vingi ametupa ambavyo wengi walitamani, lakini hawakupewa. Uhai, afya, ulinzi, rehema, chakula, fedha, shule, simu, gari, nyumba, ajira, mke, mume, watoto, na hata wazazi.
Sio kila mtu bado ana wazazi. Na wengine wamezaliwa hawajawahi kuwajua wazazi wao. Kwakweli fadhili na baraka za Mungu ni nyingi sana; ukiamua kuziorodhesha, utakesha. Sasa, kwa fadhili zote hizi alizotujalia, basi Mungu wetu anstahili kusifiwa.
*Zaburi 103:1‐5,  Zaburi 107:21,  2Nyakati 20:21
5. Mtukuze Mungu  kwa Ahadi zake.
Ni Mungu aliyetuahidi watu wake, mambo mengi sana mazuri. Ametupa ahadi kubwa mno na za thamani sana. Ni ahadi za kutupa baraka, heshima na utajiri. Kwa ahadi hizi pia, anastahili kusifiwa * 2Petro 1:3‐4,  Efeso 1:3‐4,  Kumbu 4:4‐8  
Kwa ufupi, hivi ndivyo unavyotakiwa kumsifu na kumwabudu Mungu.
Kadri unavyoanza kufanya hivi kwa vitendo, utaendelea kujifunza kufanya huduma hii ipasavyo, nawe utajikuta unakutana na nguvu za Mungu kwa namna ya tofauti maishani mwako.
MSIFU MUNGU KWA MAJINA YAKE.
Majina ya Mungu, hueleza sifa za Mungu, Tabia za Mungu au Matendo ya Mungu. Mfano; Wayahudi wanamwita Mungu El‐Shaddai. Ni neno lenye majina mawili ndani yake. ‘El’ maana yake Mungu, na ‘Shaddai’ lenye maana itokanayo na neno ‘Shad’ yaani Titi (Ziwa) la mama anyonyeshaye.

Kutokana na ukweli kwamba, titi/ziwa la mama anyonyeshaye, linampa mtoto mchanga kila kitu anchohitaji. Maziwa ya mama yake, humpa mtoto kila kitu mtoto anachohitaji. Ndani ya maziwa kuna vitamini, protini, wanga, mafuta, madini, maji, na kila kitu mtoto anachohitaji. Maziwa ya mama, yanamtosheleza mtoto kwa kila kitu. Hivyo, Waisraeli wanapomwita Mungu El‐Shaddai, wanamaanisha kuwa, kama ziwa linavyo mtosheleza mtoto, vivyo hivyo, Mungu ni ‘Mtoshelezi’ kwetu. Halleluyah!
Hivyo, kila jina la Mungu, linabeba aidha Sifa yake au Tabia yake au Matendo yake. Ndio maana Mfalme Daudi anasema “Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu … Mpeni Bwana utukufu kwa jina lake. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.” (Zab 29:1‐2) Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni Jina lake, kwakuwa lapendeza. (Zaburi 135:3). Na Bwana Yesu alitufundisha kuanza sala namna hii; Baba yetu uliye mbinguni, jina lako tukutuzwe, hakafu Ufalme
wako uje hapa duniani.  
Kwahiyo, unaweza pia kumsifu Bwana kwa majina yake. Majina ya Mungu, hueleza aidha sifa za Mungu au tabia za Mungu au Matendo makuu ya Mungu. Yafuatayo hapa chini, ni baadhi ya majina ya Mungu kwa lugha ya Kiebrania, yatakayokusaidia kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu.
MAJINA YA MUNGU
   
       Jina la Mungu                 Maana yake       Mstari wa Biblia         
1. Adonai ‐ Mungu Mwenye enzi yote ‐ Mwa 15:2‐8, Kut 6:2‐32. El‐Ohim ‐  Mungu Muumbaji       ‐  Mwa 33:20, Kol 1:16‐17
3. El‐Elyon ‐  Mungu Aliye juu zaidi       ‐   Mwa14:18, Dan 4:34
4. El‐Gibbor  ‐ Mungu Mwenye Nguvu    ‐       Isa 9:6,  Zab 147:5
5. El‐Hai ‐  Mungu Aliye Hai/Anaishi   ‐  Josh 3:10,  1Sam17:26
6. El‐Olam ‐  Mungu wa Milele                 ‐  Ufu 4:8,  Kut 3:14
7. El‐Roi ‐  Mungu Aonaye kila kitu       ‐ Mith 15:3, Zab 32:8
8. El‐Shaddai ‐  Mungu Mtoshelezi      ‐  Mdo 17:28, Kumb 8:4
9. Jehovah ‐  Ajitegemeaye kuwepo ‐Kut 6:2‐8,  Mdo 17:24‐25
10. Jehovah Shalom    ‐Mungu Amani yetu           ‐ Amu 6:22‐24
11. Jehovah Rapha   ‐  Mungu Atuponyaye                ‐  Kut 15:26
12. Jehovah Jireh   ‐  Mungu Mtoaji wetu           ‐ Mwa 22: 8, 14
13. Jehovah Nissi  ‐  Mungu Ushindi wetu          ‐ Kut 14:13‐14  
14. Jehovah Saboath  ‐  Bwana wa Majeshi             ‐  Malaki 3:7  
15. Jehovah Shammah ‐  Bwana ni Aliyepo                  ‐  Kut 3:14  
16. Jehovah Rohi   ‐  Bwana  ni Mchungaji wangu   ‐  Zab 23:1
17. Jehovah Tsidkenu  ‐  Bwana ni Haki yetu              ‐  Yer 23:6
18. Jehovah Mekaddishem  ‐  Bwana Atutakasaye  ‐  Kut 31:13  
Namna  za  kumshukuru, kumsifu,  na  kumwabudu Mungu  wetu. Kwahiyo, katika maisha yetu sisi, kama waumini, tunatakiwa kumpa Mungu wetu ibada, (kumshukuru, kumsifu na kumwabudu) kwasababu ya mambo yote hayo niliyoyataja. Tunatakiwa kumtukuza Mungu kwasababu ya sifa zake, na kwasababu ya tabia zake, na matendo yake na fadhili zake na ahadi zake kwetu.  
    
Sasa basi, hapa chini, nimekuwekea njia kuu tatu ambazo unaweza kumsifu na kumtukuza Mungu kwazo. Utengapo muda wa kwenda mbele za Mungu, unaweza kutuia njiia kuu zifuatazo; Kumtukuza Mungu kwa,
1. Kumwimbia nyimbo za kumsifu na kuwabudu
2. Kumweleza au kusimulia kwa maneno
3. Kumtolea Mungu sadaka na dhabihu 
Wako katika kazi ya Mungu
Mwl. Mgisa Mtebe
+255 713  497  654
mgisamtebe@ yahoo.com
www.mgisamtebe.co.tz