Hatua
na vipengele muhimu katika kuomba
MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU. *Rum 8:26-27 *Yoh 14:16-17
Yesu
alisema Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu. Atatusaidia na kutufundisha yote, kwa
maana pasipo yeye, sisi hatuwezi neno lolote. Na sisi peke yetu hatujui kuomba
ipasavyo, bali yeye (Roho) ajua kutuombea kwa Mungu kama vile Mungu apendavyo.
Hivyo kabla ya kuanza maombi au kusoma neno au ibada au safari au mitihani au
kikao n.k. jifunze kujikabidhi kwa Roho Mtakatifu, uombe msaada wake, akupe
ufanisi/ubora katika yote yakupasayo kufanya.
Tambua
Utu wake, Uungu na Uweza wake.
Jikabidhi
katika Nguvu ya Uongozi wake.
Tii
kila Uongozi anaokupa.
FANYA TOBA NA UTAKASO. *Isa 59:1-2, Yoh 9:31, 1Yoh 1:8-9,7
Sikio
la Bwana si zito kusikia wala mkono wake si mfupi kushindwa kututendea mambo
tumwombayo, bali maovu yetu ndiyo yanatufarakanisha na Mungu wetu. Mungu hawasikii
wenye dhambi. Hivyo chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako mbele za
Mungu na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha. Mungu ni mwaminifu kutusamehe na
kututakasa na uchafu wote. (Isa 1:18). Lakini, kabla hujafanya toba yako
binfsi;
(i) – Kwanza, samehe wote waliokukosea, hata
kama hawajaja
kukuomba
msamaha. Usipowasamehe waliokukosea, na Mungu
hataweza
kukusamehe wewe. (Math 6:12,14-15)
(ii) – Ndipo nawe ufanye toba yako binafsi. Na
Mungu atakusamehe kabisa.
Hata
kama ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe sana. (Isa 1:18, Isa 43:25)
3. MSIFU, MUABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Zab
147 na Zab 148
Msifu
Bwana kwa Matendo yake makuu, mwabudu Bwana kwa uzuri wake na kwa sifa zake.
Mwadhimishe Mungu kwa Tabia zake, wema wake, fadhili zake na baraka zake
mbalimbali anazotutendea. Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo
atakuwa tayari kukupa haja za moyo wako. Haja zetu zimefichwa nyuma ya mgomgo
wa sifa. Ndio maana Neno linasema;
‘Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu na
kumshukuru), naye atakupa
haja za moyo wako’ (Zab37:4).
Yesu
anatuonyesha mfano; angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake imekuwa “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.” (Math
6:9). Anaanza maombi kwa kumsifu Mungu. Msifu Mungu kwa kuimba na kwa
kunena/kusema/kuelezea. Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Ukifanya sifa
nzuri, ya kuufurahisha moyo wake, atakupa hata na vile ambavyo
hukutegemea/hukuomba.
4. MWELEZE MUNGU MAHITAJI NA HOJA ZAKO. *Wafilipi 4:6-7,19
Isa 43:26
Mweleze
Mungu zile hoja zilizokusukumwa kwenda kumwomba. Nenda mbele za Mungu kama
‘kuhani’ (1Pet 2:9). Kwa unyenyekevu na heshima. Lakini kabla ya kumweleza
mahitaji yako binafsi;
(i) Kwanza fanya ‘maombezi’ – ombea watu
wengine; (1Tim 2:1-4)
Viongozi
mbalimbali na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu, marafiki zako, wenye shida,
ndugu zako, nchi yako, shule yako, shirika lenu, ofisi yenu, chama chenu, n.k.
Usianze kujiombea mwenyewe tuu, zoea kuwatanguliza wengine.
(ii) Kisha fanya ‘maombi yako’– ombea haja za moyo wako.
(Math 7:7-11)
Mweleze
Mungu haja zako. Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli. Japo anazijua haja zetu,
lakini ameagiza kuwa tumwombe ndipo atafanya. ‘aombaye
hupokea’ yaani; asiyeomba, hapati. Mungu anasema tumpelekee hoja zenye
nguvu (Isa 41:21). Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili upewe (pray for good
things and big things)
5. FANYA MAOMBI YA VITA VYA ROHONI. *Efe
6:10-13 *2Kor 10:3-5
Baada
ya kumwendea Mungu na kumweleza mahitaji yako, sasa simama kama ‘mfalme’,
kwasababu wewe ni ‘mfalme’ (Ufu 5:8), tumia mamlaka yako ya kifalme, ongea na
hali/hitaji ulilokuwa unaliombea, na kwa mamlaka, amuru iwe kama vile
ulivyoomba/unavyotamani. Ndio maana Bwana Yesu alipokabidhiwa mamlaka yote na
Mungu, naye akatukabidhi sisi (kanisa lake) “Tazama,
nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui. Wala hakuna
kitakachowadhuru” (Luk 10:19, Yer 1:10, Yak 4:7). Tuma neno lenye
mamlaka katika hali/jambo ulilokuwa unaliombea, Amuru iwe vile ulivyokuwa
unamwomba Mungu iwe. Kemea kila roho ya shetani inayoweza kuwa inasababisha
tatizo katika swala lako.
6. OMBEA ULINZI JUU YA ULIYOYAOMBEA. *Math 6:13a
Baada
ya kupiga vita vya kiroho, weka ulinzi katika yale uliyoyaombea, ili shetani na
mapepo yake wasiweze kuirudia hali/jambo/mtu yule uliyemkomboa kwa maombi ya
vita. Yesu alisema shetani akifukuzwa mahali, haendi mbali, anasubiri kuona
kama atapata upenyo wa kuparudia mahali pale alipokuwa kwanza. (Math 12:43-45).
Kwahiyo, usipoweka ulinzi, kuna uwezekano wa adui kurudi na kuliharibu zaidi
lile jambo uliloliombea na kulipata.
Kumbuka,
unapoomba vizuri, unapokea papo hapo (katika ulimwengu wa roho), lakini
udhihirisho wake katika ulimwengu wa mwili, unaweza kuchukua muda fulani. Hivyo
katika muda huo wa kusubiri, shetani anaweza akapita na kuzuia au kuharibu kile
unachokisubiri kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana Yesu
alitufundisha kuombea ulinzi, “tuokoe na
yule mwovu” (Math 6:13a). Weka ulinzi juu ya mambo yako yote. Jengea
wigo wa moto wa mbinguni (2Fal 6:16-17), Yafunike kwa damu ya Yesu na agiza
malaika walinzi walinde mambo yako masaa yote. Omba hivyo kila siku. (Zab 34:7,
Zab 91:9-11, Ebr 1:13-14)
MSIFU, MWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Math 6:13b
Yesu
alianza maombi kwa kumsifu Mungu na kumtukuza. Na akamaliza maombi yake kwa
kumtukuza Mungu tena. Akasema “kwa kuwa
ufalme ni wako, na nguvu ni zako, sasa na hata milele” akamaliza. Kwahiyo nawe kwa kumaliza maombi yako,
msifu na kumshukuru Mungu tena, kwa ukuu wake, uaminifu wake, na ahadi zake juu
yetu. Ndipo ufunge maombi yako.
MUHIMU: TUMIA MAANDIKO KATIKA KUOMBA *Kol 3:16
-Katika
kuomba kwako, mara zote tumia maandiko kumkumbusha Mungu ahadi zake .(Isa
43:26). Mungu analiangalia neno lake ili alitimize. Sababu pekee itakayomfanya
Mungu akupe alichoomba, ni ili kulitimiza neno lake. Hivyo, baada ya kumweleza
unachohitaji (kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu unayemwombea) mpe Mungu
andiko/neno lake linalokupa wewe uhalali wa kuomba hicho kitu mbele zake
na kupewa.
-Hata
unapompinga na kumkemea shetani, baada ya kutoa amri yako dhidi yake, shetani
atasubiri kusikia andiko/neno linalomnyima yeye uhalali wa kushika alichoshika.
Ndio maana Yesu alimshinda shetani kwa neno la Mungu. Alisema “imeandikwa” na
shetani akashindwa. “Nao wakmshinda
(shetani) kwa damu ya Yesu na kwa Neno” (Ufu 12:11)
MBINU
ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI KWA MUDA MREFU
1. CHAGUA MAHALI PAZURI PA UTULIVU. *Mk 1:35
ili uweze kuomba kwa utulivu na kwa umakini, chagua au tafuta
mahali pazuri
patakapokupa
utulivu katika kuomba (concentration in prayer). Ndio maana Mungu
alipenda
kuongea na Musa juu ya mlima. (Kut 24:12-18). Hata Yesu alizoea kwenda
kuombea
mlimani, mahali palipo mbali na vurugu za watu, alipenda kwenda mlimani.
(Math
14:22-23). Tafuta mahali patulivu; chumbani, kanisani, mlimani (Math 6:5-6)
2. CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7
Ili
uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili
wako
viko fresh. Usilazimishe kuomba hata kama akili yako au mwili wako umechoka
sana. Kila jambo lina wakati wake. Kama umechoka sana, huo si muda wa kuomba,
bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili baadaye uweze
kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala shetani. Penda
kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini kuongea na Mungu kwa
akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri sana kwenda kuomba
mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)
3. OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum
8:26-27
Mbinu
nyingine nzuri ya kuomba kwa muda mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa Roho;
yaani kuomba kwa kunena kwa lugha. Tunapoomba kwa akili za kibinadamu, Mungu
anasikia pia, lakini maombi yako yanakuwa na mipaka / limited kwasababu akili
ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa
kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni iliyo bora zaidi. (Yuda 1:20, Mk
16:17, 1Kor 14:1-4, 15-16,7)
4. OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18
Kufunga
kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe makini zaidi kuongea na Mungu
kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi kufanya mambo ya Mungu. Na mwili
ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa kufanya mambo ya kiroho. Mbinu
mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia posho yake ya chakula. Mwili
ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na upenyo mzuri zaidi (Zab 35:13).
Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba. Ndio maana Yesu anasema ‘mfungapo’
akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo. Inasaidia.
5. OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10
Neno
la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna faida ya kuomba pamoja na
rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu, inaleta hamasa na ari ya
kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na waombaji wenzako. Pili;
nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji mmoja anafukuza adui elfu
moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili) bali elfu kumi! Shangaa!
(Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya Ki-Mungu. Kadri
mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.
Kwahiyo,
wakati mwingine, omba na rafiki yako, unayemwamini, unayeweza kumshirikisha
mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa imani, walikuwa na marafiki wa kiroho.
(Prayer Partners). Kwa Mfano:-Math 17:1-9
Musa
– alikuwa na Joshua, Haruni na Huri
Eliya – alikuwa
na Elisha
Daniel – alikuwa
na Shadrack, Meshack na Abednego.
Yesu – alikuwa
na Petro, Yakobo na Yohana.
Paul – alikuwa
na Barnaba, Timotheo na Tito.
Wewe
Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho?
Kama
huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke kujichaglia. Tulia umwombe
Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu mtakayefungamanishwa naye
katika roho, hata kama mmetengana kijiografia, lakini katika roho, mko na umoja
mzuri wa imani. (Math 18:18-19)
6. OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.
Katika
kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia kwenda mwendo mrefu. Yakupasa
kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point and weak point). Wakati wa
kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia mikao inayokua nguvu zaidi.
Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa kupiga magoti au kwa kuegemea
kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au unatembea tembea, ili kuepuka
usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua mikao inayowasaidia kuomba maombi
marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali wakiwa katika maombi, huwa
wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni mbinu nzuri pia.
Mifano
ya Mashujaa wa imani;
Ibrahim
– aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)
Daniel – aliomba
kwa kupiga magoti (Dan 6:10)
Paul – aliomba
kwa kupiga magoti (Efe 3:14)
Yesu – aliomba
kwa kulala chini (Math 26:38-39)
Eliya – aliomba
kwa kukaa chini na
kuweka
kichwa kati ya miguu (1Fal 18:42)
Mimi – huwa
napenda kuomba kwa kutembea tembea
Naweza
kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu
Nikitembea
huku nikiomba.
Wewe
Je? Unaujua mkao wa nguvu? Kama hujui, Tafuta kujua.
OMBA NA MUZIKI LAINI KWA KUMWABUDU MUNGU.
Muziki
wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana ya
kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa namna ya
pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki ukapigwa, nao
wakawa kama mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza lile hekalu hata
makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule mbinguni, kila
malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii, mpaka mpiga
kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa Mungu) alipokija juu
yake, naye akatabiri.
Najaribu
kukuonyesha, kuna connection kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu.
Kwahiyo, ukiweza kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za
taratibu, utapata (experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una
nguvu ya kuomba kwa muda mrefu. Kama unaweza, tengeneza kanda au CD maalum
yenye nyimbo nzuri unazozipenda wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi.
Utajikuta unaweza kuomba kwa muda mrefu na kwa bubujiko zuri zaidi
Mwl. Mgisa Mtebe,Bsc
Economics
Mzumbe University,+255
713 497 654
Post A Comment:
0 comments so far,add yours