Na Mwl
Deborah Lema
UTANGULIZI
Upo umuhimu wa kumjua Mungu, kabla ya kuanza kumwabudu, kabla ya
kuanza kumtegemea, kabla ya kuanza kumtumikia, kabla ya kuanza kumuomba, kabla
ya kuanza kumtangaza au kutangaza habari zake kwa mataifa.
Kwanza kabisa tutambue Mungu ni ROHO. Sawa na (Yohana 4:24)
“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli”Hivyo
usijedanganyika na hao binadamu wanaojiita Mungu. Au wengine huchonga sanamu na
Kusema ni Mungu.
Sifa kuu ya Mungu yupo kila mahali Ndio maana lolote
unalolifanya liwe jema au baya anakuona, huwezi kumficha chochote au kumkimbia.
Kasome kitabu cha (Yona 1:1-). Lakini hufanya makao mahali patakatifu.Hafanyi
makao katika mapango ya wanyang’anyi.
Hivyo
ukitaka Mungu afanye makao ndani yako dumu katika utakatifu
Baada ya kuangalia MUNGU ni nani, na baadhi ya sifa Zake kwa
uchache, pia tutazame Huyu
Mungu je, Anajidhihirishaje!? Au anaonekanaje?
Eneo hili ni pana, ntaeleza kwa uchache kadri Mungu
atakavyoniwezesha. Nianze kwa njia ya ISHARA. kipindi cha Musa Mungu
alijifunua kwa Musa kwa ishara mbalimbali. Tukisoma Kutoka 4:2-3
“BWANA akamwambia, ni nini hiyo uliyonayo mkononi mwako?
Akasema, Ni fimbo, Akamwambia itupe chini, akaitupa chini, nayo ikawa nyoka,
Musa akakimbia mbele Yake” Tukiruka mstari wa 4 twende mstari wa 5 anasemaje?
“Ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, MUNGU wa Ibrahim,
MUNGU wa Isaka, MUNGU wa Yakobo AMEKUTOKEA”
Kwa kutokujua njia au namna mbalimbali ambazo Mungu
hujidhihirisha au huonekana kwetu tunashindwa kujua au kutenda yatupasayo. Kuna
wengine husubiri mpaka aje malaika kavaa nguo nyeupe, au ngurumo kubwa Ndio
ajue ni Mungu. Lakini kumbe zipo njia nyingi na nyingine za kawaida lakini
katika ukawaida huo MUNGU hujidhihirisha ni yeye anasema nawe, au ni yeye
ameruhusu jambo fulan n.k
Hivyo usiwe mtu wa kupuuzia baadhi ya Ishara mbalimbali
zinazofunuliwa kwako, wakati mwingine hutasikia Sauti bali kwa ishara Utajua
Mungu anasema nini.
Mungu
hujidhihirisha kwa sauti ya waziwazi
Kumbe pia Mungu hujidhihirisha kwa sauti ya waziwazi kama vile
mtu anavyomsikia mtu akiongea, Mungu Pia anaweza sema nawewe Kwa sauti ya
waziwazi.
Tusome 1
Samweli 3:10-11
“BWANA akaja,akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli !
Samweli ! Akasema nena BWANA kwakua mtumishi wako anasikia. BWANA akamwambia
Samweli, Angalia nitatenda tendo katika Izraeli, ambalo kila atakayelisikia
masikio yake yatamwasha”
Ukisoma 1
Samweli 3:4-9
Mungu alipoanza kumuita Samweli au Kasema nae Samweli hakujua ni
Mungu, akadhani ni Eli, mara zote tatu BWANA alipomuita alikimbilia kwa Eli
akidhani ndie anayemuita, hadi mara ya tatu Eli alipotambua anayemuita Samweli
ni Mungu mwenyewe. Ndipo akamwambia Samwel aseme hivi …Nena BWANA
kwakua mtumishi wako anasikia…
Je, Mungu amewahi kusema nawewe Kwa sauti ya waziwazi? Kama ndio
ulijuaje ni Mungu? Au kwakua hukumuona anaekuita? . Na kama utajibu hapana, una uhakika?
Au hujui yule anayekusemeshaga ndie Mungu? Au ukisikia sauti huoni mtu huwa
unakemea? Lakini
ni vizuri kuwa mwangalifu tena sana, kwani shetani nae anaweza kusema nawe kwa
sauti
MFANYE
MUNGU RAFIKI, SEMA NAE MARA KWA MARA UTAJIKUTA SIKU MOJA ANAKUJIBU UNAMSIKIA,
ILA UTAKATIFU UNAHITAJIKA.
Tuambatane sote sehemu ijayo…
Post A Comment:
0 comments so far,add yours