Na Mwl
Deborah Lema
Je, Mungu amewahi kusema nawewe Kwa sauti ya waziwazi? Kama ndio
ulijuaje ni Mungu? Au kwakua hukumuona anaekuita?. Na kama utajibu hapana, una
uhakika? Au hujui yule anayekusemeshaga ndie Mungu? Au ukisikia sauti huoni mtu
huwa unakemea? Lakini
ni vizuri kuwa mwangalifu tena sana, kwani shetani nae anaweza kusema nawe kwa
sauti.
Mungu hujidhihirisha kupitia Neno lake
Biblia imejaa majibu, mwongozo, masahihisho na jumla ya taratibu
zote juu ya maisha ya mwanadamu. Yani katika dunia hii hakuna jipya, yote
yalishaandikwa. Lakini tutajuaje ikiwa hatusomi neno?
Huwa inatokea mtu anapata wazo, au anasukumwa juu ya jambo
fulani lakini anabaki njia panda. Lakini punde asomapo neno au mtumishi wa
Mungu akasimama kuhudumia watu anaanza kushangaa imekuaje? Maana Yale
yanayonenwa yanagusa maeneo yale yale. Kumbe ni Mungu amejidhihirisha kupitia neno lake.
Hakuna neno katika BĂblia lisilo na maana, tusome…
2
Timotheo 3:16
Kila
andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa
yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadabisha katika haki;
Ni dhahiri Neno la Mungu lina pumzi ya Mungu ndani yake.
Linaishi. Halikadhalika katika yote tunayopitia, Mungu hujidhihirisha kupitia
neno lake.
Tuamue tu sisi kutoona ama kufumbia macho, lakini majibu yetu
hupatikana katika neno lake. Ni jumumu letu kusoma na kuomba Roho Mtakatifu
atusaidie kuelewa maana kusoma tu haitakusaidia kama hautaelewa.
Unajua unachotakiwa kufanya unapokutana na jambo lolote? Ni
kulijua neno la Mungu.Tazama hapa
Marko
12:24
Yesu
akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko
wala uweza wa Mungu?
Mathayo
22:29
Yesu
akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
Maandiko hayo yadhihirisha ya kwamba, ikiwa tunayajua maandiko,
basi tutakuwa tunajua uweza wa Mungu. Na katika kujua uweza wa Mungu, basi
tutaona anavyojidhihirisha kwetu mara zote – kupitia Neno lake.
Jipangie muda kila siku wa kusoma neno la MUNGU kwa msaada wa
Roho Mtakatifu.
Baada ya kuona sehemu ya tano vile Mungu anaweza jidhihirisha
kupitia neno lake na tukashuhudiwa ndani na nje.
Mungu
anavyojidhihirisha kwa kuachilia mzigo ndani unaoleta matokeo chanya nje.
Natamani unielewe na kwa pamoja tumzalie BWANA matunda katika
Hili. Wako wengi Sana Mungu anawasukuma kufanya vitu mbalimbali lakini
hawavifanyi kwakudhani havitafanikiwa au watachekwa au watawezaje. Tusome
habari za Dorkasi katika Matendo
9:36-43
Habari hii kwa wasomaji wa neno si habari geni kwao .Sitasoma
mistari yote, Naomba kusoma mstari wa 39 Unasema hivii…
“Petro akaondoka akafuatana nao, Alipofika wakampeleka juu
orofani wajane wote wakasimama karibu naye, WAKILIA NA KUMWONYESHA ZILE KANZU
NA NGUO ALIZOZISHONA DORKASI wakati ule alipokua pamoja nao”
Sifa kuu ya jambo la ki Mungu halinaga matokeo hasi, labda ukute
ulijichanganya mwenyewe katika kulielewa au katika kulitendea kazi. Mungu
anaweza kujidhihirisha kuwa ni yeye kupitia matokeo chanya yatakayo kuja baada
ya kutendea kazi ule mzigo uliopewa ndani.Dorkasi kazi Yake ilimgusa Mungu, na
hata baada ya yeye kufa wajane hawakuona aliyeziba pengo Lake, hivyo hawakua
tayari kumzika. Lakini yote ni kwa sababu ya matokeo chanya ya ule mzgo uliokua
ndani yake.
Mungu alijidhihirisha Kuwa anatambua thamani yake duniani na
ndipo akarudishiwa uhai wake.
Wangapi wanakufa tunakimbilia kuwazika? Je, unadhani ukifa leo
watu watagoma kukuzika watake urudi? Kama ndio kwa lipi? Na kwa hilo ni kwa
wanadamu au linamgusa Mungu? Hata mimi najaribu kujibu haya maswali
maana yananihusu pia.
Nimejaribu kueleza kwa uchache vile Mungu anajidhihirisha ingawa
Bado zipo namna nyingi zaidi ambazo Mungu hujidhihirisha ikiwemo kwa njia ya
maombi na kadhalika. Tuhitimishe kwa kuona je, MUNGU ANAPATIKANA WAKATI GANI?
Ni kweli Mungu yupo wakati wote lakini Hii zaburi yasemaje hapa?
ZABURI
32:6
“Kwa
hiyo kila mtu mtauwa akuombe WAKATI UNAOPATIKANA, hakika maji makuu yafurikapo
hayatamfikia yeye”
Kuna wakati unaakili zako Timamu, unaelewa, unasikia na Unajua
Kama si kufahamu wajibu wako sahihi mbele za Mungu ambao
ukiutekeleza unapokea haki yako. Lakini ubaya tuna tabia ya kusubiri maji
yatufike shingoni Mambo hayaendi, kila njia imeshindikana Ndio
tunarudi kwa Mungu kwa machozi, lakini kumbe muda wa kumuhusisha Mungu tulikua
nao na tukaacha. Lakini tunataka tumtafute Mungu kwa dharura,
hicho kitu hakipo.
Wekeza kwa Mungu, tumia hicho kipawa chako kumtumikia Mungu,
tumia pesa zako,wakati huu ambao una akili timamu tumika , unaijua kweli, una
nguvu ya kumtumikia , unauwezo wa kwenda ibadani, huu Ndio wakati wako au huu
Ndio wakati tunaoweza kusema MUNGU ANAPATIKANA KWAKO
USISUBIRI MAMBO YAKUHARIBIKIE, USISUBIRI UWE MAUTIUTI KITANDANI,
USISUBIRI UVUNJIKE MIGUU NA MIKONO NDIO UMWENDEE MUNGU KWA MACHOZI BAADA YA
SHETANI KUKUCHAKAZA, WAKATI MUNGU ANAPATIKANA KWAKO NI SASA
ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI KATIKA KUJIFUNZA HAYA
Post A Comment:
0 comments so far,add yours