Mwalimu Christopher
Mwakasege ametoa ushuhuda huo katika semina iliyofanyika katika viwanja vya
Furahisha jijini Mwanza Semina hiyo yenye somo linaloitwa namna ambavyo Roho
Mtakatifu awezavyo kukusaidia ili upokee kile unachokiomba imeanza Tar 19-07-2011
na kuisha Tar 23-07-2011.
Alisema Roho mtakatifu
akwambiavyo omba hiyo haina MJADALA ni kuingia kwenye maombi mpaka upate
unachokiomba kwa kuwa gharama ya kuingia kwenye maombi ili kupata ulichotakiwa
kukipata ni ndogo kuliko gharama ya kukosa kile ulichoambiwa ukipate katika Maombi
hayo.
Roho mtakatifu
anapokupa mzigo wa kuombea jambo anakupa na muda ukizembea muda huo
ukipita kinakuwa ni kiporo, na kiporo kinaweza kikalika na kipo ambacho
hakiliki. .
“Tulipoenda Israel na
Fanuel Sedekia kisha akaanza kuumwa madaktari waliniambia ubongo wake kwa
asilimia tisini haufanyi kazi. Lakini walishangaa kwa nini kila mara niko pale
Hospitali wakasema kwa nini usikae tu Hotelini kisha ukawa unapiga simu
kuulizia hali ya Mgonjwa? Wao hawakujua kwa nini naenda pale kwa kuwa suala la
kupiga simu tu sio tatizo ningeweza kurudi Arusha kisha nikawa napiga simu.
Suala hapa ni kuwa
nilikuwa naenda kila mara kwa ajili ya kumfanyia maombi, nilikuwa nakaa
kandokando ya Bahari ya Galilaya nafanya maombi juu ya Sedikia kwa masaa sita
nikitoka hapo nasikia upako wa ajabu sanakIsha napanda Taxi kuelekea
Hospitali. Nikifika Hospitali madactari na watu wa ICU walikuwa washanifahamu
hivyo naenda moja kwa moja kwenye chumba cha nguo nabadili nguo kisha naingia
ICU alikolazwa.
Nikifika nambana Mungu
kwa maswali Mengi namuuliza Sedekia, hivi unaongea nini na Yesu muda wote huo
si urudi? na kisha namuuliza Yesu, hivi Yesu si unafahamu kuwa Sedekia anamke
ukimchukua mkewe atamuachia nani? Kisha baada ya maneno hayo naweka mkono juu
yake. Nilipokuwa nikiweka mkono juu yake ghafla upako wote
unakuwa kama umenyonywa.
Baada ya hapo narudi
hotelini naanza tena kumuuliza Mungu hivi Mungu kama basi husikii
maombi yangu sikia maombi ya watanzania kwa kuwa saa hiyo nilijua watanzania
wengi wanamuombea Sedekia.
Inafikia wakati nakata
tamaa lakini ndani yangu najisemea Mwakasege haiwezekani jitie moyo kisha
nabadili aina ya maombi, kwa kuwa nilikuwa na nguo zake pamoja na passport yake
nikawa naviweka kati kisha nikawa naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko hotelini
usiku nazunguka nguo zake na paspot yake huku nikifanya maombi.
Taratibu Mungu akaanza
kuniambia kuwa sedekia harudi, Kipidi hicho mimi na familia yangu tulikuwa
tumepanga kwenda kupumzika nchini Uingereza wakati wa skukuu ya Chrismass,
na booking mpaka ya Hotel tulikuwa tumeshafanya, na watoto wote wako
nyumbani wakijiuliza tunaendaje kupumzika wakati Sedekia anaumwa? Chrismass
ikapita na mwaka mpya pia kisha Sedekia akafariki.
Baada ya kifo hicho
sikuchoka nkarudi tena kwa Mungu nikamuuliza kwa nini Mungu umeamua kumchukua
Sedekia mikononi mwangu? Mungu alinijibu vitu ambavyo siwezi kuvisema hapa.
Kila siku mimi ni
mgeni katika maombi namhitaji ROHO anifundishe kwa upya kwa kuwa sijui vita
gani ninakwenda kupambana nayo, Mungu anabaki kuwa Mungu kwa kuwa hufanya
atakavyo”
Post A Comment:
0 comments so far,add yours