Yeremia 29:11, maana
nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya
mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Je, si ni jambo
la kufurahisha kujua kwamba kuna mpango wa maisha yako? Hajalishi yale
yametendeka maishani mwako, hatua zile ulienenda vibaya, la muhimu ni kujua
kwamba Mungu amekuongoza hadi hapa sasa. Amekuwa akikuongoza kwake mwenyewe.
Ukweli ni kwamba tumaini lako kamili na hatima yako iko ndani yake.
Hii inamaanisha kwamba unaweza
kuyaishi maisha yako yote kwa ajili ya Yesu na ndani yake. Na kw ajili yake, na
ahadi yake kwamba hatakuacha, sasa kuna jambo la kusisimua.
Ni safari, safari ya umilele
Unaweza kuwa unauliza, je sasa
nitafanya nini kwa vile nimempokea Kristo? Ni swali muhimu mno kwa vile
umechukua hatua ya kwanza. Hata ingawa leo hautajihisi tofauti, jua kwamba
Kristo ameanza kutenda kazi ndani yako.
Wakolosai 2:6-7 inasema, Basi
kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;
wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani,
kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.
Shina hiyo hujengeka kupitia maombi,
kusoma Neno la Mungu, Bibilia na kumruhusu Roho Mtakatifu akuongoze na
kukuelekeza.
Kuanza maisha yako na Kristo
Ahadi ya neon la Mungu, haya
ndiyo maneno ya Yesu kwa wanafunzi: Mwivi haji ila aibe na kuchinja na
kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10
Umeitwa kuishi maisha ya
ukamilifu nay a kufurahisha katika Kristo nasi tuko hapa kukusaidia kuanza
safri yako kwa nguvu.
Author: Joyce Meyer
Source: https://tv.joycemeyer.org
Post A Comment:
0 comments so far,add yours