Mtume Paulo anasema katika Waraka wake kwa Wakolosai sura ya tatu na mstari wa kumi na saba kuwa; “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”

 

Hii ina maana ya kuwa, tukila tule katika Jina la Yesu Kristo. Tukilala tulale katika Jina la Yesu Kristo. Tukizungumza tuzungumze katika jina la Yesu Kristo. Tukiimba tuimbe katika jina la Yesu Kristo. Tukitembea tutembee katika jina la Yesu Kristo. Tukisafiri tusafiri katika jina la Yesu Kristo. Tukilima shambani tulime katika jina la Yesu Kristo; na kadhalika.

 

Kwa nini tunatakiwa tufanye mambo yote katika jina la Yesu Kristo? Jina hili la Yesu Kristo lina sehemu gani katika maisha yetu ya kila siku?

 

Kama tunatakiwa kufanya mambo yote katika jina la Yesu Kristo, kwa nini hatufanyi hivyo?

 

Ukitafakari maagizo tuliyopewa katika biblia utaona ya kuwa, maisha yetu yote yanalitegemea jina hili la Yesu Kristo.

 

Kama mambo yetu yote yanatakiwa https://www.mwakasege.org yafanyike kwa jina la Yesu, basi ni muhimu tujifunze zaidi na zaidi kila siku juu ya jina hili la ajabu.

 

Ni maombi yangu kwa Mungu Baba, katika jina la Yesu Kristo ya kuwa maneno yaliyomo katika somo hili yatachochea kwa upya kiu iliyomo ndani yako ya kutaka kufahamu zaidi siri iliyomo ndani ya jina la Yesu Kristo.



Mwalimu Mwakasege


Share To:
Magpress

Bila jina

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours