Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. —YEREMIA 29:11
Iwapo
una picha mbaya binafsi kujihusu, tayari imeathiri vibaya mambo yake ya kale,
lakini unaweza kuponywa na kutoruhusu ya kale kujirudia. Ninakuhimiza kusahau
yaliyopita hata mambo yoyote hasi ambayo umehisi kujihusu na kujisukuma mbele
kuelekea vitu ambavyo Mungu amekuwekea.
Mungu
ana mpango mwema na kusudi kwa kila mmoja wetu na njia maalum na wakati
mtimilifu wa kuyafanya yatimie, lakini sio sisi wote tunayaona haya. Wakati
mwingi tunaishi chini ya kiwango cha maisha ambayo Mungu anakusudia tufurahie.
Kwa
miaka mingi sikutumia haki na faida zangu kama mwana wa Mungu. Ingawa nilikuwa
Mkristo na kuamini nitaenda mbinguni nitakapofariki, sikujua kwamba kuna jambo
ambalo lingefanywa kuhusu maisha yangu yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Nilikuwa
na picha mbaya kujihusu, na ikaathiri maisha yangu ya kila siku, pamoja na
mwono wangu wa siku zijazo.
Leo
unaweza kukubali upendo wa Mungu juu yako na uufanye upendo wake msingi wa
kujipenda na kujikubali. Pokea hakikisho lake, ukijua kwamba unabadilika na
kuwa vile anavyotamani uwe. Halafu uanze kujifurahisha—ulipo—ukiwa njiani
kuelekea ukomavu mkamilifu wa kiroho.
Acha Mungu awe Mungu katika maisha
yako. Mweke katika kiti cha dereva. Anajua analofanya.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours