Mambo ya
nyuma yasikufanye ushindwe kuifurahia leo yako au kupanga mipango kwa ajili ya
kesho yako. Hakuna ambaye hajawahi kuumizwa iwe ni maisha/ mtu / watu au hali.
Kinachotofautisha ni uamuzi wa kuachilia maumivu na machungu ya nyuma na
kusonga mbele. Kuendelea kuyashikilia na kuyabeba kama bango haiondoi uhalisia
kuwa yametokea wala hakufanyi leo yako kuwa nzuri.
Tambua
kuwa maisha yako ni jukumu lako na si mwingine yeyote. Haijalishi umeumizwa
vipi, unawajibika kuishi maisha yako kwa furaha na kufanya bidii ili kesho iwe
bora zaidi. Aliyekukosea au kukusababishia maumivu hawajibiki kukupa furaha
wala kukuondolea maumivu, ni jukumu lako asilimia mia. Amka sasa, jikung’ute
maumivu yote na uchungu wa yaliyopita na usonge mbele.
Si kwa
uweza wala nguvu zetu bali kwa msaada wa Mungu.
chanzo: https://womenofchrist.wordpress.com
Post A Comment:
0 comments so far,add yours